Duru za siasa: Ndani ya Bunge

Duru za siasa: Ndani ya Bunge

KWANINI SERIKALI IMEKOSA ''FURSA''

Viongozi wanataka kuungwa mkono na kuombewa kwa Mungu katika vita ya maouvu.

Wananchi wameitikia wito kama waathirika,habari zinazoifikia serikali hutoka kwa wananchi

Watenda maovu wana uwezo na weledi wa juu, watashindwa kwa nguvu ya umma

Nguvu ya umma ni wadau (wananchi) wanataka kuona kweli ni vita ya kuliokoa Taifa

Wanataka kuona mizizi ya tatizo na udhati wa kushughulikia si kushangilia tuu

Hivyo serikali ilikuwa na nafasi nzuri ya kuacha mjadala wa wazi bungeni

Kwa bahati mbaya yaliyotokea chini ya Naibu Spika yameiumiza serikali

Tuliona kutupiana mpira kwa viongozi husika.
Tukasikia yakiongelewa katika mikutano kwa mafumbo, wahusika wakikaa pembeni

Serikali haikupendezwa na uwazi, ...tuanze upya 'Yaliyopita si ndwele tugange yaliyopo...'

Umma umepigwa butwaa, bungeni hadi mitaani.Ukweli haupo, mambo kwa siri na uharaka

Fursa ya serkali kujidhihiri inapamba na uhalaifu/maovu imefunikwa na hoja, tetesi na hisia tu
Hisia na tetezi hata kama ni za uongo, zinapojirudia katika jamii zinaichafua serikali

1. Kwamba, Lugumi ina watu wazito wasioweza kuguswa na serikali
2. Ushiriki wa suala hili ni mpana kuliko inavyoonekana
3. Naibu spika na uteuzi tata sasa anatumika kama ilivyohisiwa
4. Bunge limepoteza maana yake halisi na kubaki kuwa 'jumuiya ya chama'
5. Vita dhidi ya maovu inapiganwa kwa kuangalia sura na si uovu

Hisia ni nyingi tu kila mmoja akisema lake la uongo au la.
Tatizo ni kuwa serikali haina nafasi ya kujibu hoja hizo.

Katika mazingira hayo, tunawaambiwaje wamuombe mungu kushinda hii vita?
Katika mazingira kama haya, vita hii ni dhidi ya uovu au ni vita tusiyojua imelenga nini?

Ukifuatilia katika mitandaoni vinara waliokuwa wa kuetetea Hapakazi wamefadhaika.
Wamesinyaa na kuduwaa kwanini kinachosemwa si kinachotendwa 'walk the talk'

Mitaani kuna hasira za ndani 'reservations' ambazo mbele ya safari zitajitokeza

Tutajadili hilio

Tusemezane
 
WANANCHI MITAANI
WANAYAONA HAWASEMI

Kuna dhana wananchi wa mitaani hawajali na hawaoni yanayoendelea
Ipo dhana wananchi wanaamini kila wanachoelezwa na serikali
Na ipo fikra kuwa ukiwaficha wananchi, umetatua tatizo

Yote si kweli, na hujirudia kwa watu kutojifunza, au kiburi au dharau ya juu
Kiburi, dharau na kutojali ni matokeo ya kuwa na nguvu wasizonazo wananchi.

Kwamba, kikundi cha watu kimedhibiti nchi kiasi cha kufanya watakavyo
Wanatumia maguvu kuminya sauti za wananchi kwa kila hali na mahali.

CCM inafahamu madhara ya hayo. Uchaguzi mkuu makada waliona aibu kunasabishwa na chama. Kilichotokea baada ya hapo ni maguvu tu.

Wananchi walikuwa sababu hizi dhidi ya CCM

1. Dukuduku (reservations) kutokana na yaliyotendwa na CCM kwa miaka mingi
2. Kinyongo (sentiments) wananchi wamebeba hasira mioyoni kwa muda mrefu
3. Chuki (grudge) inakuwepo mioyoni kila siku

Kinyongo na chuki yalitokana na mambo kufanywa kwa utashi wa watu na si umma.
Kuufanya umma wajinga, kuudharau na hata kuudhalilisha.

Kashfa zilifichwa kwa udanganyifu na mbinu chafu, kutumia vyombo vya umma n.k.

Ilifika mahali wananchi wakisema ni afadhali kuchagua shetani kuliko CCM
Hili lilionyesha kiwango cha juu cha dukuduku,chuki na kinyongo kwa CCM/Serikali zake

Hatari kubwa si katika chuki,ni pale chuki, kinyongo na dukuduku vitakapokuwa sababu.
Hili linaweza kuvuruga hali ya uvumilivu waliyo nayo wananchi

Zipo nchi bei ya mkate tu ilileta matatizo makubwa na kuangusha serikali za nchi hizo
Chanzo si bei za mkate bali chuki na dukuduku la muda mrefu liliosubiri sababu

Kwa yanayoendelea, ikitokea sababu tena ya kijinga inaweza kutuletea matatizo.
Wakati wananchi wana maisha magumu, wanafanya kazi na wanalipa kodi

Wapo wanaoiba mabilioni na kulindwa na wale wale wanaokusanya kodi, inafikirisha.

Picha inayojitokeza, ni wananchi kutumika kisiasa 'political expedient'.

Wanaaminishwa ipo nia/dhamira ya kutatua matatizo, kukabiliana na uovu n.k.
Wanaona mambo yale yale waliyozoea yakitendwa kwa mtindo ule ule

Wananchi hawana matumaini, wanakumbatia chuki, kinyongo na dukuduku.
Wanasubiri ili wahalalishe reservations zao.

Ya Bungeni kwa ujumla wake ni ushindi mtamu wa muda mfupi na tatizo chungu muda mrefu. CCM/Serikali wasijidanganye, wananchi wana weledi na ufahamu

Wanaona,wanajua kila mbinu za kulindana.Wana chuki, dukduku na kinyongo

Tusemezane
 
CREDIBILITY
Bunge,miaka michache iliyopita lilijadili masuala ya kitaifa kwa upana na kina
Wananchi wakaliamini, likawa na ushawishi na kuaminiwa. Hicho ndicho credibility

Rais alipozungumzia hali ya uovu kwa uwazi na uchungu alipata credibility
Credibility ilimjengea 'kusamehewa' mapungufu yaliyojitokeza kwa 'benefit of doubt'!

Mathalan, Rais alipomteua Mbunge na kisha kupitishwa naibu Spika, zikazuka kelele.
Ndani ya CCM, wapo walioona ilikuwa ni dharau kwa wabunge takribani 200 wa CCM.

Wananchi katika lindi la 'hapakazi na majipu' wakasema, let it be kama itasaidia nchi
Ndivyo benefit of doubt ilivyotolewa kwa hatua zilizochukuliwa kwa bahati makosa

Kadri tunavyosonga mbele, credibility ya Bunge na serikali zinatoweka.

Kinachoonekana ni bunge kupoteza nguvu kama mhimili, na serikali kulidhibiti.

Hoja ya wanaosema naibu Spika ''alipachikwa' kudhoofisha bunge inapata miguu

Fukuza fukuza ya bunge inaamsha hisia za serikali kutokosolewa.

Kimya cha wabunge wa CCM kinatoa hisia za bunge kibogoyo.

Credibility ya bunge ipo all time low usoni mwa jamii

Serikali kuchukua hatua za kuzuia mabalozi wa nje, mikutano ya kisiasa ni kutojiamini
Suala kama la Lugumi 'limejengewa' uzio na serikali. Credibility imepotea

Lugumi si tatizo kama kampuni, ni mkataba na taarifa zinavyolindwa na usiri nyuma yake.

Katika mazingira credible, umma uhakikishiwe kuwa Lugumi/serikali hakuna utata.

Bunge linalopaswa kuisimamia serikali, linaposhirikiana na serikali kuficha , inafikirisha

Kwamba, Bunge na serikali vinapoteza credibility mbele ya jamii kwa kasi na pamoja

Bunge ni chombo cha uwakilishi. Serikali ndiyo watekelezaji wa mipango ya nchi.

Leo wananchi wataambiwa nini kuhusu 'majipu' ikiwa mengine yanajengewa ulinzi?
Hisia za utumbuaji una mengine zinapata nguvu .Kisa ni serikali kupoteza credibility!

credibility haipatikani kwa double standard hata siku moja! asilani

Kwamba Lugumi haiongelewi na viongozi na ikibidi huwa ni mafumbo.
Wakati huo huo serikali inafungia waliokwepa kodi za bilioni 1.

Machoni mwa baadhi inafikirika majipu ni visasi vya kisiasa hata kama si kweli.

Kama uongozi wa Bunge na serikali wanadhani kuwatimua wapinzani, na kulimaliza suala la Lugumi wamefanikiwa, watakuwa nje ya ukweli. Hili litaitesa serikali kwa muda mrefu

Ni bahati mbaya/nzuri upinzani umepoteza nguvu zake.
Hili la Lugumi lilikuwa ni agenda pekee mbele ya umma!kwa lilivyoshughulikiwa

Ni kiongozi gani ana credibility ya kuongelea ufisadi na anavyochukizwa nao tena?

Mbele ya majukwaa, nyuso za viongozi zitasomwa 'credible?'' yaani wanaaminika?
Viongozi wataziona nyuso za wananchi na maneno 'tutawaamiani kwa lipi tena?

Tutaendelea kucheza mduara! Tunafeli kama Taifa tukishangilia

Tusemezane
 
TATIZO LETU NI MFUMO
CCM WAMEFANIKIWA KILA KONA

Katika mfululizo wa mabandiko ya ndani ya bunge, tumelieleza Lugumi na ugumu wake

Ieleweke kuwa Lugumi ni kampuni ya biashara, na lengo la biashara ni kutengeneza faida

Ni makosa kwa wanaolaumu Lugumi kama kampuni. Wanatenda ya mfanyabiashara

Na ni makosa kuituhumu kampuni au kuitolea hukumu. Hakuna anayejua ukweli
Ukweli upo ofisi ya Spika yenye taarifa na serikali inayojua mkataba na wahusika

Ni lazima tukubali kuwa mfumo wetu umetufikisha hapa .Tupo kizani

CCM walipokataa rasimu ya katiba waliona mbali.
Walitambua mbele ya safari yasiyotakiwa kuonwa na wananchi yataonekana

Inashangaza kazi ya miaka 3 inafanywa miezi 3. Walioshindwa miaka 3 hawawajibishwi.

Inasikitisha wakaguzi wa ndani'internal auditors' hawakuona tatizo kwa miaka 3

Inastaajabisha CAG kwa miaka 3 amefanya kazi bila kuona tatizo!

Inashangaza mwenye kazi 'wizara husika' hawakujua kazi haikukamilika kwa miaka 3,

kamati imeona hilo kwa mwezi mmoja.

Inafikirisha hazina walitoa malipo kwa kazi isiyokamilika.

Na inaleta shaka bunge lilitoa mabilioni bila kufuatilia mradi husika na ukamilifu wake

Vifaa vya usalama havikukamilishwa na vyombo husika vimeendelea na kazi kwa 'ufanisi'

Hayo hayakutokea kwa bahati mbaya. Yametokea kwasababu kuu mbili

1. Ima mfumo uliopo ni 'mzuri' sana wa kufanya mambo yetu bila kujulikana
2. Mfumo uliopo ni mbaya sana usioruhusu kujua yanayofanyika

Matatizo ya mikataba , ufisadi na rushwa hayakuanza leo.
Yamekuwa yakijirudia kwa mtindo ule ule kila siku.

Hakuna anayejua hitimisho lake bali sote tumeridhika ' yaliyopita si ndwele..''

Hata kwa kutumia taarifa ya naibu Spika, leo wangetumbuliwa watu kwa makumi
Majipu ni yapi, matambazi ni yapi na vipele uchungu ni vipi? wapi hapakazi wapi jipu?

Mfumo wetu umeruhusu haya! Hakuna wa kumwangalia mwingine.
Na ikitokea, mfumo umesukwa ni ' wachezaji' tu wanajua nini kinaendelea si mlipa kodi

Mfumo wetu hauna 'watch dog' na waliopo hawana meno.

Kinachotokea ni 'systemic failure' hakuna anayeweza kumwajibisha mwingine

Hatutakwepa matatizo ufisadi, rushwa na uzembe chini ya mfumo uliopo.
Hatukuweza kwa mengi yaliyopita, iweje tudhani tutaweza leo?

Hatuwezi kufanikiwa kama watu binafsi, tutafanikiwa kama mfumo.
Mfumo unaojichunguza, jisimamia na unaotoa majibu ya kweli kwa uwazi na haki

Wale waliotuuliza 'mfumo' maana yake nini, wasiulize tena swali hilo

Tusemezane
 
WM atakapokuwa katika mikutano, anaweza kuulizwa, kinga ya kuongea nje ya bunge ameipata kwa sheria gani ikiwa yeye ni kiongozi
Kwani anaongea uchochezi, kauli za uchochezi hazikubaliki kokote kule, kauli za uchonganishi, nazani ungebadili kichwa cha habari, maana umeita habari za bunge, lakini ni habari za kusemanga Wabunge wa CCM tu

Yaani wewe huoni udhaifu wa upinzani, bungeni Kuna kanuni, watii sheria na kanuni sio kulalama
 
Kwani anaongea uchochezi, kauli za uchochezi hazikubaliki kokote kule, kauli za uchonganishi, nazani ungebadili kichwa cha habari, maana umeita habari za bunge, lakini ni habari za kusemanga Wabunge wa CCM tu

Yaani wewe huoni udhaifu wa upinzani, bungeni Kuna kanuni, watii sheria na kanuni sio kulalama
Nadhani mwingine aweza anzisha thread ya kusifu uongozi wa CCM kama hafurahishwi na mabandiko ya wale wanaoeleza facts juu ya uongozi huu. Hata hivyo nchi hii ni yetu sote na uongozi uliopo madarakani tumeuchagua sisi. Hivyo tunajukumu la kuonesha pale ambapo hawafanyi vizuri. Huo si uchochezu. Hatukuchagua miungu tulichagua watu. Tusipopata watu kama mwanzilishi wa thread hii sote tutakuja lia. Tunapenda watu wapewe nafasi ya kueleza hisia zao sio lazima tuzikubali.
 
Nadhani mwingine aweza anzisha thread ya kusifu uongozi wa CCM kama hafurahishwi na mabandiko ya wale wanaoeleza facts juu ya uongozi huu. Hata hivyo nchi hii ni yetu sote na uongozi uliopo madarakani tumeuchagua sisi. Hivyo tunajukumu la kuonesha pale ambapo hawafanyi vizuri. Huo si uchochezu. Hatukuchagua miungu tulichagua watu. Tusipopata watu kama mwanzilishi wa thread hii sote tutakuja lia. Tunapenda watu wapewe nafasi ya kueleza hisia zao sio lazima tuzikubali.
Kwani kichwa cha Threads kinasemaje, alitakiwa kua huru kusema yote yanayoenenda katika bunge sio kuangalia upande wa kusemanga.
 
Nadhani mwingine aweza anzisha thread ya kusifu uongozi wa CCM kama hafurahishwi na mabandiko ya wale wanaoeleza facts juu ya uongozi huu. Hata hivyo nchi hii ni yetu sote na uongozi uliopo madarakani tumeuchagua sisi. Hivyo tunajukumu la kuonesha pale ambapo hawafanyi vizuri. Huo si uchochezu. Hatukuchagua miungu tulichagua watu. Tusipopata watu kama mwanzilishi wa thread hii sote tutakuja lia. Tunapenda watu wapewe nafasi ya kueleza hisia zao sio lazima tuzikubali.
Ahsante sana, na pia angeweza kueleza upande anaoona una tatizo kwa mantiki na hoja.

Tendo la kusubiri yaandikwe anayofikiri yeye linasikitisha.
Ni ukweli pia, ana uwezo wa kuanzisha nyuzi ku 'rebuttal' au defend anachokiona yeye.
 
Back
Top Bottom