McGahn AZUIWA KUSEMA, AJIBU MAPIGO
Trump Jr AITWA MBELE YA KAMATI YA SENETI
Katika siku za karibuni kumekuwa na kauli za ''it's time to move on' kutoka kwa viongozi wa Republicans kama McConnel, Lindsey na wengine. Kauli hiyo ina maana '' waachane na''
Ni mkakati wa kufunika suala la Mueller linalozidi kugubiga habari za Marekani kila uchao Vichwa vya habari ni Mueller, McGahn, Don Jr n.k. Hiyo ndiyo habari ya viungani DC
Kamati ya senate intelligence chini ya R. Burr imemwita Don Trump Jr
Hilo limewaudhi GOP ambao lengo ni ''move on''
Mwito ni baada ya kusoma redacted version, na inaelekea Don ana la kujibu!
Wito wa Don umemvuruga mzee wake Trump aki tweet bila huruma wala mpangilio.
Huku Don akitakiwa seneti, wanasheria wanamtaka afanye ''plead the 5th''
Ndani ya WH, McGahn ameuziliwa kutotoa ushirikiano na kamati hata kama ni Raia.
Magazeti ya NY Times na Wall Street yameeleza kuhusu WH kumtaka McGahn aseme '' hakukuwepo na obstruction of justice na kwamba Trump hakumuagiza amfukuze Mueller''.
Habari zinaeleza kuw alitakiwa kusema hayo kabla ya redacted report na baada ya kutolewa.
Maana yake ni moja AG Barr aliwatonya WH kuhusu ushuhuda wa McGahn
Ni kutokana na hilo, hakuna shaka kinachoitwa grand jury material ni uchafu wa Rais Trump na Familia yake dhidi ya Marekani.
Hiyo ndiyo sababu kubwa taarifa ya Mueller inafanywa jando
Kama ilivyoelezwa bandiko#856
Mag3 kesi zingine zipo katika state na si federal
Nguvu ya Barr kuziingilia ni ndogo, na kila kilichofichwa kitatoka hadharani
Hasira za Trump dhidi ya kuitwa mwanae zinajengeka katika msingi kuwa Don Jr atakuwa chini ya kiapo, taarifa za redacted material zipo hivyo kuna nyakati atalazimika kusema ukweli
Rais Trump anagoma kila kitu huku akisema taarifa ni total exoneration and vindication
Ikiwa ni hivyo kwanini anawazuaia akina McGahn kusema wanachojua huku akiwahukumu?
Taarifa za McGahn kumkatalia Trump mara mbili kuhusu ombi lake na huko nyuma kutaka kujiuzulu kunaeleza mengi na kwamba ana kitu anachojua ambacho ni mwiba kwa Trump
Kila mbinu inaoenekana kubuma. Jana Rud Guillian alianzisha mjadala makusudi kuhamisha habari ya Mueller. Hilo halijafanikiwa zaidi ya ku back fire WH na kampeni ya Trump
Muda si mrefu watu watajua zaidi ya wanachojua.
Watabaini Barr ameficha nini na hapo kunaweza kuwa na tatizo tena kubwa.
Tusemezane