Duru za siasa: Sakata la Mawaziri

Duru za siasa: Sakata la Mawaziri

Wakuu Nguruvi3 na FJM,
Kwa kweli hakuna mlichobakisha katika uchambuzi wenu juu ya the root-cause ya tatizo lililopo mbele yetu; nadhani miongoni mwa maswali ni muhimu ni pamoja na kwamba:

*Tutarajie Rais afanye nini katika kipindi hiki kilichobakia kuelekea 2015?

Kwa mtazamo wangu, ni vigumu sana kwa nchi kupata tiba dhidi ya ugonjwa wa "Big Man rule" pamoja na mizizi yake katika kipindi kifupi, na pia chini ya katiba ya sasa; mabadiliko yoyote yale yatakuwa tu na "face value" na kuacha the rotten "intrinsic value" intact;

Pia kwa wale wanaofuatilia media, nadhani mmeona waziri mmoja akimlaumu waziri mkuu kwamba alikuwa anampa taarifa zote, hatua kwa hatua, lakini waziri mkuu hakuchukua hatua yoyote; kwa mtazamo wangu, hili litakuja kuleta mtafaruku mkubwa sana ndani ya chama tawala iwapo waziri mkuu atabakia kwani wabunge na mawaziri wengine watakuwa na wasiwasi mkubwa wa kujimaliza kisiasa kuelekea 2015 kwa kumtumikia waziri mkuu asiyekuwa na maamuzi magumu;

Kuna haja ya Rais Kikwete kutumia busara kubwa sana katika kuteua safu itakayo kifikisha chama (ccm) kikiwa kinajitambua tambua angalau kidogo;

A mini solution kwa sasa ni:

1.Rais kuja na safu nzuri ya mawaziri ambao watasaidia serikali kuondokana na mawaziri vihiyo wasio na majibu ya maana kwa hoja za wabunge bungeni;

2.Rais kuja na performance contract ambayo mawaziri watasaini, kama ilivyofanyika ghana;

3. Rais kupunguza ukubwa wa baraza la mawaziri;

4. Serikali kutumia fursa ya bajeti ijayo kuja na vipaumbele vinavyoendana na mahitaji ya wananchi walio wengi, hoping kwamba Kinana na Nape wamekusanya maoni vizuri, na pia hoja za wapinzani katika ziara mbalimbali zimesikika;

5. Matatizo ya kimfumo yafanyiwe kazi taratibu kupitia legislations mbalimbali zinazolenga reforms katika maeneo tajwa; mchakato huu hauwezi kuchukua mwaka mmoja lakini unaweza anza sasa as long as there's a POLITICAL WILL;


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mchambuzi#21 hapo juu
Kwa kipindi ilichobaki tusitarajie jambo lolote kutoka kwa rais JK
1. Ameshatambua aliyodhani angeweza kuyafanya hajafanya na hana muda
2. Hana watu wa kumsaidia, kila mmoja anaangalia 2015 kwa mtazamo wa makundi

Kitendo cha kutangaza operesheni na kuisifia huku ikiwa imefeli kwa kiwango kizuri tu ni ushahidi
a) Anatimiza wajibu, kuendelea kukaa kimya ni aibu
b)Vyombo vilivyopaswa kumpa taarifa havina shughuli tena bali kuendelea na kujipanga
c) Kushindwa kuwatimua mawaziri kwa ridhaa yake na kutegemea bunge ni kukata tamaa
d) Waziri mkuu kushinikizwa ajiuzulu ni dalili washirika wameona sasa ni la kuvunda halina ubani.

Kuelekea 2015 kikubwa yatakayofanyika ni haya
1. Kutoa shukrani kwa waliomsaidia kumaliza ngwe kwa kugawa nafasi kama ubalozi na nyingine
2. Kufanya mabadiliko ya kile ulichokisema ni face value bila kuwa na delivery yoyote.

Kuhusu hoja za mini solution;
Hoja#5 : Mfumo umekuwepo na sidhani kama tatizo ni mfumo wenyewe.
Tatizo ni watu walioridhika na mfumo huo wakijua haupo sawa, kwa manufaa yao wakakaa kimya.

Tatizo ni uongozi wa nchi ulioshindwa kubadili mfumo au kusimamia mbovu uliopo.

Hoja#4 : Kutumia bajeti ijayo haitawezekana,hali si nzuri na wajomba'donors' wamechoka ufisadi.
Pili, sidhani yupo katika serikali anayefikiri vipau mbele na kuvisimamia.
Ni wachache sana ambao hawaungwi mkono na uongozi. Wengi wao kipaumbele ni 'season finale' 2015.


Hoja#3: Kupunguza ukubwa wa baraza la mawaziri litamsaidia kubaki japo na timu ndogo kumudu shughuli za kawaida za serikali.

Tatizo ninaloliona ni kuudhi baadhi wa watu waliojipanga kwa 2015, na JK hapendi kuudhi mtu, hapo sijui atawezaje kulikamilisha hilo wazo zuri

Hoja#2 Wakati anaanza urais, JK alipita kila wizara kupanga malengo naweza kusema ni performance indicator. Hakurudi kufuatilia nini kimefikiwa nini kimekwama.Performance indicator ya ghana ilikuja baada ya wanchi kuchoshwa na ubabaishaji kama wa Tanzania.

Ili kufanikisha PI kunatakiwa mtu awe hana urafiki au uswahiba wa aina yoyote.
Je JK naweza kufanya hivyo bila kuudhi watu! siku zote hapendi kuudhi mtu.

Hoja#1 Kwa safu nzuri pengine anaweza kuwachukua baadhi wamsaidie kazi japo kipindi kifupi ili asiporomoke zaidi ya hapo alipo.Magufuli, Mwakyembe, Tibaijuka ndio wanaoweza kumsaidia kwa ukaribu.

Wasi wasi wangu ni kuwa viongozi wanaoweza kumsaidia kama watapewa nafasi ya kufanya hivyo. Magufuli aliposimamia ubomoaji wa nyumba karibu na barabara, Rais aliyepaswa kumsaidia ndiye alimgeuga na kusema zoezi liachwe.

Mwakyembe anayepigana na Bandari na TAZARA ameachiwa mwenyewe. uongozi wa nchi haupo karibu

Kituo cha BRN (Big result now) bado kinasubiriwa kije na makakati wa big result.
Hiki kipo chini ya ofisi ya rais, kama Unit iliyoko chini ya ofisi ya rais haiwezi ku deliver, zile za nje itakuwaje.

Nimalizie kwa kusema kama ningeulizwa katika uchovu uliopo nani awe PM ningesema Mwakyembe,kwasababu zifuatazo
1. At least anafuatilia kile walichokubalina na watendaji wake
2. Haonekani kujali uswahiba zaidi ya kazi na ana uthubutu wa hata kufukuza si 'kuengua'
3. Ana uthubutu wa kufanya jambo, mfano kuanzisha usafiri wa reli. Ingawa wazo lilikuwepo katika public domain kwa muda mrefu, Mwakyembe alilifanyia kazi.
Pamoja na vitendea kazi na bajeti ndogo, tunaweza kusema amejaribu na ameonyesha inawezekana.
 
SALAMU ZA MWAKA MPYA ZA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHESHIMIWA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE KWA WATANZANIA,
TAREHE 31 DESEMBA, 2013
Ujangili wa Wanyamapori

Ndugu Wananchi;
Mwaka huu tuliongeza nguvu katika kupambana na ujangili wa wanyamapori na uvunaji haramu wa rasilimali za misitu. Hili ni tatizo la siku nyingi lakini katika miaka ya hivi karibuni limekuwa kubwa mno na kuwazidi nguvu Askari wa Wanyamapori na Maafisa Misitu.

Kwa nia ya kuwaongezea nguvu, mwaka 2010 niliagiza Jeshi la Polisi lisaidie Idara ya Wanyamapori na Idara ya Misitu katika kupambana na uhalifu huo. Operesheni kadhaa ziliendeshwa maeneo mbalimbali nchini na mafanikio ya kutia moyo yalipatikana. Lakini, kwa kutambua ukubwa wa tatizo na hasa kwa upande wa aina ya silaha na mbinu zinazotumiwa na majangili niliamua kuhusisha vyombo vingine vya usalama likiwemo Jeshi la Ulinzi. Nia ni kuongeza nguvu ya mapambano. Ndipo ilipoanzishwa "OPERESHENI TOKOMEZA".

Ndugu Wananchi;
Kazi nzuri imefanyika chini ya Operesheni hiyo. Mafanikio ya kuleta matumaini yameweza kupatikana. Mitandao ya ujangili imeweza kutambulika na wahusika wake kadhaa wametiwa nguvuni. Mitandao hiyo inahusisha watu wa aina mbalimbali. Wamo raia wa kawaida, wapo watu maarufu, wapo watumishi wa idara mbalimbali za Serikali wakiwamo wa Idara za Wanyamapori na Misitu. Watu 1,030 walikamatwa pamoja na silaha za kijeshi 18, za kiraia 1,579 na shehena kubwa za meno ya ndovu na nyara nyingine navyo vilikamatwa.Watu kadhaa tayari wameshafikishwa mahakamani.

Ndugu Wananchi;
Wahenga wamesema "kwenye wengi pana mengi". Katika utekelezaji wa Operesheni hii kumekuwepo na taarifa za kufanyika makosa kinyume na malengo na madhumuni ya Operesheni. Niliagiza baada ya kumalizika kwa awamu ya kwanza, zoezi lisitishwe kwa muda ili uchunguzi ufanyike, kasoro zitambuliwe na waliofanya makosa wachukuliwe hatua zipasazo. Wakati kazi hiyo inafanyika suala hilo lilijadiliwa Bungeni na Kamati Teule kuundwa. Matokeo yake sote tunayajua. Mawaziri wanne wamewajibika kisiasa.

Ndugu Wananchi;
Napenda kutumia nafasi hii kuwapa pole Mawaziri wetu hao kwa matatizo yaliyowakuta. Nawapongeza kwa uamuzi wa kukubali kuwajibika kwa makosa yaliyofanywa na maofisa wa chini yao. Wameonesha ukomavu wa kisiasa na kiuongozi wa hali ya juu na moyo wa uzalendo.

Kama mlivyosikia nitaunda Kamisheni ya Uchunguzi itakayoongozwa na Jaji wa Mahakama Kuu. Uchunguzi wa kina utafanywa kuhusu kadhia yote hiyo. Makosa yaliyofanyika yataainishwa na waliofanya kutambuliwa ili wachukuliwe hatua zipasazo kwa mujibu wa sheria na kwa mujibu wa kanuni za utumishi wa umma.

Ndugu Wananchi;
Ni muhimu kufanya hivi ili haki itendeke ipasavyo. Mtindo wa mzigo wa makosa ya watumishi wa umma kubebwa na viongozi wa kisiasa pekee, tena wasiokuwa na hatia ya moja kwa moja, siyo sahihi. Lazima kila mtu abebe mzigo wake inavyostahili. Ni matumaini yangu pia kwamba katika siku za usoni kunapotokea matatizo ya namna hii uchunguzi uwe wa kina ili wale hasa waliohusika na kutenda makosa wawajibishwe. Uwajibikaji wa wana-siasa peke yao hautoshi, kwani huwaacha waharibifu waendelee na kazi isivyostahili. Mtindo huu utawafanya watumishi wasione umuhimu wa kutokurudia makosa. Hata hivyo, pale kwenye ushahidi wa wazi kwamba kiongozi wa kisiasa angeweza kuchukua hatua za kuzuia madhara lakini hakufanya hivyo lazima kiongozi huyo awajibike.
Ndugu wanajamvi, kipande hicho ni sehemu ya hotuba ya rais. Ningependa tukiangalie kipande kuhusiana na mada iliyopo.

Kwanza, Rais anasema tatizo lipo muda mrefu na siku za karibuni limeongezeka sana.
Mh, kama tutayaangalia matatizo kwa muda ili kujiondoa lawama hilo bado halitasaidia.
Mh Rais yupo katika baraza la mawaziri kwa muda mrefu na ni sehemu ya ukomavu wa tatizo.

Pili, kuongezeka kwa tatizo siku za karibuni kunaeleza udhaifu wa serikali uliyotoa mwanya kwa wahalifu. Rais alipaswa ajiulize udhaifu huo ni kwanini umekua kuliko siku za nyuma.

Rais amerudia tena kauli yake kuwa operesheni Tokomeza imefanikiwa.
Akasema kuna mtandao unahusisha maafisa wanyama pori, watu maarufu, wafanyabiashara.

Duru za siasa tunashangaa kwanini rais atambue sasa ili hali ana vyombo vya ulinzi na usalama. Ina maana serikali ya JK haikujua tatizo hadi operesheni ilipoanza?


Ina maana wanyama walipokamatwa KIA hakukuwa na ufuatiliaji kujua mtandao huo.
Hii inaeleza udhaifu wa serikali kulishughulikia tatizo ni kauli tamu inayozua maswali zaidi

Tukumbuke mwanzo rais kasema tatizo ni la muda mrefu, kwa maana nyingine halikuwahi kushughulikiwa hadi operesheni ilipoanza.

Tunawezaje kuishi na tatizo kwa muda mrefu kwasababu ni dogo?
Ina maana rais hakuona ni tatizo linalokua tukizingatia amekuwa kiongzi ya uwaziri muda mrefu!

Tunajiuliza hivi waliokamatwa wamechukuliwa hatua gani na kwanini iwe hao na si mtandao wa viongozi ambao umegusa hata maeneno ya ulinzi na usalama yaliyoruhusu dege la Qatar kutua!!

Kuna sababu gani za kukamata mtu mwenye gobore na kuacha dege la kijeshi la Qatar bila kujua lilitua vipi na kwa idhini ya nani. Hapa mh anacheza na maneno, hakueleza tatizo kwa kina chake, alichokifanya ni kujaribu kuonyesha analishugulikia pengine kuonyesha kujali.

Rais anasema matokeo ya awamu ya kwanza ya operesheni Tokomeza ni pamoja na mawaziri wanne kuwajibika kisiasa.

Tumeeleza huko nyuma kuwa alichokifanya rais ilikuwa kujificha nyuma ya tangazo la kuwafukuza mawaziri kazi kwa kumtumia Pinda akikwepa kuudhi watu na si sehemu ya utaratibu wake hata kama kuna ulazima

Tunafahamu waziri aliyejiuzulu ni Kagasheki, wengine walisemwa kuenguliwa.
Duru za siasa tumehoji sana katika mabandiko yaliyopita kuhusu suala la kuenguliwa.

Alichokifanya rais ilikuwa kutumia maneno ya kisiasa asionekana kama amewafukuza kazi.
Leo anarudi kwa mlango wa nyuma na kusema wamewajibika kisiasa akimakana Pinda aliyesema wamefukuzwa. Ni utaratibu ule ule wa kukubaliana kuvunja nyumba halafu kumruka Magufuli
Ni utaratibu ule ule wa kukubaliana kuhusu Richmond na mwisho kuwaruka wenzake

Si kweli, waziri aliyewajibika ni mmoja wengine ni kutokana na shinikzo la bunge.
Rais anatakiwa asimame katika hoja, kama aliwafukuza au aliwaengua au waliwajibika kisiasa.

Kinyume chake ni kuchanganya wananchi. Hakuna anayejua rais anasimamia wapi katika hili.
Tena ameongeza kauli ya kuwapa Pole, maana yake hakuwafukuza bali walijiondoa kisiasa.

Hapa tulishasema JK ni mtu wa sura mbili, anaweza kukuuma na kurudi kupulizia lakini basi linapofanyika kwa maisha ya watu na rasilimali za taifa ni jambo la kusikitisha na hatari sana. Linauchanganya umma na vyombo vingine.

Hivi kweli kwa uchafu wa operesheni tokomeza na uzembe wa mawaziri husika rais anaweza kusema wamewajibika kisiasa na si makosa!!

Bandiko la hapo juu tumesema muda si mrefu tutawasikia mawaziri hao katika nafasi za ubalozi, huu ndio mwanzo wa kuwasafisha ili awape ulaji siku za usoni.

Udhaifu zaidi ulio onyeshwa na JK ni kuunda kamisheni kushughulikia tatizo
Hakuna aliyechukuliwa hatua wanyama waliposafirishwa KIA na dege la kijeshi, makontena yakikamatwa Hong Kong na uchafu mwingi tu ambao serikali ya JK imeufumbia macho, leo anaunda kamisheni ili ifanye nini.

Ningemwelewa kama angeanza kuwawajibisha makatibu wakuu na wakurugenzi kwa kuwaweka pembeni ili uchunguzi ufanyike, hakufanya hivyo anachokifanya ni kutupa lawama kwa kamisheni ili abakie bila kuudhi mtu.

Huu ni aina ya uongozi dhaifu sana katika historia ya nchi yetu, hakuna kiongozi anayeongoza kwa 'remote' control.

Ni ima awe na nia au basi aachie tembo wamalizike sio double standards anazozieleza.

Mh Rais anajibu hoja kuwa tatizo ni mfumo. Yeye kama raia wengine anabaki kulalamika tu, sijui nani mwenye ufumbuzi.

Nilidhani tatizo la mfumo angekuwa ameliona siku nyingi akiwa waziri na sasa rais, cha kushangaza anaendelea kulalamika na mfumo unaowaonea wanasiasa.
Hakuna mwasiasa anayeonewa kwasababu kazi ya siasa siyo professional na asiyeweza akae pembeni.

Hao anaodai wanaponza viongozi wa siasa ni yeye amewateua, ana wajibu wa kutengua teuzi na kuwachukulia hatua.

Rais hapaswi kualalamika kama wananchi wengine, nani anaongoza na nani anaongozwa.

Tatizo la ujangili si kubwa kiasi hicho, ukubwa wake unatokana na udhaifu wa uongozi wa nchi kama tulivyoona.

Kama rais analalamika na kuwafariji watu waliosababisha vifo kwa wananchi hilo ndilo tatizo.
Kama rais analalamika uwepo wa mtandao wa watu maarufu na yeye pamoja na vyombo husika hawawezi kuchukua hatua, tatizo si ujangili ni watu wa kuongoza vita ya ujangili.

Tusemezane
Mzee Mwanakijiji Mchambuzi Mkandara zumbemkuu zidane Ditto platozoom Katavi Ogah Mag3 FJM
 
Last edited by a moderator:
Hivi kuna ugumu gani wa kuwafahamu watendaji wa serikali wanaohujumu maliasili zetu.....mbona Dr. Mwakyembe kaingia Wizara ya Transport na kukuta uozo na kuchukua hatua....ingawa sio very effective.......atleast tunaweza kusema Mwakyembe amejaribu........

Hivi kweli Rais na Mawaziri wetu pamoja na vyombo vyote vilivyo chini yao anashindwa kuwa na taarifa za nani anahusika na ujangili au uhujumu wa maliasili zetu na kuchukua hatua?...........mpaka kila wakati tume ziundwe?.....I really miss Sokoine.........Hivi kwenye issue kama ya KIA......hivi kuna haja kweli ya kungoja tume iundwe ili watu wawajibishwe.....au kumuwajibisha mtu ni lazima umfukuze?.......

Inasikitisha sana unapoona Rais wa nchi anakubali kushindwa na wahujumu uchumu wa nchi yetu.....hiyo quote inaonyesha ni jinsi gani.....viongozi wetu ambavyo hawajui jinsi ya kutatua matatizo.....

Tatizo jingine walilonalo viongozi wetu ni kuwa....wanaposoma critics ndani ya JF wanakuwa offended......na kuanza kuleta kejeli kuwa watu wa JF......
 
Hivi kuna ugumu gani wa kuwafahamu watendaji wa serikali wanaohujumu maliasili zetu.....mbona Dr. Mwakyembe kaingia Wizara ya Transport na kukuta uozo na kuchukua hatua....ingawa sio very effective.......atleast tunaweza kusema Mwakyembe amejaribu........

Hivi kweli Rais na Mawaziri wetu pamoja na vyombo vyote vilivyo chini yao anashindwa kuwa na taarifa za nani anahusika na ujangili au uhujumu wa maliasili zetu na kuchukua hatua?...........mpaka kila wakati tume ziundwe?.....I really miss Sokoine.........Hivi kwenye issue kama ya KIA......hivi kuna haja kweli ya kungoja tume iundwe ili watu wawajibishwe.....au kumuwajibisha mtu ni lazima umfukuze?.......

Inasikitisha sana unapoona Rais wa nchi anakubali kushindwa na wahujumu uchumu wa nchi yetu.....hiyo quote inaonyesha ni jinsi gani.....viongozi wetu ambavyo hawajui jinsi ya kutatua matatizo.....

Tatizo jingine walilonalo viongozi wetu ni kuwa....wanaposoma critics ndani ya JF wanakuwa offended......na kuanza kuleta kejeli kuwa watu wa JF......
Ogah, tatizo la viongozi waliopo ni kubwa kulikotunavyoliona.

Waziri mkuu kasema mawaziri wamefukuzwa, rais anasema poleni mumewajibika kisiasa.
Bunge limesema waziri mkuu EL awajibike kwa uzembe, rais anasema hiyo ni ajali ya kisiasa.
Bunge linasema wateule wa rais wanachukua rushwa, juzi wamesafishwa taratibu
Magufuli anasema tusimamie sheria, rais anasema msilete kero kwa wananchi.
Hapo utaona tatizo linapoanzia.

Magazeti ameonyesha taarifa zote za kuibwa wanyama KIA, hakuna kiongozi aliyelizungumzia suala hilo, wakakakamatwa walinzi wa mlangoni.

Hivi kuna korokoni wa Tanzania anayeweza kuidhinisha ndege ya kijeshi kutua nchini?
Anayways sijui suala limekwisha au lipo mahakamani.

Meli ya Mtanzania imekamatwa ikiwa na meno ya tembo hakuna anayeshtuka meli ilibebaje mzigo isioujua.
Malori ya bangi yakikamatwa yanazuiliwa polisi hadi kesi imalizike.
Kuna sheria za wamiliki wadogo na wakubwa!

Majangili wanapoizidi serikali nguvu inatisha
Mtandao wa ndovu unajulikana, tatizo una watu wazito

Hili la wanyama ni udhaifu tu wa uongozi wa nchi na serikali.
Mchina atoke kwao aje afunge pembe serikali haijui kweli. Endapo haijui usalama wa taifa hili upo wapi!

Pamoja na kusema critic za JF bla bla, ukweli wanauona.

Mwisho wa siku rais anawajibika kwa matatizo yanayotokea.
Wanyama hawakuwahi kuuawa kiasi hiki awamu zote kwanini itokee sasa?
Kenya na South A wameweza vipi?

majibu ni kuwa hakuna aliye tayari kushughulikia tatizo kwasababu mitandao inayohusisha wauaji wa tembo ima wana mikono au ni ya washirika wao.

Rais anapolalamika kuhusu kuuawa tembo akiwa na kila chombo cha utendaji hapo lipo tatizo.
Tulitegemea rais aeleze tatizo limekwishaje si kusema ni la muda mrefu. Kama ni la muda yeye anafanya nini kulimaliza?

Kagasheki kasema makatibu wakuu walipanga mipango ya kumweka pembeni. Makatibu wakuu wanateuliwa na rais wakiwaemo wakurugenzi, leo badala ya rais kuongoza anakabidhi kazi zake kwa tume ya kimahakama.

Majangili si tatizo ni dalili za tatizo la ombwe la uongozi.
 
Nguruvi3,


Wakati wa saga la mawaziri Omar Nundu na Cyril Chami na baadae Jairogate,wabunge wengi, hasa wa CCM akiwemo mama Anna Kilango, waliongea sana juu mfumo wa uongozi/utendaji kwenye Wizara. Na kubwa ilikuwa ni kwamba mawaziri wako kama 'ceremonial figures' kwenye wizara zao kwani nguvu kubwa inakuwa kwa katibu na wakuregenzi. Na wengi walikuwa wanasema hawa makatibu hawasukumiki maana nao ni Presidential appointees.

Pia kulikuwa na mapendekezo (toka kwa wabunge) kuwa kama wizara inaboronga, basi adhabu isiishie kwa wateule wa kisiasa - yaani waziri- bali iwe kwa wote, waziri, naibu waziri, katibu mkuu na watendaji wote waliohusika. Kwa kumbukumbu zangu, hata rais mwenyewe alionekana kukubaliana na huo ushauri, na aliwahi kunukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa 'kuanzia sasa' nidhamu itatolewa kwa 'wote'.

Lakini tatizo la nchi ni lile lile - maneno bila vitendo. Huu mchezo wa kuchomoa mtu mmoja mmoja ni kiini macho. Matatizo yatabakia pale pale. Hivi mawaziri wanafanya kazi peke yao? Watendaji wakuu kwa nini hawaguswi. Naibu waziri au katibu wa wizara wanaachwa kwa sababu zipi?

Pili, kuna hii tabia ya wanasiasa kucheza na akili za watanzania. Chukua mfano mmoja. Lazaro Nyalandu alikuwa naibu waziri wa viwanda na biashara wakati Cyril Chami anafukuzwa. Wakati Waziri wake anafukuzwa ,yeye Nyalandu alihamishiwa Wizara ya Utalii na maliasili, ambako nako waziri wake amefukuzwa lakini yeye kabaki! Na kwa ujasiri wa kipekee tangu Kagasheki aondoke, Nyalandu amekuwa anauza sura kwenye vyombo vya habari ili aonekane ni mchapa kazi! Hivi Nyalandu alikuwa wapi wakati wamama wanabakwa? Nyalandu alisema nini wakati watu wanachomewa makazi yao?
 
Last edited by a moderator:
Asante Mkuu Nguruvi3

ukiwa na viongozi ambao ni wavivu kusoma na kutegemea watu mediocre/failures (ambao ni wavivu) waliowateua ili wawasaidie matokeo yake ndio hayo......wanabaki kupiga "mikwara" bila vitendo......kwa kweli kuna kazi kubwa sana mbele yetu.....ya wengi wetu kutambua hili suala........na hawa mediocre people waliopo kwenye nafasi nyeti ndio wepesi wa ku-dismiss hoja za nguvu.....kwa kuwa ili wafuate na kutekeleza hoja za nguvi inabidi wao wawajibike nafasi zao kwanza........sasa hapo ndio utaona dawa ni moja tu......kufumua mfumo mzima....

Mkuu FJM heshima mbele......hawa manaibu waziri hakuna lolote zaidi ya kuuza sura kwenye Wizara husika......wao huwa ni uwakilishi wa kujibu maswali bungeni, ziara ambazo waziri hawezi kuhudhuria na kwenye matangazo......hivi hawa manaibu huwa wanaigia kwenye Cabinet kweli?......
 
Last edited by a moderator:
Najaribu sana kujiuliza hivi hiyo kabineti mpya ya Mawaziri watakuwa na tofauti gani ktk wajibu wa kazi zao tofauti na hawa waloachishwa madaraka? Jamani ukweli tuuzungumze huyo waziri mpya atafanya nini kuzuia Mjangili ama mauaji ikiwa watendaji wetu ni wale wale walokuwa ktk mtandao wa Ujangili na mauaji?
 
Najaribu sana kujiuliza hivi hiyo kabineti mpya ya Mawaziri watakuwa na tofauti gani ktk wajibu wa kazi zao tofauti na hawa waloachishwa madaraka? Jamani ukweli tuuzungumze huyo waziri mpya atafanya nini kuzuia Mjangili ama mauaji ikiwa watendaji wetu ni wale wale walokuwa ktk mtandao wa Ujangili na mauaji?
Mkuu hapa umeleta point muhimu sana. Hakuna chochote kipya kama watendaji ni hao waliopo katika mtandao. Mh Rais anajua hilo lakini ujanja ujanja tu kwasababu wale watendaji hawapo kwa merit wapo kwa kufahamiana.
Nakubaliana nawe kabisa kuwa waziri ajae ni kama anaanza upya tena bila kujua mtandao. Kagasheki alikuwa anaujua na alipigwa vita na watendaji ambao ni wateule wa Rais, alipiga kelele lakini Rais hakumsaidia.
Ndio maana nasema ujangili si tatizo, tatizo ni nia ya kulishughulikia na utayari wa viongozi.
 
UJANGILI UNAVYOIDHALILISHA NCHI YETU
Habari za wiki hii ni kuhusu ziara ya rais Kikwete London kuhudhuria mkutano wa viongozi 50 chini ya mwana wa mfalme Charles.


Mkutano unajadili kuhusu viumbe hai waliokaribu kutoweka.
Ni habari iliyopamba magazeti ya UK huku Tanzania ikitajwa kufumbia macho suala la ujangili.


Maoni ya Watanzania ni kutuhumu gazeti la the daily mail la uingereza kwa kuisakama serikali. Waziri husika kakanusha habari na moja ya utetezi wake ni Tanzania kukamata zaidi ya tani 20 za meno ya tembo.


Utetezi wa aina hii si tu unamdhalilisha rais bali nchi kwa ujumla wake.

Hatukutegemea waziri aeleze Tanzania inavyozuia uuzwaji wa pembe baada ya tembo kuuawa. Tulitegemea waziri aeleze Tanzania inavyozuia tembo kuuawa.


Duru tunasema kwa hili la tembo kuna kuzembea kwa makusudi.
Imeandikwa na magazeti nchini na sasa nje, mtandao ni mkubwa ukihusisha watu ndani ya serikali.


Kusema kuwa hizi ni njama za kuichafua nchi hatukubaliani na utetezi huo, tumeshindwa kuzuia ujangili na unabaki kuwa ukweli.
Kwamba, rais anaposema ujangili umekuwepo siku nyingi ni kukwepa majukumu yake.

Hatutarajii rais aieleze dunia tatizo lina muda gani, tunategemea rais aeieleze dunia nini kimefanyika kukabiliana na ujangili kwa takwimu na vithibitisho.


Ukweli kwamba kontena lilikamatwa likiingizwa katika meli ya kijeshi, na ukweli kuwa makontena yamekwamtwa kila mahali duniani yakitokea Tanzania na hakuna anayewajibika ni ushahidi kuwa serikali imeshindwa au ina washiriki wa uhalifu huu.


Ni jambo la kushangaza kuona serikali yenye vyombo vyote vya ulinzi na usalama ikishindwa kuwachukulia hatua za kisheria wahalifu.
Kesi zinapigwa dana dana na mwisho hutoweka kinyemela huku tembo wanatekea.

Hata ilipotokea nafasi ya rais kufanya mabadiliko ya safu yake hakuna kipya.

Waziri aliyepo hana historia ya uthubutu wa kupambana na mtandao mzito wa ujangili.


Kibaya zaidi hata watajwa wa ujangili wanapowekwa hadharani serikali imewakingia kifua kwa namna moja au nyingine.


Ni kwa mtazamo huo hatudhani kuwa Waingereza wanachuki na Tanzania au Rais wetu.

Walichiokifanya ni sahihi kwa kuueleza ulimwengu lipo tatizo Tanzania na si Kenya au South Africa kwenye tembo kama sisi.


Kwamba tatizo la Tanzania si upungufu wa rasilimali watu au vinginevyo ni upungufu mkubwa wa utashi wa viongozi kusimamia kampeni dhidi ya Tembo. Ni kukosa dhamira ya kweli moyoni, na ni kukosa uchungu wa rasilimali ya nchi yetu
Ni ushiriki wa mtandao mkubwa uliopo serikali jambo lililosemwa na waziri aliyejiuzulu.


Badala ya kuwalaumu waingereza walioandika, tunapaswa kuwapongeza kwa kusem.
Serikali na wananchi wa Tanzania wameshindwa, vipi akijitokeza awaye na kulieleza hata kama hakupendezi?


Je tulitaka Waingereza waseme kuna mafanikio wakati tembo wanauawa si chini ya 30 kwa mwezi. Kuna mafanikio yapi hapo.
Na kwanini isiwe Botwsana, Kenya au South Africa.

Je si ukweli kuwa majangili wanatumia udhaifu uliopo Tanzania kumaliza tembo?


Tusemezane

 
........Kwamba tatizo la Tanzania si upungufu wa rasilimali watu au vinginevyo ni upungufu mkubwa wa utashi wa viongozi kusimamia kampeni dhidi ya Tembo. Ni kukosa dhamira ya kweli moyoni, na ni kukosa uchungu wa rasilimali ya nchi yetu
Ni ushiriki wa mtandao mkubwa uliopo serikali jambo lililosemwa na waziri aliyejiuzulu
.
...........

Mkuu...huo ndio ukweli wenyewe.....wale wazalendo wachache waliopo wanapigwa vita......iweje Waziri awajibishwe Naibu wake abaki?......tena akapandishwa ngazi na kuwa Waziri kamili!!.......haya mambo ya urafiki rafiki na kuendekeza siasa kwenye mambo muhimu ya Kitaifa ndiyo yanayotu-cost kweli kweli.......

Ni kweli Majangili wanatumia udhaifu wetu kuhujumu maliasili zetu....period!
 
Mkuu...huo ndio ukweli wenyewe.....wale wazalendo wachache waliopo wanapigwa vita......iweje Waziri awajibishwe Naibu wake abaki?......tena akapandishwa ngazi na kuwa Waziri kamili!!.......haya mambo ya urafiki rafiki na kuendekeza siasa kwenye mambo muhimu ya Kitaifa ndiyo yanayotu-cost kweli kweli.......

Ni kweli Majangili wanatumia udhaifu wetu kuhujumu maliasili zetu....period!
Ogah waziri Kagasheki aliposema majangili watandikwe risasi ile ilikuwa ni frustration ya kuona wanyama wanakwisha na jitihada zake zinakwamishwa na wanamtandao kwa kutumia serikali.

Katika mazingira ya kwaida ya kiutawala, makatibu wakuu na wakurugenzi waliodharau na kumtenga Kagasheki walitakiwa wasafishwe na pengine wawe wamesimama mbe ya vyombo vya sheria. Hakuna kilichotokea kwasababu ni mtandao mzito unaohitaji nguvu kubwa (na si ombwe) kukabiliana nayo.

Niliishiwa na nguvu za mwili (siyo zile za MMU) niliposikia waziri wa sasa akitoa uetetezi kuwa serikali inajitahidi kukabliana na majangili kwavile imekamata zaidi ya tani 20 za pembe za ndovu. Huu ndio uetetezi wa waziri anayepambana na majangili tena mbele ya jumuiya ya kimataifa.

Kwamba kwa waziri muhimu ni serikali kukamata pembe baada ya ndovu kuuawa na si kuzuia ndovu kuuawa.

Hili halina tofauti na zile 'jitijahada' za serikali za kukamata wanyama pale KIA na kuliacha dege la kijeshi likiruka katika anga za nchi yetu raha mustarehe.

Jitihada za waziri wa mali asili ni kukamata meno ya ndovu! na hapo ndipo anapotilia mkazo.
Ikifika hapo unaona ni jinsi gani tatizo lilivyo pana kuanzia juu hadi chini.

South Africa faru wanaongezeka, Tanzania wanakwisha.
Kenya hakuna kukamata meno, Tanzania wapo bize kukamata meno.

Majangili yanajua udhaifu wa serikali yetu vema sana na yanautumia kikamilifu kumaliza rasilimali.
Hatuna shida ya pesa, wafanyakazi au silaha. Tuna tatizo na uongozi wa kupambana na majangili.

 
Back
Top Bottom