Mkuu
Nguruvi3,
Asante kwa swali lako muhimu sana
#332 ambapo umeuliza hivi:
Mkuu
Mchambuzi nakubaliana na complexity iliyopo. Kutokana na bandiko lako naona kila mwanachama ana rangi zaidi ya moja. Wakati tunasubiri uendelee, swali ni kuwa katika multiple organization kama ilivyo inawekanaje Tanzania ikawa na block moja kwa kulinganisha na wanachama wengine.
Kimsingi, mjadala wangu unalenga kutafuta majibu kwa swali hili muhimu; Nitajitahidi kujadili suala hili, nikianza na hoja zifuatazo:
Nadhani tutakubaliana kwamba - sehemu kubwa ya Sura ya bara la Afrika (hasa sub Saharan Africa) ni presence of a large number of very small landlocked countries, ambazo zinategemea sana nchi jirani kiuchumi, hasa zile zenye access to the sea, a larger market (population), n.k. Ni kwa mantiki hii, nchi hizi ndogo ndogo zinazokosa mambo haya muhimu (access to sea, larger market n.k) hulazimika kujihusisha na regional integration kwa njia moja au nyingine; Hii ndio sababu ya msingi kwanini regional economic communities nyingi zimekuwa zikiibuka karibia kila kona ya bara la afrika kwa nia moja tu – kuhakikisha nchi za namna zinapambana na changamoto nilizoainisha hapo juu; Leo hii, karibia kila nchi zote za Sub Saharan Africa ni wanachama wa angalau ‘one regional economic block'; Such proliferation ina madhara mengi kiuchumi kuliko faida kwani it has been proved over and over again kwamb - multiple membership of regional economic blocks actually hinders regional integration; it doesn't foster regional integration kama wengi wanavyopenda kuamini/aminishwa; Ni kwa maana hii, kumekuwa na efforts mbalimbali barani Africa (source ikiwa ni nchi wahisani) zinazolenga kutatua tatizo hili, hasa katika kutafuta a common ground between different regional integration initiatives; Yapo makubaliano mbalimbali ambayo yameshafikiwa among various regional economic blocks in Africa, na nikipata muda nitakuja toa ushahidi juu ya suala hili;
· Iwapo the way forward sasa ‘is an attempt to harmonize initiatives zilizopo, kwanini Tanzania tusisome alama za nyakati na kuwa ahead of time kwa kufanya maamuzi magumu mapema badala ya kupoteza tu fedha za walipa kodi pamoja na fursa nyingi za kibiashara na kiuchumi kwa ujumla?
Moja ya sababu kubwa kwanini intra regional trade barani Afrika imekuwa ikisua sua ni kutokana na such proliferation, kwani multiple membership of regional economic blocks imposes high costs in time, energy and resources kwa serikali husika na hulazimisha serikali hizo to juggle between competing regulations – mfano rejea mjadala wangu
#325 on complex rules of origin kutokana na overlapping membership in preferential trading arrangements; zimejadiliwa factors nyingine zinazochangia kusua sua kwa intra regional trade kama vile miundombinu, low manufacturing capacity n.k, lakini ukweli unabakia kwamba hata haya yakitatuliwa, bado suala la soft infrastructure - effective rules and regulations sambamba na strong and independent regulatory institutions, zitaendelea kuwa kikwazo, na hizi zina uhusiano wa moja kwa moja na suala la ‘rules of origin';
Iwapo tutakubaliana kwamba moja ya sababu zinazopelekea nchi za Afrika kuwa members of multiple regional economic blocks ni pamoja na changamoto zinazotokana na nchi husika kuwa ‘landlocked', uwepo wa ‘idadi ndogo ya watu' population/market), ukosefu wa ardhi yakutosha, ukosefu wa natural resources, je:
· Tanzania tunakabiliwa na matatizo katika haya?
Sidhani, hivyo sioni sababu kwanini Tanzania tuendeleaa kuiga wenzetu wenye matatizo haya wakati sisi tuna fursa nyingi kuliko changamoto katika suala husika; Ni muhimu tukajipongeza kwa kujiondoa COMESA huko nyuma kwani uanachama wake ulikuwa hauna tija relative to uanachama wa economic blocks nyingine; uamuzi wa kujitoa ulikuwa ni wa busara sana;
Kuna wakati kulikuwa na umuhimu kwa Tanzania kuwa mwanachama wa block zaidi ya moja – SADC na EAC lakini kwa sasa "wakati huo umepitwa na wakati"; Katika kipindi cha nyuma, EAC ilivunjika baada ya wanachama kupishana kimtazamo na kimwono, lakini kwa vile wanachama wan chi za mstari wa mbele kusini mwa afrika walikuwa na lao moja – ilikuwa ni rahisi kwa Tanzania kuwa mwanachama wa SADC kuanzia 1992, huku tukiwa ni kinara wa jumuiya hii; Baada ya EAC kurudi, tumejikuta kwenye two regional economic blocks ambazo kimsingi imposes costs in time, energy and resources kwa serikali yetu; Mbali ya kuwa na shared history na wanachama wengine wa SADC, binafsi nadhani Tanzania ina fursa zaidi kiuchumi kwenye EAC kuliko SADC, kwani unlike SADC, kwenye EAC Tanzania itarejea kwenye drivers seat badala ya kuburuzwa na South Africa, Angola, Mauritius and increasingly Mozambique; Nitarejea baadae katika hili la faida za EAC vis a vis SADC kwa Tanzania;
Vinginevyo, iwapo tunakumbuka vyema, miaka ya 1960s & 1970s, Tanzania ilikuwa ni champion & driver of regional integration in Africa ambapo chini ya uongozi wa Mwalimu Nyerere, not only we drove the narrative of regional integration, bali pia to a large extent, we controlled it – kwa mfano rejea influence ya Mwalimu Nyerere on Pan African Freedom Movement For East and Central Africa (PAFMECA) from late 1950s. Nyerere was the greatest believer of African Unity who believed in step-by-step realization of that Unity; Kwa mwalimu, it didn't matter whether mchakato unaanza na Siasa au Uchumi, kwa Mwalimu, kikubwa ilikuwa ni ulazima wa safari ya muungano wa afrika kufuata ‘baby steps', tofauti na mtazamo wa Kwame Nkrumah; Mwalimu alijikuta in a serious clash (kimtazamo) na Kwame Nkrumah, kwani Nkrumah aliamini - forcefully for continental political unity based on only one ideology – Pan Africanism; Mwanzoni Nkrumah alionekana kuwa na mtazamo wenye manufaa kwa Afrika kuliko Nyerere, hivyo kuungwa mkono kwa wingi, lakini muda sio mrefu, radicalization of african unity kwa mtazamo wa Nkrumah ukaanza kuonekana kutofaa, na badala yake incremental approach chini ya Nyerere ikawa embraced, na busara za Mwalimu zinaendelea kutumiwa hadi leo;
Nianze kwa kujadili kwanini nadhani kuna fursa nyingi zaidi EAC kuliko SADC:
Fursa ya Kwanza: Tanzania ina kila sababu ya kuchaguliwa kuwa a political capital ya EAC na nchi washiriki pamoja na wale wote wanaosadia shirikisho la EAC lisonge mbele, kwa mfano EU n.k; Tanzania ina uwezo wa kuwa the most ‘honest broker' iwapo matatizo yanajitokeza katika nchi za maziwa makuu; Kwa mfano, tumeona jinsi gani Tanzania iliteuliwa kuwa makao makuu ya mahakama ya kughulikia wahalifu… - Rwanda's genocide; Vile vile historically, we have mediated conflicts nyingi sana & kuwa viewed kama a neutral stakeholder – kwa mfano mwalimu Nyerere na mchakato wa kuleta amani nchini Burundi in the 1990s, kuikomboa Uganda kutoka mikononi mwa Nduli iddi Amnin (1978/79, uteuzi wa Mkapa kusimamia mazungumzo ya amani nchini Zimbabwe - mwanachama wa SADC, 2006), involvement ya Tanzania kutatua the post – elections crisis nchini Kenya (Kibaki vs Raila saga) miaka kadhaa iliyopita n.k; Mbali ya haya, Pia Tanzania inatambulika na kuheshimika sana katika kusimamia haki, usawa, umoja, udugu, na kujitoa mhanga kwa ajili ya haya - kwa mfano suala la ukombozi Kusini mwa afrika, na pia
Nguruvi3 - uamuzi wa Tanganyika kujitolea kupoteza utaifa wake kwa ajili ya Zanzibar, 1964;
Kwa maana hii, we have enough "political capital" to enable us mediate changamoto zozote zitazojitokeza katika EAC; Kwa mfano, moja ya destabilizing factors in the region ni ugomvi baina ya sudan kusini na sudan kaskazini, na Tanzania ina uwezo mkubwa wa kuwa msimamizi wa mazungumzo ya amani hasa kwa vile hatupakani na nchi hizi, lakini muhimu zaidi, tofauti na washiriki wengine wakubwa wa EAC - Kenya na Uganda ambao wamesha chagua upande wa kuegemea katika mgogoro wa Sudan, Tanzania haijachagua upande wowote katika sakata husika;
Fursa ya Pili: Ni suala la demography & geography – Tanzania ni nchi kubwa kuliko zote ndani ya EAC, lakini pia ni nchi yenye watu wengi zaidi kuliko nchi nyingine zote za EAC; Kwa mfano, karibia 33% ya wananchi wa EAC ni watanzania (Changamoto ikibakia kujenga a strong Human Capital Base); Pia
Nguruvi3 - takribani 52% ya ardhi ya EAC ipo Tanzania; Lakini pamoja na ukubwa wa eneo la ardhi na idadi kubwa ya watu kuliko nchi zote za EAC, bado Tanzania ina eneo kubwa sana la ardhi available kwa ajili ya watu wake kuitumia kikamilifu katika uchumi wa EAC, tofauti na nchi nyingine shiriki za EAC ambazo zina uhaba wa ardhi; Hii ni kwa sababu tofauti na nchi nyingine shiriki (EAC), Tanzania has the smallest population density (47 people per square kilometers), tofauti na Rwanda ambayo inayoongoza (403 people per sqkm), ikifuatiwa na Burundi (301 people per square km), huku Uganda ikiwa na (167) na Kenya (71); Sio ajabu Tanzania inazidi kuwa kimbilio la waganda, wakenya na wanyarwanda wengi linapokuja suala la umiliki wa Ardhi, kwani Tanzania tuna a commanding advantage juu ya availability & usage of Land for development;
Nguruvi3 amelijadili hili kwa kina katika nyakati tofauti;
Mbali na masuala ya ardhi kubwa na idadi ya kubwa ya watu, Tanzania also has the largest coastal line in the region, na tuna bandari tatu (huku ya nne ikiwa njiani kujengwa Bagamoyo); Ukiondoa mapungufu machache yaliyopo ambayo zaidi ni ya kisiasa/utawala wa ovyo, kiuchumi, kwa landlocked countries kama Rwanda, Burundi na Uganda kuna faida kubwa zaidi kutumia bandari za Tanzania kuliko Mombasa (Kenya); Ni kwa maana hii, Tanzania ina uwezo wa kugeuka kuwa the gateway kwa nchi za Maziwa makuu na afrika mashariki na kati to the rest of the continent and the world; Tunachotakiwa kufanya ni kuwekeza katika hard infrastructure (bandari, barabara, reli, nishati) & soft infrastructure (effective rules and regulations sambamba na strong and independent regulatory institutions); Kwa kutekeleza haya, hatitakuwa na sababu kwanini Tanzania tushindwe geuka kuwa ‘a major trade hub of East and Central Africa';
Uwepo wa Hard and Soft infrastructure ambazo zitapelekea nchi yetu kuwa a regional trade hub vitasaidia sana utatizi wa ajira kwa vijana kwani kutazaliwa several services to facilitate trade and economic activities kama vile – accommodation/real estate, financial services, maintenance (magari, majengo na miundombinu), food (migahawa, mazao ya chakula, matunda…
😉, fuel, n.k. Uboreshwaji wa sekta za nishati, telecommunications, zitageuza Tanzania sio tu kuwa
‘the regional trade hub', bali pia
‘the regional logistic hub'; Knoweledge economy ambayo ndio inatawala uchumi wa dunia kwa sasa hutegemea sana vitu hivi; Tukifanikisha haya, tutakuwa na fursa ya kutengeneza ajira nyingi sana kwa vijana tofauti na hali ya sasa ambapo tunategemea ajira ziletwe na mining and gas activities ambazo hizi kwa kawaida hazileti ajira nyingi kutokana na kuwa ‘capital intensive' investments, instead of ‘labour intensive; Kwa maana nyingine, tusidanganyane kwamba sekta ya gas/oil zitaleta ajira ya maana Tanzania;
Fursa ya Tatu: Ni suala zima la rasilimali ambapo kwa mfano, Tanzania ina
energy potentials zaidi ya nchi zote shiriki za EAC kwa ujumla, by 30%; Hii inatufanya tuwe na fursa ya kugeuza Tanzania kuwa the
region's energy powerhouse; Vile vile kama tulivyojadili juu ya suala la rasilimali ‘ardhi', tuna ardhi kubwa yenye rutuba kuliko nchi nyingine zote za EAC, hivyo kuwa na fursa ya kugeuza Tanzania kuwa
‘a break basket' ya Eastern, Central and Southern Africa, hivyo kuweza ongeza vipato vya wakulima wetu, na taifa kwa ujumla;
Itaendelea…