Duru za siasa - Matukio

Duru za siasa - Matukio

Mkuu Nguruvi3 asante kwa bandiko lako makini.Ombi maalumu je inawezekana ukachapisha nondo hizi kwenye magazeti kama Raia mwema,Mwananchi..... na magazeti mengine mengi ili wananchi wasiotembelea mitandao ya kijamii wakachota elimu ?.
Kweli kabisa, elimu hii inatakiwa iwafikie watu wengi zaidi, Nguruvi3 tafadhali kama bado hutoi makala kama hizi kwenye magazeti ingekuwa vizuri zaidi ukifanya hivyo....
 
Last edited by a moderator:
Asante sana mkuu Nguruvi3 kwa uchambuzi makini wa hii ishu ya EAC.
Watu wamehamaki sana kutokana na Rwanda na Uganda kujitoa kutumia bandari yetu ya Dar Es Salaam wakihisi kwamba tunatengwa na tutatetereka kiuchumi. Mimi nadhani ni wakati muafaka wa kujipanga na kutumia fursa zetu zilizopo kujiimarisha. Kama jumuiya ya mwanzo ilipovunjika mwaka 1977 ilitusaidia kujitambua na kuimarisha vyanzo vya uchumi, ni wakati muafaka sasa kutumia fursa zilizopo kujiimarisha zaidi. Hawa jamaa bado wanatuhitaji sana tu.
Katavi jumuiya ya Afrika mashariki ilipokufa hakika tulikuwa katika wakati mgumu sana. Kwa wakati huo tulikuwa na miaka 16 tangu tupate uhuru. Shughuli zote za huduma na jamii zilikuwa za kutegemeana nyingi zikiwa Kenya. Mfano, viwanda vya nguo tulitegemea sana Jinja Uganda. Huduma za jamii kama posta na simu, reli na hata bandari zilikuwa Kenya n.k.

Tulianza moja kwa kujenga miundo mbinu na huduma za jamii. Tofauti ya kiuchumi iliyokuwepo kati ya Kenya na Tanzania ilikuwa kubwa sana. Miaka ya 90 tukafungua milango na bado tulikuwa ni soko la wenzetu. Miaka ya 2000 sisi tukaanza kutafuta masoko huko kwao.

Tofauti ya GDP yetu na Kenya imezidi kupungua hadi kufikia second economy ya EAC huku tukiwa na GDP inayokuwa katika kiwango kikubwa. Ingawa bado haijawa reflected kwa wananchi wa kawaida ni ukweli kuwa Tanzania inabaki kuwa tishio kwa uchumi namba 1 EAC ambao ni Kenya. Kwa hili Mchambuzi anaweza kutusaidia kudadavua.

Hakuna sababyu ya kuhamaki(panic) na kadri tunavyosema wametutenga ndivyo tunawapa nguvu ya kudhani wamefanikiwa. Ukweli ni kuwa maamuzi ya nchi yetu bado ni sahihi, hatuna sababu za ku sacrifice kwa kitu tunachoweza . Bado tuna option nyingi ikiwa ni pamoja na soko la SADC, au masoko ya nchi za kati kama Zambia, Congo na Malawi.

Mimi ningewashauri Watanzania waangalie fursa zinazotokana na changamoto hizi badala ya kudhani tumetengwa. Tuna soko zuri kwa mtu au nchi yoyote na tumesimama wenyewe baaada ya mwaka 1977.
Tuna uzoefu wa ushirikiano na matatizo ya muungano kuliko taifa lingine na hivyo experience yetu ndiyo ituongoze na si kuhamaki.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Nguruvi3 asante kwa bandiko lako makini.Ombi maalumu je inawezekana ukachapisha nondo hizi kwenye magazeti kama Raia mwema,Mwananchi..... na magazeti mengine mengi ili wananchi wasiotembelea mitandao ya kijamii wakachota elimu ?.
Ngongo na Katavi Mkono Lusuba ahasanteni sana kwa maoni yenu na michango yenu. Ukweli ni kuwa siku za nyuma kidogo nilikuwa natoa makala katika gazeti moja.

Kwa maoni yenu mnaamsha ari tena na hakika sikujua kuwa kamchango haka kadogo pengine kana igusa jamii kwa namna mlivyosema. Kwa vile nimekuwa natumia mtandao huu ambao ni faida kwa jamii nitashirikiana na akina Invisible kuangalia ushauri wenu na kuufanyia kazi. Ahsanteni sana
 
Last edited by a moderator:
NCHI YETU INAWATUMIAJE VIONGOZI WENYE UZOEFU?

Katika nchi za wenzetu viongozi wastaafu wa mataifa wametumika kama hazina kutokana na uzoefu wao wa kikazi wa kukabiliana na changamoto mbali mbali.

Marekani wastaafu,marais na makamu wao pindi wanapoondoka madarakani hufanya kazi za kimataifa kupitia taasisi zao. George Bush snr alikuwa na taasisi ya 'light' ambayo Michelle Obama ameitumia.
Bill Clinton na taasisi inayohusu umasikini na maradhi kwa nchi zinazoendelea.
George H Bush yakwakwe inayojishughulisha na saratan,AL Gore na taasisi ya kushghulia tabia nchi n.k.

Waziri mkuu wa uingereza ana taasisi inayosuhgulikia mashariki ya kati.Viongozi wengine wameshiriki hata serikalini kwa kuchukua nyadhifa ndogo. Mfano ni Israel ambako mawaziri wakuu wanakuwa n.k.

Katika kutekeleza majukumu yao viongozi hao wamewekewa mipaka ya namna ya kuongea ili kutokinzana na serikali iliyopo madarakani hata kama ni ya chama pinzani.

Lakini pia wanaandika vitabu na kutoa hotuba kutokana na uzoefu wao. Wanajenga maktaba ambazo zina nyaraka mbali mbali zisizoingiliana na usalama wa taifa .Maktaba hizo zina habari mbali mbali za viongozi wakiwa madarakani, maisha yao binafsi na uzoefu wao kikazi na menineyo ya kitaaluma na elimu kwa ujumla.

Tanzania ina bahati kwa viongozi kubadilishana madaraka na kubaki raia wakilelewa na serikali.
Hadi sasa kuna Rais Mwinyi, Rais Mkapa, mawaziri wakuu Malecela, Msuya, Warioba, Sumaye.

Baada ya kuondoka madarakani ni nadra viongozi kuwa na taasisi zao zinazoshughulikia mambo ya kijamii licha ya ukweli kuwa wanahitaji kimchango na uzoefu wakiwa wanapata malipo kwa gharama za wananchi.

Kimetokea kituko baada ya CCM kuunda baraza la wazee washauri wa chama.
Kwa kuanzi tu hilo ni kosa kwasababu baraza hilo halina meno na ni kama kikao cha kahawa.

Kuwaondoa katika nafasi za ujumbe wa kamati kuu au halmashauri kuu ni mpango wa kisiasa unaolenga kupunguza nguvu za makundi fulani yenye ushawishi yanayoona uwepo wa wazee ni kikwazo

Kinachosikitikisha, hatua hizo za CCM ni kuwachukua viongozi waliolitumikia taifa na wanaoendelewa kuhudumiwa na taifa bila kujali itikadi za kisiasa kuwafanya kama washauri wa chama chao.

Wastaafu ni hazina ya taifa na wangepaswa kuwa na baraza la ushauri la kitaifa na wala si chama.
Taifa linapita katika changamoto mbali mbali ndani na nje, ilikuwa ni busara viongozi hao kuishauri taifa na si chama kuhusu uzoefu wao wa kukabiliana na changamoto.
Hawa wanapaswa kuwa neutral ili kusimamia masilahi ya taifa.

Hebu tujiulize, hivi hawa viongozi wameshindwa kutumika katika kuendeleza huduma za kijamii kama afya na elimu? Hivi kweli serikali imeshindwa hata kuwapa kafungu ili kila mmoja awe na ki-library chake tunachoweza kusoma pamoja na mambo mengine uzoefu wake kuhusu dunia tuliyo nayo?

Leo nani anajua kwa undani makubaliano ya kuanzisha EAC baada ya mediation agreement kuunda kamati ya kutengeneza Jumuiya tuliyo nayo! Nani anaweza kujua changamoto gani nchi ilikumbana nazo wakati na kabla ya kusaini mikataba ya kuunda EAC, na SADC . Tunajua haya yalitokea siku za nyuma lakini yalishughulikiwaje?

Tatizo ni kukosa sera za kitaifa kuhusu mambo muhimu(National policy) kuhusu mipango ya uchumi na usalama ya muda mfupi na muda mrefu. Kiongozi anapoondoka hakuna kumbu kumbu za nini alifikiri, alifanya, alifanikiwa au alishindwa.Kila kiongozi anakuja na sera zake kama tulivyoona shule za kata na kilimo kwanza.

Athari zake ni wananchi kubabaika linapotokea jambo dogo tu. Hakuna anayefahamu kwa dhati nini Mkapa alifkiria kuhusu DRC au Mwinyi ukilinganisha na hali tuliyo nayo.

Duru tunasema mambo ya kitaifa yawe ya kitaifa, viongozi wa kitaifa wawe wa kitaifa na wapewe fursa za kulihudumia taifa kwa namna nyingine na wala si kula posho na kusubiri matibabu nje ya nchi.

Hivi kama bandari wameweza kufanya mikutano miwili kwa bilioni 2, huku bilioni 8 zikitafunwa katika mkutano wa partneship, wabunge kulamba mabilioni ya mfuko wa jimbo bila audit, tunaweza kusema kweli serikali haina pesa za kuwawezesha viongozi hawa kufanya mambo ya jamii?

Nao hao viongozi wastaafu lazima waelewe kuwa huduma na fursa za kulihudumia taifa ni dhamana na hivyo wanawajibu wa kuirudisha kwa jamii. Kazi yao isiwe kusubiri dhifa za kitaifa

Chester Croker naibu waziri wa mambo ya nje akishughulikiwa Afrika sasa ni mhadhiri.
Sec of state Codolleza Rice ni mhadhiri. Hivi hawa wazee wetu wameshindwa kwenda kutoa hata mihadhara katika taasisi zetu kweli.Ni uzoefu gani walioupata na wanautumiaje kuandaa kizazi cha baadaye?

Tusemezane










 
Katavi jumuiya ya Afrika mashariki ilipokufa hakika tulikuwa katika wakati mgumu sana. Kwa wakati huo tulikuwa na miaka 16 tangu tupate uhuru. Shughuli zote za huduma na jamii zilikuwa za kutegemeana nyingi zikiwa Kenya. Mfano, viwanda vya nguo tulitegemea sana Jinja Uganda. Huduma za jamii kama posta na simu, reli na hata bandari zilikuwa Kenya n.k.

Tulianza moja kwa kujenga miundo mbinu na huduma za jamii. Tofauti ya kiuchumi iliyokuwepo kati ya Kenya na Tanzania ilikuwa kubwa sana. Miaka ya 90 tukafungua milango na bado tulikuwa ni soko la wenzetu. Miaka ya 2000 sisi tukaanza kutafuta masoko huko kwao.

Tofauti ya GDP yetu na Kenya imezidi kupungua hadi kufikia second economy ya EAC huku tukiwa na GDP inayokuwa katika kiwango kikubwa. Ingawa bado haijawa reflected kwa wananchi wa kawaida ni ukweli kuwa Tanzania inabaki kuwa tishio kwa uchumi namba 1 EAC ambao ni Kenya. Kwa hili Mchambuzi anaweza kutusaidia kudadavua.

Hakuna sababyu ya kuhamaki(panic) na kadri tunavyosema wametutenga ndivyo tunawapa nguvu ya kudhani wamefanikiwa. Ukweli ni kuwa maamuzi ya nchi yetu bado ni sahihi, hatuna sababu za ku sacrifice kwa kitu tunachoweza . Bado tuna option nyingi ikiwa ni pamoja na soko la SADC, au masoko ya nchi za kati kama Zambia, Congo na Malawi.

Mimi ningewashauri Watanzania waangalie fursa zinazotokana na changamoto hizi badala ya kudhani tumetengwa. Tuna soko zuri kwa mtu au nchi yoyote na tumesimama wenyewe baaada ya mwaka 1977.
Tuna uzoefu wa ushirikiano na matatizo ya muungano kuliko taifa lingine na hivyo experience yetu ndiyo ituongoze na si kuhamaki.

Mkuu Nguruvi3,

Nakubaliana na hoja yako kwamba Tanzania ina options nyingi nje ya EAC; Lakini lipo tatizo moja: Kuna so many ambitious regional integration initiatives in eastern, central and southern Africa. Kwa mfano, EAC ina dhamira ya kuelekea towards Monetary Union lakini dhamira hii coincides with other initiatives zinazolenga kuimarisha regional economic cooperation, ikiwa ni pamoja na monetary integration, kwa mfano COMESA na SADC; Uanachama wa COMESA & SADC partly una overlap na ule wa EAC, creating conflicting obligations kwa nchi ambazo ni wanachama wa two regional organizations;

Inabidi ifikie wakati Tanzania iamue kubakia katika entity moja; Kenya wao sio wanachama wa SADC ingawa wanatamani sana uanachama wa SADC; Na haitakuwa rahisi kwa Kenya kuwa wanachama in the next foreseeable future kwani Kenya katika hatua ya awali haikuwa inaunga mkono dhamira ya SADC ambayo ilianza kama Kamati ya Ukombozi Kusini mwa Afrika, chombo ambacho Kenya haikuwa inakiunga mkono kwani wakati wenzake wanapingana na serikali ya makaburu, Kenya waliendeleza uhusiano na makaburu katika kipindi chote; Nadhani maswali ya msingi ambayo hoja zako imeyachokoza hapo juu ni je:

* Kenya inapoteza nini kwa kutokuwa mwanachama wa SADC?

*Na Tanzania itapoteza nini kutokuwa mwanachama wa EAC?

Tukumbuke kwamba Katika hatua za awali, EAC was driven by economic objectives wakati SADC was driven by political objectives; Vinginevyo, majibu ya maswali haya ni magumu bila kufanya utafiti wa kina, lakini nitajaribu kurudi na maoni yangu machache juu ya hili, nikijikita zaidi katika hoja zako hapo juu/takwimu za uchumi.
 
Mkuu Nguruvi3,

Nakubaliana na hoja yako kwamba Tanzania ina options nyingi nje ya EAC; Lakini lipo tatizo moja: Kuna so many ambitious regional integration initiatives in eastern, central and southern Africa. Kwa mfano, EAC ina dhamira ya kuelekea towards Monetary Union lakini dhamira hii coincides with other initiatives zinazolenga kuimarisha regional economic cooperation, ikiwa ni pamoja na monetary integration, kwa mfano COMESA na SADC; Uanachama wa COMESA & SADC partly una overlap na ule wa EAC, creating conflicting obligations kwa nchi ambazo ni wanachama wa two regional organizations;

Inabidi ifikie wakati Tanzania iamue kubakia katika entity moja; Kenya wao sio wanachama wa SADC ingawa wanatamani sana uanachama wa SADC; Na haitakuwa rahisi kwa Kenya kuwa wanachama in the next foreseeable future kwani Kenya katika hatua ya awali haikuwa inaunga mkono dhamira ya SADC ambayo ilianza kama Kamati ya Ukombozi Kusini mwa Afrika, chombo ambacho Kenya haikuwa inakiunga mkono kwani wakati wenzake wanapingana na serikali ya makaburu, Kenya waliendeleza uhusiano na makaburu katika kipindi chote; Nadhani maswali ya msingi ambayo hoja zako imeyachokoza hapo juu ni je:

* Kenya inapoteza nini kwa kutokuwa mwanachama wa SADC?

*Na Tanzania itapoteza nini kutokuwa mwanachama wa EAC?

Tukumbuke kwamba Katika hatua za awali, EAC was driven by economic objectives wakati SADC was driven by political objectives; Vinginevyo, majibu ya maswali haya ni magumu bila kufanya utafiti wa kina, lakini nitajaribu kurudi na maoni yangu machache juu ya hili, nikijikita zaidi katika hoja zako hapo juu/takwimu za uchumi.

Mkuu Mchambuzi na nguruvi, ni uchambuzi mzuri sana huu mnaotulutea. Mungu awabariki tuzidi kupata elimu.
Hoja na maswali uliyoaibua kimsingi yanaleta taswira pana ya changamoto iliyopo kufikia Mpango wa utekelezaji wa maendeleo ya Afrika kuhusu ushirikiano (Lagos Plan of Action). Na tatizo kubwa ni hilo la ambitious motives za kufikia level flani ya ushirikiano pasipo kuangalia uimara wa misingi ya kufikia huko na uhalisia wetu. Utaona tunapata tabu kujua zaidi kama tunahitaji nini? Ushirikiano wa Kisiasa au wa Kiuchumi? kushirikiana bila shaka ni kupoteza baadhi ya haki zako, Je Afrika tuko tayari?. Je ni kweli tuna lengo moja? What about our ethnic groups? Kwa mwenendo tunaoenda nao, I doubt kama tutafikia lengo la kuwa na sarafu moja Afrika hiyo 2028.

Nikirejea kwenye mgongano wa uanachama katika Jumuiya za kikanda, hii ni changamoto kubwa hususan katia ya hizi Jumuiya tatu za SADC, EAC na COMESA. Zote zimekuwa na ndoto za kuwa na Customs Union, lakini kiutaratibu, nchi moja haiwezi kuwa mwanachama wa Customs Union mbili labda tu kama zitakuwa na viwango sawa vya ushuru wa forodha, rules of origin na sera zinazohusiana nazo. Kwa maana hiyo hizo Jumuiya mbili zenye Customs Union itakuwa sawa na kusema moja. Ni kutokana na suala hili ndio maana hata SADC haikuweza kuwa na Customs Union kwani kuna Southern Africa Customs Union (SACU) inayozihusisha nchi za Afrika Kusini, Botswana, Namibia, Swaziland nadhani na Lesotho. Badala yake zimeamua kuishia kwenye Free Trade Area 2008, ikizingatiwa kwamba SACU sio tu jumuiy kongwe ulimwenguni, lakini pia haitaki kupoteza CU yao. Na hata wanachama wa SACU kimsingi wako afadhali kwenye uchumi na ni soko tegemeo kwa Afrika Kusini. Ni kutokana na dhamira hii ya mwingiliano wa Jumuiya ndio maana nimesoma hizi Jumuiya zinajadiliana Grand FTA Tripartite ikizihusisha nchi 26, watu kama 600million, (yaani 15+5+19=26). Sijajua kama mbio hizi zimeishia wapi kwa sasa au ziko hatua gani.

Kuhusu fursa ilizonazo Tanzania nje ya EAC, naweza kusema both, yes and no. Biashara ya EAC ni kama Bilion $4.5-5.0 kwa sasa, na Tanzania inafanya vizuri kiasi chake ikiwa Rwanda ni nchi ya pili kuwa na Biashara naye nzuri baada ya Kenya(if am not wrong). Lakini pia kuna mwingiliano mkubwa wa biashara zisizo rasmi (unrecoeded figures) ambazo zinafanywa na Watanzania walio mipakani ambazo nina imani kubwa sana juu manufaa yanayopatikana. Hivyo, kutokana na nature ya mipaka yetu na Nchi za EAC na ukweli kwamba Tanzania ni potential producer wa informal products na kuliko nchi nyingine za EAC, nadhani kujitoa EAC kutaleta athari kubwa kiasi chake katika Uchumi wetu. Sisi tunaoishi mijini huku huenda si rahisi kubaini namna hawa wa mipakani wanavyouziana kuku/ndizi/mchele na kuwasaidia katika maisha yao ya kila siku.

Aidha, Biashara ya COMESA ambayo inakadiriwa kufikia $17.5billion ina changamoto kubwa hususan za kiushindani na kiutamaduni. Huenda hii ndiyo inayomfanya Kenya (labda) aiwazie SADC ambayo ina nchi zenye utamaduni unaofanan sana tofauti na COMESA yenye nchi za Kiarab ambazo ni wazalishaji wazuri pia lakini watu wake wamekuwa too affected na bidhaa toka Ulaya na Nchi za Mashariki ya Kati na Asia, hivyo kuona kwamba ni soko gumu sana ku-survive kwa Kenya.

Kwa upande wa SADC, Tanzania pia tunafanya vizuri tukiwa na urari chanya wa Biashara kama ilivyo EAC, ingawa huko tuna Biashara kubwa kidogo. Ubaya wa soko hili ni South Africa ku-dominante biashara ikifuatiwa na Angola ambazo zinachukua zaidi ya 60% ya mauzo. Hata hivyo, bado Soko hili ni zuri kwa Tanzania kutokana sababu mbalimbali ikiwa pamoja na kukubalika kwa Tanzania miongoni mwa jamii ya watu wa SADC, na kuwepo kwa nchi nyingi tu ambazo Tanzania tuna nafasi ya ku-export Biashara (Congo DR, Zambia, Msumbiji, Zambia, Malawi, Madagscar na Sechelis).

Nachotaka kubainisha ni kwamba, Tanzania tuendelee kuwa kwenye Jumuiya zote mbili ila nirejee kwenye ushauri wa Nguruvi3, haina budi kuongeza uwekezaji kwenye miundombinu na viwanda. Hii itasaidia kunufaika na Jumumiya zote hizi mbili huku tukijiweka kwenye mazingira ya pores-border nyingi tu kwa ajili ya watu wetu wa kawaida. Katika hili la Miundombinu, nadhani hata kinachoendelea sasa, kisiturudishe nyuma kwenye ujenzi wa Reli ya DAR-KIGALI-BUJUMBURA kwani inawezekana kuweka branch kwa ajili ya Congo DR na kutoa uwanja mpana kwa wafanyabiashara wa Burundi, Rwanda kuchagua wenyewe. Reli hii si kwa ajili ya Bandari pekee, lakini pia kwa ajili ya exports zetu kwa nchi hizo iwapo viwanda vyetu vitaweza kuwa imara kutokana na matarajio ya matumizi ya nishatio ya Gesi katika uzalishaji. Aidha, ikitokea Kenya kutaka kuwa mwanachama wa SADC (japo sitarajii hili kutokea), Tanzania itafute nchi ambayo itaikatalia (kwani yeye hatoweza kutokana na kuwepo pamoja EAC). Wacha COMESA na SADC tukutane kwenye SADC, EAC, COMESA Tripartite FTA.
 
wapendwa wa bandiko hili nimepita kuweka like kwenye kila post yenu kisha ninaprint hizi nyanga nizisome vyema ahalafu baadae nitapenda kurudi hapa kwa mjadala murua kuhusu EAC na mustakabali waTanzania yetu kwa sasa. Barikiweni sana kwa uchambuzi yakinifu.
 
Mkuu Mchambuzi na Zinedine, ahsante sana kwa michango na changamoto zenu

Niweke vema kuwa niliposema Tanzania ina option sikumaanisha za kujitoa bali za kujiunga nazo.
Kuna uchumi untapped potential ndani na nje ya EAC kupitia majirani.

Huko nyuma nimesandika hakuna sababu za Tanzania kujitoa EAC lakini pia haina sababu ya kujitoa mhanga.
Nilitoa mfano wa UK ambayo ni mwanachama lakini haitumii EURO au Nchi nyingine zisizotumia Shengen.

Umuhimu wa EAC upo kwa wananchi kwa kuzingatia uwezo wa watu wetu kama ambavyo mpango wa AGOA tulivyoshindwa kuutumia kuutumia.Faida katika EAC ni soko la karibu kwa mwananchi wa kawaida na taifa kwa ujumla.

Kenya inapoteza nini kwa kutokuwa mwanachama wa SADC, hili linahusu soko.
SADC ina watu takribani milioni180.Nchi wanachama zina potentials za madini na kilimo.
Umuhimu wake kiuchumi ni mkubwa na Kenya ingependa kuwa sehemu ya SADC

Kufufuliwa kwa EAC kulikoanza na mediation agreement kuliweka wazi jumuiya iwe people centered, ijikite katika uchumi na biashara kuelekea katika political federation.Hapa tunaona political federation ikiwa nyuma ya uchumi.

SADC ilianza kwa spirit ya ukombozi na kadri siku zinavyosonga spirit hiyo inabadilika kuwa ya kiuchumi.
Kwa upande mwingine ‘political will' imetangulia uchumi prospect kubwa kuliko EAC ya sasa.

EAC imeacha ‘people centered' na sasa ni mkusanyiko wa wanasiasa.Sidhani Wakenya, Warwanda, Waganda au Warundi wanafurahia hali ilivyo hata kama viongozi wao watatu wanafuraha sana. Tunaona wananchi wanavyoonyesha wasi wasi

Tofauti na political will ya SADC, EAC inaonyesha ''political interest''.
Hivi ni vitu viwili tofauti. Political will inajenga mazingira na Political interest inaingilia mazingira
SADC wanatumia political will kujenga mazingira ya kushirikiana kiuchumi.
EAC inatumia ''political interest'' kujenga mazingira ya kisiasa zaidi.

Tunaweza kuwa na mahusiano mengine na jumuiya nyingine bila kuathiri EAC.
Kenya /Uganda/Rwanda na Burundi wapo COMESA, Tanzania ipo SADC kukiwa na uwezekano wa ku-harmonize the business to fit our model.

Ili hilo lifanikiwa ni lazima kwanza:
1. Turudi katika msingi wa jumuiya ambao ni people centered
2. Kuweka masilahi ya uchumi mbele kwa kuanza kujenga mazingira ya kuaminiana
3. Kuwaacha wataalam waongoze shughuli za jumuiya na si wanasiasa.
 
Last edited by a moderator:
PROPAGANDA ZA KUITUHUMU TANZANIA KATIKA EAC

Nimesoma gazeti la The East Africa lenye makala ikieleza Tanzania inasita sita kuwa na integration ya EAC. Makala hiyo sehemu kubwa ya ukweli imefichwa na kinachoelezewa ni propaganda.
Moja ya madai ni kuwa elimu ya Tanzania ni hafifu Watanzania wanaogopa hawatamudu ushindani.

Sijui ni kigezo gani kimetumika kusema elimu ni hafifu kwasababu elimu ina maana pana sana.
Kunaweza kuwepo kwa tofauti za hapa na pale lakini sina uhakika tofauti hizo ni kubwa kiasi hicho.
Mara nyingi sana kuna kuchanganya kati ya lugha na weledi vitu ambavyo ni tofauti kabisa hata kama kuna nyakati vinategemeana.

Tunakumbuka tulipoacha ujamaa kila jambo lilikuwa geni kwetu. Imechukua muda mfupi kwenda sambamba na wenzetu. Ni kweli kuwa Watanzania hawamudu competition katika maeneo kama Kenya, lakini competion ina tafsiri nyingi. Wakati wa Kenya wakisema competition sisi tunasema tribalism.
Sijui Waluo na Wakikuyu wana compete nini kama si tribalism.

Kitu kisichosemwa kuhusu Tanzania kuchukua hadhari ni suala la ardhi ndiyo maana tunasema hizi ni propaganda, Tofauti zipo za kijamii ambazo ni kama ukabila kwa mataifa wanachama wanaoita competition.

Wenzetu wanataka shirikisho la EA haraka haraka. Wanasahau kuwa EU kama EC ilianza miaka ziaidi ya 50 iliyopita na bado kuna matatizo wanayokumbana nayo. Tumeona jinsi muungano wa sarafu unavyofarakanisha mataifa hayo kiasi cha Wajerumani na Wafaransa kutaka sarafu zao zirejee.

Tumeona jinsi Greece inavyotishia usalama wa kiuchumi wa EU.
Lipo swali kwanini EU wasiwatose Greece ili kuepuka matatizo?

well jibu ni kuwa kuatosa ni kuua mitaji ya nchi nyingine. Greece ni moja kati ya chumi kubwa na nchi kama Ujerumani imewekeza sana kupitia EU. Kuwatosa ni kuzitosa benki na makampuni yenye mitaji yao na hivyo kuhatarisha uchumi wa Euzone nzima. Ndio maana Ujerumani inawabeba kila uchao kwa gharama kubwa.

Sisi kama EAC hatujaweza kuweka uwiano sawa wa kiuchumi, kuimarisha benki na kuzifanya zifanye kazi pamoja. Ikitokea mdororo wa uchumi hakuna atakayembeba mwenzake na huo ndio mwanzo wa kuvunjika jumuiya. Kwa mantiki hiyo process ya integration ni hatua kuanzia chini kwenda juu na si suala la kukurupuka tu. Tanzania ikieleza haya kwa experience ya mwaka 1977 inaonekana kama kikwazo.

EAC ilikubaliana kuwa kwa vyuo vikuu vya serikali ada iwe moja ili kuwezesha wanafunzi kutoka sehemu moja kusoma sehemu nyingine. Hizi ni jitihada za kuimarisha taasisi kwanza kabla ya shirikisho.

UDSM walianza mpango huo uliokataliwa na Nairobi na Kampala bila sababu.
Leo hawa ndio wanasema twende kwenye siasa chap chap ikiwa tu hatujaweza kuweka viwango sawa vya kitu kidogo na cha kawaida kwa mwananchi kama elimu ya chuo kikuu. Bado Tanzania inalaumiwa kwa kusita na wala si kwa wale waliokataa.

Tumekuwa na mahakama ya EAC. Wakati wa mzozo wa Kenya, ni Kenya hiyo hiyo machampioni wa integration waliokataa kuitambua na kuishia katika mzozo mkubwa wa kisiasa.
Kenya haisemwi kuzorotesha juhudi za integration za kimahakama bali lawanma inatupiwa Tanzania.

Kenya iliishtaki Tanzania mbele ya mataifa kuhusiana na pembe za ndovu. Kenya haikutafuta suluhu kutoka EAC bali iliangalia masilahi yake ya kiuchumi. Leo wanaituhumu Tanzania kuhusu misimamo ya baadhi ya mambo.

Nimejaribu kwa ufupi sana kueleza jinsi gani wenzetu wanavyozusha propaganda ili kuonyesha kuwa Tanzania ni tatizo. Wanasahau kuwa kuna matatzo makubwa sana kuliko Tanzania.

Sina uhakika kama Kenya wameshaondoa taofauti zao za Uluo na Ukukiyu kiasi kwamba wanaweza kuwa na political integration na Rwanda ya Wahutu na Watutsi au Uganda ya Museveni na Koni n.k.

Shirikisho linatakiwa lianze katika uchumi taratibu na kwa tahadhari kuelekea political integration, siyo suala la kulala na kuamka kukiwa na fast track ya EAC bila maandalizi. Ni kujidanganya.

Tusemezane
 
Mkuu Nguruvi3 asante kwa bandiko lako #329,Niongeze kidogo hapa kuhusiana na mikutano ya nchi za Kenya,Uganda na Rwanda huku Tanzania na Burundi zikiwekwa kando.

Kenya imekuwa ikikumbana na ushindani mkubwa kutoka Tanzania katika sector ya utalii,hasa baada ya Tanzania kuchukua hatua kadhaa za kurekebisha miundombinu inayokidhi mahitaji ya utalii ikiwemo kuongeza hotels,lodges and camps.Tanzania sasa inakadiriwa kufikisha idadi ya watalii milioni moja miaka kumi au kumi na tano hali ya utalii Tanzania ilikuwa katika hali mbaya sana.Bodi ya utalii pamoja na mashirika kadhaa wamewekeza sana katika sector ya utalii na hivyo kuongeza idadi kubwa ya watalii wanaotembelea vivutio vya Tanzania ukilinganisha na vivutio vya Kenya.Baada ya nchi ya Kenya kubaini inazidi kuachwa nyuma huku jirani yake na mshindani wake mkubwa Tanzania ikizidi kuchanja mbuga na kuitimulia vumbi iliamua kupitishia ajenda zake EAC kwamba kuwepo na soko la pamoja katika sector ya utalii.Ikitumia ujanja wa sungura ilitaka iwepo visa moja itakayoweza kutumika kwa nchi zote mwanachama wa EAC.Kenya imekimbilia Uganda na Rwanda ambazo si nchi washindani katika soko la utalii huku ikijaribu kuingiza hoja zake za kijinga kwamba Tanzania inakwamisha intergration.

Ujenzi wa bandari ya Bagamoyo umeistua sana Kenya kwani inajua itakapokamilika bandari yake ya Mombasa itakumbana na ushindani mkubwa toka Tanzania.Kenya imekimbilia karata ya udhaifu wa uhusiano baina ya Tanzania na Rwanda kuhujumu bandari ya Bagamoyo kabla haijaaza kufanya kazi.Museveni anaingiaje katika ushirikiano huu haramu,ni wazi sababu za Rais Kagame kuitenga Tanzania zinajulikana wazi mosi ni ushiriki wa Tanzania katika kikosi cha kusaka amani DRC,pili msimamo wa Rais Kikwete kuitaka Rwanda izungumze na waasi na mwisho Rwanda iliingia EAC ilikupunguza msongamano wa raia wake wanaofikia idadi ya watu milioni 11 wanaishi katika eneo la 10,169 sq miles.Tanzania ilitarajiwa kutatua tatizo la uhaba wa ardhi wa nchi zote wanachama wa EAC ingawa Rwanda inazidiwa sana la mrundikano wa watu katika eneo dogo ukilinganisha na nchi nyingine wanachama wa EAC.Gen Museveni ana tamaa za kutawala nchi za EAC Tanzania imeendelea kuwa kikwazo cha ndoto zake hii pia ni sababu kubwa hasa ikitiliwa maanani ana mwandaa mwanae Brigadier Muhoozi Kainerugaba kutawala Uganda huku yeye akiwekeza nguvu kubwa kutawala EAC.

Ukitazama minyukano ya siasa za EAC utabaini Kenya inaongozwa na tamaa za kiuchumi zaidi huku Rwanda na Uganda zikitumika kuiadhibu Tanzania kwa ukaidi wake wa kulinda ardhi yake isinyakuliwe kiolela.Ni wazi pia Rais Kenyatta anapata uungwaji mkono wa Rais Kagame na Museveni dhidi ya mashtaka yake ICC.

Jambo moja muhimu ambalo waTanzania yapasa kujiuliza ni kwanini katika mikutano ya nchi zote tatu suala la ardhi halikuzungumzwa ?Badala yake masuala ya miundombinu na utalii yalichukua nafasi kubwa !.


Tanzania kupitia waziri wake wa Mambo ya nje tayari imeziandika barua nchi za Rwanda,Kenya na Uganda ikitaka kujulishwa mikutano baina ya nchi hizo ililenga nini na kwani Tanzania inatengwa.
 
Mkuu Nguruvi3 na wadau wengine,

Naomba mniwie radhi kwa kuchelewa kurudi kama nilivyo ahidi, ili kuendelea na mjadala wangu kufuatia hoja iliyotolewa ya Nguruvi3 (rejea bandiko #322 ) kwamba:

Tofauti ya GDP yetu na Kenya imezidi kupungua hadi kufikia second economy ya EAC huku tukiwa na GDP inayokuwa katika kiwango kikubwa. Ingawa bado haijawa reflected kwa wananchi wa kawaida ni ukweli kuwa Tanzania inabaki kuwa tishio kwa uchumi namba 1 EAC ambao ni Kenya. Kwa hili Mchambuzi anaweza kutusaidia kudadavua.

Katika bandiko #325 , nilianza kwa kujadili kwamba kuna tuna regional integration initiatives nyingi kupita kiasi ambazo zinapelekea kupotea kwa tija, na nikahimiza kwamba kuna umuhimu kwa Tanzania kuchagua kubakia katika block moja wapo so as to maximize the benefits, or rather – potential benefits; Katika hili, nikahoji je:

*Kenya inapoteza nini kwa kutokuwa mwanachama wa SADC?

*Na Tanzania itapoteza nini kutokuwa mwanachama wa EAC?
Zinedine alikuja kwa uchambuzi mzuri sana kwenye bandiko #326 ambapo mbali ya kujadili initiatives za EAC, SADC na COMESA, in relation to Tanzania pamoja na faida zake, vile vile alitukumbushia juu ya uwepo wa SACU; Katika kuhitimisha, @zidadine alijenga hoja juu ya umuhimu wa Tanzania kuendelea kuwa mwanachama wa initiatives zote mbili – yani EAC na SADC, huku akimuunga mkono Nguruvi3 juu ya umuhimu wa Tanzania kuwekeza katika viwanda na miundombini ili kuwa katika nafasi bora zaidi ya kutumia fursa zilizopo katika hizi economic blocks;

Pengine ili kuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kubaini juu ya faida ya kuwa mwanachama wa block moja vis a vis block nyingine au kuwa mwanachama kwa zaidi ya block moja, nadhani kwanza ni muhimu tukatazama picha halisi ikoje katika hizi regional blocks, huku tukiweka SADC ‘at the centre', bearing in mind kwamba SADC is the largest economic block in the continent (Sub Saharan Africa);

Karibia nchi zote zilizo wanachama wa SADC pia ni wanachama wa angalau ‘one other regional economic block(s)' if not ‘preferential trade area(s)':

· Nchi saba kati ya nchi kumi na tano wanachama wa SADC pia ni wanachama wa COMESA – nchi hizi ni DRC, Madagascar, Malawi, Mauritius, Swaziland, Zambia, & Zimbabwe;
·
· Nchi moja tu mwanachama wa SADC (Tanzania) ni mwanachama wa East African Community (EAC).

· Nchi mbili tu za SADC (Angola & DRC) pia ni wanachama wa Economic Community of Central African States (ECCAS).

- Je, mchanganyiko huu una tija?

Ingawa Tanzania ilishajitoa COMESA, bado tunaathiriwa sana na complicated & restrictive rules of origin; Kwa mfano, unakuta ni vigumu kwa wanachama EAC kuingia into preferential trade arrangements katika maeneo Fulani Fulani ya biashara/bidhaa na Tanzania kwasababu Tanzania ina uanachama katika blocks nyingine zenye malengo sawa na EAC, hivyo unakuta kwa mfano - the fact kwamba ingawa bidhaa Fulani Fulani zimetokea Tanzania kwenda EAC hivyo to qualify for preferential treatments za kibiashara, tatizo linakuja pale ambapo their point of origin sio Tanzania bali nchi nyingine zisizo wanachama wa EAC kama vile Malawi, Zambia, au Mozambique (wanachama wa SADC); Such overlapping membership in preferential trade areas zina affect sana the intra regional trade, bearing in mind kwamba kwa sasa, the engine of economic growth kwa nchi kama Tanzania is TRADE - we need more trade, especially intra - Africa trade kuliko FOREIGN AID or FDI;

· Nchi mbili za SADC (Angola & DRC) pia ni wanachama wa Economic Community of Central African States (ECCAS).

· Nchi mbili za SADC (Angola & DRC) pia ni wanachama wa Economic Community of Central African States (ECCAS).

· Nchi moja mwanachama wa SADC (the DRC) ni mwanachama wa Economic Community of the Great Lakes States (CEPGL).

· Nchi mbili wanachama wa SADC ((Madagascar and Mauritius) ni wanachama wa ‘the Indian Ocean Commission (IOC)'.

· Nchi tano za SADC (Botswana, Lesotho, Namibia, Swaziland, South Africa) ni wanachama wa Southern Africa Customs Union (SACU); tukumbuke kwamba SACU ni initiatives ya muda mrefu kuliko initiatives nyingine hapo juu, na kumekuwepo na free flows of goods baina ya nchi wanachama kwa muda mrefu sana;

Hata katika SADC economic block, kuna tofauti kubwa sana miongoni mwa wanachama; kwa mfano, DRC sio signatory to the establishment of the SADC free trade area. Pia, kutokana na tatizo la rules of origin (see above), nchi nyingi wanachama wa SADC wameamua to retain preferential bilateral trading agreements na wanachama wengine wa SADC members, kwa nia yaku - circumvent the complex rules of origin and lingering tariff protection zilizokubaliwa chini ya SADC. Kwa mfano, Zimbabwe, has a separate trade agreements with Botswana, DRC, Namibia, Malawi, Mozambique, and South Africa – wakati kama ilivyo Zimbabwe – the DRC, Namibia, Botswana, Malawi, Mozambique and RSA ni wanachama wa SADC;

Suala lingine linahusu negotiations on 'Economic Partnership Agreements' (EPAs) baina ya wanachama wa SADC na Jumuiya ya Ulaya (EU), suala ambalo linaongezea complexity kwenye regional trading arrangements zilizopo; Kwa mfano, wanachama wa SADC wametapakaa katika makundi mbali mbali ya EPA kama ifuatavyo:

1. Botswana, Lesotho, Mozambique, Namibia, and Swaziland - they have signed for an interim Economic partnership Agreement (EPA) na kujitamblisha as the "SADC" group;
2. Angola (second largest economy in the SADC block), bado hajajiunga ingawa ameashiria kujiunga na EPA siku za mbeleni;
3. South Africa (the largest economy in the SADC) bado hajijiunga na EPA, lakini iwapo atajiunga, ni dhahiri uanachama wake utakuwa subject to differential treatment from the rest of the group kutokana na ukubwa wake kiuchumi n.k; preferential treatment za namna hii sip progressive katika regional economic block initiatives;

4. Tanzania has signed an interim EPA lakini kwa pamoja na wenzake wa EAC, sio kupitia SADC;
5. Madagascar, Mauritius, and Zimbabwe, wote hawa wame sign an interim EPA kama sehemu ya 'Eastern and Southern Africa group';
6. Malawi & Zambia, bado wanafanya negotiations kujiunga;

7. Na DRC wao ni sehemu ya Central African negotiating group kuhusiana na EPA.

Given all these challenges, ni dhahiri kwamba advantages za kuwa katika block moja vis a vis (EAC & SADC) ni comparative advantage, sio absolute; Zinedine, nadhani utakubaliana nami katika hili; Now where do we (Tanzania) have the comparative advantage?


Itaendelea……
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mchambuzi nakubaliana na complexity iliyopo. Kutokana na bandiko lako naona kila mwanachama ana rangi zaidi ya moja. Wakati tunasubiri uendelee, swali ni kuwa katika multiple organization kama ilivyo inawekanaje Tanzania ikawa na block moja kwa kulinganisha na wanachama wengine.

 
Last edited by a moderator:
Nachotaka kubainisha ni kwamba, Tanzania tuendelee kuwa kwenye Jumuiya zote mbili ila nirejee kwenye ushauri wa Nguruvi3, haina budi kuongeza uwekezaji kwenye miundombinu na viwanda. Hii itasaidia kunufaika na Jumumiya zote hizi mbili huku tukijiweka kwenye mazingira ya pores-border nyingi tu kwa ajili ya watu wetu wa kawaida. Katika hili la Miundombinu, nadhani hata kinachoendelea sasa, kisiturudishe nyuma kwenye ujenzi wa Reli ya DAR-KIGALI-BUJUMBURA kwani inawezekana kuweka branch kwa ajili ya Congo DR na kutoa uwanja mpana kwa wafanyabiashara wa Burundi, Rwanda kuchagua wenyewe. Reli hii si kwa ajili ya Bandari pekee, lakini pia kwa ajili ya exports zetu kwa nchi hizo iwapo viwanda vyetu vitaweza kuwa imara kutokana na matarajio ya matumizi ya nishatio ya Gesi katika uzalishaji. .
@Zinedine labda niseme sijui kama kuna viongozi wa nchi yetu wanaosoma vitu kama hivi na kutafakari.

Hapa kuna hoja kuu mbili muhimu sana.
1. Kuhusu miundo mbinu ulichosema ndicho nilichosema wasi wasi ni kukosekana kwa watu makini na uongozi unaoweza kuona zaidi ya kesho. Huu ndio ukweli kuwa miundo mbinu ni sehemu ya ukombozi.
Nchi zote zilizoendelea dunia miundo mbinu ni kipaumbele hasa reli kwa kuzingatia ukubwa na unafuu

Miundo mbinu ina faida mbili.
Kwanza, kuimarisha na kuunganisha usafiri wa ndani . Kwamba kunakuwepo na main infrastructure kama reli uliyosema ya Dar Kigali Bujumbura wakati huo huo ikihudumia mikoa katika usafirishaji wa bidhaa za matumizi na za kilimo(Tributaries)

Pili,miundo mbinu ina imarisha sehemu nyingine za uchumi kama vile bandari, utoaji ajira n.k.
Tanzania railway ilikuwa mwajiri namba moja nchini,kuanguka sekta hiyo kumeongeza unemployment kubwa

Hofu yangu ni kuona miundo mbinu kama TAZARA inakuwa na migogoro isiyokwisha.
Kibaya zaidi suala hilo limeachiwa mameneja na wala sio uongozi wa nchi.

Suala la TAZARA ni la uongozi wa juu kabisa wa nchi kwasababu TAZARA haikujengwa wala kusimamiwa na mameneja. Ulikuwa mradi mkubwa sana wa China kuwahi kufanyika katika Afrika.
Vipi leo mradi huu ambao ni tayari uachiwe tu kushughulikiwa na mameneja wasio na ufahamu, walafi na wabadhirifu ambao hawana vision ya jambo lolote wakati huo huo uongozi wa taifa ukiwa unaona kama tatizo la mradi wa kisima cha maji marefu!!!!

Tuna the big four kwa kilimo na Tazara imepita kati kati, hivi kweli tunaweza kusema Tazara imekufa kwasababu hakuna biashara! kama si ujinga ni kitu gani hicho.

Hapa ndipo naona hata mradi wa reli ya kati au uliyoshauri zinaweza kuwa ndoto kwasababu hakuna watu wenye vision, I mean viongozi wanaoona pengine miaka 10 ijayo achilia mbali 50 kama wenzetu

Tutaachwa nyuma kwasababu tu ya viongozi na si nchi au wananchi.
Jaribu kufikiri kuwa bunge letu limejaa wasomi, vijana na wazee. Hata siku moja hutasikia watu wakilumbana kwa hoja nzito kama hizi, utasikia spika na naibu wake wakiendeleza nyimbo za vyama, wakivuruga utaratibu wa bunge na kulifanya bunge la hovyo sana katika historia na EA.
Kwa mwendo wa bunge la makinda na Ndugai lazima wenzetu watatuacha tu.

Mijadala mizito ya masuala ya kitaifa inalindwa na spika na naibu wake ili kulinda masilahi ya watu na si nchi.
Hakuna mjadala wowote ule wa maana ndio maana nasema hoja nzito zipo tatizo ni hili la akina Ndugai na Makinda waliogeuza bunge uwanja wa hovyo.

Tuseme ukweli tusiogope vinginevyo tutaachwa nyuma na wenzetu.
 


Jambo moja muhimu ambalo waTanzania yapasa kujiuliza ni kwanini katika mikutano ya nchi zote tatu suala la ardhi halikuzungumzwa ?Badala yake masuala ya miundombinu na utalii yalichukua nafasi kubwa !.
Ngongo ahasante kwa bandiko lako hapo juu. Nijibu hoja hii ya mwisho kuhusu ardhi, hilo haliwezi kuzungumziwa ndani ya EAC kwasababu hakuna mwenye nafuu nalo. Kenya na Uganda walitaka kuzipiga kwasababu ya KM 1, Rwanda inahamisha raia wake nchi jirani sasa wataongelea ardhi kwa lipi? Hicho hasa ndio msingi wa chuki ndani ya EAC.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Nguruvi3,

Asante kwa swali lako muhimu sana #332 ambapo umeuliza hivi:
Mkuu Mchambuzi nakubaliana na complexity iliyopo. Kutokana na bandiko lako naona kila mwanachama ana rangi zaidi ya moja. Wakati tunasubiri uendelee, swali ni kuwa katika multiple organization kama ilivyo inawekanaje Tanzania ikawa na block moja kwa kulinganisha na wanachama wengine.

Kimsingi, mjadala wangu unalenga kutafuta majibu kwa swali hili muhimu; Nitajitahidi kujadili suala hili, nikianza na hoja zifuatazo:

Nadhani tutakubaliana kwamba - sehemu kubwa ya Sura ya bara la Afrika (hasa sub Saharan Africa) ni presence of a large number of very small landlocked countries, ambazo zinategemea sana nchi jirani kiuchumi, hasa zile zenye access to the sea, a larger market (population), n.k. Ni kwa mantiki hii, nchi hizi ndogo ndogo zinazokosa mambo haya muhimu (access to sea, larger market n.k) hulazimika kujihusisha na regional integration kwa njia moja au nyingine; Hii ndio sababu ya msingi kwanini regional economic communities nyingi zimekuwa zikiibuka karibia kila kona ya bara la afrika kwa nia moja tu – kuhakikisha nchi za namna zinapambana na changamoto nilizoainisha hapo juu; Leo hii, karibia kila nchi zote za Sub Saharan Africa ni wanachama wa angalau ‘one regional economic block'; Such proliferation ina madhara mengi kiuchumi kuliko faida kwani it has been proved over and over again kwamb - multiple membership of regional economic blocks actually hinders regional integration; it doesn't foster regional integration kama wengi wanavyopenda kuamini/aminishwa; Ni kwa maana hii, kumekuwa na efforts mbalimbali barani Africa (source ikiwa ni nchi wahisani) zinazolenga kutatua tatizo hili, hasa katika kutafuta a common ground between different regional integration initiatives; Yapo makubaliano mbalimbali ambayo yameshafikiwa among various regional economic blocks in Africa, na nikipata muda nitakuja toa ushahidi juu ya suala hili;

· Iwapo the way forward sasa ‘is an attempt to harmonize initiatives zilizopo, kwanini Tanzania tusisome alama za nyakati na kuwa ahead of time kwa kufanya maamuzi magumu mapema badala ya kupoteza tu fedha za walipa kodi pamoja na fursa nyingi za kibiashara na kiuchumi kwa ujumla?

Moja ya sababu kubwa kwanini intra regional trade barani Afrika imekuwa ikisua sua ni kutokana na such proliferation, kwani multiple membership of regional economic blocks imposes high costs in time, energy and resources kwa serikali husika na hulazimisha serikali hizo to juggle between competing regulations – mfano rejea mjadala wangu #325 on complex rules of origin kutokana na overlapping membership in preferential trading arrangements; zimejadiliwa factors nyingine zinazochangia kusua sua kwa intra regional trade kama vile miundombinu, low manufacturing capacity n.k, lakini ukweli unabakia kwamba hata haya yakitatuliwa, bado suala la soft infrastructure - effective rules and regulations sambamba na strong and independent regulatory institutions, zitaendelea kuwa kikwazo, na hizi zina uhusiano wa moja kwa moja na suala la ‘rules of origin';

Iwapo tutakubaliana kwamba moja ya sababu zinazopelekea nchi za Afrika kuwa members of multiple regional economic blocks ni pamoja na changamoto zinazotokana na nchi husika kuwa ‘landlocked', uwepo wa ‘idadi ndogo ya watu' population/market), ukosefu wa ardhi yakutosha, ukosefu wa natural resources, je:

· Tanzania tunakabiliwa na matatizo katika haya?

Sidhani, hivyo sioni sababu kwanini Tanzania tuendeleaa kuiga wenzetu wenye matatizo haya wakati sisi tuna fursa nyingi kuliko changamoto katika suala husika; Ni muhimu tukajipongeza kwa kujiondoa COMESA huko nyuma kwani uanachama wake ulikuwa hauna tija relative to uanachama wa economic blocks nyingine; uamuzi wa kujitoa ulikuwa ni wa busara sana;

Kuna wakati kulikuwa na umuhimu kwa Tanzania kuwa mwanachama wa block zaidi ya moja – SADC na EAC lakini kwa sasa "wakati huo umepitwa na wakati"; Katika kipindi cha nyuma, EAC ilivunjika baada ya wanachama kupishana kimtazamo na kimwono, lakini kwa vile wanachama wan chi za mstari wa mbele kusini mwa afrika walikuwa na lao moja – ilikuwa ni rahisi kwa Tanzania kuwa mwanachama wa SADC kuanzia 1992, huku tukiwa ni kinara wa jumuiya hii; Baada ya EAC kurudi, tumejikuta kwenye two regional economic blocks ambazo kimsingi imposes costs in time, energy and resources kwa serikali yetu; Mbali ya kuwa na shared history na wanachama wengine wa SADC, binafsi nadhani Tanzania ina fursa zaidi kiuchumi kwenye EAC kuliko SADC, kwani unlike SADC, kwenye EAC Tanzania itarejea kwenye drivers seat badala ya kuburuzwa na South Africa, Angola, Mauritius and increasingly Mozambique; Nitarejea baadae katika hili la faida za EAC vis a vis SADC kwa Tanzania;

Vinginevyo, iwapo tunakumbuka vyema, miaka ya 1960s & 1970s, Tanzania ilikuwa ni champion & driver of regional integration in Africa ambapo chini ya uongozi wa Mwalimu Nyerere, not only we drove the narrative of regional integration, bali pia to a large extent, we controlled it – kwa mfano rejea influence ya Mwalimu Nyerere on Pan African Freedom Movement For East and Central Africa (PAFMECA) from late 1950s. Nyerere was the greatest believer of African Unity who believed in step-by-step realization of that Unity; Kwa mwalimu, it didn't matter whether mchakato unaanza na Siasa au Uchumi, kwa Mwalimu, kikubwa ilikuwa ni ulazima wa safari ya muungano wa afrika kufuata ‘baby steps', tofauti na mtazamo wa Kwame Nkrumah; Mwalimu alijikuta in a serious clash (kimtazamo) na Kwame Nkrumah, kwani Nkrumah aliamini - forcefully for continental political unity based on only one ideology – Pan Africanism; Mwanzoni Nkrumah alionekana kuwa na mtazamo wenye manufaa kwa Afrika kuliko Nyerere, hivyo kuungwa mkono kwa wingi, lakini muda sio mrefu, radicalization of african unity kwa mtazamo wa Nkrumah ukaanza kuonekana kutofaa, na badala yake incremental approach chini ya Nyerere ikawa embraced, na busara za Mwalimu zinaendelea kutumiwa hadi leo;

Nianze kwa kujadili kwanini nadhani kuna fursa nyingi zaidi EAC kuliko SADC:

Fursa ya Kwanza: Tanzania ina kila sababu ya kuchaguliwa kuwa a political capital ya EAC na nchi washiriki pamoja na wale wote wanaosadia shirikisho la EAC lisonge mbele, kwa mfano EU n.k; Tanzania ina uwezo wa kuwa the most ‘honest broker' iwapo matatizo yanajitokeza katika nchi za maziwa makuu; Kwa mfano, tumeona jinsi gani Tanzania iliteuliwa kuwa makao makuu ya mahakama ya kughulikia wahalifu… - Rwanda's genocide; Vile vile historically, we have mediated conflicts nyingi sana & kuwa viewed kama a neutral stakeholder – kwa mfano mwalimu Nyerere na mchakato wa kuleta amani nchini Burundi in the 1990s, kuikomboa Uganda kutoka mikononi mwa Nduli iddi Amnin (1978/79, uteuzi wa Mkapa kusimamia mazungumzo ya amani nchini Zimbabwe - mwanachama wa SADC, 2006), involvement ya Tanzania kutatua the post – elections crisis nchini Kenya (Kibaki vs Raila saga) miaka kadhaa iliyopita n.k; Mbali ya haya, Pia Tanzania inatambulika na kuheshimika sana katika kusimamia haki, usawa, umoja, udugu, na kujitoa mhanga kwa ajili ya haya - kwa mfano suala la ukombozi Kusini mwa afrika, na pia Nguruvi3 - uamuzi wa Tanganyika kujitolea kupoteza utaifa wake kwa ajili ya Zanzibar, 1964;

Kwa maana hii, we have enough "political capital" to enable us mediate changamoto zozote zitazojitokeza katika EAC; Kwa mfano, moja ya destabilizing factors in the region ni ugomvi baina ya sudan kusini na sudan kaskazini, na Tanzania ina uwezo mkubwa wa kuwa msimamizi wa mazungumzo ya amani hasa kwa vile hatupakani na nchi hizi, lakini muhimu zaidi, tofauti na washiriki wengine wakubwa wa EAC - Kenya na Uganda ambao wamesha chagua upande wa kuegemea katika mgogoro wa Sudan, Tanzania haijachagua upande wowote katika sakata husika;

Fursa ya Pili: Ni suala la demography & geography – Tanzania ni nchi kubwa kuliko zote ndani ya EAC, lakini pia ni nchi yenye watu wengi zaidi kuliko nchi nyingine zote za EAC; Kwa mfano, karibia 33% ya wananchi wa EAC ni watanzania (Changamoto ikibakia kujenga a strong Human Capital Base); Pia Nguruvi3 - takribani 52% ya ardhi ya EAC ipo Tanzania; Lakini pamoja na ukubwa wa eneo la ardhi na idadi kubwa ya watu kuliko nchi zote za EAC, bado Tanzania ina eneo kubwa sana la ardhi available kwa ajili ya watu wake kuitumia kikamilifu katika uchumi wa EAC, tofauti na nchi nyingine shiriki za EAC ambazo zina uhaba wa ardhi; Hii ni kwa sababu tofauti na nchi nyingine shiriki (EAC), Tanzania has the smallest population density (47 people per square kilometers), tofauti na Rwanda ambayo inayoongoza (403 people per sqkm), ikifuatiwa na Burundi (301 people per square km), huku Uganda ikiwa na (167) na Kenya (71); Sio ajabu Tanzania inazidi kuwa kimbilio la waganda, wakenya na wanyarwanda wengi linapokuja suala la umiliki wa Ardhi, kwani Tanzania tuna a commanding advantage juu ya availability & usage of Land for development; Nguruvi3 amelijadili hili kwa kina katika nyakati tofauti;

Mbali na masuala ya ardhi kubwa na idadi ya kubwa ya watu, Tanzania also has the largest coastal line in the region, na tuna bandari tatu (huku ya nne ikiwa njiani kujengwa Bagamoyo); Ukiondoa mapungufu machache yaliyopo ambayo zaidi ni ya kisiasa/utawala wa ovyo, kiuchumi, kwa landlocked countries kama Rwanda, Burundi na Uganda kuna faida kubwa zaidi kutumia bandari za Tanzania kuliko Mombasa (Kenya); Ni kwa maana hii, Tanzania ina uwezo wa kugeuka kuwa the gateway kwa nchi za Maziwa makuu na afrika mashariki na kati to the rest of the continent and the world; Tunachotakiwa kufanya ni kuwekeza katika hard infrastructure (bandari, barabara, reli, nishati) & soft infrastructure (effective rules and regulations sambamba na strong and independent regulatory institutions); Kwa kutekeleza haya, hatitakuwa na sababu kwanini Tanzania tushindwe geuka kuwa ‘a major trade hub of East and Central Africa';

Uwepo wa Hard and Soft infrastructure ambazo zitapelekea nchi yetu kuwa a regional trade hub vitasaidia sana utatizi wa ajira kwa vijana kwani kutazaliwa several services to facilitate trade and economic activities kama vile – accommodation/real estate, financial services, maintenance (magari, majengo na miundombinu), food (migahawa, mazao ya chakula, matunda&#8230😉, fuel, n.k. Uboreshwaji wa sekta za nishati, telecommunications, zitageuza Tanzania sio tu kuwa ‘the regional trade hub', bali pia ‘the regional logistic hub'; Knoweledge economy ambayo ndio inatawala uchumi wa dunia kwa sasa hutegemea sana vitu hivi; Tukifanikisha haya, tutakuwa na fursa ya kutengeneza ajira nyingi sana kwa vijana tofauti na hali ya sasa ambapo tunategemea ajira ziletwe na mining and gas activities ambazo hizi kwa kawaida hazileti ajira nyingi kutokana na kuwa ‘capital intensive' investments, instead of ‘labour intensive; Kwa maana nyingine, tusidanganyane kwamba sekta ya gas/oil zitaleta ajira ya maana Tanzania;

Fursa ya Tatu: Ni suala zima la rasilimali ambapo kwa mfano, Tanzania ina energy potentials zaidi ya nchi zote shiriki za EAC kwa ujumla, by 30%; Hii inatufanya tuwe na fursa ya kugeuza Tanzania kuwa the region's energy powerhouse; Vile vile kama tulivyojadili juu ya suala la rasilimali ‘ardhi', tuna ardhi kubwa yenye rutuba kuliko nchi nyingine zote za EAC, hivyo kuwa na fursa ya kugeuza Tanzania kuwa ‘a break basket' ya Eastern, Central and Southern Africa, hivyo kuweza ongeza vipato vya wakulima wetu, na taifa kwa ujumla;


Itaendelea…
 
Naam! Mchambuzi, shukran sana
Nichangie kidogo kuhusu proliferation ya regional blocks. Nakubaliana nawe kabisa kuwa wingi haujaweza kusaidia lengo.Mfano, kuna NEPAD ingawa si regional block kimtazamo wa dunia ni regional block ya Africa ambayo sioni matunda yake

COMESA, PTA, SADC na nyingine nyingi nadhani zinaleta ugumu kwa nchi wanachama siyo katika resources tu bali decision making. Nakumbuka kulikuwa kuna overlapping kubwa ya Tanzania kuwa SADC na EAC, suluhu ikawa kujitoa COMESA.

Kwa upande mwingine nadhani proliferation inachangiwa sana na poor performance. Kwa mfano, ECOWAS ni moja kati ya block kongwe Afrika, ukiangalia wameweza ku achive nini economically sidhani tunaweza kujivunia lolote. Zaidi ni kisiasa.Pengine hilo linachagiza uundwaji wa block nyingine kama mbadala ingawa ni solution mbovu the least to say. Ni sawa na kumhamisha mgonjwa kitanda bila kutoa tiba muafaka.

Unajenga hoja kuhusu Tanzania kubaki EA, niliafiki hoja hii wakati najadili hoja za Zinedine kwa kuangalia geo-position, potential ya resource na ready market kwa uchache. Ukataka turudi katika glory ya 1960-90"s
Kwa mtazamo wako nimeona hoja ya sisi kupoteza leadership katika block.
1. Je, tatizo ni nini hasa? Ni ukosefu wa soft infrastructure au ni lack of leadership

Kuna uwezekano wa kuwa na soft infrastructure kukakosekana leadership, na kuna uwezekano wa kuwa na leardership isiyoweza kuaandaa soft infrastructure.
Lipi hasa ni tatizo.

2. Umejenga hoja kuwa tunaweza kuwa vinara EA kama honest broker jambo ambalo ni kweli kabisa. Ukasema ni bora kujijenga katika misingi hiyo kuliko kusubiri kuburuzwa na south Afrika
Swali : Ni kipi bora kushindana ili tufikie namba moja(compete to attain number one) au kuwa kinara kwa majaaliwa tu ''by default'

3. Je huduma za jamii haziwezi kuwa eneo la kutusaidia pia.

ahsante
 
Mchambuzi na Nguruvi3 ni waalimu wazuri, kama mko vyuoni bila shaka wanafunzi wenu wanaenjoy sana. Shukrani nyote. Nitarudi mara nyingine ila naomba nichangie kidogo tu.

Katika Bandiko Na. 331, Mchambuzi ulitoa swali tata sana juu ya wapi Tanzania ina Comparative Advantage baina ya SADC na EAC (aidha specific au general). Tunashukuru kwamba umekuja kufafanua vizuri kwenye Bandiko Na. 335 (ambalo nimekosa muda wa kulisoma in detail, nadhani nitarejea tena wakati mwingine). Ila kuna Jambo moja la msingi uliloainisha kwneye Bandiko hilo ambalo nimeliona kwa haraka, na ndilo lililonifanya niwe na idea niliyoitoa hapo awali kwamba Tanzania isijitoe popote miongoni mwa Jumuiya hizi mbili. Regional Trade Hub na Regional Logistic Hub niongeze na nyingine Regional Tourist Hub.

In long run, huko ndipo Tanzania inatakiwa ijielekeze. Ukiangalia haraka haraka, mgawanyo wa hizi Hub kama vile unaonyesha kwamba Regional Trade Hub ni Dar(kupitia Bagamoyo Mega Port+ Central Line); Regional Tourist Hub ni Arusha na Regional Logistic Hub huenda Mtwara ambapo mkazo unaweza kuwa ni kwenye masuala ya Gesi na bidhaa zake ingawa inawezekana pia ikawa DAR given that, Serikali itakuwa tayari kupisha Dar uwe mji wa Kibiashara zaidi na kuhamisha Makao makuu yake japo Tanga (kama haja yao Bahari ambako kule Dododma haipo).

Mgawanyo huu ambao umetokana na God-given Strategic position ya Tanzania, utabaini kwamba Tanzania haiwezi kuepuka kuwa mwanachama wa Jumuiya zote mbili. Na kwavile SADC haina dalili za kufikia kuwa na Customs Union for long time to come (Kwani sioni dalili za kuiua SACU ambayo ni kongwe tena ina tariff Bands nyingi sana ukilinganisha na EAC au COMESA). Vilevile, kwa upende wa SADC, vyovyote ilivyo South Afrika ni Pioneer asiyehitaji kuchokozwa, kama Korea walivyoacha kumchokoza Japan katika maendeleo yao. Tutumie mazingira yetu kupambana na hawa wadogo, lakini Durban Port-hatuiwezi wala hatutaiweza kwa kuwa ile imeshikwa na wajomba-Whites japo panapo majaaliwa ya kujengwa kwa Bagamoyo Port, itakuwa kubwa kuliko Durban, ila si rahisi kuwa Busy kama Durban.

Ni kweli overlapping membership katika Afrika hata kwingineko ulimwenguni ni changamoto kubwa ya hizi RTAs. Hali inazidi kuwa mbaya baada ya kuongezeka kwa Bilateral Arrangements ambazo hazina dalili ya kupungua. Mwingiliano huu unasumbua sana kwenye kuweka hivyo vigezo vya kuijua bidhaa uasili wake (Rules of Origin). Lakini, kinachoumiza kichwa na kuleta matumaini mapya, uzalishaji sasa hivi hauna sura ya "Whollly Produced" badala yake unafanyika kwa Regional Networking Production/Global production chain. Hali hii ya uzalishaji italeta taratibu mpya za matumizi ya hii kitu RoO kwasababu huenda kukakosekana nchi moja pekee ambayo itakuwa na over (let say 40%) ya uasili wa uzalishaji wa bidhaa hiyo au baadhi ya nchi ambazo uzalishaji umepitia kuwa-qualified kuruhusiwa na Bloc area flani. Kwa hiyo hizi overlapping zitapelekea kuwapo kwa "Disguise of Breissing" au "Supply creates its own demand"(Say's Law).

Kwa kuwa Network Production bado inaonekana kuwa mbali kwa Afrika, namna rahisi ya kukabiliana na hizi Overllaping membership ni kuimarisha non-customs revenues na kisha ku-push customs unions for individual RTAs. Kwa vile Taratibu haziruhusu Nchi moja kuwa member wa Customs Union mbili vinginevyo ziwe na similar customs procedures, maana yake ni kwamba nchi za Kiafrika zitalazimika ku-harmonize internal & customs procedures zao ili ziwe katika "Common" Customs Union kuwa na internal free movements of goods. Hapa ndio utakuja kuona wajibu wa Tanzania kuwa na mkakati madhubuti wa kuwa na Hizi Hub ulizozizungumzia Mchambuzi.

Kwa msingi huu, Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo, Ujenzi wa Reli ya Kati na Ujenzi wa Bandari ya Mtwara na Ujenzi wa Reli huko Kusini kuziunganisha na Nchi za Kusini za Kusini Magharibi pamoja na ujenzi wa miundombinu ya Kisasa na yenye kuvutia kule Arusha, Mara kwa ajili ya Utalii ni mambo yanayotakiwa kuwa kipaumbele kama Serikali yetu ingekuwa inaona miaka 50 Ijayo. Kuiteua Arusha kuwa "Real Tourism Hub" yenye facilities za kisasa na ujenzi wa Bagamoyo Mega Port ni kutengeneza comparative advantages za Regional economic Hub. Kwani imekuwa proved kwamba comparative Advantage is dynamic term that can be created iwapo nchi itaamua na kuitengeneza-sio god-given. By the way God-given comparative advantage nyingi hususan Afrika hazijaisaidia Afrika.

Aidha, kuongezeka kwa Taasisi za elimu ya juu na udahili ni tumaini jema kwa kutengeneza nguvukazi ya kutosha katika miaka michache ijayo-given mkazo utawekwa kwenye ubaora wa elimu tuitoayo bdala ya wingi ambao katika miaka kumi iliyopita tumejitahidi.
 
Naam! Mchambuzi, shukran sana
Nichangie kidogo kuhusu proliferation ya regional blocks. Nakubaliana nawe kabisa kuwa wingi bhaujaweza kusaidia lengo.Mfano, kuna NEPAD ingawa si regional block kimtazamo wa dunia ni regional block ya Africa ambayo sioni matunda yake

COMESA, PTA, SADC na nyingine nyingi nadhani zinaleta ugumu kwa nchi wanachama siyo katika resources tu bali decision making. Nakumbuka kulikuwa kuna overlapping kubwa ya Tanzania kuwa SADC na EAC, suluhu ikawa kujitoa COMESA.

Kwa upande mwingine nadhani proliferation inachangiwa sana na poor performance. Kwa mfano, ECOWAS ni moja kati ya block kongwe Afrika, ukiangalia wameweza ku achive nini economically sidhani tunaweza kujivunia lolote. Zaidi ni kisiasa.Pengine hilo linachagiza uundwaji wa block nyingine kama mbadala ingawa ni solution mbovu the least to say. Ni sawa na kumhamisha mgonjwa kitanda bila kutoa tiba muafaka.

Unajenga hoja kuhusu Tanzania kubaki EA, niliafiki hoja hii wakati najadili hoja za Zinedine kwa kuangalia geo-position, potential ya resource na ready market kwa uchache. Ukataka turudi katika glory ya 1960-90"s
Kwa mtazamo wako nimeona hoja ya sisi kupoteza leadership katika block.
1. Je, tatizo ni nini hasa? Ni ukosefu wa soft infrastructure au ni lack of leadership

Kuna uwezekano wa kuwa na soft infrastructure kukakosekana leadership, na kuna uwezekano wa kuwa na leardership isiyoweza kuaandaa soft infrastructure.
Lipi hasa ni tatizo.

2. Umejenga hoja kuwa tunaweza kuwa vinara EA kama honest broker jambo ambalo ni kweli kabisa. Ukasema ni bora kujijenga katika misingi hiyo kuliko kusubiri kuburuzwa na south Afrika
Swali : Ni kipi bora kushindana ili tufikie namba moja(compete to attain number one) au kuwa kinara kwa majaaliwa tu ''by default'

3. Je huduma za jamii haziwezi kuwa eneo la kutusaidia pia.

ahsante


Mkuu Nguruvi3,

Samahani kwa kutorudi mapema tofauti na nilivyoahidi; nikianzia na swali lako hapo juu, binafsi nadhani tatizo la msingi ni katika maeneo yote mawili: Kwanza ni lack of soft infrastructure na pili ni lack of leadership; suala la soft infrastructure ni kama nilivyojadili na chanzo cha hili ni lack of political will; Pili ni suala la leadership, tunapwaya sana katika hili, na sababu kubwa ya msingi kwanini tumepoteza leadership katika suala zima la EAC ni kwamba hatuna "confident engagement" tofauti na enzi za mwalimu; Dr Mwakyembe aliwahi jadili hili bungeni wakati wa mchakato wa kuchagua wabunge wa EAC; Dr Mwakyembe alisema hivi:

We should not hide from the fact that Tanzania's status in EAC has taken a hit in recent years because we have been sending incompetent people to represent us"

Tofauti na miaka ya Mwalimu, Tanzania haipo tena as enthusiastic na EAC regional integration na ni moja ya sababu kubwa kwani the project inasua sua kwa ujumla wake; Katika ngazi zote za leadership, hakuna confident engagement bali timid defensiveness - mara tunatoza ushuru magari kutoka kenya na kupelekea kufungwa kwa mpaka maeneo ya Taveta mwanzoni mwa 2012; hii ilikuwa ni kinyume na common market protocol, na hata waziri sitta alilikemea hilo; mwaka 2011 tukapiga marufuku exports ya nafaka kwa hoja kwamba it was unregulated trade, sasa why not regulate it? Unregulated trade ina thamani kubwa (in dollar terms) zaidi ya regulated trade in this trading block; mwishoni mwa mwaka 2011 at a summit in Bujumbura tukaogopa sana suala la political federation kwa hoja kwamba ardhi yetu itatumika vibaya na pia kuogopa suala la common defense pool; suala la ardhi pamoja na uzito wa hoja bado ni sisi wa kujilaumu, na ni kule kule kwenye suala la lack of soft infrastructure ambapo serikali yetu ingeweza kabisa kunufaisha wananchi iwapo ingefuata mapendekezo ya tume ya shivji juu ya migogoro ya ardhi in the 1994; mfano mwingine juu ya our timid nature katika EAC ni pale mahakama kuu ilipoingilia kati kesi kati ya east african development bank na kampuni moja ya kitanzania "blueline" ambayo ikifisadi dollar karibia milioni 140 na kupelekea EADB kuwa katika hatari ya kufilisika;

Kwa kweli hatuna haja ya kuwa waoga katika safari ya EAC integration kwani kama nilivyojadili katika uzi uliopita, tuna both comparative and competitive advantage relatibe to wenzetu wote; Hizi siasa za kulinda maslahi ya wananchi katika muktadha wa EAC huku tukipuuza maslahi hayo katika uchumi wa nyumbani ni unafiki tu wa viongozi; tunahitaji viongozi ambao sio apprehensive and
defensive bali wenye confidence katika engagement ya EAC integration;

Nitarejea kujadili zaidi suala la EAC vis a vis SADC...


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Zinedine,

Wazo kwamba Tanzania iendelee kuwa mwanachama wa EAC na SADC ni wazo zuri as long as kunakuwa na harmonization katika regional integration; Hii ni kwa sababu, moja ya changamoto kubwa zilizopo hivi sasa on ‘trade integration' ni suala la overlapping membership of several states katika COMESA, SADC, SACU na EAC; Nchi husika wamegundua kwamba overlapping membership bila ya kuwa harmonized ni harmful na sio helpful for regional integration; Kutokana na hili, ndio maana mwaka 2008, a tripartite summit baina ya SADC, COMESA na EAC iliundwa; Mwaka huo huo, kukafanyika makubaliano on a single free trade zone covering the 26 countries that covers these three regional economic blocks; Mwaka 2012, wakuu wa nchi husika (katika mkutano wa OAU) wakaamua to finalize the Tripartite Free Trade Area by 2014; Iwapo hii initiative itafanikiwa, the economic zone/trade zone will cover over 50% African Population and over 50% of its GDP; Swali linalofuatia ni je:

Hii harmonization itawezekana?

Ni mapema sana kubaini hilo lakini ukweli unabakia kwamba – major constraint is the lack of political will kwani hizi blocks zimekuwepo kwa muda mrefu sana lakini hazijasaidia lolote katika upanuzi wa biashara baina ya nchi za bara la Africa; Intra trade in Africa inaendelea kuwa sio zaidi ya 10% of the total trade, na hali hii imekuwa hivyo kwa miaka mingi sana;

Vinginevyo ‘Overlapping memberships' baina ya various regional arrangements ina gharama zake kubwa; Kwa mfano - negotiating resources and capacity zimekuwa stretched sana across the region; Kuna suala la administrative costs zinazohusiana na complex rules of origin kama tulivyojadili awali; Vile vile kuna suala la ‘multiple membership fees' ambazo zimekuwa very expensive to pay and maintain kwa nchi husika. Mbaya zaidi, conflicting objectives among rival arrangements (SADC, EAC, COMESA, SACU) zimechangia sana kusuasua kwa progress katika maeneo mengi; Ingawa leo hii, blocks zote zimekamilisha mchakato wa kuunda customs union (EAC,SADC, COMESA), inazidi kuwa wazi kwamba conflicts of membership ni suala linalohitaji ufumbuzi wa haraka, lakini POLITICALLY, this may prove difficult;
 

]Wanaduru, unaangalia namna ya kuboresha ukumbi ili mada ziwe endelevu, zenye mahaitimisho.
Pia kuwepo na mada katika eneo lingine ambazo zitakuwa ni za hoja zinazojitokeza.Katika jitihada zingine muda si mrefu baadhi ya mada zitaonekana katika magazetini .Taratibu zitakapokamilika tutawafahamisha
EAC
Kuhusu mada inayohusu sakata la EAC tutaendelea na kile kilichojitokeza kwa wiki mbili tatu.
Kwanza ni kauli za katibu mkuu wa EAC Dr Sezibera kuhusu Tanzania.

Kauli zake ni za kuishambulia Tanzania bila kujibu hoja zinazotolewa na Tanzania.
Mathalan, Tanzania inahoji iweje kuwepo na mikutano bila sekretariati ya Jumuiya kutaarifiwa.

Majuzi Sezibera ametoa mwaliko kwa Tanzania kuhudhuria mkutano unaohusu wahamiaji haramu Kigali.
Kwa hali isiyotegemewa waziri Sitta wa masuala ya EA ameshindwa kuhudhuria kwasababu za kutathmini operesheni ya Kimbunga.

Tanzania haitaki suala hilo liwe la Jumuiya. Kuondoa wahamiaji haramu ni haki ya kila mwanachama kwa kuzingatia ukweli kuwa hakuna makubaliano ya mataifa haya kuhusu kuhama kwa watu na mitaji.
Yaliyopo ni makubaliano ya baadhi ya nchi ambayo hayana nguvu za kisheria bali MoU.

Haieleweki kwanini Dr Sezibera ameingia katika ushabiki badala ya utendaji.
Hili linaongeza hofu ya Jumuiya wakati zikijipanga kuwa na pesa ya pamoja( Single Currency .
Dr Sezibera alipaswa kuangalia matatizo ya EU kabla ya kutanguliza masilahi yake binafsi au ya nchi yake.


Kwa mfano, nchi za Ujerumani na Ufaransa zimeanza madai ya kurudi kwa pesa(Dotchi Mark na Franca) kutokana na mdororo wa uchumi ukanda wa Ulaya (Eurozone) unaoziathirika zaidi kama watoaji(donors).

Nchi za EU ambazo zimefikia kiwango cha watu kuhama pamoja na mitaji yao( Human and capital movement) bado kuna matatizo, sijui EAC inayoelekea katika muungano wa kifedha (monetary union) ipo katika hali gani.

Zaidi ya mitaji na watu ni lazima kuwe na uwiano katika shughuli zinazohusu mambo ya kodi na ushuru, uchumi, benki n.k. kama msingi wa kuwa na muungano wa kifedha.

Kitu cha muhimu kukumbuka ni kuwa muungano wa kifedha (EAMU) unahusu sera za nchi wanchama na ni msingi wa kutengeneza taratibu 'policy ya nchi hizo'. hivyo EAMU lazima ifanywe kwa uangalifu na utashi wa kisiasa 'political will' ili kuepuka ya Greece na Spain

Wakati Burundi nayo ikilalama kuhusu kutengwa hatudhani kuwa muda muafaka umefika kufanya baadhi ya mambo kwa kukurupuka. Kunaonekana wazi kutokuwepo kwa umakini bali msukumo wa kisiasa tu.

Inawekanaje kuwe na na visa ya pamoja bila kuangalia mapato na matumizi yanayotokana na visa hizo?
Hatudhani kuwa mapato yatokanayo ni kidogo, la hasha! vinginevyo mwanachama wa KKK bwana Kenyatta asingekataa visa ya pamoja ya washirika watatu. Hadi sasa upo mzozo na Kenya inahoji kuhusu mgawanyo wa mapato utokanao na utalii. Ni hoja hiyo hiyo Tanzania iliyo nayo.

Haiwezekani mzigo wa kutunza vyanzo vya visa ambavyo ni utalii uachiwe nchi husika huku mapato yakigawanywa sawa sawa!

Ni fungu gani litatumika kuhudumia maliasili hizo. Leo Tanzania inapambana na majangili kwa gharama kubwa, vipi kirahisi tu kuwe na visa ya pamoja tukifahamu Uganda, Burundi na Rwanda hazina vyanzo vikubwa kuliko Tanzania na Kenya.


Kwa maneno mengine kusita kwa Kenya kunatokana na kutokuwepo kwa Tanzania.
Visa ya pamoja ni muhimu sana kwa Kenya Tanzania ikiwemo, vinginevyo Kenya inapoteza kwa nchi nyingine na huo ni mvutano uliopo kichini chini.


Duru tunasisitiza kuwa EAC ijengwe kwa misingi ya wananchi na si viongozi.
Kasi inatakiwa bila kuathiri uangalifu. Kuna kasi zingine za kuburuzana hasa katika mambo ya uchumi.
Nchi hizi zinategemeana sana na hatudhani kuwa uwepo wa EAC ya 'kanda' peke yake unatosha bila kuwepo kwa EAC kama block.


Katika wakati huu EAC inahitaji kiongozi imara, mkweli na mwenye maono.
Duru inasikitishwa na utendaji wa sasa wa Dr Sezibera uliojikita katika ushabiki zaidi ya taaluma, weledi na maono.

Pamoja na matatizo yanayoikumba EAC, katibu mkuu wa sasa ni tatizo kubwa kuliko matatizo yaliyopo na suluhu ya kudumu ni kumuondoa ili apatikana mwingine kama waliotangulia. Kuendelea kuwa na Sezibera hakutazaa matunda zaidi ya kuchochea migogoro na kuvunjika kwa EAC kutokana na kushindwa kuhimili mikiki ya kisiasa.

Tusemezane

(Katika siku zijazo tutaangalia kwa kina udhaifu wa hotuba ya mwezi ya JK, mzozo wa rasimu na jinsi CCM itakavyoshindwa kutokana na mbinu chafu na anguko la muungano mikononi mwa JMK)
 
Back
Top Bottom