Inaendelea....
Tumesema kuwa NEC na CC ndizo nguzo za chama na kama utazikamata basi utakuwa salama. Vita ndani ya UVCCM, UWT na Wazazi ni vita ya makundi na si ya watu. Kwa mfano, UWT kuna Sofia Simba ambaye ni msemaji mku wa kambi ya mtanadao -mafisadi na Anne Kilango aliye katika kundi la CCM wazee.
Unapokuwa na wajumbe wa NEC muhimu kama hawa utakuwa umefanikiwa sana. Maamuzi yao yataathiri chaguzi zote za ngazi za chini na kuleta wajumbe wengi zaidi ndani ya NEC.
Katika mchakato huu kuna watu ambao ni waathirika wa NEC na CC watake wasitake. Tunakumbuka kuwa Kigwangalla alikuwa mshindi wa tatu, baada ya Bashe kuenguliwa kwa kigezo cha Uraia. Bashe ni mfanyakazi katika moja ya mashirika ya watuhumiwa nchini. Kugombea kwake kulilenga kuongeza nguvu ndani ya bunge na chama kama sehemu ya mtandao.
Kuondolewa kwake kulikuwa 'technically' na wala haikukusudiwa. Hili lilikuwa kuepusha kashfa kama ingedhihirika vingenevyo.
Lucas Selelii ndiye alikuwa wa pili kwahiyo alipaswa kuchukua nafasi hiyo. Yeye alienguliwa kwasababu alikuwa mwiba mkali ndani ya bunge. Kuenguliwa kwake kulifanyika ndani ya CC iliyokuwa inamilikiwa na wathumiwa wa ufisadi. Ilikuwa ni foul play kubwa sana. Kwanza alichezewa shere na Yusuf Makamba baada ya kugawa jimbo aliporuka kikwazo hicho hakuvuka ndani ya CC.
Kigwangalla akachukuliwa kwasababu ya uhusuiano wake na 'jikoni'. Ni utaratibu huo huo wa kupitia NEC na CC Ulimweka Kigwangalla madarakani kama mbunge ndio utatumika kummaliza. Utatumika kwasababu ya misimamo yake juu ya serikali.
Kwa hili Kigwangalla ni 'victim' na ngazi yake kisiasa inategemea majaliwa zaidi. Kwa bahati mbaya yeye hajielewi na tumesikia kashfa kama za vitumbua na kutishiana. Ukweli ni kuwa anacheza karata ngumu sana.
Deo Filikunjombe naye ni victim kwa misimamo yake ambayo mingi inalenga katika kusimamia kilicho kweli. Sina uhakika wa yeye kugombea popote, ukweli ni kuwa ni lazima aandae makazi ya siku zijazo maana kwa kutokuwa na kundi litalaomtetea ndani ya NEC au CC hatima yake ni maajliwa sana.
Makongoro Nyerere ambaye ni maarufu kwa 'kule site' wanasema mafisadi..... naye ni victim. Tofauti na wenzake yeye ana ngao ya jina kubwa na huenda kumwacha nje ya sytem kunaweza kuzua makubwa. Wamiliki wa CC na NEC kwasasa hapendi arudi katika uongozi, wakati huo huo wapo wanaotaka jina hilo libaki kama heshima kwa Nyerere. Ni kazi nzito kumuengua kwa mizengwe lakini tayari jitihada zinaendelea ili aenguliwe mapema huko Musoma kabla hajafika NEC au CC kukwepa lawama.
Nape Jnr, yupo matatani sana. Kijana huyu aliyekuwa na mtazamo wa kitaifa zaidi aliwahi kukorofishana na kinara wa mtandao mzee EL. Kwa vile umiliki wa NEC na CC ni wa mtandao naye alionja adha kwa kuenguliwa kutoka UVCCM technically. Si kuwa hakuna aliyekuwa anajua umri wake! la hasha, walimkatizia mbele kwa kutumia wingi wao katika vyombo vya maamuzi wakamtupa nje.
Nape aliporejea kama katibu mwenezi alianza kwa ari, nguvu na kasi mpya kwa kuwalenga mafisadi. Jitihada zake zimepigwa break kwasababu maamuzi ni ya CC na NEC na yeye hakuwa na usaidizi wa kutosha katika kufanikisha hili.
Ametuhumiwa kukivuruga chama na kwa kiwewe tu ameacha hoja za kitaifa zilizomjenga na kuishambulia Chadema kwa hoja za hovyo sana. Hili ni baada ya kushindwa kuwashughulikia mafisadi ndani ya chama chake wanaomiliki CC na NEC.
Majuzi NEC ilimtuhumu na kutaka sekretariati ifanyiwe mabadiliko ya kumondoa. Nguvu ya NEC na CC inaonekana
Ni nguvu hiyo inayotaka Wilson Mukama naye aondolewe kwa kushindwa kukiendesha chama. Mukama ndiye aliyetoa mapendekezo ya kuvunjwa kwa sekretariati zote zilizokuwa na wajumbe waliotokana na mafisadi au ushawishi wa mafisadi. Naye ni next victim
Wengine ni akina Mwambalaswa, Mwakyembe kwa uchache tu.
Lipo kundi ambalo litakuwa 'victim of circumstance' na ambalo haliwezi kuathirika moja kwa moja na uamuzi wa NEC au CC, au kuathirika kwao kunaweza kuwa na matatizo katika chama.
Mfano ni Magufuli ambaye kwa kutajwa tajwa kuhusu kuwania urais tayari alishaundiwa zengwe kuwa analeta kero kwa wananchi. Kuna watu kama akina Membe ambao kutajwa tajwa kwao kunaundiwa zengwe kwa vile si rahisi kuwa-deal moja kwa moja kwa kutumia NEC au CC.
Tumemsikia EL akisema wizara ya mambo ya nje ina matatizo huku akiwa amefanya ziara za balozi mbali mbali. EL anajua bajeti ya wizara ni ndogo, pamoja na udogo huo pia wizara haipati mgao stahiki. Maana yake ilikuwa moja kuanza kumchafua Membe kwasababu ni ngumu sana kupitia CC au NEC bila kuwa na ushahidi au zengwe la kutosha.
Lakini wasi wasi mkubwa wa EL ni kuwa CC na NEC inaweza kuja na watu tofauti kwa hiyo ni vema 'udongo ukauwahi ungali maji'.
Nadhani hadi hapa tunaona ni kwanini ni muhimu sana kuwa na nguvu katika chama kuliko serikali. Ubunge ni zao la chama, serikali ni zao la chama na chama ndicho kimeshika hatamu kwa mujibu wa CCM.
Mpambano uliopo wa uchaguzi wa chama si wa kupata viongozi wa kukivusha chama katika nyakati hizi ngumu, ni mkakati wakujipanga kwanza ndani ya vyombo vya CC na NEC ili kuwahangaikia 'waharibifu' kabla ya kuhangaika na wapinzani.
Mgombea wa CCM ajaye hatapatikana kwa merits bali nguvu ndani ya chama hasa CC na NEC.