Je unafahamu kuwa AG wa zamani Lorreta Lynch katika nafasi yake kama AG ameshawahi kuuliza swali kuhusu uchunguzi kwenye mahojiano na akajibu "hajui"?
Majibu ya Lorreta Lynch
Kama "underlying evidence" zimejumuishwa kwenye "full report" ya Mueller, kwanini House Judiciary Committee chini ya mwenyekiti wake Jerry Nadler wali-issue subpoena ya "full report" na "underlying evidence" badala ya "full report" peke yake?
Kama Rosenstein "hakupaswa kushiriki kwenye maamuzi katika uchunguzi ambao yeye mwenyewe ni shahidi", Je, aliwezaje kushiriki kwenye kuusimamia huo uchunguzi ambao yeye mwenyewe ni shahidi?
Usi-quote barua yote, nataka utafakari barua wewe kama wewe.
Barua ya Mueller ilikuja kabla ya kutolewa "redacted report" na AG Barr yenye kurasa 448. Kwenye barua ya Mueller, anasema summary ya AG Barr haija-capture "context, nature, and substance" ya kazi na hitimisho lake kwa maana ya "introductions" na "executive summaries" ya Vol I na II zenye kurasa 19.
Nakuuliza
Mwalimu ,Je, Kama AG Barr alikuwa na nia ya kuficha ", kwanini baadae alitoa ripoti kwa umma (redacted) yenye hizo sehemu (kurasa 19) na kila kitu kwenye kurasa 448? Kwanini alimwambia Mueller kuwa anataka kutoa ripoti kwa umma, na kuwa hataki kuitoa ni "piecemeal"?
Huu uzi ni masuala yote ya US chini ya Trump. Uchunguzi wa Hillary ulifanyika kabla na wakati wa kampeni za Urais za mwaka 2016. Hillary aliondolewa hatiani na FBI Director Comey wakati wa kampeni yake na Trump. Uchunguzi dhidi ya Trump ulianza kabla hajawa Rais, wakati wa kampeni za Urais na Hillary mwaka 2016, na baada ya kuwa Rais. Kwahiyo uchunguzi wa Hillary unaingia kwenye huu uzi. Kama huna jibu unasema huna, nimekuuliza maoni yako binafsi.
Pia, unamaanisha nini unaposema "Hatuwezi kutumia uchunguzi wa Hillary ku-justify kilichofanyika kwa uchunguzi wa Trump"?