Duru za siasa: Mtazamo, chaguzi za serikali za mitaa

Duru za siasa: Mtazamo, chaguzi za serikali za mitaa

BAADA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

CCM INA KAZI KUBWA YA KUJITATHMINI
WAPINZANI WANA KAZI KUBWA YA KUTAHMINI

Matokeo yamwisho ya chaguzi za serikali za mitaa yamepatikana

CCMimeshinda katika asilimia 77kwa wastani katika kila eneo la mtaa na vijiji.

Hilo nipunguzo kubwa sana ikitiliwa maanani nguvu kubwa iliyotumika kuhujumu uchaguzi

Kwanza,mapingamizi yaliyowekwa na CCM ni mengi, huenda yangebadili sura iliyopo

Pili, kama kawaida CCM ilipata msaada wa serikali na vyombo vyake
Tatu, ni anguko la takribani asilimia Zaidi ya 10 kutoka uchaguzi uliopita
Nne, uborawa matokeo kwa CCM, ngome zimevunjwa mikoa iliyokuwa na ‘taboo'' auloyal kwa CCM imeanguka

Tumeeleza sababu kubwa zinazoweza kuchangia

Moja,wananchi kuchoshwa na kashfa zinazoiandama serikali ya CCM
Pili, hasira za wananchi kutokana na kudharauliwa maoni yao katika katiba
Tatu, ubabewa CCM wa kutumia wingi katika kuburuza taifa

Haionekani kama CCM wataweza kujitahmini

Tumeeleza kunyosheana vidole kulikoanza na makundi yenye masilahi taofauti

Tathmini yaCCM inaweza kufanyika kama kiini macho.
Uhalisia ni kuwa CCM wana wakati mgumusana kwa kuzingatia makundi tuliyoeleza mabandiko yaliyopita


Ingawa kunashamra shamra za CCM kuhusu ushindi, ukweli ni kuwa ndani ya mioyo yao kunadukuduku kubwa.

CCM wanatambua namba za ushindi ni mbaya kwa siku zausoni. Ni kama vile wamefungua mlango maji yaingie


Haitaonekana haraka haraka, ni katika kipindi cha mwezi au miwili, mtafaruku utajitokeza.
Hilo ni suala la muda, nani mafunge pake kengele.
Mtifuano huo utazaa mtatizona ufa mkubwa. CCM haitakuwa na nafasi ya kujitathmini kiuhalisia


WAPINZANI
Kazi kubwawaliyo nayo si kujivunia hatua waliyofikia.
Wapinzania wana wajibu na kaziya kutathmini matokeo.
Yatakuwa ni makosa makubwa kama wapinzani wataendelea mbele bila kujua nini kimetokea.


Hapoku takuwa na masuala kadhaa

Kwanza,lazima wajiulize, je ni hasira za wananchi au ni mapenzi ya mabadiliko?

Pili, nin imwamko wa wananchi. Je, ni kutambua haki zao au ni kukabiliana na udhalimu?

Tatu,kwanini wananchi wameamua kulinda kura zao. Je, ni kukataa rushwa au nikupungua kwa watoa rushwa

Nne, ninikinawasukuma wananchi kubadilika? Kashfa, kutosikilizwa au ubabe wa ccm

Tano, Je,muungano wao(UKAWA) umeleta matumaini mapya au ni bahati nzuri tu imejitokeza?

Sita, kwenda mbele, je nini kinawakera wananchi Zaidi, nini vipau mbele vyao.

Bila kutathhmini hayo, wapinzani wanaweza jikuta wakifurahia jambo wasilojualinatokana na nini.
Hilo linaweza kuwa mwiba na kilio siku za mbeleni.



Tusemezane
 
Barubaru,ninashangaa unaposema kuingiza hoja zako kutavuruga uzi.
Mbona tayariumeshavuruga?

Hata sionihoja zako zenye tuhuma zinaingiaje katika uzi huu wa serikali za mitaa.

Ningekushauriutoe ushahidi katika uzi unaowezakuanzisha.
Ni haki yakondani ya jamvi isyohitaji ruhusa ya mtu

Ima hili lahisia zako, tuwaachie wasomaji waamue kwa mitazamo yao na si kwa ushawishiunaoufanya

Mwisho,narudia tena kuwa jambo unalohisi ni haki yako
Kama umeshadraw conclusion, ubaki nayo kama haki yako.
Unapoipenyezakwa hila, ni fitna.

‘’Nitasemaninachokusidia kueleza si kile mtu anachotarajia kusikia’’Kwa wasomajinawaomba radhi kwa kutoka nje ya mada.

Hakikisha unachisema au kuandika basi kiwe ni UKWELI NA KISIWE KINA USHABIKI AU CHUKI. kwani hivyo ni sumu kubwa sana katika uchambuzi wowote.

Wajapan wana usemi mmoja '' Lets share our similalities and cerebrates our differences''

'

Pole sana

 
UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA WATOA UJUMBE MZITO
CCM NA MAKUNDI SASA NJIA PANDA

NGUVU YA WANANCHI INAWATISHA
HOFU YA KUKUTANA NA KANU NA UNIP MAKTABA IMETANDA

Makundi ya Urais 2015 yapo kazini katika mitandao ya jamii yakiendelea kuhamasisha kambi zao kuungwa mkono.
Huko ni kwenye twitter, face book na blogs.

Kinachoonekana ni kunadi watu wao bila msingi kwanini fulani anafaa kubeba bendera.
Tunasikia ile hoja ya kuleta maendeleo inayotumiwa na kila mmoja

Hayo yanatokana na CCM kuwa na wakati mgumu.
Matokeo ya chaguzi za mitaa yametia baridi kwa watarajiwa kueleza misimamo yao.

Tulieleza huko nyuma, hakuna anyeajua kwa uhakika ni kitu gani kimezusha hasira dhidi ya chama kikongwe walichozoea CCM.
Ni kimbunga kinachopita kisicho na maelezo ya kina

Watarajiwa wanaingiwa na woga.
Hawajui wazungumzie kashfa, katiba au ubabe wa CCM au udhaifu wa uongozi wa chama unaokipeleka mahali pa baya.
Hawajui kama ni nguvu ya upinzani imeongezeka na nini hasa kinachotoa msukumo wa nguvu hiyo

Ni kwa mantiki hiyo, makundi ya CCM na wapambe wamekuwa waoga kuzungumzia sera, hoja na issue zinazowagusa wananchi wakichelea kutoudhi wananchi au chama.

Ukiangalia makundi ya CCM hakuna anayeeleza japo kwa ufupi ‘platform yake''
Ingawa itasemwa wakati bado, katika hali ya kawaida tungeshaanza kusikia wapambe wakijinasibu na kauli kama ''huyu anapambana na rushwa'' huyu anasimama hapa katika katiba n.k

Hofu itaendelea baada ya kutangazwa kura ya maoni ya katiba ya Chenge
Wagombea/wapambe watarudi nyuma kujiingiza kichwa kichwa katika suala wasilojua kama ndilo limeleta adhabu ya serikali za mitaa

Hofu nyingine ni kzungumzia mambo yatakayoudhi wahafidhina wanaomiliki chama kama kashfa za kifisadi

Uchaguzi wa serikali za mitaa umetoa ujumbe.
Kwamba, hakuna anayejua katika mchanganyiko ni kipi hasa kimeudhi wananchi na majibu yake si rashisi

Mfano, kama Mtwara wamekasirishwa na suala la gesi, je Morogoro na Singida wamekasirishwa na nini?

Yakizungumzia suala la katiba, je, ni matokeo ya muundo wa katiba pendekezwa au ni ubabe wa CCM kupindisha sheria au ni kudharauliwa kwa maoni ya wananchi kupitia tume ya Warioba?

Katiba ya Chenge inajulikana kama ya mafisadi.
Nani atapigia debe katiba hiyo ili apambane na nguvu ya wananchi.
Lakini pia nani ataacha kupiga debe ikiwa mafisadi ndio wanaomtengeneza mfame'' king maker''

Katika mazingira yaliyopo, lazima atatafutwa mchawi aliyesababisha chaguzi za serikali za mitaa kuwa tatizo.
''Mchawi'' mkubwa anayetafutwa ili kufuta ukweli ni uongozi wa CCM wa JK, Nape na Kinana.

Kwa bahati mbaya nani amfunge paka kengele ikiwa hao ndio wameshika mafaili muhimu?

Tusemezane
 
KIWEWEKINAITESA CCM
WANACHUKUA HATUA, TAYARI KUMEKUCHA


Tulielezachaguzi za serikali za mitaa zimeleta kiwewe kikubwa ndani ya CCM
Zimetafutwa sababu za CCM kupoteza ushawishi maeneo ya kujidai huko vijijini na baadhi ya kanda kama ile ya kusini

Tulisema,mambo yanayoiumiza CCM si moja au mawili, ni jeuri na kiburi kilichojengw akatika ulevi wa madaraka.

Kiburi cha kusahau nchi inabadilika, Tanzania ya leo si ya jana. Kiburi kilichojengwa na Imani vyombo vya dola vina nguvu zaidi ya umma na vinamilikiwa na CCM


Kiburi kama cha kuburuza katiba, na kuficha ufisadi si sababu kuu, bali ni vichochoe vya hasira walizo nazo wananchi kwa muda mrefu. Ni sababu za kutafuta namna ya kukamata fimbo na kuwaadhibu CCM kwa kiburi kilichowazidi

Huko nyuma CCM ilitumia mbinu ya kamati za uchunguzi, mchakato na maneno matamu kulaghai umma.
CCM walidhani hilo litadumu daima. Tunakumbuka kauli za vua gamba zilivyodharauliwa na ‘wamiliki wa CCM''
Na kwa jeuri wakarudi kuendelea na ufisadi wananchi wakiona
kwa macho yao


Jana CCMimewasimamisha wajumbe watatu kushiriki vikao vya CC na NEC
Hatua hiyo ni katika kurudisha Imani ndani ya jamii kuwa CCM inaweza kuchukua maamuzi magumu.

CCM haikuweza kuchukua hatua kwa miaka 8 ya wizi, ufujaji na ufisadi, ni jambo la kushangaza kama inaweza kuchukua hatua dhidi ya watu wenye pesa waliosimimishwa

Tangazo lao CCMlisemalo kamati ndogo ya maadiliinafanya kazi, ni mbinu zile zile za kuwahadaa Watanzania ili kupitisha muda hoja ife kimya kimya. Ndivyo EPA, Richmond n.k zilivyoundiwa kamati na sasahatujui zimetoa matokeo gani

CCM ilishindwa kuvua magamba, leo inawezaje kwa watu wale wale iliyowashindwa siku za nyuma.

Huu ni mchezo wa kucheza na akili za Watanzania kuelekea uchaguzi.
Suala la akina Chenge/Ngeleja/Tibaijuka halihitaji miaka 10 kuchunguzwa.

Ni sualala kuzungumzwa kwa wiki 2, leo linaundiwa kamati moja baada ya nyingine, nikununua muda na kuendelea kuwafanya Watanzania mazumbu kuku.



Kwa bahati mbaya, CCM imezinduka kukiwa kumekucha, uharibifu umefanyika
Njia iliyobaki ni kuimarisha maeneo muhimu kama tume ya uchaguzi ili kuweza kufanikisha wizi wa kura. Kinyume chake inaonekana maafa yanakuja, ni kwa kiasi gani, hilo linabaki kuwa swali

Tusemezane
 
Back
Top Bottom