Duru za siasa: Vurugu za katiba zinalinyemelea taifa. Hali si shwari

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Posts
15,773
Reaction score
32,431
MARIDHIANO NI BORA KULIKO KATIBA YENYEWE

CCM HAINA HOJA, SASA INATEMBEZA KIPIGO KWA KASI NA VIWANGO

WARIOBA KATETEA NCHI, WANANCHI MTAMWANGALIA HADI LINI?

Wana duru,
Kutokana na mazingira ya kisiasa nchini, tutakuwa na sehemu I-IV kuhusiana na suala la katiba. Tumezungumzia jambo hili katika nyuzi nyingi,lakini ipo haja ya nyakati a kuliungumzia zaidi

Sehemu ya I

RASIMU YA CHENGE YADODA.

Ni takribani mwezi umepita baada ya katiba ya CCMijulikanayokuandikwa.
Katiba pendekezwa imepigiwa debe na Rais bila mwangi. ZNZ wamejaribu bila majibu.
Wananchi wamesusakuijadili kwa hasira na kuchoka

Makada wa CCM wamehangaika katika mitandao ikiwemo JF kuhamasishawananchi wajadili.
Hii ni katika harakati za kutaka uhuni na mzoga uliopatikanaDodoma ujadiliwe ili kupata uhalali wa kisiasa.
Hata hivyo mambo ni magumu nahakuna dalili za kubadilika.

KWA NINI MAMBO NI MAGUMU?

Kwanza ni ukweli usio na shaka katiba ya CCM iliandikwakabla ya bunge.
Hili sasa halina shaka na tumelizungumzia muda mwingi, kabla nabaada.

Pili,Maoni ya wananchi kupitia tume ya Wariobayamedharauliwa na hivyo wananchi wameamua kususia ili kazi ya Chenge/Sittaitakapokamilika, kazi ya kuandika katiba ya wananchi ianze upya

Tatu,katiba pendekezwa haiuziki kwa maana kuwa ni kinyume na yale yalitotuhumiwa kutoka tume ya Warioba. Mfano, suala la gharama CCM walisemaS3 itaongeza.

Kwa rasimu ya Chenge/Sitta suala hilo limekuwa kinyume kwanigharama ni kubwa kuliko ilivyosemwa kwa S3

(ii) Suala la serikali kuu kutokuwa na vyanzo vya uhakika.Nalo limeonekana halina jibu.
Serikali kuu inayosemwa ni Tanganyika, wakatiWarioba alisema ni ya nchi mbili.

Kwa mantiki hiyo, chanzo cha uhakika chamapato ya muungano ni Tanganyika.
Swali linakuja, je hiyo si kero kwaWatanganyika?

iii) Kuvaa koti: Imedhihirika kuwa muungano wa katiba yaChenge imevalisha Tanganyika koti kubwa kuliko ilivyo sasa au livyokuwaimependekezwa na tume ya Warioba.

Kwa msingi huo, katiba ya CCM haina kipya na wala hainamahali pa kuzungumzia mbdala mwema kinyume na maoni ya tume. Katiba ya CCMhaizuki

(iii) Wananchi wanuliza, wapi maoni yanayotoa katiba yaChenge yamepatikana? Hakuna majibu.

Inaendelea...
 
Shemu ya II

WARIOBA ANASINGIZIWA ILI KUUZA KATIBA YA CCM ISIYOUZIKA

Jitihada za CCM ni kueleza kuwa katiba ya Chenge nimaboresho ya rasimu ya Warioba.
Hii ni kuwafanya wananchi waaminimaoni yao yalizingatiwa na Chenge/Sitta wakati wa kuandika katiba yao.

Majuzi Prof Mwandosya ametoa siri kuwa, kazi ya kumtukana Warioba ilikuwa kupata ushindi.
Yaani ushindi ili katiba ya CCM iingie sokonikunadiwa na wala si ya rasimu ya tume ya Warioba.

Kwa mtazamo huo mfupi, inaonekana wazi, maoni ya tume ya Warioba yanazingatiwa kama sehemu ya kuuza rasimu ya CCM, wakati ukweli ni kuwakatiba nzima ya CCM imeondoa hata moyo wa rasimu ya Warioba. Vifungu 1 na 6haviujadiliwa hadi leo.

WARIOBA ATISHWA

Baada ya kudhalilishwa sana na Rais pamoja na Wabunge, Mzee Warioba na timu yake wameendelea kuwaeleza wananchi kuhusu upotoshajiunaofanywa kwa kuwachafua.

Wakati Warioba akilaumiwa kwa kukosa takwimu, CCM inasema katiba ya Chenge ni maoni ya tume ya Warioba.

Hii maana yake ni kuwa, CCM inataka jina la Warioba litumikekunadi katiba ya Chenge, wakati huo huo jina la Warioba litumike katika kuwadhalilisha wajumbe na tume.

CCM wamefanya jaribio la kumtisha Warioba kuhusu vikao namwenendo wake.
Kwa bahati nzuri au mbaya kutegemea upande wa msomaji, Wariobahawezi kutishwa na vijana waliopo katika NEC au CC ya CCM.

TUME YA WARIOBA YATOAELIMU ILI KUEPUKA UPOTOSHAJI NA KUBEBA LAWAMA.

Tume ya Warioba imeamua kutoa elimu ya umma kama sehemu ya Watanzania ili waweze kujua nini wananchi walipendekeza, nini CCM imefanya tenakwa ulinganifu.

Jumapili, tume imeandaa kongamano kuhusu katiba ile ile ya CCM.
Ikumbukwe, CCM waliondoa tovuti ya tume ya Warioba ili wananchi wasioneupande wa pili.
Tume imeamua kuwa na majadiliano na wananchi kwa maana kuumbili

  1. Ili kuwahakikishia kuwa kile kinachosemwa nikatiba ya Chenge yenye maoni ya Tume ya Wariona si kweli. Hakuna kitu kamahicho, hiyo ni katiba iliyotokana na rasimu nyingine kabisa.
  2. Kwaonyesha wananchi pande mbili za shilingi waweze kufanya maamuzi kutokana na kuelewa na si kuchanganywa. CCMimewachanganya wananchi kwa kusema katiba inatokana na tume, wakati huo huowanasema tume imekusudia kuvunja muungano. Tume ya Warioba inaweka mambo sawia.

CCM WAENDELEZA UBABEWA NGUMI ZA DODOMA

KEISSY ALINUSURIKA,WARIOBA( Makamu wa Rais mstf ) APEWAKIBANO
Itakumbukwa kuwa wabunge wa CCM kutoka znz nusura ‘wamtoe'roho Mbunge Keissy aliyesema znz ni mzigo. Wabunge hao hawakujibu kwanini simzigo, bali walimtafuta Keissy ili wamtwange Makonde.
Hizo zilikuwa dalili zakuishiwa hoja.

Dalili hizo sasa zimeshamiri. Jumapili, Makamu wa Rais Mstaafu, waziri mkuu alishambuliwa na kundi la vijana wa CCM kwa sababu tu alikuwaanatoa maoni yake kama raia wengine.
Kundi hilo ni la vijana linalosaidikiwa kuandaliwa na CCMmahususi ili kukabiliana na maoni wasiyoyataka. Kumbuka, hapo juu tumeeleza kuwakatiba imedoda, na CCM wasingependa imwagiwe maji baridi Zaidi.

Inaendelea….
 
Sehemu ya III

KWANINI WARIOBA NATUME YAKE WANAPEWA KIBANO

Mzee Warioba anapewa kibano ili kuhakikisha kuwa hakuna mtuanayeongea tofauti na lugha ya CCM inayotaka wanananchi wajadili katiba yaChenge.

Jitihada zilianza kwa kufunga tovuti ya tume, kuwafukuza akinaMansour Himidi na kuwatisha mzee Butiku na Salim.

Inawauma sana CCM pale wanapotokea watu wakakumbusha uhuniuliofanywa hadi wapinzani wakaondoka, uhuni uliofanywa CCM walipobaki wenyewe,na uhuni uliofanywa kuchukua rasimu ya Chenge na kuifanya ya taifa kupitia tumeya kukusanya maoni ya Samwel Sitta iliyokutana na wananchi takribani 37 tu.

Kubwa Zaidi ni CCM kutotaka kusikia kuhusu tuhuma zao dhidiya tume na ukosenakaji wa majibu kwa katiba yao.
Hawataki kusikia wananchiwanahoji kuhusu matatizo ya nchi hii kwa miaka 50, na huko tuendako.

Wanachotaka ni kujadili rasimu ya Chenge tu.

SABABU ZA CCM KUTOA KICHAPO MAHUSUSI KWA MZEE WARIOBA

CCM haiwezi ‘kumwadabisha' Mzee Warioba kama walivyofanyakwa Mansour Himid
Pili, CCM wanataka tume inyamazishwe wananchiwalishwe maadili na katiba ya Chenge kwa nderemo na vifijo.

Tatu, Kumdahlilisha mzee Warioba ili kukamilishampango wa kulinyamazisha taifa.
Kinachotakiwa ni kujadili katiba yaChenge/Sitta

Nne, kutafuta njia za kumhusisha Mzee Warioba na vurugu.
Hiini baada ya hoja kuwa Warioba anataka kuvunja muungano kushindikana kwa hojazenye mantiki.

Hoja namba nne, ni muhimu sana kwasababu ndiyo imetokeaJumapili.

KUMHUSISHA MZEE WARIOBA NA VURUGU

Hoja hii inatumika ili kuwatisha watu kuwa mzee Wariobaanaandaa vurugu nchini.
Hoja za vurugu zmezungumzwa sana na viongozi wa CCM nakilichobaki ni kutafuta namna ya kumhusisha Warioba na vurugu ili nia yaoikamilike.

Vijana waliomshambulia mzee Warioba, mmoja wao ni mwenyekitiwa UVCCM Chipukizi, Paul Makonda. Makonda amempiga mzee Warioba kibao wakatianaongoza kundi lake la kuleta vurugu katika kongamano.

Kutoa maoni ni haki ya raia, na kustahamiliana katika maonini sehemu ya demokrasia.

Kupigana si haki wala demokrasia ni kosa kisheria.
Katika mazingira hayo, Makonda anakosa la shambulio la mwili kwa mzee Warioba.

Inaendelea….
 
Sehemu ya IV
CCM walimfukuza Mansor Himid kwasababu tu alikuwa na maoniya S3.
Hilo likawa kosa kubwa kiasi cha kutopewa nafasi ya kuskilizwa.

Inategemewa kuwa mwenyekiti wa Chipukizi na kada wa chama katika ngazi ya juukama Makonda atachukuliwa hatua za kisheria na kichama!

Kwa sasa inasemekana wapo mahubusu.
Katika mazingira fulani CCMwangekuwa wametoa tamko laiti ingekuwa ni wapinzani.

Hilo hakijafanyika na walahaitegemewi kufanyika.
Sababu kubwa ni kuwa akina makonda wametumwa na CCM nahivyo kila jitihada zitalenga kuwalinda.

LENGO LATIMIA

Lengo la CCM limetimia kwasasa. Kwamba wataanza na kauli zakonyesha kuwa Warioba na tume wanataka kuleta vurugu nchi. CCM hawataeleza kuhusu mazingira ya vuruguwaliyotengeneza.
Tutasikia matamko ya mawaziri na viongozi wa chama, sikuhusu uhalifu wa Paul Makonda bali kuhusu tume.
Hii itafanyika ili kufungamidomo watu na tume na kutoa nafasi kwa katiba ya Chenge.

WANANCHI LAZIMA WAAMKE

WARIOBA KATETEA NCHI SANA KWA HESHIMA YAKE

SASA NI ZAMU YA WANANCHI KUITETEA NCHI YAO.

Warioba na tume yake wamedhalilishwa sana, wamenyanyaswa nakusingiziwa kila aina ya ubaya na uchafu. Hata hivyo, wamesimama kidete kuteteamasilahi ya taifa na wala si ya vyama vyao.

Imefika mahali, makamu wa kwanza wa Rais na waziri mkuumstaafu anazabwa kibao na mtoto mdogo sana kama Paul Mkaonda eti kwa kosa lakusimama katika utaifa.

Kwamba, uzalendo sasa unageuka kuwa uhalifu na wala siuhalifu kuwa ushenzi na ubazazi.
Wananchi wa taifa hili watakuwa watu wa ajabusana wakiacha hali iliyopo iendelee bila kukemea.

CCM haina moral authority ya kulaani mpango wao.
Nia ya CCMkuvuruga mchakato imefanikiwa. Sasa wanataka wananchi wasijadili hatima ya nchiyao.

Hii ikiendelea ipo siku CCM wataamisha wananchi watandikweviboko bila sababu.
Makamu wa Rais kaanza kupigwa kibao, hatujui wengineitakuwaje.
Wananchi lazima wasimame kidete kutetea uhuru wa maoni,uhuru na hatima ya taifa lao bila woga au kufungwa na siasa za vyama. Hili laCCM kutumia vijana kuanzisha vurugu ni jambo la hatari sana.

TULIONYA

Katika mabandiko ya duru, tulionya kuwa vurugu zitazukakutokana na uhuni uliotendeka Dodoma, kukosa marishiano ya kitaifa na kukosauongozi wa kitaifa.
Haya tunayoyaona ni madogo sana,hali itakuwa tete Zaidi yakiingiamitaani.

Tunayoyaona na matunda ya kazi ya Sitta/Chenge na JK. Na tuliwahikuseme ipo siku mikono yao itakuwa haiasafishiki, si jasho bali..

Hivi wananchi wa Tanzania tuna tatizo gani? Kwaninitunasubiri haki katika sahani ya dhahabu?
Tutasubiri akina Warioba wangapiwazaliwe ili tuweze kuzuia uhuni huu na kutetea nchi yetu?

Tusemezane
 
Nimependa sana hitimisho lako nililo BLUE.

Sasa si wakti wa kusemezana BALI NI WAKTI WA KUILIMISHANA NA KUCHUKUA HATUA.

Tutasubiri akina Warioba wangapiwazaliwe ili tuweze kuzuia uhuni huu na kutetea nchi yetu?
Hapana tusisubiri , kwa kuanza tuanze na ususiaji baridi kwa wale wote(individuals) waliohusika moja kwa moja na uchakachuaji na wale wote wanaratibu vurugu dhidi ya maoni tofauti juu ya Katiba pendekezwa.

Mfano wa ususiaji baridi ni kama ifuatavyo. Kama muhusika ana tumia usafiri wa daladala akifika kituoni na akapanda daladala ambalo lina abiria ndani basi abiria walioko ndani ya daladala washuke na wale ambao walikuwa hawajapanda wasipande daladala hiyo. Tukiweza hii wote kwa pamoja tutakuwa tumeanza kuwapa taarifa wahusika kuwa kubwa zaidi linakuja. Njia hii inaweza kutumika maeneo mengine pia.
 
njia ya kususa itakuwa ngumu bro, na imeshafeli kuanzia kule mjengoni, kwa mfano wa daladala ndo kab isaa, maana tunaowasusia hawatumii usafiri huo wa makabwela, kwenye kupiga kura ukisusa ndo imekula kwetu, huko kwenye kumbi mbali mbali akiwepo mtawala mmojawapo kwa ujinga wa watanzania watamsogelea na kupiga nae picha, dawa ni moja tu, kuagiza silaha kupitia hata Kenya au Rwanda na kuingia msituni na kupambana na hao wahuni wachache wasiozidi hata milioni moja, ni kwa jasho na damu tu ndipo haki itapatikana, YES kwa JASHO NA DAMU na sivinginevyo.
 
CCM IMEVIA, SERA HAKUNA TENA

WAZEE WASHANGILIA UHUNI, ''WAPIGWE'' NDIO SERA YA CCM

ALIANZA PINDA, SITTA ABARIKI VURUGU

Waziri mkuu Pinda aliwahi kusema wapinzani ‘wapigwe tu'' bila kujali athari za kauli yake kwa mustakabali wa taifa.

Tumeona Polisi wakichukua hatua za kukamata, kusoma mashtaka na kutoa kipigo bila kutumia vyombo vya kisheria na kinyume na utaratibu wa utawala bora wakiitika wito wa Pinda

Kutofautiana kimawazo katika jamii ni jambo lisilokwepa.
Hata katika family level bado misiguano ya mitazamo tofauti ni jambo la kawaida.

Kwa chama kikongwe kama CCM barani Afrika, ni jambo la kusikitisha kuona kimeshindwa kusimamia sera kama chama tawala na sasa kinahubiri vurugu.

Tumesikia Profesa Mwandosya akizungumzia ushindi katika katiba.
Kwamba, maneno ya kumdhalilisha mh Warioba ili kupata ushindi wa CCM na si taifa

Katiba ni nyaraka ya taifa, ushindi ni pale taifa linapokuwa pamoja katika maridhiano, kupanga na kuamua.

Kitendo cha Profesa kutoa matamko kama Mwandosya kinatisha.

Leo waziri na mwenyekiti wa bunge la CCM Samwel Sitta ametoa kauli za kushabikia vurugu alizofanya mwenyekiti wa CCM chipukizi Paul Makonda na kundi lake

Alichokifanya Makonda ni kinyume na dhana ya Mwalimu Nyerere ya kupingana bila kupigana.
Makonda hakusimama kutetea hoja kwa kupingana, alikwenda mbali kama mwakilishi wa CCM kuandaa kundi la vurugu

Warioba ni makamu wa Rais mstaafu na waziri mkuu. Ni jaji na mzee mwenye heshima katika uso wa dunia.

Ameongoza taasisi za kimataifa hadi alipopewa dhamana nzito ya kusimamia mchakato wa katiba.

Mzee Warioba ameshiriki sana katika upatanishi hasa kule visiwani na ametumiwa katika suluhu za matatizo ya nchi kama ilivyokuwa kwa tume ya kuchunguza mianya ya rushwa.

Zaidi ya hapo, Mzee Warioba ni mzazi mwenye wajukuu.
Kitendo cha kuvamiwa akitoa maoni kama mzee, Mtanzania na kiongozi kinapaswa kulaani na wananchi wote bila kujali itikadi zao za kisiasa.

Kwasasa CCM imepoteza mwelekeo.
Si chama kinachohubiri amani tena.
Ni chama kinachotafuta ushindi hata kama ni kwa damu .

Alichosema Sitta kinaaminisha kuwa Warioba angeuawa hilo lingekuwa jambo la kujitakia.

Hatuwezi kuamini kauli hii imetolewa na kiongozi wa taifa hili.
Tulidhani Sitta likuwa na dhamana kubwa ya kuwalea akina Makonda kama alivyolelewa na Mwalimu Nyerere

Hili la mzee Warioba huku Sitta akiendelea kushabikia ni jambo la kuhuzunisha.

Kwa maneno mengine, Sitta anabariki uhalifu wa vijana ilimradi tu chama chake kipate ushindi kama alivyosema Mwandosya na wala si taifa kupata ushindi.

Ni mwendelezo wa kauli za ‘wapigwe' za waziri mkuu wa Tanzania Mizengo peter kayanza Pinda.

Tunaogopa kauli hizi kwasababu huko mitaani kusiko na ulinzi mambo ni tofauti. Hakutakuwa na kuongea bali ‘vipigo' vikijibiwa na vipigo.

CCM kama imelifikisha taifa hapa, na hakuna mwenye wasi wasi, basi awaye aende kumuona Daktari.

CCM inapobariki uhalifu ni mwanzo wa mwisho wa mani ya nchi hii.
Nani atakuwepo mitaani kusikiliza wana vijiwe wakichapana makonde?

Mwisho wa Makonde ni kuchukua mapanga.
Mungu tunusuru maana wanakotupeleka akina Sitta ni pa baya.

CCM kwa hili watabeba dhamana kubwa sana. Wanapalilia vurugu nchini

Ni majuzi tu akina Lowassa na Makamba walikuwa kanisani wakimwombea radhi Sitta kwa kutukana viongozi wa dini. Haionekani kama Sitta anajuta na anafahamu athari za kauli zake kwa taifa.

Viongozi wa dini, ni wakati msimame na kukemea uhalaifu huu unaofanywa na viongozi wa CCM kama akina Sitta

Kwa Mh Sitta na CCM, tafadhali jiandaeni kubeba lawama zinazofuata kutokana na hili.

Yakimalizika kwa Warioba, yaathamia kwa akina mama na watoto.
Samwel Sitta na CCM muwe tayari kutengeneza makazi ya viumbe hao ambao leo mnawatia katika hati hati ya maisha yao.

CCM kwa hili la kuandaa akina Makonda na vijana wake hamtakwepa lawama au fedheha.
Ni aibu kwenu, taifa na nchi.

Hivi ndivyo mna mwenzi mwalimu Nyerere kweli! Kwa kutuma vijana wakafanye vurugu na si kuongea!

CCM nchi inapokwenda ni pa baya

Tusemezane
 
......
Hatuwezi kuamini kauli hii imetolewa na kiongozi wa taifa hili.
Tulidhani Sitta likuwa na dhamana kubwa ya kuwalea akina Makonda kama alivyolelewa na Mwalimu Nyerere

Hili la mzee Warioba huku Sitta akiendelea kushabikia ni jambo la kuhuzunisha.

Kwa maneno mengine, Sitta anabariki uhalifu wa vijana ilimradi tu chama chake kipate ushindi .....

Jenerali Ulimwengu aliwahi kuandika katika gazeti la The East African, kuwa akiona mtoto kizaliwa hapa Afrika...anaona mkimbizi mtarajiwa, kutokana na vurugu za vita zinazoratibiwa na watawala(kama sijakosea sana tafsiri kwa kiswahili). Mwanzo niliona hili ni kweli linaweza kutokea kwa baadhi ya sehemu za Afrika lakini siyo Tanzania. Lakini taratibu naanza kuona kuwa hata hapa Tanzania tuko kwenye hatari ya kuanza kuzalisha wakimbizi, kwa namna kauli za watawala zinavyopalilia kuhasimiana baina ya watanzania huku wakichochea kuporomoka kwa nidhamu ya vijana nchini.

Nadhani sasa tujikite katika kujadili namna gani tutaweze kudhibiti hali hii ili kile alichokiona Jenerali Ulimwengu kisitokee Tanzania. Barubaru kashauri vizuri sana kuwa muda huu ni wa kupeana ilimu/elimu namna ya kukabiliana na hali hii. Nami nimemuunga mkono kwa kutoa wazo ni nini chakufanya...vile vile na zumbemkuu katoa ya kwake (imebeba hisia kali sana).
 
Hakika hii ni dalili dhahiri ya Utawala kuanguka, tukitazama historia ya mataifa mengi duniani ambayo yalivimbiwa madaraka na kudharau wananchi, siku za mwisho matukio yalikuwa Kama haya ya CCM. CCM ilijenga uhalali wake wa kutawala kwa kutumia mikakati mikuu miwili:

1. Kuunganisha wananchi (national unity) kwa njia mbalimbali kisera, kiitikadi n.k.
2. Kushirikisha wananchi Katika kuchagua wananchi (popular participation).

Katika yote haya, tunaona common denominator ni Neno "wananchi", na Ndio maana Utawala wa mwalimu ulipata uhalali mkubwa wa kutawala na wananchi Wala hawakujali sana suala la katiba ya nchi. Leo Katika CCM, hakuna suala lolote la Dhati linalohusisha Neno au Dhana ya "wananchi", hakuna. Kila kitu kinachohusu wananchi, hakina maslahi na CCM Tena, kwani walio muhimu kwa chama Leo hii ni tycoons wa ndani wanaokusaidia chama pesa, na pia tycoons wa nje ya nchi ambao Haki ya mungu kwa wananchi (ardhi na rasilimali) zingekuwa na CCM kuwa ni Haki ya mzungu.

Ndio maana mazingira Kama haya yanahitaji sana, Mageuzi ya kikatiba (constitutional reforms) ambayo yataweka Mbele maslahi ya wananchi walio wengi bila ya kuweka vipaumbele Katika itikadi za vyama. Kwa maana nyingine, Katika mazingira ya sasa, legitimacy ya serikali yoyote madarakani inatakiwa itokane na katiba iliyotokana na maridhiano, katiba ambayo watawala na watawaliwa wataiheshimu na watailinda. Hayo Ndio jaji warioba alilenga kuwapatia wananchi, hasa baada ya kusikia maoni, malalamiko na vilio vyao kwa maelfu. Kwa Tabia ya sasa ya CCM, maana yake ni Kwamba CCM inakataa Kwamba wananchi wana vilio, matamanio, malalamiko mengi ambayo suluhisho lake lipo Katika katiba mpya ambayo itaendana na maoni Yao na ndoto zao juu ya taifa wanalotaka, na la kuwaachia vizazi vyao vya baadae.

Mwalimu nyerere aliona haya muda mrefu sana. Kwa mfano mwaka 1987, miaka mitano Kabla ya kurudishwa kwa Mfumo wa vyama vingi nchini, miaka zaidi ya mitano kabla ya kuzaliwa kwa vyama vya CUF, NCCR, na chadema, miaka 27 Kabla ya kuzaliwa kwa UKAWA, mwalimu nyerere alinukuliwa akisema maneno haya (daily news):

[“It is not that peace has come by itself. The source of peace in Tanzania is not that the Arusha Declaration has done away with poverty even a little bit. Isn’t there this poverty we are still living with? This poverty is right here with us. It is not the same economy we are grappling with? The fact is not that the Arusha Declaration has banished poverty even by an iota – nor did it promise to do so. The Arusha Declaration offered hope. A promise of Justice, hopes to the many, indeed the majority of Tanzanians continue to live this hope. So long as there is this hope, you will continue to have peace. Here in Tanzania we have poverty but no ‘social cancer’. It is possible it has just begun. But otherwise we don’t have a social cancer. There isn’t a Volcano in the making, that one day it is bound to erupt. We have not yet reached that stage because the people still have hopes based on the stand taken by the Arusha Declaration. It did not do away with poverty but it has given you all in this hall, capitalists and socialists alike, an opportunity to build a country which holds out a future of hopes to the many.

To be sure, you few Waswahili, do you really expect to rule Tanzanians through coercion, When there is no hope, and then expect that they will sit quiet in peace? Peace is born of hope, when hope is gone, there will be social upheavals. I’d be surprised if these Tanzanians refuse to Rebel, why?

When the majority don’t have any hope you are building a volcano. It is bound to erupt one day. Unless these people are fools. Many in these countries are fools, to accept being ruled just like that. To be oppressed just like that when they have the force in numbers, they are fools. So Tanzanians would be fools, ******, if they continued to accept to be oppressed by minority in their own country. Why?

Therefore we cannot say that we have now reached a stage when we can forget the Arusha Declaration. Don’t fool yourselves. This would be like that fool who uses a ladder to climb and when he is up there kicks it away. Alright, you are up there, you have kicked away the ladder, right, so stay there because we will cut the branch. You are up there, we are down here and you have kicked away the ladder. This branch is high up, we will cut it. Your fall will be no ordinary fall either.

Let me say no more. It is sufficient to say we should accept our principles, we should continue with our principles of building peace and peace itself. Tanzanians should continue to have faith in the party, in the government and in you in positions. Tanzanians should see you as part of them not their enemies."]

Wataalam wa lugha watatusaidia na tafsiri kwani maneno haya huu Ndio Wakati wake kwa wananchi Kuanza kuyafanyia kazi maneno haya ya mwalimu kwa Vitendo.

Miaka Kama nane baada ya mwalimu kutoa kauli hii (mid 1990s), baada ya kuona CCM ikizidi kuwatelekeza wananchi, mwalimu aliendelea kukosoa CCM na viongozi wake.Ikafikia hatua Mwalimu Nyerere akatamka Kwamba yupo tayari kurudisha kadi yake namba moja ya CCM, hasa pale alipofanyiwa mambo ya Dharau, udhakalishaji na ya kitoto na viongozi wa CCM, pale chama kilipowatuma ngwilizi na majogo kwenda Butiama kumhoji mwalimu kwanini alikuwa Ana kikosoa chama na kwanini alikuwa anaunga Mkono upinzani. Ni busara tu zilikuja kutumika Vinginevyo CCM Leo ingekuwa haipo.

Kwa kweli kwa hatua tuliyofikia Leo chini ya uongozi wa ccm, tunu pekee ambayo wananchi wataweza kumpa mwalimu nyerere ni kwa wananchi kuchukua maamuzi magumu na kuandamana kumwomba warioba na wenzake wajitoe CCM na kubakia Raia wa kawaida. Vinginevyo, akina jaji warioba ilitakiwa watumie nyerere day ya mwaka huu kutangaza Rasmi kujitoa CCM Kama njia ya kumuenzi mwalimu na kuomba wananchi Wawaungr Mkono. Warioba na wenzake ni bora wakaondoka CCM kuliko kuendelea kuelezea umma jinsi gani CCM inalitumia vibaya jina la mwalimu. Huu ni Wakati wa mzee warioba na wenzake kuwaeleza wananchi jinsi gani jina la mwalimu kitaweza kutumiwa vizuri na kwa manufaa ya walio wengi Katika muktadha wa katiba mpya.

Vinginevyo ni kwanini hakuna kiongozi wa kufuata nyayo Kama za mwalimu na kuthubutu kutangaza nia ya kuondoka CCM? Amejaribu Sumaye, lakini Huyu ni kwa condition Kama hatosimamishwa na CCM 2015 lakini hasa iwapo mshindi atapatikana kwa rushwa. Viongozi wa aina ya akina Sumaye sio wa kuaminiwa na wananchi kwani Katika suala la katiba mpya, wameonyesha Kwamba wao ni wale wale Kama akina Sitta, Chenge, na wenzao, kwani hawatumii nafasi zao kukosoa ubovu wa mchakato wa katiba mpya, wanaothubutu ni akina jaji warioba, sasa kwanini wasiende Mbali na kujitoa CCM sasa hivi Kama njia ya kumuenzi mwalimu kwa Dhati? Kwa kufanya hivyo jaji warioba na wenzake watapoteza nini kikubwa zaidi ya heshima Mbele ya umma?

Hoja za kujitoa CCM ni nyingi kwa akina warioba Mbele ya umma. Mbali ya katiba mpya, jaji warioba alikuwa ni Mwenyekiti wa tume ya mkapa iliyochunguza ufisadi serikalini na kutoa ripoti yake, ambayo haikufanyiwa kazi. Kwahiyo jaji warioba anapojadili suala la maadili Kama Tunu ya taifa, anayo mengi moyoni ambayo yatasaidia wananchi Kupata ujasiri zaidi wa kuikataa katiba inayolazimishwa na CCM.

Turudie Tena, kwanini jaji warioba na wenzake wasiitishe mkutano na kutangaza kujitoa CCM na kushawishi Wengine Wawaunge Mkono Katika mkutano wa hadhara? Tupo wengi ambao tutamuunga Mkono.

Vinginevyo je Ina maana Kwamba jaji warioba bado Ana amini CCM itakuja badilika na kurudi kuwa chama cha wananchi Ndio maana hajafikiria umuhimu wa kujitoa kwa maslahi ya taifa letu?

Kwanini nyerere Ndio Awe ni kiongozi pekee wa ngazi ya juu wa chama kusema CCM sio mama yake? Lipi lililo muhimu kwa nyerere foundation kumuenzi baba wa taifa zaidi ya kufuata nyayo zake Katika hili Katika kipindi muafaka Kama cha hivi sasa?

Wapo wanafiki Kama Wassira ambao waliondoka CCM kutokana na uroho wa madaraka na kuhamia NCCR. Leo Anasema eti alihama CCM na kwenda NCCR kwa sababu ya mzee wa warioba. Anajaribu aminisha umma Kwamba mzee warioba ni tatizo kwa chama, taifa, na muungano, na Ndio maana miaka 20 iliyopita, alihamia NCCR. Hii ni hoja dhaifu sana.

Wanafiki Wengine waliodiriki kuhama CCM kwa ajili ya maslahi ya uongozi ni Sitta, nape nnauye na wenzao ambao waliunda CCJ. Lakini baada ya kuahidiwa madaraka ndani ya CCM, wakarudi CCM na kuacha umma ukishangaa jinsi gani kumbe hawakuwa na lengo la kutetea maslahi ya wananchi Bali mlo wao. Tazama Vitendo vya Sitta bungeni, Tazama kauli za nape nnauye, yote ni ushahidi Kwamba kumbe hawakuwa wanajali maslahi ya wananchi Bali vyeo na fursa za ndani ya CCM na serikali yake.

Kwanini akina mzee warioba wasiondoke CCM sasa? Kwani wana nini cha kupoteza? Je bado wanafadhiliwa na CCM? Je hawakuwa na mwalimu nyerere kwa Dhati? Je Hawana maamuzi magumu? Je bado wana amini Kwamba CCM itabadilika na Kwamba wataweza chochea mabadiliko wakiwa ndani? Je ni Kwamba maisha Yao yatakuwa hatarini? Kati ya CCM na vyombo vyao vya dola na wananchi, Nani atakuwa ni mlinzi wa kuaminiwa zaidi kwa wazee hawa iwapo wataondoka?

Mwalimu nyerere alipata kusema hivi:

• iwapo wananchi hawatopata mabadiliko kupitia CCM, basi watayatafuta kupitia chama kingine.

Pia akaja kusema:

"Kiongozi bora hawezi kupatikana nje ya CCM."

Je kauli Mbili hizi zina maana gani Katika mazingira ya sasa?

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Wanajamvi, tafsiri hii si rasmi. Ni tafsiri yangu ili kuhakikisha hatuachi mtu yoyote nyuma kwasababu tu ya lugha.
Ninaomba radhi kwa mapungufu au makosa yatakayojitokeza. Si nia yetu ni ubinadamu!

Mchambuzi;11042826]["It is not that peace has come by itself. The source of peace in Tanzania is not that the Arusha Declaration has done away with poverty even a little bit. Isn't there this poverty we are still living with?

This poverty is right here with us. It is not the same economy we are grappling with? The fact is not that the Arusha Declaration has banished poverty even by an iota – nor did it promise to do so. The Arusha Declaration offered hope.

A promise of Justice, hopes to the many, indeed the majority of Tanzanians continue to live this hope. So long as there is this hope, you will continue to have peace.

Here in Tanzania we have poverty but no ‘social cancer'. It is possible it has just begun. But otherwise we don't have a social cancer.

There isn't a Volcano in the making, that one day it is bound to erupt.
We have not yet reached that stage because the people still have hopes based on the stand taken by the Arusha Declaration. It did not do away with poverty but it has given you all in this hall, capitalists and socialists alike, an opportunity to build a country which holds out a future of hopes to the many.

To be sure, you few Waswahili, do you really expect to rule Tanzanians through coercion, When there is no hope, and then expect that they will sit quiet in peace? Peace is born of hope, when hope is gone, there will be social upheavals. I'd be surprised if these Tanzanians refuse to Rebel, why?

When the majority don't have any hope you are building a volcano. It is bound to erupt one day. Unless these people are fools. Many in these countries are fools, to accept being ruled just like that. To be oppressed just like that when they have the force in numbers, they are fools. So Tanzanians would be fools, ******, if they continued to accept to be oppressed by minority in their own country. Why?

Therefore we cannot say that we have now reached a stage when we can forget the Arusha Declaration. Don't fool yourselves. This would be like that fool who uses a ladder to climb and when he is up there kicks it away. Alright, you are up there, you have kicked away the ladder, right, so stay there because we will cut the branch. You are up there, we are down here and you have kicked away the ladder. This branch is high up, we will cut it. Your fall will be no ordinary fall either.

Let me say no more. It is sufficient to say we should accept our principles, we should continue with our principles of building peace and peace itself. Tanzanians should continue to have faith in the party, in the government and in you in positions. Tanzanians should see you as part of them not their enemies."]
'''Siyo kwamba amani imejitokeza yenyewe.
Chanzo cha amani Tanzania si kwamba Azimio la Arusha limeondoa umasikini hata kidogo. Je, si umasikini huu ambao tunaishi nao?

Umasikini upo na tunao hapa. Si kweli kuwa ni uchumi huu tunaohangaika nao? Ukweli ni kuwa Azimio la Arusha halijaondoa umasikini hata kidogo na wala haitumainiki kuwa hivyo.

Azimio la Arusha linatoa matumaini.
Matumaini ya haki kwa walio wengi, na hakika Watanzania wengi wanaendelea kuishi katika matumaini haya. Midhali yapo matumaini utaendelea kuishi kwa amani.

Tanzania tuna umasikini lakini si saratani ya kijamii, kuna uwezekano imeshaanza. Vinginevyo hatuna ‘saratani ya kijamii''

Hatuna volkeno inayorindima kwamba ipo siku italipuka.
Hatujafikikia hatua hiyo kwasababu watu wana matumaini kutokana na msimamo uliochukuliwa na Azimio la Arusha.

Azimio halijamaliza umasikini lakini imetoa kila kilichopo, ubepari na ujamaa kwa ufanano, fursa ya kujenga nchi yenye matarajio kwa wengi.

Hivi kwa uhakika, nyie waswahili, hivi mnategemea kuitawala Tanzania bila kuwepo matumaini, pasipokuwepo matumaini,mkitegemea watakaa kimya kwa amani?

Amani ni zao la matumaini, amani ikiondoka kutakuwa na mtafaruku katika jamii. Nitashangaa kama hawa Watanzania hawataasi, kwanini?

Hivyo hatuwezi kusema tumefikia hatua ya kusahau Azimio la Arusha. Msijidanganye.

Hili ni kama lile la mjinga kutumia ngazi kupanda, akifika juu akaipiga mateka. Sawa, mpo juu na mumeipiga ngazi mateke,sawa, hivyo kaeni pale.

Kaeni hapo kwasababu tatukata tawi.
Mpo juu, tupo chini na mumepiga teke ngazi. Hili tawi lipo juu sana, tutalikata.
Anguko lenu halitakuwa la kawaida.

Nisiseme zaidi. Inatosha kusema tunapaswa kukubali misingi yetu, tuendelee na misingi yetu ya kujenga amani na amani yenyewe.

Tanzania iendelee kuwa na imani na chama,serikali na nyie wenye mamlaka.
Tanzania iwaone nyie kama miongoni mwao na si maadui''
 
Hakika hii ni dalili dhahiri ya Utawala kuanguka, tukitazama historia ya mataifa mengi duniani ambayo yalivimbiwa madaraka na kudharau wananchi, siku za mwisho matukio yalikuwa Kama haya ya CCM. CCM ilijenga uhalali wake wa kutawala kwa kutumia mikakati mikuu miwili:

1. Kuunganisha wananchi (national unity) kwa njia mbalimbali kisera, kiitikadi n.k.
2. Kushirikisha wananchi Katika kuchagua wananchi (popular participation).

Katika yote haya, tunaona common denominator ni Neno "wananchi", na Ndio maana Utawala wa mwalimu ulipata uhalali mkubwa wa kutawala na wananchi Wala hawakujali sana suala la katiba ya nchi. Leo Katika CCM, hakuna suala lolote la Dhati linalohusisha Neno au Dhana ya "wananchi", hakuna. Kila kitu kinachohusu wananchi, hakina maslahi na CCM Tena, kwani walio muhimu kwa chama Leo hii ni tycoons wa ndani wanaokusaidia chama pesa, na pia tycoons wa nje ya nchi ambao Haki ya mungu kwa wananchi (ardhi na rasilimali) zingekuwa na CCM kuwa ni Haki ya mzungu.

Ndio maana mazingira Kama haya yanahitaji sana, Mageuzi ya kikatiba (constitutional reforms) ambayo yataweka Mbele maslahi ya wananchi walio wengi bila ya kuweka vipaumbele Katika itikadi za vyama. Kwa maana nyingine, Katika mazingira ya sasa, legitimacy ya serikali yoyote madarakani inatakiwa itokane na katiba iliyotokana na maridhiano, katiba ambayo watawala na watawaliwa wataiheshimu na watailinda. Hayo Ndio jaji warioba alilenga kuwapatia wananchi, hasa baada ya kusikia maoni, malalamiko na vilio vyao kwa maelfu. Kwa Tabia ya sasa ya CCM, maana yake ni Kwamba CCM inakataa Kwamba wananchi wana vilio, matamanio, malalamiko mengi ambayo suluhisho lake lipo Katika katiba mpya ambayo itaendana na maoni Yao na ndoto zao juu ya taifa wanalotaka, na la kuwaachia vizazi vyao vya baadae.

Mwalimu nyerere aliona haya muda mrefu sana. Kwa mfano mwaka 1987, miaka mitano Kabla ya kurudishwa kwa Mfumo wa vyama vingi nchini, miaka zaidi ya mitano kabla ya kuzaliwa kwa vyama vya CUF, NCCR, na chadema, miaka 27 Kabla ya kuzaliwa kwa UKAWA, mwalimu nyerere alinukuliwa akisema maneno haya (daily news):

[“It is not that peace has come by itself. The source of peace in Tanzania is not that the Arusha Declaration has done away with poverty even a little bit. Isn’t there this poverty we are still living with? This poverty is right here with us. It is not the same economy we are grappling with? The fact is not that the Arusha Declaration has banished poverty even by an iota – nor did it promise to do so. The Arusha Declaration offered hope. A promise of Justice, hopes to the many, indeed the majority of Tanzanians continue to live this hope. So long as there is this hope, you will continue to have peace. Here in Tanzania we have poverty but no ‘social cancer’. It is possible it has just begun. But otherwise we don’t have a social cancer. There isn’t a Volcano in the making, that one day it is bound to erupt. We have not yet reached that stage because the people still have hopes based on the stand taken by the Arusha Declaration. It did not do away with poverty but it has given you all in this hall, capitalists and socialists alike, an opportunity to build a country which holds out a future of hopes to the many.

To be sure, you few Waswahili, do you really expect to rule Tanzanians through coercion, When there is no hope, and then expect that they will sit quiet in peace? Peace is born of hope, when hope is gone, there will be social upheavals. I’d be surprised if these Tanzanians refuse to Rebel, why?

When the majority don’t have any hope you are building a volcano. It is bound to erupt one day. Unless these people are fools. Many in these countries are fools, to accept being ruled just like that. To be oppressed just like that when they have the force in numbers, they are fools. So Tanzanians would be fools, ******, if they continued to accept to be oppressed by minority in their own country. Why?

Therefore we cannot say that we have now reached a stage when we can forget the Arusha Declaration. Don’t fool yourselves. This would be like that fool who uses a ladder to climb and when he is up there kicks it away. Alright, you are up there, you have kicked away the ladder, right, so stay there because we will cut the branch. You are up there, we are down here and you have kicked away the ladder. This branch is high up, we will cut it. Your fall will be no ordinary fall either.

Let me say no more. It is sufficient to say we should accept our principles, we should continue with our principles of building peace and peace itself. Tanzanians should continue to have faith in the party, in the government and in you in positions. Tanzanians should see you as part of them not their enemies."]

Wataalam wa lugha watatusaidia na tafsiri kwani maneno haya huu Ndio Wakati wake kwa wananchi Kuanza kuyafanyia kazi maneno haya ya mwalimu kwa Vitendo.

Miaka Kama nane baada ya mwalimu kutoa kauli hii (mid 1990s), baada ya kuona CCM ikizidi kuwatelekeza wananchi, mwalimu aliendelea kukosoa CCM na viongozi wake.Ikafikia hatua Mwalimu Nyerere akatamka Kwamba yupo tayari kurudisha kadi yake namba moja ya CCM, hasa pale alipofanyiwa mambo ya Dharau, udhakalishaji na ya kitoto na viongozi wa CCM, pale chama kilipowatuma ngwilizi na majogo kwenda Butiama kumhoji mwalimu kwanini alikuwa Ana kikosoa chama na kwanini alikuwa anaunga Mkono upinzani. Ni busara tu zilikuja kutumika Vinginevyo CCM Leo ingekuwa haipo.

Kwa kweli kwa hatua tuliyofikia Leo chini ya uongozi wa ccm, tunu pekee ambayo wananchi wataweza kumpa mwalimu nyerere ni kwa wananchi kuchukua maamuzi magumu na kuandamana kumwomba warioba na wenzake wajitoe CCM na kubakia Raia wa kawaida. Vinginevyo, akina jaji warioba ilitakiwa watumie nyerere day ya mwaka huu kutangaza Rasmi kujitoa CCM Kama njia ya kumuenzi mwalimu na kuomba wananchi Wawaungr Mkono. Warioba na wenzake ni bora wakaondoka CCM kuliko kuendelea kuelezea umma jinsi gani CCM inalitumia vibaya jina la mwalimu. Huu ni Wakati wa mzee warioba na wenzake kuwaeleza wananchi jinsi gani jina la mwalimu kitaweza kutumiwa vizuri na kwa manufaa ya walio wengi Katika muktadha wa katiba mpya.

Vinginevyo ni kwanini hakuna kiongozi wa kufuata nyayo Kama za mwalimu na kuthubutu kutangaza nia ya kuondoka CCM? Amejaribu Sumaye, lakini Huyu ni kwa condition Kama hatosimamishwa na CCM 2015 lakini hasa iwapo mshindi atapatikana kwa rushwa. Viongozi wa aina ya akina Sumaye sio wa kuaminiwa na wananchi kwani Katika suala la katiba mpya, wameonyesha Kwamba wao ni wale wale Kama akina Sitta, Chenge, na wenzao, kwani hawatumii nafasi zao kukosoa ubovu wa mchakato wa katiba mpya, wanaothubutu ni akina jaji warioba, sasa kwanini wasiende Mbali na kujitoa CCM sasa hivi Kama njia ya kumuenzi mwalimu kwa Dhati? Kwa kufanya hivyo jaji warioba na wenzake watapoteza nini kikubwa zaidi ya heshima Mbele ya umma?

Hoja za kujitoa CCM ni nyingi kwa akina warioba Mbele ya umma. Mbali ya katiba mpya, jaji warioba alikuwa ni Mwenyekiti wa tume ya mkapa iliyochunguza ufisadi serikalini na kutoa ripoti yake, ambayo haikufanyiwa kazi. Kwahiyo jaji warioba anapojadili suala la maadili Kama Tunu ya taifa, anayo mengi moyoni ambayo yatasaidia wananchi Kupata ujasiri zaidi wa kuikataa katiba inayolazimishwa na CCM.

Turudie Tena, kwanini jaji warioba na wenzake wasiitishe mkutano na kutangaza kujitoa CCM na kushawishi Wengine Wawaunge Mkono Katika mkutano wa hadhara? Tupo wengi ambao tutamuunga Mkono.

Vinginevyo je Ina maana Kwamba jaji warioba bado Ana amini CCM itakuja badilika na kurudi kuwa chama cha wananchi Ndio maana hajafikiria umuhimu wa kujitoa kwa maslahi ya taifa letu?

Kwanini nyerere Ndio Awe ni kiongozi pekee wa ngazi ya juu wa chama kusema CCM sio mama yake? Lipi lililo muhimu kwa nyerere foundation kumuenzi baba wa taifa zaidi ya kufuata nyayo zake Katika hili Katika kipindi muafaka Kama cha hivi sasa?

Wapo wanafiki Kama Wassira ambao waliondoka CCM kutokana na uroho wa madaraka na kuhamia NCCR. Leo Anasema eti alihama CCM na kwenda NCCR kwa sababu ya mzee wa warioba. Anajaribu aminisha umma Kwamba mzee warioba ni tatizo kwa chama, taifa, na muungano, na Ndio maana miaka 20 iliyopita, alihamia NCCR. Hii ni hoja dhaifu sana.

Wanafiki Wengine waliodiriki kuhama CCM kwa ajili ya maslahi ya uongozi ni Sitta, nape nnauye na wenzao ambao waliunda CCJ. Lakini baada ya kuahidiwa madaraka ndani ya CCM, wakarudi CCM na kuacha umma ukishangaa jinsi gani kumbe hawakuwa na lengo la kutetea maslahi ya wananchi Bali mlo wao. Tazama Vitendo vya Sitta bungeni, Tazama kauli za nape nnauye, yote ni ushahidi Kwamba kumbe hawakuwa wanajali maslahi ya wananchi Bali vyeo na fursa za ndani ya CCM na serikali yake.

Kwanini akina mzee warioba wasiondoke CCM sasa? Kwani wana nini cha kupoteza? Je bado wanafadhiliwa na CCM? Je hawakuwa na mwalimu nyerere kwa Dhati? Je Hawana maamuzi magumu? Je bado wana amini Kwamba CCM itabadilika na Kwamba wataweza chochea mabadiliko wakiwa ndani? Je ni Kwamba maisha Yao yatakuwa hatarini? Kati ya CCM na vyombo vyao vya dola na wananchi, Nani atakuwa ni mlinzi wa kuaminiwa zaidi kwa wazee hawa iwapo wataondoka?

Mwalimu nyerere alipata kusema hivi:

• iwapo wananchi hawatopata mabadiliko kupitia CCM, basi watayatafuta kupitia chama kingine.

Pia akaja kusema:

"Kiongozi bora hawezi kupatikana nje ya CCM."

Je kauli Mbili hizi zina maana gani Katika mazingira ya sasa?

Sent from my iPhone using JamiiForums

Ahsante sana mkuu hakuna kitu umeacha.
 
Wanajamvi, tafsiri hii si rasmi. Ni tafsiri yangu ili kuhakikisha hatuachi mtu yoyote nyuma kwasababu tu ya lugha.
Ninaomba radhi kwa mapungufu au makosa yatakayojitokeza. Si nia yetu ni ubinadamu!

'''Siyo kwamba amani imejitokeza yenyewe.
Chanzo cha amani Tanzania si kwamba Azimio la Arusha limeondoa umasikini hata kidogo. Je, si umasikini huu ambao tunaishi nao?

Umasikini upo na tunao hapa. Si kweli kuwa ni uchumi huu tunaohangaika nao? Ukweli ni kuwa Azimio la Arusha halijaondoa umasikini hata kidogo na wala haitumainiki kuwa hivyo.

Azimio la Arusha linatoa matumaini.
Matumaini ya haki kwa walio wengi, na hakika Watanzania wengi wanaendelea kuishi katika matumaini haya. Midhali yapo matumaini utaendelea kuishi kwa amani.

Tanzania tuna umasikini lakini si saratani ya kijamii, kuna uwezekano imeshaanza. Vinginevyo hatuna ‘saratani ya kijamii’’

Hatuna volkeno inayorindima kwamba ipo siku italipuka.
Hatujafikikia hatua hiyo kwasababu watu wana matumaini kutokana na msimamo uliochukuliwa na Azimio la Arusha.

Azimio halijamaliza umasikini lakini imetoa kila kilichopo, ubepari na ujamaa kwa ufanano, fursa ya kujenga nchi yenye matarajio kwa wengi.

Hivi kwa uhakika, nyie waswahili, hivi mnategemea kuitawala Tanzania bila kuwepo matumaini, pasipokuwepo matumaini,mkitegemea watakaa kimya kwa amani?

Amani ni zao la matumaini, amani ikiondoka kutakuwa na mtafaruku katika jamii. Nitashangaa kama hawa Watanzania hawataasi, kwanini?

Hivyo hatuwezi kusema tumefikia hatua ya kusahau Azimio la Arusha. Msijidanganye.

Hili ni kama lile la mjinga kutumia ngazi kupanda, akifika juu akaipiga mateka. Sawa, mpo juu na mumeipiga ngazi mateke,sawa, hivyo kaeni pale.

Kaeni hapo kwasababu tatukata tawi.
Mpo juu, tupo chini na mumepiga teke ngazi. Hili tawi lipo juu sana, tutalikata.
Anguko lenu halitakuwa la kawaida.

Nisiseme zaidi. Inatosha kusema tunapaswa kukubali misingi yetu, tuendelee na misingi yetu ya kujenga amani na amani yenyewe.

Tanzania iendelee kuwa na imani na chama,serikali na nyie wenye mamlaka.
Tanzania iwaone nyie kama miongoni mwao na si maadui''
Nguruvi3, tunashukuru kwa tafsiri. Maneno haya ya mwalimu yanapatikana kwa urahisi zaidi kwenye chapter ya Issa Shivji iliyopo ndani ya kitabu cha haroub Othman(Ed), cha mwaka 2000. Kitabu cha haroub Othman kinaitwa: "Reflections on Leadership in Africa: 40 years of independence, na Chapter ya Shivji Ipo titled: Critical Elements of a New Democratic Consensus in Africa (kurasa 25-38).

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Kuna maswali kauliza Mchambuzi kuhusiana na uanachama!
Tutarejea kuyaangalia.

Kinachofuata ni kuangalia kwanini CCM wanakereka Warioba anapoongea ikiwa wanadai wametumia rasimu yake, wengine wakisema Warioba ameokota maoni kutoka kusikojulikana.

Kwanini CCM inafanya vurugu na akina nani wapo nyuma ya vurugu hizi.

Kuna madai kuwa nchi za magharibi zinatumika, lakini pia kuna habari za kikundi cha Watanzani waishio nchi za magharibi kutumia CCM kwa mafao yao. Sijui hawa nao itasemwaje.

Kuna habari ilivuja kuhusu vurugu jumamosi iliyopita ambayo leo tunajua ni kweli.
Tunafuatilia organization hiyo inafanywa vipi na kwa masilahi gani.

Hawa akina makonda ni punda wa kubeba mzigo, wenye mzigo wapo

Tutaangalia athari za Makonda na group yake kwa taswira ya CCM.
Je, CCM ilitenda haki kwa Mansour Himid kama inavyotakiwa itende haki kwa Makonda?
Kwanini double standard na kwanini wazee kama Sitta wapo nyuma ya makundi haya ya wahuni.

Tunaangalia haya katika mabandiko yanayofuata.
 
Hakika hii ni dalili dhahiri ya Utawala kuanguka, tukitazama historia ya mataifa mengi duniani ambayo yalivimbiwa madaraka na kudharau wananchi, siku za mwisho matukio yalikuwa Kama haya ya CCM. CCM ilijenga uhalali wake wa kutawala kwa kutumia mikakati mikuu miwili:

1. Kuunganisha wananchi (national unity) kwa njia mbalimbali kisera, kiitikadi n.k.
2. Kushirikisha wananchi Katika kuchagua wananchi (popular participation).

Katika yote haya, tunaona common denominator ni Neno "wananchi", na Ndio maana Utawala wa mwalimu ulipata uhalali mkubwa wa kutawala na wananchi Wala hawakujali sana suala la katiba ya nchi. Leo Katika CCM, hakuna suala lolote la Dhati linalohusisha Neno au Dhana ya "wananchi", hakuna. Kila kitu kinachohusu wananchi, hakina maslahi na CCM Tena, kwani walio muhimu kwa chama Leo hii ni tycoons wa ndani wanaokusaidia chama pesa, na pia tycoons wa nje ya nchi ambao Haki ya mungu kwa wananchi (ardhi na rasilimali) zingekuwa na CCM kuwa ni Haki ya mzungu.

Ndio maana mazingira Kama haya yanahitaji sana, Mageuzi ya kikatiba (constitutional reforms) ambayo yataweka Mbele maslahi ya wananchi walio wengi bila ya kuweka vipaumbele Katika itikadi za vyama. Kwa maana nyingine, Katika mazingira ya sasa, legitimacy ya serikali yoyote madarakani inatakiwa itokane na katiba iliyotokana na maridhiano, katiba ambayo watawala na watawaliwa wataiheshimu na watailinda. Hayo Ndio jaji warioba alilenga kuwapatia wananchi, hasa baada ya kusikia maoni, malalamiko na vilio vyao kwa maelfu. Kwa Tabia ya sasa ya CCM, maana yake ni Kwamba CCM inakataa Kwamba wananchi wana vilio, matamanio, malalamiko mengi ambayo suluhisho lake lipo Katika katiba mpya ambayo itaendana na maoni Yao na ndoto zao juu ya taifa wanalotaka, na la kuwaachia vizazi vyao vya baadae.

Mwalimu nyerere aliona haya muda mrefu sana. Kwa mfano mwaka 1987, miaka mitano Kabla ya kurudishwa kwa Mfumo wa vyama vingi nchini, miaka zaidi ya mitano kabla ya kuzaliwa kwa vyama vya CUF, NCCR, na chadema, miaka 27 Kabla ya kuzaliwa kwa UKAWA, mwalimu nyerere alinukuliwa akisema maneno haya (daily news):

["It is not that peace has come by itself. The source of peace in Tanzania is not that the Arusha Declaration has done away with poverty even a little bit. Isn't there this poverty we are still living with? This poverty is right here with us. It is not the same economy we are grappling with? The fact is not that the Arusha Declaration has banished poverty even by an iota – nor did it promise to do so. The Arusha Declaration offered hope. A promise of Justice, hopes to the many, indeed the majority of Tanzanians continue to live this hope. So long as there is this hope, you will continue to have peace. Here in Tanzania we have poverty but no ‘social cancer'. It is possible it has just begun. But otherwise we don't have a social cancer. There isn't a Volcano in the making, that one day it is bound to erupt. We have not yet reached that stage because the people still have hopes based on the stand taken by the Arusha Declaration. It did not do away with poverty but it has given you all in this hall, capitalists and socialists alike, an opportunity to build a country which holds out a future of hopes to the many.

To be sure, you few Waswahili, do you really expect to rule Tanzanians through coercion, When there is no hope, and then expect that they will sit quiet in peace? Peace is born of hope, when hope is gone, there will be social upheavals. I'd be surprised if these Tanzanians refuse to Rebel, why?

When the majority don't have any hope you are building a volcano. It is bound to erupt one day. Unless these people are fools. Many in these countries are fools, to accept being ruled just like that. To be oppressed just like that when they have the force in numbers, they are fools. So Tanzanians would be fools, ******, if they continued to accept to be oppressed by minority in their own country. Why?

Therefore we cannot say that we have now reached a stage when we can forget the Arusha Declaration. Don't fool yourselves. This would be like that fool who uses a ladder to climb and when he is up there kicks it away. Alright, you are up there, you have kicked away the ladder, right, so stay there because we will cut the branch. You are up there, we are down here and you have kicked away the ladder. This branch is high up, we will cut it. Your fall will be no ordinary fall either.

Let me say no more. It is sufficient to say we should accept our principles, we should continue with our principles of building peace and peace itself. Tanzanians should continue to have faith in the party, in the government and in you in positions. Tanzanians should see you as part of them not their enemies."]

Wataalam wa lugha watatusaidia na tafsiri kwani maneno haya huu Ndio Wakati wake kwa wananchi Kuanza kuyafanyia kazi maneno haya ya mwalimu kwa Vitendo.

Miaka Kama nane baada ya mwalimu kutoa kauli hii (mid 1990s), baada ya kuona CCM ikizidi kuwatelekeza wananchi, mwalimu aliendelea kukosoa CCM na viongozi wake.Ikafikia hatua Mwalimu Nyerere akatamka Kwamba yupo tayari kurudisha kadi yake namba moja ya CCM, hasa pale alipofanyiwa mambo ya Dharau, udhakalishaji na ya kitoto na viongozi wa CCM, pale chama kilipowatuma ngwilizi na majogo kwenda Butiama kumhoji mwalimu kwanini alikuwa Ana kikosoa chama na kwanini alikuwa anaunga Mkono upinzani. Ni busara tu zilikuja kutumika Vinginevyo CCM Leo ingekuwa haipo.

Kwa kweli kwa hatua tuliyofikia Leo chini ya uongozi wa ccm, tunu pekee ambayo wananchi wataweza kumpa mwalimu nyerere ni kwa wananchi kuchukua maamuzi magumu na kuandamana kumwomba warioba na wenzake wajitoe CCM na kubakia Raia wa kawaida. Vinginevyo, akina jaji warioba ilitakiwa watumie nyerere day ya mwaka huu kutangaza Rasmi kujitoa CCM Kama njia ya kumuenzi mwalimu na kuomba wananchi Wawaungr Mkono. Warioba na wenzake ni bora wakaondoka CCM kuliko kuendelea kuelezea umma jinsi gani CCM inalitumia vibaya jina la mwalimu. Huu ni Wakati wa mzee warioba na wenzake kuwaeleza wananchi jinsi gani jina la mwalimu kitaweza kutumiwa vizuri na kwa manufaa ya walio wengi Katika muktadha wa katiba mpya.

Vinginevyo ni kwanini hakuna kiongozi wa kufuata nyayo Kama za mwalimu na kuthubutu kutangaza nia ya kuondoka CCM? Amejaribu Sumaye, lakini Huyu ni kwa condition Kama hatosimamishwa na CCM 2015 lakini hasa iwapo mshindi atapatikana kwa rushwa. Viongozi wa aina ya akina Sumaye sio wa kuaminiwa na wananchi kwani Katika suala la katiba mpya, wameonyesha Kwamba wao ni wale wale Kama akina Sitta, Chenge, na wenzao, kwani hawatumii nafasi zao kukosoa ubovu wa mchakato wa katiba mpya, wanaothubutu ni akina jaji warioba, sasa kwanini wasiende Mbali na kujitoa CCM sasa hivi Kama njia ya kumuenzi mwalimu kwa Dhati? Kwa kufanya hivyo jaji warioba na wenzake watapoteza nini kikubwa zaidi ya heshima Mbele ya umma?

Hoja za kujitoa CCM ni nyingi kwa akina warioba Mbele ya umma. Mbali ya katiba mpya, jaji warioba alikuwa ni Mwenyekiti wa tume ya mkapa iliyochunguza ufisadi serikalini na kutoa ripoti yake, ambayo haikufanyiwa kazi. Kwahiyo jaji warioba anapojadili suala la maadili Kama Tunu ya taifa, anayo mengi moyoni ambayo yatasaidia wananchi Kupata ujasiri zaidi wa kuikataa katiba inayolazimishwa na CCM.

Turudie Tena, kwanini jaji warioba na wenzake wasiitishe mkutano na kutangaza kujitoa CCM na kushawishi Wengine Wawaunge Mkono Katika mkutano wa hadhara? Tupo wengi ambao tutamuunga Mkono.

Vinginevyo je Ina maana Kwamba jaji warioba bado Ana amini CCM itakuja badilika na kurudi kuwa chama cha wananchi Ndio maana hajafikiria umuhimu wa kujitoa kwa maslahi ya taifa letu?

Kwanini nyerere Ndio Awe ni kiongozi pekee wa ngazi ya juu wa chama kusema CCM sio mama yake? Lipi lililo muhimu kwa nyerere foundation kumuenzi baba wa taifa zaidi ya kufuata nyayo zake Katika hili Katika kipindi muafaka Kama cha hivi sasa?

Wapo wanafiki Kama Wassira ambao waliondoka CCM kutokana na uroho wa madaraka na kuhamia NCCR. Leo Anasema eti alihama CCM na kwenda NCCR kwa sababu ya mzee wa warioba. Anajaribu aminisha umma Kwamba mzee warioba ni tatizo kwa chama, taifa, na muungano, na Ndio maana miaka 20 iliyopita, alihamia NCCR. Hii ni hoja dhaifu sana.

Wanafiki Wengine waliodiriki kuhama CCM kwa ajili ya maslahi ya uongozi ni Sitta, nape nnauye na wenzao ambao waliunda CCJ. Lakini baada ya kuahidiwa madaraka ndani ya CCM, wakarudi CCM na kuacha umma ukishangaa jinsi gani kumbe hawakuwa na lengo la kutetea maslahi ya wananchi Bali mlo wao. Tazama Vitendo vya Sitta bungeni, Tazama kauli za nape nnauye, yote ni ushahidi Kwamba kumbe hawakuwa wanajali maslahi ya wananchi Bali vyeo na fursa za ndani ya CCM na serikali yake.

Kwanini akina mzee warioba wasiondoke CCM sasa? Kwani wana nini cha kupoteza? Je bado wanafadhiliwa na CCM? Je hawakuwa na mwalimu nyerere kwa Dhati? Je Hawana maamuzi magumu? Je bado wana amini Kwamba CCM itabadilika na Kwamba wataweza chochea mabadiliko wakiwa ndani? Je ni Kwamba maisha Yao yatakuwa hatarini? Kati ya CCM na vyombo vyao vya dola na wananchi, Nani atakuwa ni mlinzi wa kuaminiwa zaidi kwa wazee hawa iwapo wataondoka?

Mwalimu nyerere alipata kusema hivi:

• iwapo wananchi hawatopata mabadiliko kupitia CCM, basi watayatafuta kupitia chama kingine.

Pia akaja kusema:

"Kiongozi bora hawezi kupatikana nje ya CCM."

Je kauli Mbili hizi zina maana gani Katika mazingira ya sasa?

Sent from my iPhone using JamiiForums

Mchambuzi umeongea point za maana sana. labda tuanze kugusa moja moja. Kwa sasa kuna watu ambao ni waumuni wa kweli wa CCM kama vile mzee Warioba ambao licha ya uchafu wa chama, na licha kuwa they will not lose a thing if they leave the party, bado wako ndani ya chama. Mzee Warioba ni my view is Die hard CCM. Lakini kuna wengine ambao ni CCM Maslahi, wanaweza kuwa na ideas nzuri na mtazamo mzuri, lakini kutokana na matumbo hawawezi kutoka ndani ya chama.

Mfano mzuri ni mchakato wa katiba, kuna wengi tu ndani ya CCM ambao hawakutaka Katiba ya Chenge, lakini walilazimkika kuikubali kwa kuwa kinyume na hivyo ingeharibu kitumbua chao. Kwa hiyo walijikuta mahali walipotakiwa kufanya uamuzi wa kuangalia maslahi yao na kusema fcuk CCM fcuk the country, to hell with morals. Siwezi kuwalaumu sana watu wenye akili na uwezo ndani ya CCM ambao hawapendi kwenda upinzani. Bado hatuna formidable opposition kuwekeza kushawishi wana CCM baadhi ya wanaCCM. Kwa hiyo suala la kupoteza heshima lipo, lakini they can live with it. Wassira ni mfano mzuri.

Umetoa mfano mzuri kuhusu Sitta na Nnape. Ninachoona ni kuwa wanajua wazi kabisa kuwa wanachoamini na wanachoongea havilingani. Sitta ni kama Kinana, ukiw ana uchafu wako mwingi umeukusanya, ukienda kinyume na interest zao basi wanakubomoa. Survival yao ni kufanya kibaya ili wajipendekeze na kulinda vitumbia vyao. I do not see many in CCM leadership, who have interests of Tanzania at heart or of the party for that matter.

Na kuhusu kauli ya Mwalimu, nadhani aliitoa mwaka 1995 sina hakika. That is 20 years ago. Wakati huo alikuwa anawaonya CCM kuwa kama hawatamchagua Mkapa, waliokuwa wanaelekea kubaya, na kama wangemchagua wangekuwa wamefanya ajambo la maana.

Lakini kama ukimsoma vizuri Nyerere, mwishoni mwishoni alikuwa anatoa kauli nyingi sana ambazo zilikuwa zinaonesha wazi kuwa hata yeye alikuwa amechoshwa na CCM. Alikuwa anajua uchafu mwingi sana ndani ya CCM, uchafu wa chama na individuals ndani ya Chama. You can remember alivyowaambia tume wamuwidhinishe Mrema kuwa mbunge wa Temeke, na kukosoa vikali CCM kwa kuwa detached kutoka kwa wananchi.

Tunachokiona sasa cha CCM kutokuwa chama cha wananchi, kilianza kuonekana toka wakati Nyerere akiwa hai, so in my view tunaelekea kwenye yale aliyosema Nyerere. Upinzani wa kweli na madhubuti utatoka ndani ya CCM. Mchambuzi ni living example ya ushahidi huu, uko ndani ya CCM unakosoa vikali ubovu ndani ya chama, just a matter of time more voices of wisdom will follow suit. Climax itafikia pale chama kikipasuka na kuwa vyama viwili tofauti, i see it coming in less than ten years. Chaguzi mbili zijazo zitatusaidia kuleta hili.
 
njia ya kususa itakuwa ngumu bro, na imeshafeli kuanzia kule mjengoni, kwa mfano wa daladala ndo kab isaa, maana tunaowasusia hawatumii usafiri huo wa makabwela, kwenye kupiga kura ukisusa ndo imekula kwetu, huko kwenye kumbi mbali mbali akiwepo mtawala mmojawapo kwa ujinga wa watanzania watamsogelea na kupiga nae picha, dawa ni moja tu, kuagiza silaha kupitia hata Kenya au Rwanda na kuingia msituni na kupambana na hao wahuni wachache wasiozidi hata milioni moja, ni kwa jasho na damu tu ndipo haki itapatikana, YES kwa JASHO NA DAMU na sivinginevyo.
Wakuu zumbemkuu na jitegemee ,inasemwa kuwa nguvu kubwa na ya maana katika maisha ya mwanadamu ni kutumia akili, maarifa na ufahamu.

Kwasasa wananchi wetu wengi hawana ufahamu wa nini kinafanywa na hawa watawala.

Ukisoma bandiko la Mchambuzi , Nyerere alisema kuwa atashangaa kama haitafika siku wananchi wakaasi.
Na atashangaa kama Watanzania watakaa kimya.

Hii ina maana yale maneno yake yanaanza kutimia.
Yanatimia baada ya wananchi kung'amua mbinu zao kila uchao.

Kazi kubwa si kupambana na kikundi hiki, kazi nzito ni kutoa elimu ya umma kuhusu kujitambua na kutambua haki zao. Hiyo ndiyo silaha muhimu sana katika kukabiliana na kikundi cha wahuni.

Nadhani ni vema zaidi kutoa elimu kwanza watu wajitambue na watambue haki zao.
Kwa mfano, kama mwananchi haelewi madhara ya kuuza shahada ya kura, ni unlikely anaweza kushiriki kususia.
Si kwamba hataki bali hajui umuhimu wa kufanya hivyo.

Nguvu ya umma ni muhimu sana katika mapambano ya fikra.
Hapa kinachotokea ni kikundi cha watu kufanya ''exploitation' kwasababu kinaelewa sehemu kubwa ya jamii haielewi matatizo yanatokana na nini. Watakapokielewa, kikundi hicho kitashindwa kwa nguvu ya umma tu bila tusi.

Sasa kazi ya ilm inaanzia wapi. Ni kuwaonyesha wapi kuna tatizo na kwanini.
Mfano, utakuwa umempa mwananchi nguvu kubwa sana ya kifikra kama utaonyesha jinsi ambavyo CCM wanababaisha watu.

Wananchi waelezwe, kwanini jambo kama katiba linakuwa la chama na si la taifa?
Kwanini Mwandosya apate ushindi wa nyaraka ya taifa ambayo CCM ni sehemu tu na wala siyo taifa kwa ujumla.

Kuendelea kuwaonyesha, kwanini CCM waseme hawajabadili rasimu ya Warioba wakati huo huo wanasema Warioba hakupata maoni ya watu. Hapa ni kuweka black and white na kuuliza, CCM inasimamia wapi katika hoja kama hii.

Ni kutoa elimu ya jinsi gani umasikini wa wananchi unavyochagizw na kikundi cha watu.
Mfano, leo kuna bilioni zaidi ya 3 zimetengwa kuhakikisha katiba ya Chenge inapita.

Swali la kumuuliza mwananchi, katiba ni nyaraka inayomhusu kwanini wawepo watu wanaotumia mamilioni kuhakikisha imepita? Pesa hizo ambazo ni kodi yao zimetoka kasma gani ya serikali na bajeti ipi. Hapa ndipo ufisadi ungejulikana na uwajibikaji kuchukua nafasi

Ni kumweleza mwananchi, zile pesa za kununua dawa MSD tulizoambia serikali haina, hizi za kuhonga vyombo vya habari zimetoka wapi? Na mwananchi huyo huyo ajiulize, gharama zinazotumika zitatua vipi matatizo yake.

Elimu ihusu kumwelesha mwananchi kwanini CCM wanatoa vipigo kwa akina Warioba.
Kuna kitu gani wasichotaka kisikike na kwanini.
Na kwanini wasitetee katiba ya Chenge kwa hoja bali vurugu na vipigo kwa kutumia makundi ya wanaCCM.

Siku idadi kubwa itakapoelewa, ni rahisi kuwaambia sasa tususie abcd kwasbabu tayari wana ufahamu wa uhuni na madhila wanayofanyiwa.

Itakuwa ni rahisi kuwaambia, utamaduni wa kupiga kura kivyama ndio chanzo cha matatizo yao.
Hoja kubwa ni kuwaamsha ili waweze kuwahoji wawakilishi wao kuhusu maamuzi wanayofanya kihuni.

Mfano, hivi kwanini wabunge wa CCM walioshiriki uhuni wa Sitta na Chenge wasipigwe fullstop ya kuachaguliwa tena. Ni hadi wananchi watakapokuwa na nguvu ya kuanza ku deal na watu kama wabunge, viongozi wa kikundi watapa ujumbe.

Ndivyo walivyofanya Zambia, ndivyo KANU ilivyopelekwa maktaba. Leo wabunge na serikali za nchi hizo zinajua fika bila ku-deliver wananchi wanahukumu yao.
 
Bongolander
Ahsante kwa mchango wako hasa nikizingatia umejibu hoja nyingi nilizotaka kuzieleza au kuuliza.

Kuna tatizo kwa upande wetu wananchi. Kama ulivyosema, kazi ya CCM na kundi lao ni kuhakikisha wanawabana watu kwa kutumia nguvu za kashfa zao kama ulivyosema kwa Sitta.

Hata hivyo, wananchi wanapaswa pia kuanza kuhoji. Hivi hawa wanaosema wanagombea urais wana misimamo gani pekee nje ya chama chao.

Juzi mzee Warioba kapokea kipigo. Hawa watu wanaotaka uongozi mbona wamekaa kimya.
Kwanini wasubiri kuongelea makanisani na si kwenye majukwaa ya siasa.

Tatizo ninalo liona katika hoja ya upinzani wa kweli utatoka CCM ni ile ya makapi.
Wale watakaokosa ulaji CCM wataondoka na kuhamishia matatizo kwingine. Ndio akina Mrema na Hamad Rashid.

Kwa mtazamo wangu, sidhani CCM inaweza kumeguka na kutoa upinzani. Kilichopo ni CCM kuondoka kabisa.
Inapofikia mahali sasa ni mapigo na si sera, sioni nani anaweza kutoka CCM na kuanzisha upinzani wa kweli.

Ninachokiona ni kifo cha CCM haraka kuliko inavyotegemewa. Hakuna wa kutetea chama! hawa akina Makonda!
 
KWANINI CCM HAWATAKI KUMSIKIA WARIOBA?

Tumeona vipigo vinavyotolewa na CCM. Hakuna jambo la kushangaza katika hili.
Mwenyekiti wa CCM alifungua pazia kwa kumdhalilisha Warioba na tume yake
Wakafuata makada ndani ya bunge lao. Wote walimfanya Warioba 'public enemy number 1''

Kitendo cha CCM kukaa kimya kina maana nyingi.
Kwanza, ni kujenga mazingira ya kumhusisha Warioba na vurugu walizofanya kwa kumtumia Paul Makonda na genge lake CCM inaogopa kumwajibisha Paul kwasababu ametumwa na anabeba siri nyingi za waliomtuma.

Haiwezekani Mansour Himid aseme S3 CCM imwajibishe. Kwa kauli tu!
Makonda aliyeonekana akiongoza vijana wa CCM kutoa adhabu kwa Warioba ameachwa atambe.
Hii ni ushahidi usio na shaka kuwa mbinu za kumdhuru Warioba ziliratibiwa na CCM.

Mwenyekiti JK kamkejeli Warioba akiwa Mwanza, huku mwenyekiti wa bunge la CCM akishadidia kipigo kana kwamba hilo lilikuwa jambo la busara na Warioba subiri zaidi.

Akina Nape na wengine wamekaa kimya kuhusu kipigo cha Warioba.
Wanafahamu undani wa mpango huo na kitendo cha kumtosa Makonda kitatoa siri zisizotakiwa kujulikana.

CCM ina njia mbili tu. Moja, kusimama na kusema uovu huo haukubaliki au kukaa kimya na kubeba lawama za vurugu.

Mbele ya safari, CCM hawatakuwa na maadili tena ya kuongelea amani na utulivu.
Upi huo ikiwa wao ndio wana andaa magenge ya kuzusha vurugu katika jambo lililohitaji majadiliano tu

KWANINI CCM WANABARIKI UOVU HATA KWENYE MIJADALA?

CCM haitaki kusikia tume ya Warioba ikizungumza jambo.
Kuna sababu kuu mbili zinazowasukuma kufanya hivyo hadi kufikia mahala pa kuhamasisha vurugu kama tulizoona.

  1. Hawataki hoja zao za kubabaisha zijulikane kwa wananchi

  1. Utetezi wao ni kuwa katiba iliyopo imetokana na rasimu ya Warioba.
  2. Rasimu ya Warioba haikubeba mawazo ya wananchi

Hoja hizi mbili zinakinzana sana. Iwapo rasimu ya Warioba haikutokana na mawazo ya wananchi, iweje CCM iseme katiba ya Chenge ni zao la rasimu ya Warioba?

Pili, je, katiba ya Chenge imetokana na rasimu gani kama ya Warioba si halali.
Kuna takwimu gani nzuri zaidi au mfumo gani bora uliotumika kuhakikisha kuwa katiba ya Chenge ni ya wananchi?

Kutokana na mambo hayo, CCM haitaki kabisa kusikia tume ya Warioba ikitoa ufafanuzi wa nini kimetokea kwani kufanya hivyo itawaumbua.

CCM wanafahamu katiba ya Chenge ni ya mafichoni na hivyo wasingependa kwenda mbali zaidi siri zao kubainika.

Inaendelea
 
1.CCM hawataki tume ya Warioba kwasababu tume itaweka wazi ubabaishaija walioufanya kwa wananchi.

  1. Kuna hoja za S3 kuwa mzigo
  2. Serikali ya muungano kutokuwa na vyanzo vya uhakika vya mapato na jeshi kupindua nchi
  3. Kumbebesha mzigo mlipa kodi
  4. Tanganyika kuvaa koti la muungano
n.k.

WARIOBA ALISEMA NINI
Katika hoja zake, Warioba kwanza alionyesha kuwa katiba si zao la rasimu.

Jambo hilo CCM hawataki kulisikia ndio maana hawana jibu kama katiba yao ni zao la rasimu au ni kitu kingine kwavile rasimu ya tume ilikuwa haramu kwa mujibu wao.

Warioba akaonyesha jinsi ambavyo Tanganyika itavaa koti la muungano zaidi ya kuvua.
Rasimu yake ilikuwa na mambo 11, katiba ya Chenge na Sitta ina 16.

Hii maana yake ni kuwa rasimu ya Warioba ililenga ku address matatizo zaidi kuliko ya Chenge.
CCM hawatki kusikia kwasababu hoja ya Tanganyika kuvaa koti haina jibu.

Kuhusu gharama, Warioba kasema rasimu ilionyesha vyanzo vya serikali ya muungano.
Katiba ya Chenge haina vyanzo, chanzo kikubwa cha muungano ni serikali ya Tanganyika.
Hoja ya jeshi kupindua nchi imekufa.

Hii maana yake ni kuwa katiba ya Chenge imejibu hoja za Wazanzibar kwa kuwabebesha Watanagnayika mzigo mzito kuliko waliokuwa nao sasa hivi.
Hoja ya vyanzo vya uhakika hawana jibu. Hwataki kumsikia Warioba akibainisha.

Hoja za namna hiyo ni nyingi ambazo CCM imeshindwa kuzitolea majibu.
Hata pale itakapotoa majibu, kutakuwa na utata mkubwa sana, yaani tatizo ni kubwa kuliko lilivyo.

Mfano, suala la ardhi limebaki kuwa la muungano. Kule znz ni la SMZ. Suala la gesi limeondolewa.
Lakini gesi inapatikana katika ardhi ya muungano.

Sasa znz watavuna vipi gesi ambayo mmiliki wa ardhi iliyomo ni rais wa JMT?
Lakini pia, suala la gesi lina utata.
Ile ya znz ni ya znz na ile ya Tanganyika ni ya wote. Hapa kuna haki na usawa wa muungano?
Haya ndiyo CCM wasiyotaka wananchi kusikia.

Kuna suala la mzigo wa viongozi. Hii ilikuwa hoja ya CCM kuwa wananchi watabeba mzigo mzito.
Katiba ya Chenge inaonyesha marasi watakuwa wengi kuliko rasimu ya Warioba.
Haya ndiyo CCM wasiyotaka kuyasikia katika ufafanuzi.

CCM wanaelewa hawana hoja za kutetea uhalifu na katiba ya Chenge.
Wanachotaka ni wananchi kuamini tu kuwa katiba ya Chenge iliyogawa maeneo ya wafugaji na wakulima ni bora sana. Hawataki wananchi waelezwe au wachambue maana ya katiba na kama ya Chenge imefikia hata nusu ya katiba.

Ni kwa mukatadha huo, CCM hawana hoja na hoja zinazowazonga ni nyingi kuliko majibu waliyo nayo.
Hili ndilo linawasukuma kufika mahali wanahamasisha uvunjaji wa sheria.
Wanahamasisha wazee kama Warioba wapigwe. Ni ombwe la hoja na ombwe la uongozi.

Kikubwa zaidi ni pale katiba ya Chenge inaposusiwa.
CCM wamebaini katiba ya Chenge haizuki, si kwa wananchi hata kwa wanachama wake. Hivyo njia bora ni kuzia mijadala na njia rahisi ni kuhamaasisha vurugu kwa kutumia makundi ya vijana kama akina Makonda.

Piga piga wanazohamasisha CCM hazitazaa majibu. CCM wajiulize kwanini katiba ya Chenge imesusiwa.
CCM wajiulize je yale malalamiko ya wananchi yamepatiwa majibu.
Na CCM wajiulize, ule uharamu wa bunge la CCM unaleta maridhiano ya kitaifa?

Vurugu ni tatizo kubwa CCM inaliandaa kwa taifa hili. Suala la katiba litakapofika mitaani litakuwa tatizo kubwa.
Itakuwa si piga piga bali piga nikupige. Ndivyo nchi jirani zilivyoanza.

Moto huo hautazimika kwa askari. Moto huo utawaka na hatakuwepo CCM au awaye.
Hili la katiba halina maridhiano na ndicho chanzo cha piga piga.

Mbinu ya kutaka kumyamazisha Warioba na tume kwa kutumia vurugu ili wamsumange zimegonga mwamba.
Taifa limeona kwa macho jinsi CCM ilivyosiriki kikamilifu katika mbinu chafu za kutaka kuleta madhara katika maisha ya wanadamu. Mbinu zilizolenga kumdhuru mzee Warioba na tume.

Tusemezane
 
MPANGO ULIKUWA ''MZURI'
JARIBIO LIKAFANYWA BILA WELEDI

CCM WANA MAMBO 2 YA KUFANYA

Mpango wa kuleta vurugu ulikuwa umepangwa ‘vizuri' ili kumhusisha Mzee Warioba na tume yake katika vurugu. Hili lingesaidia sana kutoa picha mbaya ya iliyokuwa tume likilenga kuonyesha, inatumiwa au ina lengo la kuleta vurugu.

CCM walipanga kutumia mwanya huo kumdhalilisha zaidi Mzee Warioba na pengine kutumia slogan yao ya amani na utulivu katika kampeni zake.

Kwa bahati mbaya waliofanya mpango huo hawakuwa na weledi au walikosea kiufundi.
Mabango yaliyotolewa katika mkutano yalihusisha CCM.
Vurugu zilizotokea zilimhusisha kiongozi wa CCM bwana Makonda

Kwa kufanya vurugu, nchi na duni iliona CCM walikusudia kuleta vurugu katika mjadala ambao haukuwa na chembe za uvunjifu wa amani.

Katika mpango huo, ilikuwa almanusra Mzee Warioba na wengine wajeruhiwe au wadhurike.
CCM haikuwa imelenga huko, ilikuwa imelenga kumtia doa.

Bahati mbaya waliopewa kazi walienda mbali na kufikia hatua ya kuhatarisha maisha ya makamu wa Rais mtstaafu na waziri mkuu pamoja na wahshiriki wengine.

CCM ilitakiwa ifanya ‘damage control' kwa kukemea tukio ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mbele ya sheria wahusika. Aidha ilipaswa kumuadhibu au kuwaadhibu wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine.

Tatizo linaloikabili CCM ni kuwa na viwango tofauti vya maamuzi ‘double standard'
Kwa mfano, Mansour Himid wa CCM znz aliadhibiwa kwa msimamo wa S3 tu bila tusi au kunyanyua mkono.

Wanachama 6 wa CCM-znz walikataa kupiga kura au walipiga kura ya hapana katika bunge lao.
Na pia wapo watu waliopinga msimamo wa CCM kwa namna tofauti.
Hao wote hawajawahi kuchukuliwa hatua yoyote.

Kuwachukulia hatua waliovuruga mjadala kwa kutumwa inakuwa ni ngumu zaidi.
Hapa ndipo tunaona ukimya wa CCM kwasababu ni mwiba wenye pande mbili.

KWANINI WANAHUSISHWA NA VURUGU

CCM inahusishwa na vurugu kwa namna nyingi.
Kwanza, mwenyekiti wake alihusika katika kuidhalilisha tume ya Warioba alipofungua bunge.
Pili, mwenyekiti wa bunge la CCM alishiriki katika vitendo vya udhalilishaji ikiwa ni pamoja na kuruhusu makada kama Komba kuwatukana akina Warioba.

Tatu, viongozi wa CCM walishiriki kuchochea vurugu katika maeneo kama ya kanisani yakimhusisha waziri wa serikali ya CCM bw, Lukuvi.

Waziri mkuu aliwahi kutoa kauli ya ''wapigwe''

Hivyo kwa Mtanzania wa kawaida haya ya akina Makonda na kundi lake yanaweza kusomeka kama utekelezaji wa maagizo ya viongozi wa CCM.

Katika hali hiyo, CCM ilikuwa na njia mbili tu

  1. Kubaki kimya umma ukiamini kuwa walihusika na tukio la uvunjifu wa amani lililolenga kudhuru watu. Kwamba, wananchi waamini vurugu nyingine za nyuma zilikuwa na mkono wa CCM. Hilo wana weza kubaki nalo wakiendelea kukaa kimya
  2. Kuchukua hatua za kukemea na hata kuwafikisha mbele ya sheria wanaohusika ili umma uone na utambue kuwa, vurugu hazikuwa za CCM.

Katika mambo hayo 2, CCM inabeba mzigo mzito sana. Leo viongozi wa CCM wanawezaje kuhubiri amani na utulivu ikiwa wao ni sehemu ya uvunjifua wa amani tena ukiwalenga makada, wazee na watu wenye heshima nchini?

CCM pia itabidi iwaeleze wananchi, wapi demkorasia na utawala wa sheria inao hubiri.
Kama Mansour alifukuzwa kwa msimamo tu bila tusi, leo kwanini walionyanyua viti na kuponda weananchi waachwe huru.

CCM imesimamia vipi utawala wa sheria ikiwa wananchi hawana nafasi ya kushiriki shughuli zao bila uvunjifu wa amani unaoletwa na CCM?

Ndio maana tunasema, jaribio la kumhusisha mzee Warioba na wenzake katika vurugu za nchi limekwama kwa gharama kubwa ya CCM.

Vipi watasema wanamwenzi Nyerere ikiwa Mwalimu alisema watu wapingane bila kupigana?
Je, ndio CCM aliotaka Mwalimu Nyerere? Na je kwa mashambulizi wanayoonyesha, ndiko kumuenzi mwalimu?

Tusemezane
 
Back
Top Bottom