Duru za siasa - Mgongano wa mawazo

Duru za siasa - Mgongano wa mawazo

JingalaFalsafa,
Katika mtazamo wangu mimi hakuna mtu asiyemtegemea mwenzake hata huyo mkulima Muhogo anakutegemea wewe kama mteja wa mhogo wake na ndi sababu tangulizi ya maamuzi yake kulima Mhogo, in fact hakutegemei wewe kumsaidia kuung'oa isipokuwa utegemezi wake kwako ni uzito wakazi yenyewe kwa thamanisho utakao upa mhogo wake. Kama isingekuwepo wewe mlaji basi asingelima ule mhogo ulomsinda kuung'oa.. Lengo kuu ni kutoshelez amahitaji ya jamii husika(demand). Hivyo mkulima wa mhogo ni tegemezi la wewe sio kumsaidia maana hakuna msaada wa bure bali mhogo wake upate kufika sokoni.. Ebu nakuomba fikiria mfano huu huu na Barricks.. Wao wamekuja tusaidia kuchimba mhogo wetu (dhahabu) halafu mhogo huo unakuwa wao au kulingana n na Ubeberu.. sana sana watatupa asilimia 49 nkwa sababu tu wametusadia kuung'oa na kuupeleka sokoni wakati wahitaji ni wao sio sisi. Je unatak kunambia Barricks wana kila haki ya kumiliki Mhogo wetu kwa sababu tu wametusaidia kuung'oa?..

Swala kubwa la kiuchumi ni malipo bora kwa msaada wako. utapimwa kulingana na thamani ya kazi, mali na juhudi ulloiweka ili ikuwezeshe nawe ukue kimaisha na sii kukutajirisha. Hivyo gharama zangu zote zinathamini msaada wako kwa kuelewa soko litaweza vipi kununua mhogo wangu na pengine hata wewe kunuua mhogo wangu ili ukailishe familia yako..Maana maisha riziki yako saa itatokana na huo mhogo wangu..

Dhana yangu kubwa ktk Ubepari ni kwamba maendeleo yoyote hutokana na ubunifu ktk kukidhi mahitaji. Ubunifu ambao unatazama mahitaji ya watu ktk mazingira na nyakati hivyo thamani ya ubunifu huo hauwezi kutajirisha isipokuwa kwa thamanisho la wanunuzi walokubali sio tu kununua bali wenye uwezo pia wa kununua mali hizo ili kukidhi mahitaji yao..Ni mzunguko usiokwisha lakini lazima uanzie mahala..

Sasa sema tunapopishana wengi ni ktk kutambua MAHITAJI na MATAMANIO. Dunia ya leo ktk Ubepari matamanio yamechukua nafasi kubwa sana kuwa ndio maendeleo lakini infact tunaweza kuishi pasipo matamanio hayo..Na matajiri wakubwa duniani wametokana na matamanio yetu badala ya mahitaji yetu. Leo hii shule zetu zinafundisha lugha ya kiingereza na kuthaminiwa kuliko elimu dunia yenyewe pamoja na kwamba Ujinga ndio adui yetu.

Matamanio ndio yametufanya tununue suti na saa za Gucci badala ya kutazama mahitaji ya nguo kujisetiri. Na ukitazama kwa makini dunia hii ya leo MATAJIRI wote wale asilimia moja wanaserve MATAMANIO na sii mahitaji yetu..Wale wanao serve mahitaji yetu ndio wanaitwa Middleclass wafanya biashara wadogo wadogo. Hivyo kimsingi tunaposema tuzalishe Middle class ina maana zaidi tuyachukue mahitaji yetu mbele ya Matamanio.

Hata ukitazama maradhi yaliyopo na yanayoongoza kuua yametokana na matamanio zaidi.. HIV, cancer
na maradhi mengi yametokana na matamanio zaidi ya ukiangalia malaria, Ukoma na Ndui halafu maajabu tumeacha kabisa ku deal na magonjwa yetu ya asili sasa hivi tunatibiwa ktk magonjwa ya matamanio zaidi na kwa gharama kubwa..Vita yetu sasa sio maradhi tu bali imejengeka hata ktk kupambana na Matamanio, na vita hii sidhani kama tutaishinda.

Mkuu wangu sisi wahitaji ndio tunamjenga tajiri, sisi ndio tunathaminisha rasilimali, juhudi na nguvukazi zote, sisi ndio tunathamisha hadi vito, madini na maliasili zote kwa matamanio yetu. Kifupi MHITAJI ndiye anayetengeza soko, anayewapa utajiri wenye ubunifu hata ktk maswala ambayo sii muhimu ktk maisha ya mwanadamu hivyo sisi wahitaji ndio huweka thamani ya mali, nguvukazi na wala sii tajiri ambaye kabla hajawekeza hututazama sisi akafanya business study ya btamaa zetu na tunahitaji nini kukidhi hizo tamaa kisha kupima uwezo wetu.

Si Ubepari ulomfanya China kutengeneza vitu cheap na vingine fake ila kunatokana na mahitaji yetu wenyewe. Demand, supply na Price vinaambata siku zote na hupevuka tu kuwa utajiri pale wahitaji wanapoweza kununua. Na maadam Riziki ya MTU ni MAHITAJI yake na hayapati ufumbuzi sehemu nyingine isipokuwa kwa binadamu mwenzake. Pengine swala kubwa la kuelewa kwa nini tunasoma ELIMU dunia ni kutuwezesha sisi kuwa wabunifu, kuwa na uwezo wa kufikiria jinsi ya kukidhi mahitaji yetu na sio kuwa msaada tutani (kuajiriwa) kumwezesha tajiri afanikiwe. Kama utatazama lengo la ajira ni kumwezesha mwenye mali kutajirika badala ya kuzalisha ili kukidhi mahitaji basi Ubinafsi utaanza na wewe maana unafikiria kumsaidia mtu ili nawe ufaidike kwanza badala ya kumsaidia mtu ili aweze kukidhi mahitaji ya jamii.

Hao wahindi 10 walioinuka ni wahindi walokwenda nchi za Marekani, Uingereza au Ujerumani na wakaungana kujenga nguvu ya kutoana. Leo hii wao wameshika chumi za nchi hizo paispo kumtumia mtu mweusi. Sisi wenyewe ndio hatua ushirika, hakuna mji wala nchi hata moja duniani utawakuta weusi wakishirikiana kubuni biashara au kuijenga jamii yao isipokuwa kila mmoja wao anafikiria UTUMWA ndio nafasi poekee aliowekewa hapa duniani. NI fikra na mawazo ya mtu mweusi ndiyo yanamweka ktk nafasi hiyo.. Akisema NO! basi sidhani kama kuna mtu anayemuweza mtu mweusi na wanajua wote..
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mkandara,

Asante sana kwa mchango wako mzuri; hoja zako zime stimulate my thinking, na naomba nijadili kidogo ingawa sitakuwa na mtiririko au mpangilio mzuri sana.

Kwanza, ni kuhusu neno 'AKILI'; nakubaliana na wewe kwamba tafsiri ya neno 'AKILI' ina utata, lakini mimi nadhani utata juu ya neno hili bado ungekuwepo hata kama dunia nzima ingekuwa inazungumza lugha moja tu; hii ni kwa sababu, hakimu kuhusu nani ana akili na nani hana akili, ni binadamu mwenyewe; Kwa mfano, umetaja neno 'SANITY' ambalo kwa uelewa wa jumla jumla, maana ya ‘Sane' - ni pale mtu anapoonekana kwamba he/she has a ‘SOUND JUDGEMENT', au ni mtu aliye ‘FREE FROM MENTAL DISORDER', au mtu ambae yupo ‘REASONABLE'. Lakini swali linalofuatia ni kwamba, ON WHOSE TERMS? Kwa bahati mbaya, HAKIMU juu ya nani ni SANE nani INSANE ni BINADAMU MWENYEWE/MTU, ambae anahusishwa na dhana tuliyoijadili i.e. Katiba za nchi nyingi (hata kwetu) zinaposema kwamba kabla ya mtu kushika nafasi fulani fulani za uongozi, ni lazima awe na akili timamu; je, tuna uhakika gani katika asilimia mia moja kwamba huwa tunachagua viongozi SANE (wenye Sound Judgement, walio Reasonable, walio Free from Mental Disorder)?

Tukiwa bado katika dhana hii ya ‘SANITY', je wanaotoa hukumu kwamba fulani ni ‘SANE au ‘INSANE', je kuna universal definition? Watu wanaotoa hukumu hii, je wote wamepimwa viwango vyao vya SANITY katika mazingira yanayofanana ili hukumu zao ziwe ‘Standardized'? Kwa maana nyingine, je, anaetoa hukumu hiyo nchini Marekani, mwingine nchini Australia, Canada, Ufaransa n.k, je wote hawa tumewapima viwango vyao vya SANITY ili tuwe na a standardized way to judge sanity and insanity? Hapa tusisahau pia kwamba mtu kuwa SANE maana yake ni kwamba yupo REASONABLE, na kuwa REASONNABLE maana yake ni kwamba kuwa FAIR, FREE FROM BIAS, FREE FROM SELF INTEREST, DECEPTION…;

Suala lingine ambalo umelijadili ni kuhusu whether or not BINADAMU ni most the most intelligent creature. Nakubaliana na wewe kwamba binadamu sio the most intelligent creature na ushahidi upo wazi kabisa. Kwanza, sisi na wanyama wengine kama tembo, nyati, n.k, tunaishi kwa kutumia UBONGO, hivyo kufanya UBONGO kuwa the Common Denominator kwetu sote; Pili, tunafahamu kwamba tunaishi kwa kutegemea vitu vinaitwa FIVE SENSES, na hizi zinafanya pale tu zinaposhirikiana na UBONGO; Sasa tukijidadisi na wanyama wengine, WHO MAKES MORE SENSE OF THE WORLD? Je sisi tuna uwezo ‘to make more sense of the world around us that other animals? – kwa mfano when it comes to abilities to see under different circumstances (eyes), uwezo wa kusikia (ears), uwezo wa kunusa (smell) etc. Hakuna ubishi kwamba kuna wanyama wengi waliotuzidi katika haya;

Pia kuna suala la ‘COMMON SENSE', ambalo wanadamu tuna tabia ya kutumia dhana hii kama njia ya kujipima ubora wetu na binadamu wengine; maana ya Common Sense kwa ujumla wake ni sawa tu na ile ya SANITY i.e. kuwa na "SOUND JUDGEMENT" ambayo binadamu wote wanategemewa kuwa nayo ili kuasaidiana na changamoto katika mazingira wanayoishi. Je, who makes better judgement katika mazingira yake bila ya kuathiri mazingira hayo kwa faida ya vizazi vya sasa na vya baadae? Definitely ni wanyama kwani tofauti na wanyama wengine, Binadamusisi tupo SO CONSUMED WITH SHORT TERM ECONOMIC GAINS KULIKO KWA MFANO THE ECOSYSTEM AMBAYO NDIO MHIMILI WA MAISHA YETU; kwa mfano, tupo obsessed na OIL huku tukujua wazi madhara yake kwenye ecosystem, lakini muhimu zaidi, huku tukijua wazi kwamba tuna uwezo wa kutumia nishati mbadala kwa urahisi na kwa gharam ndogo zaidi lakini We lack a very low level of INTELLIGENCE to comprehend that, or TO MAKE SENSE OF SUCH LOGIC;

Mifano mingine ipo mingi tu, - kwa mfano tunajua fika kwamba kuna aina fulani ya vilevi au vyakula ambazvyo matumizi yake yan athari kubwa kwa afya zetu na za wale wanaotuzunguka; lakini tupo tayari kuja kugharamia afya zetu baadae, au hata kufa ili mradi tu in the short run, we enjoy/we get leisure from consuming such, jijengea social status ya namna fulani n.k.katika haya, hakuna kiwango chochote cha maana cha intelligence au logic; Pia katika suala la siasa/uongozi, unakuta kuna Mijitu ambayo jamii inawaona kwamba ni Intelligent, Sane, etc, lakini unakuta ni hao hao wanakuwa upande wenye nia ya kuchakachua Katiba mpya ili mradi tu wafanikishe their short term gains (money, power, respect), bila ya kujali kwamba madhara kwa vitukuu vyao na vizazi vyao vya baadae yatakuwa makubwa; Lakini bado ni mijitu hii hii ambayo kutwa tunaipigia makofi na kuifagilia kwamba wapo BRAINY kwa maana ya kwamba they have unusual/impressive/extraordinary level of intelligence;

Mwisho niseme tu kwamba binadamu tuna tabia moja ya ajabu sana – Mtu aki ‘Behave' kwa namna tusiyoipenda, tunamuondoa kwenye UTU na kusema wazi kabisa kwamba "He/She is Behaving like an Animal, wakati ukweli ni kwamba kama tulivyokwisha ona, we are not the most intelligent species; Tuna ushahidi tosha kwamba kuna wanyama wa porini na hata wa kufuga, chungu nzima ambao ‘they behave with more Grace, Dignity, Wisdom & Morality kuliko Sisi Binadamu; Na kama ulivyogusia suala la RIGHT & WRONG, ambalo ni suala la MORALITY, hii ndio the most important measure of INTELLIGENCE. Mbwa tunaofuga majumbani kwetu kwa mfano, wote ni CANNIBALS – kwani hata nyama ya mtu kwao ni Chakula, lakini ni mara chache sana kusikia mbwa amekula binadamu, which means mbwa wengi behave with more grace, dignity, wisdom, morality, na pia Intelligence and SANITY kuliko binadamu wengi. Ndio maana mtu akiniita ‘MBWA WEWE', na kudhania amenitusi, mara nyingi huwa najihisi UTU ZAIDI.
Mkuu hapo kusema kwamba binadamu siyo the most intelligent creature sikubaliani kabisa na wewe.

Naomba utembelee zaidi kuhusu cognitive vs behavioral psychology na mengi hapo juu utapata majibu yake.

Kwasababu mifano uliyoitumia,haiendani kabisa na hoja unayojaribu kuijenga,especially kuhusu sisi wanadamu ambao pia ni "wanyama" vs wanyama.Kwamba mbwa wana behave with more dignity,wisdom,morality na intelligence kuliko binadamu wengi,haliwafanyi mbwa kuwa zaidi ya binadamu kwenye terms za intelligence.Kumbuka ni binadamu huyo huyo aliyemtrain mbwa na pia kuona kwamba ni mnyama anayeweza kuishi naye na kupata ulinzi wake pamoja na mengineyo.Hoja hii ni vyema tukaijadali kwa misingi ya saikolojia.

Kwa mfano intelligence pia inaweza kutafsiriwa kama "The capacity to acquire and apply knowledge,especially toward a purposeful goal",ni kweli kuwa wanayama nao ni intelligent,lakini kusema ni zaidi ya wanadamu,then ninaweza kushangazwa na tafsiri yako ya intelligence.

Wanadamu kwa ujumla wetu,tumeweza kuya overcome mazingira kwa kiasi kikubwa kuliko wanyama wengine,hata maamuzi tunayoyafanya,yanajumuisha pia na wanyama hata wa porini,ambao baadhi yetu wanadamu huwa tuna fight ili waendelee kuwepo.

Kuna tabia nyingi tu ambazo tunashare na wanyama wote,lakini ikija kwenye intelligence,tumewazidi,otherwise wao ndiyo wangekuwa wanatuamulia mambo badala ya sisi kufanya hivyo.
 
Safi sana Mkuu wangu Mkandara:
MATAMANIO:
Kama utakumbuka vizuri hapo nyuma pindi naelezea misingi ya dhana ya "Private Ownership", nilisema kuhusu haya mambo mawili ambayo Binadamu anazaliwa nayo, yaani UTU/MANTIKI na HULKA/MATAMANIO. Na nikasema "Mtu makini anaongozwa na MANTIKI na si HULKA zake" Na nikasema ili binadamu aweze kuishi MANTIKI, ni lazima AFUNGWE kuepuka Matamanio yake.
Sasa mkuu wangu, ni wazi tunakubaliana kwamba tumefikishwa hapa kutokana na kuishi matamanio, na si MANTIKI. Mimi nasema, ili binadamu asifuate MATAMANIO yake, anatakiwa AFUNGWE asiachwe huru hata kidogo! Alazimishwe! Hapa ni wazi TUNAUA dhana ya kumuacha mtu huru juu ya "Private Ownership", lengo ni kumfanya mtu asifuate matamanio yake bali MANTIKI, yaani UTU! Na UTU ni KUFIKIRIANA, sasa tutawezaje kuwafanya watu wafikiriane hali kila mtu anatafuta mkate wake binafsi? Hapa ndipo napoona haja ya kuwa wamoja. Ni Lazima TUFUNGWE ili tuishi pamoja, tusiachwe huru hata kidogo, kwani tutaangukia matamanio yetu, na matokeo yake ndio huu UOZO uliousema mkuu wangu!
Wapi pagumu mkuu wangu?
Naomba upime kila jambo katika misingi ya kujenga KUFIKIRIANA ama KUKINZANA! Hapo ndipo Utakapoona UOZO wa mifumo, sera, falsafa, nk. nyini tu!
Lets Live Logic!
*Kama ulivyosema mwenyewe mkuu wangu, kwamba hao wahindi kumi walipofika ugenini wakaungana kujenga nguvu na wameushka uchumi! Sasa kwa nini sisi hatuoni haja ya kuungana humu ugenini tulimo(ukoloni mamboleo) ili kushinda? Je, hyo Private Ownership inatuunganisha au kututenganisha zaidi? Kuna haja ya kuing'ang'ania. Kwanini basi tusiandae mazingira ya kizazi chetu kijacho kutoikuta?
Wahindi Ugenini walikuwa 10 in 1, umoja wao ukawafanya wafikiriane! Niambie individualism inawezaje kutufanya tufikiriane! Matokeo ya Private Ownership ni dhuluma kati ya mtu na mtu, ufisadi kati ya mtu/watu na jamii/umma, na ukoloni kati ya taifa na taifa. Kama tunachagua KITU kuwa kipimo cha Maendeleo yetu basi na tuwaache kina Rostam na Lowasa wajilimbikizie tu, kwani hcho ndicho kiphmo na njia iliyoiweka USA ilipo! Lakini kama tunakubali kuwa Kipimo cha Maendeleo yetu kama Afrika ni UTU, basi na tuvunje kwanza Private Ownership!
Mungu wetu anaita sasa!
 
Safi sana Mkuu wangu Mkandara:
MATAMANIO:
Kama utakumbuka vizuri hapo nyuma pindi naelezea misingi ya dhana ya "Private Ownership", nilisema kuhusu haya mambo mawili ambayo Binadamu anazaliwa nayo, yaani UTU/MANTIKI na HULKA/MATAMANIO. Na nikasema "Mtu makini anaongozwa na MANTIKI na si HULKA zake" Na nikasema ili binadamu aweze kuishi MANTIKI, ni lazima AFUNGWE kuepuka Matamanio yake.
Sasa mkuu wangu, ni wazi tunakubaliana kwamba tumefikishwa hapa kutokana na kuishi matamanio, na si MANTIKI. Mimi nasema, ili binadamu asifuate MATAMANIO yake, anatakiwa AFUNGWE asiachwe huru hata kidogo! Alazimishwe! Hapa ni wazi TUNAUA dhana ya kumuacha mtu huru juu ya "Private Ownership", lengo ni kumfanya mtu asifuate matamanio yake bali MANTIKI, yaani UTU! Na UTU ni KUFIKIRIANA, sasa tutawezaje kuwafanya watu wafikiriane hali kila mtu anatafuta mkate wake binafsi? Hapa ndipo napoona haja ya kuwa wamoja. Ni Lazima TUFUNGWE ili tuishi pamoja, tusiachwe huru hata kidogo, kwani tutaangukia matamanio yetu, na matokeo yake ndio huu UOZO uliousema mkuu wangu!
Wapi pagumu mkuu wangu?
Naomba upime kila jambo katika misingi ya kujenga KUFIKIRIANA ama KUKINZANA! Hapo ndipo Utakapoona UOZO wa mifumo, sera, falsafa, nk. nyini tu!
Lets Live Logic!
*Kama ulivyosema mwenyewe mkuu wangu, kwamba hao wahindi kumi walipofika ugenini wakaungana kujenga nguvu na wameushka uchumi! Sasa kwa nini sisi hatuoni haja ya kuungana humu ugenini tulimo(ukoloni mamboleo) ili kushinda? Je, hyo Private Ownership inatuunganisha au kututenganisha zaidi? Kuna haja ya kuing'ang'ania. Kwanini basi tusiandae mazingira ya kizazi chetu kijacho kutoikuta?
Wahindi Ugenini walikuwa 10 in 1, umoja wao ukawafanya wafikiriane! Niambie individualism inawezaje kutufanya tufikiriane! Matokeo ya Private Ownership ni dhuluma kati ya mtu na mtu, ufisadi kati ya mtu/watu na jamii/umma, na ukoloni kati ya taifa na taifa. Kama tunachagua KITU kuwa kipimo cha Maendeleo yetu basi na tuwaache kina Rostam na Lowasa wajilimbikizie tu, kwani hcho ndicho kiphmo na njia iliyoiweka USA ilipo! Lakini kama tunakubali kuwa Kipimo cha Maendeleo yetu kama Afrika ni UTU, basi na tuvunje kwanza Private Ownership!
Mungu wetu anaita sasa!
Nashukuru sana kwa maelezo yako japokuwa bado napingana kwa kukubali kutokubaliana ktk hili.. Kuishi MANTIKI ni kusihi kwa kukidhi MAHITAJI yetu haiwezi kupoteza dhana ya Private ownership hata kidogo. Nakuomba unifahamu vizuri naposema Private ownership kuwa ni HAKI ya mwanadamu tofauti kabisa na UHURU wetu unaotakiwa kupimwa kutokana na Mahitaji yetu badala ya Matamanio..

Nakubaliana sana na wewe unaposema Uhuru wa mtu lazima ufungiwe ktk Mahitaji lakini sio pale penye haki ya mtu huy huyo. Pengine unachanganya mahala padogo sana. Mwenye MATAMANIO sio mwekezaji isipokuwa ni mwenye tamaa au matamanio ni MTUMIAJI (consumer), yule mwenye tamaa kutumia mkitu hicho yaani huyu ndiye anayeiweka demand ya matamanio ndiye atakiwa kunyimwa uhuru wa matamanio yake...Lakini haki yake ktk kuzalisha haiwezi kupokonywa maana maendeleo hutokana na WATU wenye ubunifu wa mahitaji yetu. Hivyo utakapo pokonya haki ya watu kubuni basi hata hayo MAHITAJI hayataweza kupata ufumbuzi.

Mkuu wangu nimezisoma hizi nadharia kwa makini sana nakutazama undani wake kabla sijafikia kukubaliana na Ubepari na wapi mipaka yake. Naamini ktk Ubepari wa Kijamaa nikiwa na maana ya kukubali UTU wetu ktk riziki na Mahitaji yetu kwamba hutokana na MTU. Kwa hiyo tunachoweza pekee kukifanya ni ku - regulate MATAMANIO tukaiweka haramu ktk baadhi ya vitu visivyokuwa muhimu ktk maisha yetu hivyo vikakosa soko la ndani na hivyo kumkwaza huyo private owner kuwekeza ktk kitu ambacho hakina soko.

Kama unakumbuka wakati wa Nyerere wazungu walitumaliza walipoondoa soko la katani, Pamba na Chai hivyo tukaanguka kiuchumi na ukawa mwanzo wa kifo cha kilimo cha malighafi hizo nchini.. Sasa hali kama hiyo tunaweza kuitumia ktk MATAMANIO pasipo kuathiri Mahitaji yetu na bila shaka havitaweza kupata soko lakini hatuwezi kuzuia utengenezaji wake. Ndio maana nikatoa mfano wa China.. Tusiwalaumu China hata kidogo maana wao wanatengezeza vitu feki kutokana na MATAMANIO yetu sisi, na kama tutapiga marufuku vitu feki, tukaondoa uhuru wa watu kutamani vitu feki itawalazimu China wasivitengeneze maana hakuna soko.

Leo hii Marekani kwa Matamanio yao ya Cocaine wamejaribu sana kuzuia Uzalishaji wa cocaine lakini haiwezi kuwasaidia ikiwa nsoko la Matamanio linazidi kuongezeka. Itakuwa jambo bora sana kwao kuzuia Uhuru wa mtu ktk matamanio yaani wale vijugu wao ndio wapigwe vita kuliondoa soko kwanza. Hapo itakuwa rahidsi sana kushusha uzalishaji wa Cocaine, lakini nimekuja gundua kwamba Conaine ni big business kwa serikali ya Marekani na wanaiendesha hivyo makusudi kuliweka soko la Cocaine juu ili wao wenyewe washiriki..

Nasi Nyumbani tunaendelea kuiga ktk matamanio iwe Sigara na Pombe vyote hivi vinaendelea kuuzwa kwa sababu vinachangia sehemu kubwa ya pato la seirkali..Je, tunaweza kuishi pasipo sigara na Pombe? biola shaka maana haya ni matamanio na unaweza kabisa kusema tunaweza kuzuia Uzalishaji wa sigara kwa sababu ni private ownership..Ukweli utabakia kwamba maadam wateja wapo, soko la sigara na Pombe vitaendelea kuuzwa, kuingia nchini hata kama tutaweka jeshi kiasi gani. Kuharamisha matumizi yake na wananchi wenyewe wakaelewa umuhimu wa MAHITAJI mbele ya MATAMANIO, ndio njia pekee ya kuzuia vitu hivyo kuzalishwa.

Kwa hiyo ukitaka kuutazama Ubepari ktk sura nzuri nayoizungumzia mimi ni katika MAHITAJI. Kila mmoja wetu anatakiwa kwenda shule kujielimisha ili kukidhi mahitaji yetu ambayo hayawezi kutimia pasipo uwekezaji na uwekezaji unatokana na ubunifu wa soko la mahitaji. Kumbuka tu kwamba MAHITAJI yetu yanazidi kukua kila siku kutokana na mazingira tuliyopo.

Private ownership haihusiani na nguvu ya UMOJA wa watu isipokuwa kufikia malengo ya kufanikiwa. Wale wahindi wameweza kutoka kwa sababu walilenga kutogawana Umaskini bali mchango wa maskini zile nguvu zao kuwa chimbuko la uwekezaji wao wakliwa na lengo ya kutoka ktk umaskini. Hivyo kuna kutumikia mahitaji muhimu ya binadamu na kuna kutoka ktk Umaskini..Inakuwa kama vile UPATU wa maisha hivyo kila mtu atatoka ktk Umaskini badala ya kugawana umaskini ili waishi..

UTU wa Mdanganyika sii Mantiki bali ni umejawa HULKA na MATAMANIO..Leo hii mkuu wangu ukishuka Bongo na Dollar zako 50,000 ndugu na jamaa zako watategemea wewe uwakatie hizo 50,000. Na hata ukisema unataka kuanzisha biashara wao watafikiria jinsi gani watafaidika na huo mtaji badala ya kufikiria kama zitawekezwa ktk biashara ya MAHITAJI yaliyopo nchini utaweza kuzalisha faida ambayo itawatoa hata wao baada ya mafamikio.

Wabongo watafanya kila hila ktk UTU wa mahitaji yao uyakidhi kwanza mahitaji yao, iwe hajalipa kodi, hana bauli sijui ada ya mwanaye, hivyo unarudhishw aktk kufikiri kimaskinii kugawana mtaji uliopo na ukianza kutatua matatizo ya watu, utaondoka huna hizo 50,000 na hakutoka mtu. Utawaacha na matatizo yale yale kama ulivyowakuta na ndivyo tunavyoishi wengi wetu kwa kupanda mbegu ili tukidhi mahitaji yetu hivyo ikiyokea mavuno mabaya tutakula hadi mbegu..

Ubepari unatukumbusha kwamba unachokiuza (EXPORT) ndicho kinachokuwezesha wewe kukabiri unachokihitaji toka kwao (IMPORTS)..Iwe familia, kabila au Taifa na ndio maana mafanikio ya Kiuchumi ya Tanzania hayawezi kuhesabiwa ni ya Kenya au Uganda. Kama taifa sisi tuna own mali zetu tuna own otajiri wa Tanzania.. Hilihaliwezi kuepukwa..Sisi tulianguka na Ujamaa kwa sababu tulifikiria tunaweza kukidhi mahitaji yetu sisi wenyewe tukiuziana wenyewe pasipo kuwategemea watu wa nje kumbe UTU wetu ktk mahitaji hayawezi kutoka mikononi mwetu bali kwa watu wengine - TUNATEGEMEANA..
 
Nakubaliana sana na hoja Mkandara.
Nawashukuru wengine mnaozidi kutiririka kwa mantiki.Tuendelee
 
Nakubaliana sana na hoja Mkandara.
Nawashukuru wengine mnaozidi kutiririka kwa mantiki.Tuendelee
Shukran mkuu wangu unajua hapa tunaizunguzia mustakabali wa Taifa letu bna ni rahisi sana kwa mtu kulaani Ubepari kama hatazingatia kwamba sisi ni MAFUKARA tu sio maskini wa rasilimali na maliasili. Na kama tutaijenga ile nadharia ya UJAMAA wa KUFIKIRIANA kwa kutotazama mazingira tuliyopo na kuenzi haki yetu ya ku own Utajiri Mungu alotujalia basi bila shaka tutakwama sisi wenyewe ktk nadharia hiyo.

Na inatulazimu kufikiria private Ownership kwa maslahi ya Tanzania, hivyo Dhahabu, gasi, mafuta na mali zote zilizomo nchini ni zetu sisi, hivyo mashirika ya nje yanapokuja kuwekeza nchini lazima wafahamu kuwa hiyo ni mali yetu kwanza. Na je tunaweza vipi kuingia ktk mazingira haya ya Utandawazi?.. rahisi kabisa tufanye kama walivyofanya wengine wenye maliasili na rasilimali kama zetu na wakafaidika nazo japokuwa iwe tofauti kidogo tu..

Tunaunda mashirika yetu ya taifa iwe mafuta, gasi au dhahabu kama walivyofanya Botswana na yeyote anayekuja wekeza nchini analikuta shirika tayari ambalo limemilikishwa mali hizo. Na ndivyo walivyofanya Saudia, Qatar, Dubai na Abudhabi japokuwa wao mali hizo ni za Sultan wenye jukumu la juu kuutawanya utajiri wa nchi hzo kwa wananchi wake. Ndivyo Nyerere alivyotu andaa wakati wake japokuwa hakukubaliana na Ubepari kwa dhana ile ya Kupingana na Uberereru ambao ndio mfumo halisi ya utajiri wa nchi za magharibi. Kila maliasili tulokuwa nayo aliweka shirika lake na tukawa tunadai share ya umiliki lakini nchi nyingi za Magharibi walichomoa kutokana na kutokuwa na imani na nchi za Kijamaa.

Ebu fikiria leo kama Barricks ingekuwa soko la Marekani au Canada tukiwa na share ya asilimia 50 kama walivyofanya Botswana!..Ebu fikiria hiyo gasi ya Songo Songo tungekuwa wamiliki wabia ktk soko la Australia au Uingereza. Mbona Uingereza BP waliweza kuungana na Shell kwa mafuta ya Holland na wakaendela muungano wao hadi majuzi tu..Iweje sisi tuwe na wasiwasi kwamba hatuwezi ikiwa mafuta, gasi dhahabu ni vitu adimu sana na muhimu ktk MAHITAJI yetu kulingana na MAZINGIRA tuliyopo?. NI lazima tukubali na kuamini kwamba dunia hii kiuchumi kila nchi ina struggle for existence! Maidha ya Nchi yoyote ile ni Uchumi wake hivyo tunakulana na spieces yetu itaweza tu ku survive ikiwa nasi tunajifunza namna ya kutajirika maana Umaskini ni kifo cha kiuchumi..Utajiri ndio afya ya nchi yoyote na hivyo tujali sana vile tulivyojaliwa kuwa navyo wakati wengine hawana.

Kizingiti kikubwa kilichopo mbele yetu ni sisi wenyewe. Umaskini tulonao umetuondoa UZALENDO, na kwa bahati mbaya sana Azimio la Zanzibar limetuondolea hata TUMAINI maana sasa twalana wenyewe..Tumekuwa kama ng'ombe walonenepeshwa na Nyerere only to end up on our own dinner plates. Tumeipoteza dira kiasi kwamba kila mmoja wetu anataka yeye atoke kwanza iwe rais, waziri hadi vijakazi majumbani sisi wote ni MAFISADI tulogubikwa UBINAFSI wa kutoka ktk umaskini kama kaa wa bahari ktk tenga la mvuvi, na tusipojiandaa leo vema basi bila shaka tunaishia ktk karai la mafuta ya moto.

Hatuna sababu kabisa ya mtu mmoja mmoja kutoka wka msaada wa wengine maana hatuwezi panda ngazi moja watu wote itabomoka. Na wala hatuwezi kufikiria akitoka mmoja ni Ubinafsi ikiwa tunmeweka malengo ya kutupiana kamba kwa wale waliotangulia juu. Yote haya yanawezekana ikiwa tutaweka nia thabiti ya kuondokana na Umaskini kama wale wahindi niliwataja hapo juu..

Majuzi tu waziri wetu wa nishati na Madini ametangaza ku review mashirika 26 tayari shares ktk walllstreet zimeshuka ati wakisema kumetokea great uncertainty. Who own those shares? sio sisi isipokuwa yule alokuja kutusaidia kuung'oa Mhogo..Na wala sii wanunuzi wa gasi yetu ila wanagombania kununua umiliki wa mali yetu sokoni japokuwa sii wao walotusaidia kuchimba tena wahawajui Songo songo iko wapi Tanzania. Huu ndio UBEBERU aloukataa Nyerere, mali yetu kuwekwa sokoni ikagombaniwa kuwa miliki yao ktk puto wakati mali yetu haijauzwa...

Huu ni wakati wa Kuutafuta UZALENDO kwa nguvu zote na hatutaweza kufanikiwa kama tutashindwa kukomesha Ufisadi ambao umetokana na KUTOFIKIRIANA kwa lugha yangu huita UBERERU na siii Ubepari..Na ili tuweze kurudisha UMOJA wetu ni lazima tuweke malengo ya kuondokana na UMASKINI.. Adui yetu UMASKINI lazima uwe kioo chetu wote kwamba tutatoka tu ikiwa tutafanya kadhaa wa kadhaa..Na yule anayesaliti mfumo we Kijamii ambao utatukuza UTU wetu kwanza na tukajali maliasili na rasilimali zetu kuwa ndizo nguzo pekee tulobakia nazo na hizi ni MALI zetu we own them.. basi bila shaka Umaskini utakuwa historia. Tutaanza na wapi?. KULAZIMISHANA kuwa kitu kimoja, kulazimishana kuondoa tofauti zetu na kwamba sisi wote ni ndugu na maskini tunaotaka kuondokana na Umaskini, Ujinga na Maradhi..Siasa ya UJAMAA irudi ktk misingi ya UTU wetu, kutukuza vipaji, mila na desturi zetu ktk Uzalishaji na usambazaji ili kukidhi mahitaji yetu - Private ownership.
 
Mkuu Mkandara, unanikumbusha kitu kimoja kinaitwa PPP(Public private partnership). Hata huko ubepari ulipoota mizizi bado wanakubali kuwa kuna mambo lazima yafanywe kwa ushirikiano. Mfano, niliona bara bara inajengwa na inakuwa ya kulipia ukiingia hadi kutoka. Kilichosukuma hilo kilikuwa uwezo kidogo wa serikali ya jimbo kujenga barabara hiyo kwa muda mfupi.Interest ya serikali si kutengeneza faida bali kumlinda consumer na kupata japo 'mrahaba' wa kufanyia shughuli zingine.

Umegusia kuhusu kuandaliwa, hili nakubali sana na nadhani ndio ilikuwa dira ya Nyerere. Haikuwa na maana hakutaka kuchimba madini au kuita wawekezaji, alichotaka ni kuwa ikitokea hivyo basi tuwe tayari kufaidika na na hilo.
Inasikitisha kuona jitihada za kuandaa mabwawa ya nishati zimekuwa kama bure, badala ya sisi kuwahudumia hao wawekezaji ili tuvune wao ndio wanasambaza umeme!

Nadhani kuhusu private ownership, hilo si tatizo kabisa kama tutakuwa na kanuni, sheria na taratibu za kusimamia.
Kwa vile hatuna 'earth moving equipments' basi tulipaswa tuwaite wenye hivyo vyombo huku tukitarajia kupata ili kujenga uwezo. Hilo halitokei tumeamua kuacha kila kitu wazi.

Lakini pia tujiulize NMC, RTC, TRC, ATC zilikuwa zetu kwa kile kinachosemwa kufikiriana, mbona hatuoni matokeo ya kufikiriana? Sidhani kufikiriana ni kumhujumu Precision Air, nadhani ni kumwezesha kimazingira ya biashara nasi kupitia kwake tujenge uwezo wa kuwawezesha wasio na uwezo. Hapa njia rahisi ni kuwapa elimu na huko ndiko kufikiriana.

Tuangalie sababu halisi na si mifumo, nami ningesema hatujawa na watu wa kutuongoza na kusimamia thamani zetu.
Ni rahis kusema private ownership ina matatizo, lakini hatujaangalia kwanini UDA imekufa.
Ni rahisi kusema private ownership ina matatizo lakini hatujiulizi miaka 10 gesi ya songo songo ipo ubungo, kwanini magomeni wapikie kuni bado?
Ni rahisi kusema mabepari wametudhulumu lakini hatujiulizi ilikuwaje wakaja na kuigawa TTCL kuwa celtel halafu wakaingia mitini na mtaji? Ni kwa msaada wa nani. Ubaya wa private ownership umepigiwa chapuo na nani?
 
Mkuu Jmushi1,

Nashukuru kwa maoni yako ambayo yanazidi kuamsha mjadala; Kwanza naomba niseme tu kwamba mimi sipingani na wewe, ni kwamba tu nina mtazamo tofauti na nitajitahidi kufafanua juu ya hili; Katika mjadala wangu, ingawa inawezekana nisigusie mengi ya msingi, nitajitahidi kujenga hoja zangu based on masuala yafuatayo:

Kwanza, je definition ya intelligence ipo universally accepted?
Pili, tutapojaribu ku-analyse intelligence za wanyama, tunatumia analytical approaches or frameworks ambazo zipo balanced au zinapendelea zaidi binadamu?
Tatu, how do we detect intelligence in humans vis-à-vis in non-human animals kama mbwa n.k?
Mimi nadhani one can argue kwamba binadamu ni more intelligent kuliko all other non-human animals kwa kutegemea na analytical framework au approach anayoitumia; Kwa mfano, wewe ume-base on the literature juu ya cognitive, behavioral psychology etc; Ebu tuitazame kidogo approach yako;

Tukianza na Cognitive psychology, hili ni tawi la saikolojia linalotafiti internal mental processes za binadamu, hasa kutafiti jinsi gani BINADAMU (sio wanyama kwa ujumla) PERCEIVE, THINK, SPEAK, REMEMBER & SOLVE PROBLEMS. Tutakuja tazama haya kwa undani baadae kidigo;

Tukihamia kwenye Behavioral Psychology, hii hujikita zaidi kuelezea/kutafiti shughuli (activities) zote zinazohusisha THE PHYSICAL & THE MENTAL, hasa jinsi gani glands na muscles zina-respond kwa MATUKIO YALIYOPO NJE YA KIUMBE HAI, HASA BINADAMU. In the process, Behavioral Psychology inazingatia kanuni kadhaa ili kufanikisha malengo yake, ikiwa ni pamoja na:

Kanuni ya KWANZA: Tabia ya BINADAMU inaweza kueleweka iwapo tu itafananisha na pia kuhusisha uchunguzi wa TABIA YA WANYAMA WASIO BINADAMU;
Kanuni ya PILI, Behavioral Psychology inachunguza tabia ambazo ni OBSERVABLE & MEASURABLE PEKE YAKE, na kama hazikidhi haya mawili, TUPA KULEE!!
Kanuni ya TATU, Behavioral Psychology ina consider kwamba KNOWLEDGE ni suala linalotoka kwa MWALIMU KWENDA KWA MWANAFUNZI;
Kanuni ya NNE, Kazi ya MWALIMU ni KUBADILISHA TABIA YA MWANAFUNZI, SIO MWENENDO WA FIKRA ZAKE;
Na Kanuni ya TANO, Binadamu huweza ku- master jambo kutokana na REPETITION, and this mastery is equated to UNDERSTANDING; kumbuka hapa kwamba practice makes perfect na tutaona kwa wanyama kama vile dolphins;

Kwahiyo mkuu Jmushi1, hii ndio sehemu kubwa ya analytical framework ambayo umeitumia to build your case on why you strongly believe and think kwamba Binadamu is superior to wanyama when it comes to the issue of INTELLIGENCE;
Sasa kwa vile the common denominator katika hoja zetu ni neno INTELLIGENCE, naomba niingie kwenye mjadala wa kutafuta definition ya neno hili; Kwa maelezo yako ambayo nakubaliana nayo kwa kiasi kikubwa, Intelligence ni pamoja na "Ability to acquire and apply knowledge towards a purposeful goal". Lakini while we are on this, rejea kanuni ya Behavioral Psychology hapo juu kuhusu knowledge kwamba kuna Mwalimu na Mwanafunzi na pia kwamba kazi ya Mwalimu ni kubadilisha TABIA, sio kubadilisha MWENDENDO WA FIKRA ZAKE; nadhani kwa mbali utaona mapungufu ya h ii approach kwani ipo biased, hasa ule mfano wako kwamba Binadamu ndio wana train wanyama kama mbwa, ukiwa na maana kwamab wakiweza kujifunza, ndio tunaanza kuwaita kwamba wapo smart etc;

Wanazuoni mbali mbali wa Saikolojia wamekuwa wakisema kwamba definition ya Intelligence imejaa utata mwingi sana (it is a controversial concept) na kwamba hakuna a universally accepted definition; kutokana na hili, wanasayansi wamekuja na definition mbalimbali katika kujaribu ku-challenge such bias, na ndio maana katika tafiti kama hizi, hakuna mtu aliyepo RIGHT au WRONG, au mwenye final analysis and answer; hata watafiti wanaopewa tuzo za Nobel ni kwamba wametoa mchango mkubwa katika kuendelea kubaini ukweli juu ya masuala kama haya – NA HAWAPEWI TUZO KWA SABABU TAFITI ZAO NDIO SAHII AND FINAL!

Naomba nitumie definition ya intelligence that is offered by scientists kwani kwa mtazamo wangu, kidogo ipo more generous: According to mwanasayansi mmoja by the name of Gottfredson (1997), Intelligence implies:

"Mental capability that involves, among other things the ability to reason, plan, solve problems, think abstractly, comprehend complex ideas, learn quickly and learn from experience"

Note: Kuhusu suala la learning hapa, it's not BOOK – LEARNING, but rather a much broader & deeper meaning on capability to comprehend our surroundings, making sense of things, finding out what to do best to adjust to an external environment etc;

Nadhani mpaka hapa tumeshaona kuna maupungufu katika kutegemea Cognitive & Behavioral Psychology to determine the levels of intelligence baina ya humans and non-humans animals; suala hili sio straight forward kama wengi wanavyopenda kufikiri; ni kutokana na hili, ndio maana tafiti huwa hazifi; HATA MTU AKITUNUKIWA TUZO MIA MOJA ZA NOBEL, NI KWAMBA HE OR SHE HAS JUST SCRATCHED THE SURFACE TOWARDS THE SAID KNOWLEDGE!

Now, turudi kwenye definition uliyotumia kujenga hoja yako on ‘intelligence' i.e. "Ability to acquire and apply knowledge towards a purposeful goal"; Swali linalofuatia ni Je, how do we measure mental capacities of non-human animals vis-as-vis humans?

Ni kutokana na pengo na udhaifu mkubwa uliojitokeza katika ufahamu katika suala hili ndio maana tafiti hazijafa na badala yake zinazidi kuibuka kila kukicha; kwa mfano, watafiti mbalimbali wamependekeza different approaches za kupima intelligency capacity za wanyama, kwa mfano "Animal Cognition" Approach ambayo inatafiti the Mental Capacity ya wanyama nje ya binadamu, and this approach ime gain umaarufu kutokana na watafiti wengi kubaini mapungufu ya Cognitive and Behavioral approaches towards understanding levels of intelligence on human and non human animals;

Kama tunavyomuelewa Darwin, huyu alikuwa ni mmoja wa watu wa kwanza kabisa kutupatia uelewa juu ya intelligence ya wanyama; alifungua njia katika utafiti huu; Lakini pamoja na kazi yake hii nzuri, kulikuwa na mapungufu kadhaa, kuu ikiwa ni pamoja na kwamba – He placed humans and animals on a continuum in terms of intelligence capacities; hii inaendana sana na evolution theory kwamba wanyama hupitia stages tofauti za Maendeleo ya ubongo i.e. a continuum from left to right towards higher levels of intelligence; Miaka ya baadae, ikaja gundulika kwamba Scientifically, this approach was a failure; Na hoja zako kidogo zinaegemea on DARWISM, lakini kama nimekosea tafadhali nisahihishe;

Tukirejea kwenye ile kanuni ya behavioral psychology kwamba - inachunguza tabia ambazo ni OBSERVABLE & MEASURABLE ONLY, na nje ya hapo, TUPA KULE, watafiti wa animal psychology have determined kwamba kuna certain UNSEEN PSYCHOLOGICAL PROCESSES ambazo researchers tend to overlook or ignore; this is inherent to behavioral psychology (rejea kanuni hiyo hapo juu); huu ni ushahidi mkubwa sana kwamba katika hili, tunakabiliwa na tatizo kubwa sana la "METHODOLOGY", katika kuelekea kupata ukweli juu ya intelligence capacity among animals; Wataalamu wanalielezea jambo hili as: ANTHROPOMORPHISM i.e. tabia na mazoea yetu sisi wanadamu to interpret tabia za wanyama kwa vigezo vya how we feel, perceive them, based on our motivations, thoughts and so forth; Mkuu Jmushi1, kuna kila dalili kwamba pia wewe ni victim wa hili.

Vinginevyo watafiti mbalimbali wamebaini kwamba drawing conclusions to animals' reasoning, insight and consciousness is unnecessary and misleading; Moja ya tafiti interesting and influential in the said field ni ile ya hivi karibuni ya Fischer & Menzel (2010) – "Animal Thinking: Contemporary issues in Comparative Cognition". Kwa mujibu wa watafiti hawa, wanyama ni goal seeking agents that acquire, store, retrieve and internally process information at many levels of cognitive complexities; By means of lab experience,s they were able to observe animals pushing levers, pull strings, respond to images on PCs in discrimination, attention, memory and categorization contexts; what this tells us ni kwamba hata kwa vigezo vya kibinadamu, kuna baadhi ya mambo ambayo wanyama wanafanana na sisi;

Kwa kumalizia, ningependa kusema yafuatayo:

Kwanza, I strongly believe kwamba intelligence kati ya binadamu na wanyama inategemeana kwanza how you approach the concept of intelligence, the variable you use to determine the levels of intelligence, lakini vile vile External Environment. Katika hili la External Environment ndio nataka nifungie mjadala wangu. Kumbuka katika katika Behavioral Psychology, suala la msingi hapa ni kwamba:


  • This field deals with research on activities zote zinazohusisha THE PHYSICAL & THE MENTAL, hasa jinsi gani glands na muscles zina-respond kwa matukio YALIYOPO NJE YA KIUMBE HAI;
  • Binadamu huweza ku- master jambo kutokana na REPETITION, na this mastery ipo equated na UNDERSTANDING; remember hapa pia kwamba practice makes perfect;
  • Vile vile tuchukue definition yako ya intelligence kwamba ni the capacity to acquire and apply knowledge towards a purposeful goal;
  • Na pia behavioral Psychology ina consider kwamba KNOWLEDGE ni suala linalotolewa na MWALIMU KWENDA KWA MWANAFUNZI;

Given these four points peke yake, kuna mambo kadhaa ambayo yanatufanya tu – question our intelligence vis-à-vis wanyama wengine; kwa mfano, Binadamu hawezi kutumia usafiri wa anga, ardhi au maji bila technology kumuongoza anapoenda vinginevyo atapotea; lakini ndege kama njiwa, dolphins, na wanyama wengine mbalimbali kama paka wana sense of direction kuliko sisi mbali tu; kwa mfano, inakuwaje ukimtupa paka hata umbali kiasi gani, bado anaweza kurudi nyumbani, je na yeye anaulizia directions kama sisi Gas Stations?

Pili, research shows kwamba moja na mambo makubwa yanayo tutenganisha na wanyama wengine ni uwezo wetu to communicate, lakini research shows kwamba kumbe DOLPHINS are capable of holding MULTIPLE CONVERSATION AT ONE TIME, sisi je? Tunajisifia eti kwa multi- tasking;
This further strengthens the argument kwamba – the real problem hapa ni kwamba it all depends on how you define intelligence; kuna certain definitions and analytical frameworks zitaonyesha kwamba binadamu ni superior lakini zipo nyingine zitaonyesha kwamba wanyama wapo superior when it comes to INTELLIGENCE;

Tatu, tukumbuke kwamba most intelligence tests are based on problem solving or pattern recognition which are very much HUMAN TRAITS ANYWAYS, Kwahiyo by default, we will look superior to non-human animals; Lakini pia kwa models hizi hizi za kibinadamu, mara nyingine matendo ya wanyama hutuacha na butwaa kama lile la paka, dolphin, na hata la mbwa kwenda to the main road na kusubiria gari la polisi kisha kumfanya Polisi aamue kumfuata huyo mbwa, kumbe nyumba ya senior citizen ilikuwa inaungua moto huku yeye akiwa ndani and trapped; pia kuna ile news ya sungura kumwamsha usiku mama mwenye nyumba ambae hakuwa anajua nyumba yake inawaka moto na alikuwa usingizini, lakini sungura huyu alijua madhara yale na kumuokoa mama yule; yote haya tunayaona kwenye TV marekani, na zipo hata You Tube;

Na Mwisho, huu ni mgongano tu wa mawazo anyways, and thanks to nguruvi3 kwa hili;
 
Vyema wakuu wangu:
Labda niseme haya tu, kisha yetu yawe macho na masikio.....
*Binafsi naamini katika UTU-MANTIKI kama msingi mkuu wa maisha ya binadamu, katika kuleta maendeleo ya kweli yapimwayo na mahitaji ya NYAKATI na MAZINGIRA mahususi kwa eneo fulani. MAHITAJI hayo ni yale YASIYOKINZANA, yaani yenye MANTIKI. Binafsi katika kutafakari yepi hasa ni mahtaji muhmu ya binadamu, siwezi ishia physical and biological needs tu kama tunavyoaminishwa, bali pia ni psychological needs. Harakati zozote za mwanadamu, katika kukidhi mahitaji yake hayo matatu, yanapokinzana, basi maisha huwa BURE na UPUUZI MKUBWA! Sasa ili kuepusha UKINZANI HUO, ni lazima kuwepo na UUWIANO SAHIHI (mizani sahihi-MANTIKI, mimi naita UTU) katika harakati zake mwanadamu za kukidhi mahitaji yake. Biological needs zinapokinzana na physical/psychological needs maisha ya mwanadamu huwa ni bure!
Dhana ya kuondoa Ukinzani ni lazima ianzie ndani mwake mtu, yaani harakati zangu ktk kukidhi mahtaji yangu zisikinzane zenyewe, baina ya mtu na mtu, watu na watu hadi jamii na jamii!
Binafsi leo, siwezi kushangaa chochote na kujiuliza KWANINI kimetokea au kinatokea, NEVER! Kwani naamini wazi kabisa, kwamba MSINGI MKUU WA MAISHA YETU UMESHAKIUKWA, KILICHOBAKI NI UPUUZI TU! Siwezi kushangaa mboga kusinyaa hali mzizi umeng'olewa.
Huyu katupa mtoto chooni, yule kamuua mama yake, yule kaiba mali ya umma, huyu kaingia mkataba feki, huyu kibaka kachomwa kafa, yule ana meli na ndege huyu atembea na viraka, sheria kumfunga asiye na makosa, kiongozi katukana wananchi, daktari kuomba rushwa ICU, wezi kujiita wakombozi, wanafiki kulindwa kwa nguvu zote, padri/shehe kabaka mtoto, huyu kabadilisha mfumo wa elimu huyu kaurejesha, baba kumkumbatia bintiye akiwa na vazi la ufukweni kwenye mashindano ya ulimbwende, vita, magonjwa, njaa, n.k. Hayo yote ni mazao ya KUKIUKWA KWA MANTIKI, na kuamua kuishi HULKA/MATAMANIO, Matamanio sio juu ya MAHITAJI yake mtu, bali ni TAMAA zake mtu za kutaka UKUU/KUJIKWEZA. Mjomba wangu kijijini kununua bidhaa feki ya mchina si kusukumwa na MATAMANIO, bali KUNA WATU JUU YAKE WALIOJIKWEZA na KUMFANYA DUNI, akalazimika kupata bidhaa duni pia. Maana sahihi ya Kuishi HULKA ni KUPIGANIA UKUU/KUJIKWEZA, MIMI KWANZA-UMIMI-UBINAFSI-PRIVATE OWNERSHIP=UBEPARI. Kamwe siwezi kuupigia makofi! Hulka zipo kwa kila mtu, hata mimi natamani kuwa juu ya watu, lakini ole nikaruhusu ziniongoze...bora nife. Leo kila kitu kiko hivyo, mfumo tunaoishi ni zao la watu kutafuta UKUU. Sera tunazoishi zipo kuwafanya watu fulani kuwa juu, dini, falsafa, itikadi, n.k. IWAPI MANTIKI, U WAPI UTU LEO HII kuzuia uovu unaofanywa na HULKA zetu. Si vyema kuona Nyoka na ukasema si nyoka ni kipepeo, ole maana watoto wako nao hupendelea maeneo hayo!
Mungu wetu anaita sasa!
 
Back
Top Bottom