Asante kwa maelezo mazuri juu ya kile kinachoendelea huko US kuhusu uchaguzi.
Hapa Mwalimu wangu pamoja nawengine mmeniacha njia panda. Kwa mara ya kwanza nilipoleta humu habari za rigging ya uchaguzi kutoka kwa Trump, mnilipinga vikali na kubeza suala hilo.
Sasa wakati huu mnasema kuna uwezekano wa kuvuruga uchaguzi kwa njia za udukuzi, Je. hiyo hiyo hacking tutaamini vipi kuwa imefanywa na nchi za nje? Na sasa kama hacking inawezekana, hapo "ujecha jecha "unashindikanaje kufanywa na wenye nguvu(White power in white house) kumuweka wanayemtaka?
Rigged election ya Trump hakuwahi kuieleza kwa system.
Alichosema ni rigged election kwasababu ya media.
Hilo ndilo tumezungumzia muda mrefu na kusema hakuna mahali alipo justify system nzima tofauti na wewe uliyesema rigged system ipo kwa mujibu wa Trump.
Kwa maana kuwa mlikuwa na hoja moja mkisoma page tofauti. Hilo ndilo tulisema si kweli
Kuhusu interference, homeland security imebaini kuwa Russia kwa mujibu wao wanataka kufanya hacking. Hapo madai ya Trump yatakuwa halali hata kama yalikuwa ya media.
Wlichokusudia ni kuvuruga zile voting system majina kuonekana tofauti na kuleta vurugu
Vyama vyote vimeelezwa kuhusu hali hiyo . Wataalam wanasema uchaguzi wa Marekani ni localized, kama rigging itakuwa localized na si nationwide. Leo wamaongelea sana hilo
Tulikueleza pia kuwa uchaguzi ule ni ngumu ku rig as whole kwasababu upo localized
Sasa sioni hoja yako ni ipi baada ya hilio, siioni kwasababu hawana utaratibu wa kukusanya matokeo na kutangaza kama Tz.
Kesho media zinapata matokeo right away na penye matatizo yanashughulikiwa kama ilivyotokea North Carolina na Iowa
Iowa mfuasi wa Trump amekamatwa akitaka kupiga kura mara 2, na sasa anakabiliwa na kosa la felony ambalo adhabu ni miaka 5 au faini ya 5000 kama sijakosea
Utajitahidi sana kuufanya uchaguzi wa Marekani uonekane sawa na wa Tanzania, katika hilo utajichanganya mwenyewe au wanasema fool yourself kwasababu ni vitu visivyoweza kulinganishwa hata kidogo.