Duru za siasa - Matukio

Mkuu Mchambuzi
Wakati tukisubiri uendelee kuhusu asasi za kirai na kijamii |(civil society) nitumbukize senti moja hapo mstari wa mwisho kuhusu vyombo vya habari.

Sheria ni kweli ina matatizo kwakuzingatia iliwekwa ili kukidhi haja ya mfumo wa wakati huo.
Sheria hiyo imetumika ndivyo sivyo na kuwa mpini wa kuua demokrasia.

Kwa upande mwingine tuna tatizo kubwa sana la waandishi wa habari. Fani ya habari bado ipo nyuma kwa kutoa waandishi ambao nadiriki kusema wengi hawakidhi viwango. Waandishi wamebadilika kutoka katika kiini cha kazi zao ikiwa ni kutafiti, kuhakiki na kutaarifu na sasa wamekuwa reporters.

Nachelea kusema sijui wangapi wanaweza kuona maana halisi ya bandiko kama lako na nini wanaweza kupata kutoka hapo. Fani ya uandishi mara nyingi hutegemea inputs ndipo mambo kama research yanafuata.
Kwamba mwandishi anatakiwa akione kitu halafu akifuatilie mbali na kinavyoonekana (Investigative jouranalism).

Tunatakiwa tuwe na waandishi ambao ni wataalam wa fani na si 'one size fits all'
kwa mantiki hiyo uwezekano wa mtu kueleza nini civil society na role yake katika jamii inaweza kuandikwa na kueleweka.

gfsonwin
katika bandiko lako hapo juu kuna kitu kimenigusa. Kuhusu mzozo wa EAC nadhani rais anamchango mkubwa wa kuzorota kwa hali. Simaanishi maamuzi yake ninamaanisha jinsi anavyokabliana na suala hilo.

Kwa mfano, rais JK amefanyakazi kama waziri wa mambo ya nje kwa miaka 10.
Amefanya kazi na marais 2 na hivyo kuingia katika vikao vikubwa vya maamuzi yakiwemo yaliyohusu EAC.

Rais JK alikuwa mwenyekiti wa jumuiya kwa nyakati fulani. Kwa maneno mengine ana uzoefu wa hali ya juu kuhusu EAC.Sielewi imekuaje hadi imefikia kiwango hicho bila yeye kufahamu au kuwasiliana na umma ili uelewe nini kinatokea.

Kuna uwezekano maamuzi yake yakawa sahihi na pia yaweza kuwa siyo. Hiyo si hoja, hoja kubwa ni kuwa na communication breakdown kati ya serikali na wananchi hivyo kuwafanya wabaki wanahisi hisi na si kuwa na uhakika na hali iliyopo. Hii ni failure kwa uongozi the least to say.
 

mkuu Nguruvi3 nakushukuru kwa mchango wako wenye kina katika bandiko lako hili. Lakini hapa naomba nirudi tena kusema jambo moja dogo sana amablo mie binafsi linanitatiza.

Leo hii imeripotiwa kwamba Mhe Samwel Sitta amesema kwamba rais atakwenda kushiri katika mkutano wa marais wa EAC. HOJA YAKE binafsi mie nimeielewa lkn imeniach ana mswali kadhaa juu yake;

mie najiuliza hivi rais wetu huwa anawajibika kwa nani?? ni wazi kwamba anawajibika kwa wananchi kama ndivyo kwann sisi ambao ndo tunaomuwajibisha yeye kama yeye hasemi na sisi?? umesema swala la communication breakdown lakin mimi silioni kwa maana unayoiona wewe ila mimi kwa mara ya kwanza naomba nitamke wazi kwamba rais wetu anatudharau sisi wananchi wake na ndio maana kauli zake hata pale inapobidi atoe kauli yeye humuacha mtu kutoa kauli hiyo.

Kama raisi anagelisema haya basi maswali mengi ambayo yako kwenye vichwa vyetu tungemuuliza tofauti na sitta alivyomsemea na kusema yeye hana la kusema juu ya Tanzania kutengwa................

Nimekuwa mfuatiliaji wa maswala ya Marekani kwa muda mrefu sana lijapo swala la maslaha ya wananchi utamwona raisi kasimama anawaambia wananchi nini kinachofwata, tumeona majuzi tu Obama akihutubia wanachi wake juu ya kuivamia serbia, na hata aliposimamisha kwa muda shughuli za serikali kwasababu ya bajeti.

nimependa sana hii tabia yake kwasababu huulizwa maswali na hutoa majibu ya kina kwa wananchi wake sasa leo hii sisi raisi hana muda wa kutusikiliza wala hana muda wa kuongea na sisi. ukichunguza hotuba zake za kila mwezi ambazo na yeye pi aliziiga kwa Mkapa sawa huwa zina address matukio ya mwezi huo lkn bado hazitoi majibu ya kina wakati mwingine.

Kitendo cha sisi kuanza kuisi umetengwa EAC yeye alipaswa ashtuke manake si anasoma habari?? kisha afanye uchunguzi wake binafsi na aje na majibu kwetu sisi wananchi, na sio kusemewa na Sitta wakati Sitta mwenyewe anasema hana la kusema juu ya nchi kutengwa EAC.
 
Last edited by a moderator:
YAH: Nafasi Na Changamoto Zinazozikabili Asasi Za Kiraia na Kijamii Katika Kuleta Mabadiliko Ya Kweli Tanzania

Wakuu Nguruvi3 et al, Naomba mniwie radhi kwa kutorudi kwa wakati kujadili hoja zangu viporo; Naomba niingie moja kwa moja kwenye hoja husika, nikilenga hasa suala la Mabadiliko kupitia Katiba Mpya;

Mjadala kuhusiana na nafasi na changamoto zinazozikabili Asasi Za Kiraia/Kijamii (Civil Society) itaeleweka Zaidi iwapo tutaijadili katika muktadha unaosisha Serikali (STATE) na Jamii (Community); Katika nchi kama Tanzania, pande mbili hizi (STATE & COMMUNITY) traditionally zimekuwa zikikinzana kimsimamo na kimtazamo katika suala zima la siasa na nafasi yake katika maendeleo ya nchi – kijamii na kiuchumi, kama ifuatavyo:

Kwa upande mmoja – State (Serikali) ina characteristics na pia inahusika Zaidi na masuala yafuatayo: ·

-
Legacy ya ukoloni pamoja na incorporation ya serikali (state) katika jumuiya ya kimataifa ya nchi huru duniani (international community of the so called ‘sovereign states'); ·
-
Uamuzi wa kupendelea Zaidi ‘top-down approach' to development or change katika taifa (mfano, sera za maendeleo, mabadiliko kama vile ya katiba n.k); ·
-Na katika miaka 25 iliyopita, kushindwa kwa serikali kuhimili pressure kutoka kwa umma kutokana na serikali kushindwa kusimamia ipasavyo liberalization & globalization kwa faida ya walio wengi nchini.

Kwa upande pili wa mlinganyo (equation) huu ni Jamii (Community) ambayo ina charecteristics na pia inahusika Zaidi na masuala yafuatayo: ·

-Pre-colonial past (kwa mfano rejea maamuzi ya Mwalimu kuingiza nchi kwenye Ujamaa ndani ya miaka sita ya uhuru wa Tanganyika); ·
-Reciprocity culture ambayo ina mizizi mirefu katika jamii yetu – kwa mfano, uwepo wa long term interdependent exchanges between partners (both between individuals and also individuals and institutions), na moja ya mifano mizuri ni mahusiano baina ya chama tawala (CCM) na jamii wakati wa chaguzi ambapo reciprocity culture uonekana wazi; Hali hii haitakiwi kuwepo katika jamii iliyopiga hatua – yani huwa hakuna long term relations between exchange partners, badala yake, wapiga kura huwa ni rational and incorrupt, and if you don't deliver, mwingine anapewa fursa; ·
-
Pia, tofauti na characteristic ya state kuhusiana na ‘top – down' approach to development, kwenye upande wa JAMII, huwa ni preference ya ‘bottom – up' approach to development. ·
-Vile vile, tofauti na Serikali (state), kwenye jamii kuna matumaini ya kweli ya african renaissance/revival kwa manufaa ya walio wengi, na jamii constantly inakuwa ikitafuta platform ambayo inaonekana ni more effective kufanikisha hilo (je, mbadala wa kweli wa CCM ni Chadema?);

Katika muktadha wa mahusiano baina ya pande hizi mbili, serikali (state) stands to abuse power kwa faida ya wachache na pia kuondoa matumaini ya maisha bora kwa watanzania walio wengi, hukku jamii (community), pamoja na changamoto inazokabiliana nayo, stands for a better and a brighter future. Nadhani hadi hapa tunaweza kuona kwa urahisi kwanini Serikali (state) na jamii (community) wanakuwa na mvutano na mara nyingine uadui, na hali hii inakuwa manifested in the state – civil society relationship.

Sasa tukihamishia mjadala wa hapo juu kwenye suala la katiba: Tangia uhuru, kinachowashikilia watanzania kuwa pamoja haijawahi kuwa ni suala la national constitution & legal framework; Badala yake imekuwa ni a perceived need to guard against a common enemy (nje na ndani ya nchi); hadi leo hii, chama tawala kinaendelea kujenga hoja kwamba ‘national unity' (tena unconditionally), is a pre-requisite for national development; Katika muktadha huu, serikali (kupitia a top-down approach) inaona kwamba ndio yenye mamlaka ya mwisho ya kuamulia wananchi sera, priorities, na pia pace ya mabadiliko, ikiwa ni pamoja na suala la katiba mpya; Chini ya mazingira haya, criticisms are intolerable, vinginevyo nguvu ya serikali inaweza kutumika to eliminate yoyote mwenye kupingana na serikali;

Ndio maana, licha ya matumaini makubwa miongoni mwa watanzania wengi kuhusiana na mchakato wa katiba mpya, binafsi naamini kwamba we still have a very long way to go before we turn into a true ‘liberal democracy'. Kuna kila aina ya ushahidi kwamba uongozi wan chi (CCM) hauna haraka ya kufikia lengo hili. Katika kipindi chote tangia uhuru wan chi yetu, serikali imekuwa ikipendelea Zaidi to manage the process of transition carefully, na kujaribu ku - balance the pursuit of political liberalization na wasiwasi waku juu ya madhara ambayo yanaweza kutokea katika civic peace and social harmony, two values ambazo ndio pekee zilizobakia kuipa serikali ya CCM legitimacy mbele ya umma. Kwa hali hii, demokrasia nchini Tanzania is more likely kuendelea kuchechemea kwa muda kwani kuna dalili kubwa kwamba itaendelea kuwa managed from the ‘top down', huku serikali ikifanya kila hila ili civil society isinyakue mchakato husika, kwani ikitokea hivyo, given the antagonism discussed hapo juu baina ya JAMII na SERIKALI, ruling elite na taasisi zao zinazoendesha nchi kwa mtindo wa informal institutions kuliko formal institutions, watakuwa katika hali mbaya sana;

Itaendelea...
 
Wana duru tulisimama kidogo kutoa nafasi kwa Mchambuzi kumalizia mada yake akipata wasaa.
Wakati tunamsbiri tutarejea kwa uchache yaliyojitokeza hasa hotuba ya rais.
 
...........................
 
Rais ametoa hotuba pengine kwa kuzingatia ukweli huo hapo juu
 
Duru za Siasa - Matukio inalitazamaje suala la mpambano wa viongozi wa Chadema kushambuliana wenyewe kwa wenyewe kwenye mitandao ya kijamii kwa mustakabali wa Chadema na taifa zipi athali zake.
 
Duru za Siasa - Matukio inalitazamaje suala la mpambano wa viongozi wa Chadema kushambuliana wenyewe kwa wenyewe kwenye mitandao ya kijamii kwa mustakabali wa Chadema na taifa zipi athali zake.
@Ritz kwa muda duru imelifuatilia suala hili kwa uangalifu, umakini na kwa kina.

Duru imefikia hatua nzuri kabisa ya kulizungumzia kwa kuzingatia mambo yafutayo.
1. Historia ya tatizo
2. Chimbuko la vurugu za sasa (kwanini sasa)
3. Sababu za mtinange unaondelea CDM (sababu kuu tatu)
4. Makundi yanayohusika
5. Hatima na mustakabali wa vurugu hizi kwa taifa
6. Nini CDM wafanye kujinusuru.

Tunaomba wana duru uvumilivu wa masaa 48 tu tutakuwa mtandaoni. Hataonewa mtu hata hurumiwa mtu, ukweli utatamalaki.
 
MTAFARUKU, MPAMBANO NA KUSIGISHANA KWA CHAMA CHA CHDEMA
MZOZO WA VIONGOZI NA UONGOZI


Sehemu ya kwanza

Katika siku za karibunu Chadema imejikuta katika mtafuruku unaohusisha viongozi na kutikisa uongozi mzima. Kuna wanosema mtafaruku huu ni mdogo na wengine wakidai ni kukua kwa chama.
Ukweli usio na shaka mgogoro huu ni mkubwa, mzito unaotishia uhai wa Chama kwa vigezo vya kijamii na kisiasa.


Kuna sababu kuu mbili zainazopelekea hali kutotulia na kuongezeka kwa uhasama.
1. Sababu kutoka ndani ya chama
2. Sababu kutoka nje ya Chama.

Hatuwezi kuliongelea tatizo bila kujua chanzo chake japo kwa uchache. Kwa muktadha huo tutakuwa na sehemu tatu zinazohusu mada hii. Tunatanguliza samahani kwa urefu wa mada, uhuhimu wa kufanya hivyo ni mkubwa kuliko kuliangalia tatizo kijuu juu.

A: Kuasisiwa kwa chama:
Tunafahamu waasisi wa chama ni wale waliokataa kukubaliana na sera za chama tawala nayakati hizo.
Wengi walipoteza nafasi zao kwa kupingana na 'establishment' ndani ya CCM.

Kwa bahati mbaya kutokana na mvuto wa Mwalimu wakati huo ,nyota zao zilifunikwa na wao kuonekana kama 'wahaini\. Mmoja wapo ni mwasisi mzee Edwin Mtei.

Chadema kikawa chama cha watu wasiokubaliana na CCM na wenye 'resentment' kikiungwa mkono na watu wa mikoa ya kaskazini zaidi. Kuungwa mkono si kutokana na asili ya viongozi bali mwamko na kiwango kikubwa cha uelewa kuliko sehemu nyingi za nchi. Uasi wa mikoa ya kaskazini dhidi ya CCM ni wa kihistoria.

Mzee Mtei aliendeleza chama katika ngazi ya kitaifa tbila kuingia mikoani au vijijini.
Mrithi wake marehem Bob Makani hakuwa tofauti sana na Mtei, pengine utofauti wake ulikuwa kukijenga chama katika bunge kwa kiasi fulani. Na hatimaye akachukua Mbowe ambaye ni mwenyekiti hadi sasa.

Kitu kimoja kikubwa kilichofanywa na Mtei na Makani ni kuwajenga vijana kujiunga na chama.
Hapo ndipo walipowapata akina Mbowe .

Tofauti na watangulizi wake Mbowe aliamua kukieneza chama katika taasisi kama vyuo ambako alifanikiwa kuwaingiza akina Zitto n.k.

Mbowe ana sifa kubwa ya kukisambaza chama. Alipogombea urasi alifahamu hawezi kushinda lakini hiyo ndio ilikuwa njia rahisi ya kukieneza chama. Kwa hilo ni credit ambayo haiwezi kuondolewa kwake.

Chadema ni chama chenye historia ya kubadilisha viongozi bila migogoro.
Ni chama chenye historia ya kuteua mgombea wa nafasi ya Urais kwa mwanachama wa kawaida wa chama.

B:
Mgogoro ulianza katika uchaguzi wa Mwenyekiti kipindi cha pili. Ni wakati huo vijana walioingia CDM walishakuwa maarufu kwa ujenzi wa hoja bungeni. Mmojawapo ni Zitto. Vijana hao walitaka nafasi zaidi ndani ya chama pengine kwa kutaka kufanya mageuzi ya haraka au kwasababu za uongozi tu kwa kuzingatia umaarufu.

Wazee wa CDM kwa kuzingatia utaratibu waliokuwa nao wa kuchagua viongozi waliona chama bado ni kichanga kukabidhi vijana wasio na uzoefu na pengine hilo lingepunguza nguvu za chama.

Walizingatia jitihada za Mbowe na kudhani alihitaji muda zaidi kukijenga chama.
Hata hivyo uamuzi huo ulikinzana na dhana ya demokrasia ambao ni msingi wa chama chao.
Ingawa suala lilimalizwa ukweli ni kuwa halikumalizwa kwa maridhiano bali wengi wape.

Mtafaruku wa pili ni ule wa kuwania nafasi ya kuongoza upinzani.
Huu pia ulimhusisha Mbowe na Zitto . Maamuzi yaliyotolewa hayakuonekana kufuata misingi ya demokrasia(principles) bali kanuni za mardhiano' consensus'
Hili likazidisha ufa kati ya Mwenyekiti Mbowe na Naibu katibu mkuu Zitto

Ykatokea makundi mawili makubwa ndani ya chama.
Kundi la Mwenyekiti linalotetea uendelezaji wa chama kwa kufuata misingi ya waanzilishi na kundi la Zitto linalodhani kuna umuhimu wa mageuzi ya uongozi na kwamba ni wahanga'victims' ndani ya chama.

Kundi la pili la Zitto likaamua kujiimarisha ili kujenga himaya kwa kukusanya vijana.
Ni kundi hili lililojaribu kufanya mapinduzi batili likiwa na akina Kafulila.

Hakuna siri kiongozi wa kundi hilo ni Zitto. Ndipo ulipotokea mtafaruku wa pili uliopelekea akina Kafulila na Sungura kujiondoa ndani ya chama baada ya kunyang'anywa madaraka.
Walitambua wazi kuwa bila madaraka wasingeweza kufikia lengola mageuzi kwa njia za haraka

Zitto anaamini kuwa kutofanikiwa kwake ni matokeo ya kutokuwa katika kundi la 'wazee' au inner cicricle na njia rahisi ni kuanzisha makundi ili yapenyeze katika uongozi wa taifa.

Ni kwa msingi huo aliunda kundi jingine ambalo leo tunaijua kama Chadema 'Masalia'.
Kundi hili lilikuwa na makamu mwenyekiti wa BAVICHA na wanachama wengine.

Kundi hilo lilifanikiwa sana kupenya katika ngazi na ofisi kuu za chama.
Mbinu za kuwachafua viongozi zikaanzia na kila mara kukawa na taarifa za kuchafuana ambazo zilikuwa zinatoka ndani ya chama.Baadhi ya wanachama wakaodnolewa katika nafasi hizo akiwemo Mwigamba.

Kutokana na kuvunjika kwa kundi la masalia na lile la viongozi ndani ya ofisi za chama, ukaanzishwa mtandao mwingine unaohusu viongozi katika ngazi za mikoa.
Lengo likiwa ni lile lile la awali la kutengeneza mazingira ya kukabiliana na kundi la uongozi 'establishment'

CHIMBUKO LA VURUGU ZA SASA.

Itaendelea sehemu ya pili mchana huu......
 
CHIMBUKO LA VURUGU ZINAZOENDELEA

Inaendele...
Chimbuko la vurgu zinazoendelea sasa ni kutokana na kufukia ukweli wa mzozo nilioueleza hapo juu na ni baina ya makundi mawili, kundi liliko madarakani likiwa na mwenyekiti na katibu mkuu, na kundi la Naibu katibu mkuu, mshauri wa Chama na mtandao uliojengeka wa kimikoa.

Makundi haya yana wapiga debe ambao ndio wameleta mtafaruku huu uonekane dhahiri.
Mtifuano uliopo kati ya Lema na Zitto ni uwakilishi tu wa matatizo ya muda mrefu.

Uongozi wa juu umegawanyika katika makundi yafuatayo
1. Kundi linaloamini kufanya kazi kwa kuleta mageuzi (Neutral)
2. Kundi linalowania uongozi kwa matamanio kuwa sasa ni wakati wao(Power struggle)
3. Kundi linaloamini katika CDM kama ilivyoasisiwa na misingi yake (establishment)
4. Kundi la wasaliti ambao wanatumiwa kukihujumu CDM (Traitors)

Kundi la 1 linakereka sana na hali ilivyo ndani ya chama na kwa bahati mbaya hili lina wapiganaji kindaki ndaki wasio na sauti sana ndani ya chama.

Kundi la 2 linajenga mtandao wa kukabliana na kundi la 3 kwa kuamini kuna mambo kama ukanda n.k. na njia
rahisi ni kujenga mtandao wao. Ndilo limekuwa chimbuko la matatizo kila mara.

Kundi hili haliamini katika mageuzi kama hatua(process) linaamini katika hatua za nguvu (radical intervention) na lipo tayari kutumia mbinu chafu hata kama kufanya hivyo kutaumiza chama(bomoa leo tutajenga kesho)

Kundi la 3 linaamini mageuzi ni hatua na linafuata taratibu za makubaliano (consensus) zaidi kuliko demokrasia. Kwasasa limegundua kupungua kwa nguvu yake kutokana na mtandao wa kundi 2 kuwa mkubwa.
Limeamua kujibu mapigo

Kundi la 4 ndilo hatari sana. Hili linawashirikisha watu kutoka chama tawala ili kuhakikisha CDM inakufa kabla ya uchaguzi ujao.

Kundi hili linaungwa mkono na wana CCM kwasababu linafanya kazi iliyokusudiwa.Wapo wanachama wa kundi la 2 ambao ni washiriki wa kundi hili katika jitihada zile zile za kuwania uongozi(power struggle)

Tatizo lililozushwa na Mwigamba halimhusu yeye binafasi.
Mwigamba ni mwakilishi wa mtandao uliojengeka ambao unaona muda unazidi kwenda na mkakati haujafikia mhali pa zuri.

Ni kwa msingi huo madai ya Mwigamba kama 'mkulima masikini' ni kuwepo kwa uchaguzi kwavile mtandao umeimarika vema. Mwigamba si tatizo bali wale walioko nyuma yake ambao ni viongozi.
Mwigamba alipochukuliwa lap top ghafla likatokea kundi lililotaka kumuunga mkono hadarani la wenye viti wa mikoa. Ikumbukwe kuwa kuna katibu mkuu wa mkoa aliwahi kukihama chama kwasababu zile zile za Mwigamba

Tatizo la Lema kumshambulia Zitto si la kisera au misimamo ya chama.
Ni kundi la uongozi linajibu mapigo kwa kushambulia chanzo.
Ndio maana husikii Lema akijibishana na Mwigamba, tumtemeke au mwingine na uongozi umekaa kimya kushughulikia jambo hili.

Tatizo ambalo tumewahi kulisema hapa duru za siasa siku nyingi sasa lipo wazi.
Chadema imejengwa katika misingi ya personality. Kuna watu ambao ni chama na chama ni wao.
Laiti taratibu zingekuwa zinaongoza chama wala tatizo lisingefika hapa lilipo.

Kungekuwa na uwazi katika kuendesha shughuli za chama na kuruhusu mawazo mbadala hata kama hawakubaliani,
kusingekuwa na viongozi wanaojenga makundi yanayotishia uhai wa chama.

Na kwavile kuna ufa, CCM inautumia vema ufa huo kudhoofisha chama.
Inatumia maneno na kashfa zinazotokana na wanachadema kuufanya mtafaruku kuwa mkubwa zaidi.

Tazama jinsi shughuli za CDM zilivyozorota(M4C) na uenezaji wa chama ulivyofifia.
Haya ndiyo CCM inayapenda na imetumia vyombo vya habari rasmi na vya kijamii katika kuendeleza mgogoro ambao ni mkubwa hata bila kuongeza nguvu kutoka nje.

Kibaya kinachoimaliza CDM ni kuvunjika moyo kwa wanachama(political base) ambayo imekuwa inafanya kazi kwa moyo na sasa ikijikuta haina viongozi wa pamoja bali makundi.
Hili linaimaliza sana CDM na linahitaji kuangaliwa kwa ukaribu.Huwezi kufanikiwa kisiasa bila kuwa na strng political base. Si kundi la uongozi au linalowania likalofaulu kwa kuua political political base.

Personality zinaweza kusaidia tu kwa muda mfupi,kwa muda mrefu ni maafa makubwa sana. Ndicho kiliikumba NCCR na CUF na hakuna shaka kama hakuna umakini CDM ipo katika orodha

NINI MUSTAKABALI WA CHADEMA KWA TAIFA

Itaendelea
 
NINI MUSTAKABALI WA CHADEMA NA TAIFA

Mustakabali wa CDM utategemea sana hatua za haraka na za makusudi watakazochukua. Kwa upande wa taifa mstakabali utaangaliwa kwa namna mbili.

1. Kwa chama tawala CCM na wale wasiopenda mabadiliko ya kiuchumi na kijamii kifo au mtafaruku ndani ya CDM ni faraja kwao. Hiyo ni njia rahisi ya kuhakikisha kuwa chama tawala kinaendelea kutawala tena katika hali tuliyokuwa nayo miaka kadhaa kabla na baada ya vyama vingi.
Ni fursa kwa kundi au makundi ya watu kufanya watakavyo 'business as usual'

2. Kwa upande wa umma wa wananchi wenye kupendelea mabadiliko ya kiuchumi na kijamii hili litakuwa ni pigo kubwa. Ni kurudi katika zama za serikali kulala, wezi kutamalaki na kila aina ya uchafu kushamiri.
Uwepo wa vyama vya upinzani ni sehemu muhimu sana ya check and balance.

Tumeshudhudia jinsi bunge lililosheheni wabunge wa chama kimoja likipitisha maazimio kwa njia za masilahi yao na si masilahi ya umma. Tuanzo kumbu kumbu za jinsi bunge lilivyoficha habari zinazoathiri maisha ya wananchi kila siku. Leo watu hawajui kwanini tunalipa umeme kwa bei ya juu kuliko nchi zote za EA.

Ni kutokana na sababu namba 1 duru tunaamini kuwa pamoja na kuwa na mzozo wa ndani wa CDM, kuna uchochezi unaotaka nje. Uchochezi unaopenyezwa kwa kuangalia safu za uongozi wa juu wa CDM.
Kwavile CDM imejengwa kwa personality atakayetikisa personality hizo atakuwa ameleta kishindo kikubwa

Kwa mfano mwenyekiti wa CCM anapoanadama na mwanachama wa CDM na kueleza wazi kuwa huuni wakati wa vijana kutawala nchi, ni dhahiri alikusudia kuwatia kichwa vijana hao ili wajisikie kuwa sasa ni wakati wao na inapaswa wafanye jambo. Ndiyo haya tunayoyaona ya vijana kuacha siasa za uchumi na jamii na kujiingiza katika siasa za 'uharamia' kwa kutumia mitandao, kuchafuana na kuchafua viongozi wengine.

Lakini pia ikumbukwe kuwa CCM wametumbukiza mbegu za ukabila ambazo zimeota vema ndani ya CDM.
Kundi linalopinga uongozi linatumia hiyo kama hoja muhimu sana hata kama linafahamu hakuna ukweli.
Hii ni mbegu waliyopanda akina Nchemba na Nape na sasa inachanua.
CDM wakubali au wakatae huo ni ukweli.

CCM imetumbukiza mbegu ya udini. Nayo pia inatumika katika kubomoa chama.
Mbegu hiyo inatumiwa na baadhi ya viongozi wa CDM kujilinda kwa namna fulani. Inawalinda kwasababu hatua zozote zinaweza kutafsiriwa katika maana isiyokusudiwa na kuleta mantiki isiyokuwa na ukweli.

Mgogoro wa Chadema unachagizwa sana na CCM, hata hivyo ni lazima CDM wajilaumu kwa kutoa nafasi kwa mahasimu wao kutumia udhaifu wao.
Kwavile haionekani kama CDM wanajielewa suala hilo linaweza kuamua mustakabali wao kama ilivyokuwa kwa NCCR na CUF.

CHADEMA WAFANYE NINI KUJINUSURU
Itaendelea.....
 
CHADEMA WAFANYE NINI KUJINUSURU

Gogoro la Chadema ni kubwa na lenye mizizi mirefu na mizito.
Ni mgogoro unaoweza kukivuruga chama kama hatua za haraka na makusudi hazitachukuliwa.


Hakuna busara kwa viongozi kuwa katika hali ya kukataa 'state of denial' ya uwepo wa tatizo kubwa.
Na hakuna hekima wala busara kwa viongozi kuamini kuwa kukaa kimya ni njia ya kumaliza tatizo.


Umuhimu wa kulishughulikia tatizo ni mkubwa kwasababu muda si mshiriki mzuri.
Mzozo wote unaofukuta umejikita katika viongozi na uongozi na wala si wanachama.

Kuelekea uchaguzi wa 2015 mzozo huo utakuwa mkubwa zaidi. Harakati za akina Zitto, Lema, Mwigamba na Tuntemeke ni kiashirio kizuri kuwa kadri muda unavyosonga bomu linakarikibia kulipuka.

Tatizo si wanchama na wapenzi wa CDM. Tatizo lipo katika viongozi na uongozi.
Chama kimejengwa katika mardhiano'consensus' badala ya demokrasia.
Kimejengwa katika personalities badala ya wanachama.

Ili kuweza kukabiliana na tatizo, baada ya kukubali kuwa kuna tatizo(kuacha state of denial) mambo yafuatayo yafanyike haraka sana kabla ya mwezi March 2015 kama CDM ingependa kushamiri.

1. Chama kikubali uwepo mgongano wa mawazo ndani yake na kwamba hilo si kosa bali ni sehemu ya demokrasia.
Kuwepo na uwazi wa uendeshaji wa chama na taratibu zifuatwe ikiwemo kalenda ya shughuli za chama.

2. Uchaguzi wa chama ufanyike haraka ili kukijenga chama tayari kwa hatua zinazofuata.

3. Kukirudisha chama nikononi mwa wanachama
Kuwepo na jitihada za makusudi kabisa kuvunja nguvu ya personality( s) zinazodhani chama ni wao na wao ni chama.

Personality hizo zidhibitiwe kwa kutumia kanuni na sheria za chama bila kujali umhimu wao.

Hakuna personality iliyo juu ya chama na kwamba chama kwanza na watu na haiba zao baadaye.

4. Chadema izingatie demokrasia ya kutoa uhuru wa kushiriki katika mambo ikiwemo chaguzi
Iachane na utamaduni wa chama kuongozwa kwa misingi ya maridhiano 'consensus'.

Chadema kimekuwa na wala hakina upungufu wa viongozi na hakuna sababu za maridhiano bali demokrasia iachwe ichukue mkondo wake.


5. Kuvunjwa kwa makundi
Baraza la wadhamini na ile la wazee waingilie kati na

a)kuvunja uongozi uliopo na kuitisha uchaguzi kama njia ya dharura ya kutafuta muafaka

b) Kuwachukulia hatua madhubuti wanakaokiuka misingi ya uendeshaji wa chama hata kama ni viongozi
c) Kuwafukuza wanaoendesha kampeni chafu dhidi ya wanachama na chama chao

d) Kwaonya na kuwataka
i) Mh Mbowe avunje kundi lake la vijana linaloshambulia viongozi wengine.
Akina Lema wachukulie hatua za kinidhamu kwa kukiuka misingi ya chama na uongozi.

ii)Zitto achukuliwe hatua za kinidhamu kwa kuwa kinara wa migogoro kwa kutumia vijana ndani ya ofisi za Chadema , katika mitandao na avunje mtandao anaoujenga kwa nia ya kuvuruga chama.

6. Wasaliti wote wa chama wapewe nafasi ya kujieleza na ikidhihirika vinginevyo wafukuzwe ndani ya chama mara moja.

7. Uongozi kupewa jukumu la kuchukua hatua za haraka pale kunapotokea fununu za ukorofi kuliko kusubiri mgogoro ufukute kama uliopo.

Katika kutekeleza hayo lazima kuwepo na hatua za ukakasi (radical intervention) ambazo hazitaangalia personality ya mtu ndani ya chama bali ushiriki wake katika kuzua au kueneleza migogoro.
Hilo halitarajiwi kuwa jambo jepesi lakini ndio jibu la kudumu la tatizo lililopo.

Hatutegemei mwanachama wa kawaida aje na jibu lakini wanachama wana majibu.
Wachague viongozi kwa kuzingatia sifa za uongozi, historia zao za mambo ya kisiasa na ushiriki wao katika ujenzi wa chama.
Wanachama wachukue ownership ya chama na kuwatuma viongozi watende na wala isiwe kinyume chake.

Na wala CDM wasitegemee kuwa Mbowe na Zitto wanaweza kuvunja kambi zao kirahisi.
Ni wanachama wanaoweza kuvunja ngome hizo kwa kuwakataa wale wanaoongoza na wapiga debe wao.

Duru tunamalizia kwa kusema mgogoro uliopo si wa Cahadema kama chama, ni wa viongozi wawili wenye makundi ndani ya chama, mwenyekiti Mbowe na naibu katibu mkuu Zitto. Hawa ndio wachawi wa CDM.

Hadi pale wanachama watakaposimama na kusema Mbowe na Zitto hatutaki mnayoyafanya, CDM inaelekea kule CUF na NCCR walipopumzika.

Wanajamvi tusemezane
 
Nguruvi3,

Mkuu wangu lazima ufahamu kwanza mzizi wa fitna unatoka wapi kisha unapofanya mabadiliko unakuwa unajenga badala ya kuziba nyufa ilihali nguzo hazipo tena.
Mimi mtoto wa mujini nafahamu fika kwamba hizi zote ni jitihada za kukiua chama na hao kina Mbowe na Zitto ni sababu au nyenzo zinazotumika kuukuza mgogoro ambao kusema kweli haupo.

CCM ina mbinu nyingi sana za kukimaliza chama au mtu yeyote anayekuwa threat kwao. Na moja ya mbinu zake ni kuingiza majasusi chamani ambao wameingia hadi ktk mishipa ya damu ya chama, sasa wanaifanya kazi yao. Niliwahi kusema zamani ya kwamba hapakuwa na mgogoro baina ya Zitto na Mbowe isipokuwa uliundwa na ukashika moto.

Tatizo kubwa la CDM ni uendeshaji wa chama hiki kama NGO ambapo kuna watu wanajua fika kwamba wakiwa karibu na Mbowe watafaidika kisiasa iwe madaraka ya ndani ya chama au kupewa nafasi ya kugombea Ubunge, udiwani na kadhalika. Hawa watu wote ni wachumia tumbo ambao wepesi kumeza lishe wanayopewa ili kujipendekeza kwa Mbowe.

Mimi binafsi namfahamu Mbowe vizuri sana, na namuaminia sana japo tayari jina lake limekwisha haribiwa kisiasa lakini bado ni kiongozi mzuri na bora kisiasa. naweza sema Mbowe ni mwanasiasa bora kuliko vijana wote wa CDM, isipokuwa tatizo lake image yake imekwisha tiwa dosari kulingana na sifa wanazo ziamini Watanzania.

Kwa upande mwingine Zitto ni shupavu, mzalendo na kwa siasa za CCM yeye ni weakest link yao maana hafanani na wengineo maana yeye toka zamani ni muumini wa mfumo wa kihafidhina, lakini viongozi wengi wa CDM ni wajamaa kiitikadi japo wamejiunga na Chadema ili wapate kupanda majukwaani. Na hili utaliona ktk hotuba zao,majigambo yao lakini mimi husema hawa wote ni wanafiki maana wanapopewa nafasi za uongozi, huo Ujamaa wao hukoma pale pale na kuwa hawana tofauti na viongozi wa CCM maana hupingana na Zitto hata ktk matumizi ya fedha za walipa kodi.

Kwa kumalizia tu, ni kwamba haya yote yamepangwa na CCM kama mbinu mojawapo ya kukimaliza chama kabla ya uchaguzi wa mwaka 2015. Na kinachokosekana CDM ni Hekima na Busara maana kumejaa vijana wasiofikiri na kupima uzito kabla ya kusema ama kuandika. Kwa nini ikiwa mtu ana mashtaka yoyote kuhusu Zitto au Mbowe malalamiko hayo yasipelekwe ktk vikao vya chama isipokuwa inaanzia ktk magazeti na mitandano wakati huyo mlalamikaji ni kiongozi ndani ya chama?. Huyu mtu huwa ana lengo gani haswa kama sio kutumika ili kukivuruga chama kabla ya 2015. Wengine huanza kutoa tuhuma zao baada ya kufukuzwa madaraka, hii kweli inaingia akilini! tena basi bila aibu hujiunga na CCM na kunadi ati anazo siri za Chadema, hizo siri gani hizo uloficha hadi ufukuzwe na CDM wasiwe na wasiwasi kukufukuza. Na mbona hao wengine walotoka CCM hawakuja na siri za CCM au huko hakuna siri?.
 
Mkuu Mkandara , ahsante kwa bandiko
Kama umenisoama vema nimeeleza kwa kina kuhusu chagizo la mgogoro kuanzia nyakati hizo hadi sasa.

Nimeelaza kuwa CCM walitumia karata ya ukanda na ukabila. Karata hiyo imekufa baada ya kuonekana kuwa CDM ina nguvu sehemu nyingine kuliko katika kanda yao. Mfano ni Mwanza.

Wakatumia kete ya udini ambayo imekufa baada ya kuona CDM inaungwa mkono na sehemu kubwa ya Watanzania bila kujali itikadi zao.

Kwasasa wanatumia udhaifu wa viongozi ndani ya CDM kukidhoofisha chama.
Karata hii inaonekana kufanya kazi.Kwa mfano, iweje CCM wamalize masuala yao kama ya mafisadi kimya kimya lakini waunge mkono wana CDM wanaokichafua chama chao kwa mgongo wa demokrasia ndani ya chama?

Kuna demokrasia gani CCM wanaweza kuieleza kama mfano. Si uhuru wa kusema au wa kutenda lakini wameshikilia bango hasa wanapotokea watu ndani ya CCM kutenda yale yale CCM isiyokubaliana nayo.

Ni makosa kuilaumu CCM kwasababu ndio kazi wanaotarajia kuifanya baada ya kukosa hoja licha ya kuwa madarakani.Kinachofanywa na CCM ni 'survival' tu kwasababu mbinu za kihoja hazina mashiko tena.

Watu wa kulaumiwa ni viongozi wa CDM na vijana wao ambao hawatafakari kwa kina yale yanayotokea bali kuongozwa na hisia tu.

Mbowe, nimeeleza ni mwanasisa na mchango wake kwa chama ni mkubwa.
Hata hivyo chama kimefikia mahali pa kujitanua zaidi na lazima mbinu na taratibu zibadilike kutokana na ukuaji wake.

Chama kiendeshwe kwa taratibu na viongozi wawe tayari kukabiliana na changamoto.
Huu si muda wa kuendesha chama kwa 'consesus' yaani maridhiano.
Kuna mapungufu kwa upande huo na katika kuziba mapungufu hayo Mbowe amevutika katika matumizi ya vijana badala ya kuchukua hatua za kisheria, kanuni na nidhamu kuimarisha chama.

Kwa upande wa Zitto, naye ni mwanasiasa mahiri na mchango wake katika chama unathamaniwa kama sitakosea.
Tatizo linalojitokeza kwa Zitto ni kutengeneza makundi ndani ya chama.
Mgogoro wa akina Kafulila, Zitto alitajwa.Mgogoro wa masalia Zitto alitajwa. Na huu mgogoro wa Mwigamba Zitto ametajwa.

Tatizo ambalo wengi hawapendi kuliongelea ni kuwa sasa hivi CDM inajiimarisha kuelekea vijijini.
CDM ina hazina kubwa ya viongozi kwa bahati mbaya utamaduni wa kutegemea Personality unakimaliza chama.
Na CCM wanajua vema ukitikisa 'personality ABC' chama kinayumba na wanapiga hapo kwa mapigo.

Ni kwa msingi huo nimeshauri uitishwe uchaguzi ili uongozi mpya upewe nafasi ya kurejesha nidhamu na utokane na wanachama wenyewe. Hili litasaidia sana kuvunja makundi yaliyopo.

Mimi siamini kuwa CCM ni tatizo, nina amini kuwa tatizo ni CDM wenyewe wanaojenga ufa na CCM kuutumia kuwavuruga.

Mkuu Mkandara hakuna shoka linalokata bila mpini, kwa hili nasema CCM ni mpini tu shoka lenyewe lipo ndani ya CDM.

Mgogoro huu ni mkubwa hata kama watu wanakataa. Umehusisha vijana ambao sasa hawafugiki tena.
Vijana hao ni wa makundi ya Mbowe na Zitto.
 
RE: MGOGORO WA UONGOZI NDANI YA CHADEMA

Nguruvi3,

Wengi tulikuwa tunasubiri umalizie mada yako kuhusiana na mfarakano inayoendelea ndani ya Chadema. Umefanya kazi nzuri sana, hasa ya kutuelimisha juu ya masuala mengine ambayo hatukuwa tunayatazama kwa undani kiasi hicho. Naomba nichangie kidogo kwenye mada ifuatavyo:

Kwa mujibu wa maelezo yako, kinachoendelea ndani ya Chadema ni uwepo wa makundi mbalimbali madogo ndani ya kundi kubwa au kwa lugha ya wenzetu, factions. Mara nyingi, hasa katika demokrasia zilizokomaa, uwepo wa factions ni feature ya kawaida katika demokrasia ya vyama vingi, na sio lazima iwe ni kitu ni kitu ‘destructive' kwani katika siaza za Vyama - huwa kuna constructive factions & destructive factions. Kwa upande mmoja, Constructive factions mara nyingi (sio mara zote) revolves around zaidi onindividuals/personalities, and on the other hand, Destructive factions mara nyingi (sio mara zote), revolves Zaidi around Issues;

Kwa maelezo yako hapo juu, factions zilizopo Chadema hivi sasa ni mchanganyiko wa constructive and destructive factions. Swali linalofuatia ni je:

· Ni factions zipi zina "a constructive function" na factions zipi zina "a destructive function" kwa Chadema na
Demokrasia ya Tanzania kwa ujumla?

Binafsi sina majibu Zaidi ya maoni tu kwamba kundi ulilifafanua kama kundi namba moja ndio kundi pekee lenye "pure constructive function" yani:

Kundi linaloamini kufanya kazi kwa kuleta mageuzi (Neutral)

Kundi llingine naona kama vile lipo kwenye border line baina ya kuwa constructive and destructive factions, na hili ni kundi namba mbili, yani:

Kundi linalowania uongozi kwa matamanio kuwa sasa ni wakati wao(Power struggle)

Naliweka kundi hili katika border line kwa sababu kuu moja kwamba - zaidi ya kutaka generational changes in leadership, kundi hili halina mtazamo/sera ambazo zinatushawishi kwamba zitakuwa ni mbadala wa kweli kwa CCM. So far, linaonekana ni kundi ambalo linataka kwenda kufaidi madaraka na resources zinazoendana na uongozi wa juu wa chama, na sio kitu kingine.

Kundi ambalo kwa mtazamo wangu naliona ni "pure destructive faction" ni kundi namba nne ulilojadili hapo juu, yani:
Kundi la wasaliti ambao wanatumiwa kukihujumu CDM (Traitors)
.

Na sababu juu ya kwanini kundi hili ni pure destructive faction for Chadema na ujenzi wa demokrasia ya vyama vingi kwa ujumla nchini, ni sababu ambazo zipo wazi, hivyo sina haja ya kuingia katika mjadala huo kwa kina.

Kundi namba tatu linaweza kuwa either way – pure constructive or pure destructive, yani kundi ulilojadili kama:

Kundi linaloamini katika CDM kama ilivyoasisiwa na misingi yake (establishment)

Kundi hili linaweza kuwa "pure constructive faction" iwapo nia yake ya dhati ni pamoja na kudhibiti kundi namba nne yani:
Kundi la wasaliti ambao wanatumiwa kukihujumu CDM (Traitors)
,

Lakini pia iwapo nia yake ya dhati ni kuhakikisha kuendeleza ‘conservatism' juu ya masuala Fulani Fulani mpaka wakati muafaka ufike.

Lakini pia linaweza kuwa "pure destructive" iwapo nia yake ni kutoruhusu chama kiende mikononi mwa wengine kwa sababu za ovyo ovyo tu kama ukabila, ukanda, ukoo na mambo yanayofanania na haya.

Katika nchi za wenzetu wenye demokrasia zilizokomaa, madhumuni makuu ya factions huwa ni pamoja na haya yafuatayo:

1. Kushinikiza sera Fulani au Policy agenda Fulani.
2. Kuzuia sera Fulani au policy agenda Fulani mbadala isipite.
3. Kuunga mkono watu Fulani Fulani ndani wenye malengo ya uongozi ndani ya chama.

Swali linalofuatia ni je:

· Madhumuni haya matatu yana uhusiano na kundi lolote ulilojadili hapo juu?

Kwa haraka haraka, binafsi naona makundi yote manne uliyojadili yanahusiana na dhumuni namba tatu hapo juu yani
Kuunga mkono watu Fulani Fulani ndani wenye malengo ya uongozi ndani ya chama.
Pengine ndio maana mijadala mingi juu ya factions ndani ya vyama vya siasa inatuelimisha kwamba factions politics mara nyingi revolves around personalities ambapo watu wachache play key roles, acting like magnets kwa watu wengine wenye similar mindsets or interests. Vinginevyo madhumuni ya factions niliyojadili kama namba moja na namba mbili hapo juu, yani:

· Kushinikiza sera Fulani au Policy agenda Fulani, na
· Kuzuia sera Fulani au policy agenda Fulani mbadala isipite.

Sijafanikiwa kuona kama madhumuni yana uhusiano wowote na makundi uliyojadili. Sana sana labda kama ni kuhusiana na kundi namba nne kutumika na CCM Kimkakati (sio Kisera) kuhakikisha kwamba Chadema haifanikishi malengo yake ya kuchukua utawala wan chi, 2015.

Mwisho nikuulize, je, kuna uwezekano wowote kwamba chanzo cha factions ndani ya Chadema kinatokana na:

· Failed expectations ambazo zimepelekea polarization and divisions within the party?
· Politics of exclusion within the party?

Na je, kama haya yapo, ufumbuzi wake ni nini: Politics of accommodation au Politics of Compromise?

Kama tunakumbuka vizuri historia ya TANU, chama hiki kilipata misukosuko mingi kutokana na intergenerational conflicts. Ni bahati tu kwamba chini ya mfumo wa chama kimoja, ikawa ni rahisi kwa TANU na baadae CCM kuwapatia Vijana ajira katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya chama – UVCCM, ambapo wengi pia wakawa wanapata fursa ya kupenya kwenye nafasi mbalimbali kama vile ubunge, ukuu wa wilaya, n.k. Utamaduni huu bado unaendelea hadi leo vinginevyo CCM ingeshakufa siku nyingi kutokana na kushindwa to accommodate factions.

Tofauti na CCM, Chadema haina resources za kutosha to accommodate factions ndani ya Chama. Matarajio ya umma kwa chadema yamekuwa ni makubwa sana kuliko uwezo wa Chadema kukidhi matarajio hayo na pia kuliko uwezo wa Chadema kupambana na CCM, hasa pale CCM inapotumia resources and organizational capacity yake kupambana na mafanikio ya Chadema in the electorate. Chadema ifanye uamuzi wa haraka: je, kuelekea 2015,

· Chama Kiegemee Zaidi upande wa Political Party au upande Political Movement?

VariablePolitical OrientationPolitical Party
OrientationCauseIssues
Level of operationRegimeGovernment
Main area of operationSocietyParliament
Method of OperationMobilizationPersuasion
Member orientationDiffuseSpecific
Claims to resourcesNo formal limitsConstrained by rule of law

Chadema ichague sasa, kwani haiwezekani kutumikia mabwana wawili. Hata TANU (1950s), mafanikio yake kutokomeza Chama tawala cha mkoloni (UTP) yalitokana na TANU kujipanga Zaidi kama a political movement kuliko chama cha siasa; kwa kufanya hivyo, kulipunguza incentives za umma (plus viongozi wa TANU) kupoteza muda katika kushabikia na kuchochea mapungufu ya TANU kama vile poor organization, lack of financial resources and factionalism; Lengo likabakia moja tu kwamba – kumtoa mkoloni na kuikomboa nchi irudi mikononi mwa maskini ambao ndio walikuwa ni wengi; Kuitoa CCM madarakani ni muhimu kwa demokrasia ya Tanzania kwa maana moja tu: Kukipa Changamoto CCM, na kuzaa vyama viwili vikuu vya siasa nchini kwani hiyo ndio njia pekee ya CCM kujirekebisha; CCM haiwezi jirekebisha ikiwa madarakani:

cc Ritz, Zinedine, gfsonwin, Mkandara
 
Last edited by a moderator:
Mchambuzi na Nguruvi3 nashukuru sana kwa michango yenu juu ya hali ya mgogoro ndani ya CDM.

nimesoma michango yenu na kuikubali sana lakini sasa kuna mambo nami pia ningependa kuongezea ambayo naona hayapo.

kwanza kabisa CDM inatakiwa ijue kwamba ni chama chenye nguvu na kimeweza kuwin trust ya watua akwa kiwango cha hali ya juu. lakin pia kwa chenyewe kuwa chama basi lazima misukosuko itatokea tu manake wao sio malaika useme hawata tofautiana hata lugha tu.

kama ndivyo basi CDM wanatakiwa waichukue hii kama changamoto kwao na sio kama adhabu ama uonevu kwao ili wasimamie misingi imara ya upinzani ili kuleta tija kwenye demokrasia ya kweli.

CCM ukweli inahitaj kupata mbadala japo wa 5 yrs ili sasa ijipange upya lakin hii haiguarantee kwamba CCM wako kimya kwenye kusaka nafasi ya kuendelea kubaki madarakani. kama ndivyo lazima wajue kwamba cdm wanakazi kubwa kuwaondoa na wanaye taka kumwondoa hawata mwondoa kwa nguvu ya mtutu ama ya bomu bali kwa nguru ya kuwa na political stability ndani ya chama na kuwa na sera nzuri zenye ushawish wa kutekelezeka na sio zile za kuifanya Kigoma dubai miaka 10 sasa bado hata hadi ya jiji la tanga haijafikia.

jambo jingine CDM wala isihangaike kupambana na maadui zake kwa kuwa-attack maadui bali ipambane nao kwa sera, utendaji mzuri na kuwa na watu clean wanaoweza kushika mshumaa wa chama. iachane kabisa na siasa za kusema nani anastahili kuwa mwenyekiti wa chama bali igeukie kwenye kura iwe mwamuzi na mtu achagulkiwe na watu.

Lakin pia CDM itambaue kwamba trust ambayo wananchi wanayo juu yake ni kubwa sana na hivyo kushindwa kufanya kile kinachokusudiwa na wananchi wengi basi ni kuwaonea sana na kuwavunja moyo haw ambao wanawaamini.
 
Last edited by a moderator:
Binafsi sikupendezwa na kile kili/nachoendelea Chadema, hata hivyo nikubaliane na Mchambuzi kwamba, Chadema hakina budi kubadilika na kuwa na ukomavu zaidi wa ku-focus kwenye kujenga imani ya uthabiti na uimara wa uongozi utakaoweza kuwatofautisha na chama kilichopo madarakani. Na zaidi, mimi nitakuwa na -attention na siasa za nchi yetu mpaka tutakapokuwa na chama kimoja tu (chenye nguvu zaidi) cha upinzani. Hii itaifanya siasa iwe katika sifa za ushindani wa kweli kuliko sasa hivi ambapo kuna vyama vipo kwa ajili ya kutawanya kura za upinzani ili kukipa ushindi chama kimoja tu. Naamini ushindani wa pande mbili zaidi kuliko tatu, nne, na kuendelea
 
Last edited by a moderator:
gfsonwin
Hoja zako mbili nazitamana kwa mitazamo miwili
1. Chadema imepata umaarufu si kwasababu ya watu bali watu waliosimama vema kutetea sera na umma.
Watu waliojipambanua na jamii kuwaona kama wasemaji wao.

2. Kwa kusimamia masilahi ya umma kama chama cha upinzani, CDM ili 'win' nyoyo za watu kwa matumaini yao

Badala ya kuchukua imani kama changamoto wamechukua nafasi hiyo kama sehemu ya kutaka ukubwa, umaarufu wa mtu binafsi na kusahau bila watu hakuna chama.

Unapoungwa mkono na mamilioni ya Watanzania automatic unapata uhalali wa uongozi wa umma, wao ni viongozi wa umma. Tatizo ni pale kila mmoja anaon uwepo wa CDM ni kwasababu yake. Ubinafsi umeshaingia.

CCM wanafahamu kuwa kuushaiwshi umma kwamba wanaweza kufanya jambo tofauti na miaka mingi iliyopita ni ndoto.Wanachokifanya ni kudhoofisha anayeonekana ni tatizo. Hapa si TLP au CUF ni CDM, wanatumia udhaifu wa ubinafsi kukabiliana na CDM na hadi sasa wamefaulu sana.

Mfano, Nape amesikika akisema CDM wafanye uchaguzi ama sivyo atawashtaki kwa msajili.
Haiwezekani Nape anayeshinda na kula na wahalifu wa nchi hii aone umuhimu wa CDM kufanya uchaguzi. Haiwezekani Nape anayezuia demokrasia ndani ya chama chake aone demokrasia ndani ya CDM.

Anachokifanya Nape ni kutumia madhaifu ya siku za karibuni kuendeleza mgogoro.
Anafahamu uchaguzi kwa wakati huu CDM ikiwa mapande utawafaidisha CCM.

Yeye yupo mikoani anaimarisha CCM huku CDM wakiwa wamesimamisha kampeni zao kama M4C.
Hata ziara zao mikoani sasa hivi zimegubikwa na malumbano ya wanachama na viongozi ngazi za kitaifa.
Hii ni destruction ya hali ya juu sana.

CCM wanafahamu wakati huu chama kikiwa kimegawanyika, chaguzi ambazo naturally hugawa vyama kama CCM itazidi kupigilia msumari wa moto juu ya donda bichi.

Ni makosa kumlaumu Nape. nachokifanya ndicho anachokitaka. Makosa ni ya CDM kuanza malumbano tena ya kipuuzi kabisa katika mitandao, kukashfiana na hata kutuhumiana katika mambo yenye itikadi za chama kama suala la posho za bunge. Leo nani anaweza kusimama na kusema CDM wanasimama wapi katika suala hilo.
Zinedine , nafasi ya kuwa na chama kikuu imejitokeza mara tatu.

Kwanza NCCR, pili CUF na sasa CDM. Mara zote hizo wananokiangusha chama si wananchi ni wanachama viongozi.
Hakuna sababu ya wananchi kusubiri kizuke chama kingine kama uyoga.
Nadhani wanapaswa kuchukua ownership ya mambo ya kisiasa.

Ownership ni kama sasa ambapo badala ya watu kulumbana kwa hoja za kitoto, wangesimama kwa pamoja na kusema hili ndiyo hili hapana. Huyu anasema kweli huyu muongo na wawakatae watu hao mara moja
 
Mkuu Mchambuzi
Kwanza niseme uwepo wa factions ndani ya chama ni jambo la afya kabisa.
Kinachotakiwa ni factions kutimiza majukumu kama ulivyo aanisha na niongeze ziwe na lengo la kukiinua chama

Hivyo sivyo ndani ya CDM kwa sasa. Kinachoendelea ni factions za kuumizana bila kujali gharama za chama.

Nimeandika mara nyingi kuwa kupingana kwa mawazo ndani ya chama tena kwa uwazi ndio demokrasia na uhai w. Nimemuunga mkono Zitto katika baadhi ya hoja na kumpinga zingine bila kumhukumu kwanini ana mtazamo tofauti pengine na chama chake.

Kilichoimaliza CCM ni kutokubaliana na mawazo tofauti. Kila aliyepinga kama Kolimba aliitwa na kutishiwa kitumbua.Nadhani wao wamebadilika kiasi, najaribu kufikiria ingekuwa enzi hizo akina Filikunjombe, Lugora, Mwambalwasa wasingekuwa viongozi. Bado safari yao ni ngumu lakini basi wanajaribu.

Factions zilizpo CDM si za kujenga chama ni za kuua chama. Factions za kujificha na kutoa tuhuma nyuma ya mitandao ni destructive force. Imefika mahali CDM hawawezi kupingana bila kutumia mitandao.
Hivi kiongozi wa CDM hawezi kusimama na kuuambia uongozi hili si jema ni hadi ajifiche kwa majina bandia.


Factions inanyowakilisha 'neutral' ninaionea hurum. Hii imejaa watu wanaoamini katika mabadiliko bila kujali nafasi zao siku za baadaye. Utawakuta Shinyanga, Singida, Ukonga katika mashina wakifanya kazi ya chama
Ni nadra kuwasikia katika mizozo wanaamini katika matokeo mazuri.


Factions zilizobaki ni 'pure destructive'
1. Lile kundi linaloangalia uongozi umeeleza vema kabisa na wala siongezi kitu.

2. Kundi linaloamini CDM ya asili lina tatizo moja. Linaamini katika kutenda mazuri, kwabahati mbaya limejaa wahafidhina 'extreme conservative' ambao hawawezi kukubaliana na mabadiliko hata kama ni chanya.

3. Wasaliti" Hili ndilo linazamisha CDM lina ukaribu sana na kundi la 1 hapo juu.

Je, ufumbuzi ni politics of accommodation au politics of compromise?
Niseme hakuna accommodation wala compromise,. Makundi hayo yanaweza kuua chadema kama yatapewa fursa.

Nitatoa mfano, CCM wanafanya politics of accomodation. Tazama jinsi inavyowatesa na ni suala la muda utaona ufa mpana sana ambao ndio utakuwa kaburi lake kama kutakuwa na mbadala.

CUF wanafanya politics of compromise ona chama kilivyokosa msimamo na mwelekeo. Mwenyekiti anasema hili, katibu mkuu lile, kiongozi wa CUF bungeni hili, msemaji wa chama lile, naibu katibu mkuu vile n.k. ilimradi tu kuna compromise ya kuishi kama wana CUF

NCCR ilitokea radical intervention, chama kikadhoofika sana lakini bado kipo na kinajikongoja.

CDM hakihitaji politics of accommodation kwasababu kufanya hivyo kukiwa na makundi matatu yanayokinzana ni kulea ugonjwa. Wamejaribu sana ku accomodate kiongozi wa kundi linalowania uongozi wa CDM kwa kutomchukulia hatua na amekuwa ndiye 'culture media' ya waasi wa CDM na kila siku anawaletea matatizo.

Wamejaribu politics of compromise kwa vikao vya kuondoa tofauti zilizopo katika makundi.
Hiyo ime feli kwasababu hakuonekani kuwa na muafaka bali ni chuki za chini chini na kuchekeana kinafiki.

CDM wanahitaji radical intervention kama NCCR. Kuna namna mbili
1. Kuwaweka pembeni katika uongozi viongozi wa makundi yanayoleta uharibifu usio wa lazima
3. Kuwaondoa katika chama kwa kuwafukuza.

Hakuna kiongozi wa CDM anwyeweza kutenda hayo hapo juu kwasababu uongozi mzima upo katika accomodation na compromise hata kama kuna hatari. Ndicho kinaendelea sasa hivi kwa mwenyekiti, katibu mkuu, kamati kuu na vyombo vingine kujifanya hakuna mzozo wakati mzozo ni mkubwa sana.

Wanaoweza kuisadia CDM ni wanachama. Na wafanye haya
1. Wakubali kuwa kuna tatizo linalosababishwa na viongozi kuvurugana.(waache denial state)
2. Washinikize yawepo maongezi ya wazi juu ya tatizo
3. Waondoe tofauti zao zinazojengwa na mirengo ya viongozi, watambue kuwa umoja wao ndio salama ya chama.
4. Wameze ukweli kuhusu makundi wanayoshabikia na wayanyooshee vidole bila aibu au haya
5. Wachukue hatua nilizozisema hapo juu
a) Kuwaweka kando viongozi wanaoleta ghasia na uchochezi hata kama ni personality za chama
b)Kuwafukuza katika chama wanaohusika kama wasaliti n.k.

Hii ndiyo salama ya CDM. Vinginevyo August 2014 tutakuwa tunaongelea CDM kwa njia nyingine.
Nimewahi kuwaonya kuhusu mgogoro wa masalia, nikaeleza chanzo chake na watu walioko nyuma yake.
CDM wakapuuza maoni na miezi 5 baadaye wakaonja shibiri ya akina Shonza. Na hili nasema ni suala la muda.

Nitaendelea na hoja zaingine ulizozianisha.

 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…