Mchambuzi
JF-Expert Member
- Aug 24, 2007
- 4,850
- 9,434
Nguruvi3,MPANGO ULIKUWA MZURI
JARIBIO LIKAFANYWA BILA WELEDI
CCM WANA MAMBO 2 YA KUFANYA
Mpango wa kuleta vurugu ulikuwa umepangwa vizuri ili kumhusisha Mzee Warioba na tume yake katika vurugu. Hili lingesaidia sana kutoa picha mbaya ya iliyokuwa tume likilenga kuonyesha, inatumiwa au ina lengo la kuleta vurugu.
CCM walipanga kutumia mwanya huo kumdhalilisha zaidi Mzee Warioba na pengine kutumia slogan yao ya amani na utulivu katika kampeni zake.
Kwa bahati mbaya waliofanya mpango huo hawakuwa na weledi au walikosea kiufundi.
Mabango yaliyotolewa katika mkutano yalihusisha CCM.
Vurugu zilizotokea zilimhusisha kiongozi wa CCM bwana Makonda
Kwa kufanya vurugu, nchi na duni iliona CCM walikusudia kuleta vurugu katika mjadala ambao haukuwa na chembe za uvunjifu wa amani.
Katika mpango huo, ilikuwa almanusra Mzee Warioba na wengine wajeruhiwe au wadhurike.
CCM haikuwa imelenga huko, ilikuwa imelenga kumtia doa.
Bahati mbaya waliopewa kazi walienda mbali na kufikia hatua ya kuhatarisha maisha ya makamu wa Rais mtstaafu na waziri mkuu pamoja na wahshiriki wengine.
CCM ilitakiwa ifanya damage control kwa kukemea tukio ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mbele ya sheria wahusika. Aidha ilipaswa kumuadhibu au kuwaadhibu wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine.
Tatizo linaloikabili CCM ni kuwa na viwango tofauti vya maamuzi double standard
Kwa mfano, Mansour Himid wa CCM znz aliadhibiwa kwa msimamo wa S3 tu bila tusi au kunyanyua mkono.
Wanachama 6 wa CCM-znz walikataa kupiga kura au walipiga kura ya hapana katika bunge lao.
Na pia wapo watu waliopinga msimamo wa CCM kwa namna tofauti.
Hao wote hawajawahi kuchukuliwa hatua yoyote.
Kuwachukulia hatua waliovuruga mjadala kwa kutumwa inakuwa ni ngumu zaidi.
Hapa ndipo tunaona ukimya wa CCM kwasababu ni mwiba wenye pande mbili.
KWANINI WANAHUSISHWA NA VURUGU
CCM inahusishwa na vurugu kwa namna nyingi.
Kwanza, mwenyekiti wake alihusika katika kuidhalilisha tume ya Warioba alipofungua bunge.
Pili, mwenyekiti wa bunge la CCM alishiriki katika vitendo vya udhalilishaji ikiwa ni pamoja na kuruhusu makada kama Komba kuwatukana akina Warioba.
Tatu, viongozi wa CCM walishiriki kuchochea vurugu katika maeneo kama ya kanisani yakimhusisha waziri wa serikali ya CCM bw, Lukuvi.
Waziri mkuu aliwahi kutoa kauli ya wapigwe
Hivyo kwa Mtanzania wa kawaida haya ya akina Makonda na kundi lake yanaweza kusomeka kama utekelezaji wa maagizo ya viongozi wa CCM.
Katika hali hiyo, CCM ilikuwa na njia mbili tu
- Kubaki kimya umma ukiamini kuwa walihusika na tukio la uvunjifu wa amani lililolenga kudhuru watu. Kwamba, wananchi waamini vurugu nyingine za nyuma zilikuwa na mkono wa CCM. Hilo wana weza kubaki nalo wakiendelea kukaa kimya
- Kuchukua hatua za kukemea na hata kuwafikisha mbele ya sheria wanaohusika ili umma uone na utambue kuwa, vurugu hazikuwa za CCM.
Katika mambo hayo 2, CCM inabeba mzigo mzito sana. Leo viongozi wa CCM wanawezaje kuhubiri amani na utulivu ikiwa wao ni sehemu ya uvunjifua wa amani tena ukiwalenga makada, wazee na watu wenye heshima nchini?
CCM pia itabidi iwaeleze wananchi, wapi demkorasia na utawala wa sheria inao hubiri.
Kama Mansour alifukuzwa kwa msimamo tu bila tusi, leo kwanini walionyanyua viti na kuponda weananchi waachwe huru.
CCM imesimamia vipi utawala wa sheria ikiwa wananchi hawana nafasi ya kushiriki shughuli zao bila uvunjifu wa amani unaoletwa na CCM?
Ndio maana tunasema, jaribio la kumhusisha mzee Warioba na wenzake katika vurugu za nchi limekwama kwa gharama kubwa ya CCM.
Vipi watasema wanamwenzi Nyerere ikiwa Mwalimu alisema watu wapingane bila kupigana?
Je, ndio CCM aliotaka Mwalimu Nyerere? Na je kwa mashambulizi wanayoonyesha, ndiko kumuenzi mwalimu?
Tusemezane
Umejadili hoja ya msingi sana, kwa kweli Kati ya jaji warioba na viongozi wa sasa wa CCM, ni dhahiri Kwamba jaji warioba ni kiongozi anayejishughulisha zaidi na kumuenzi mwalimu nyerere kuliko genge la viongozi lililochakachua mchakato wa katiba. Kwa mfano, Katika kitabu chake cha TUJISAHIHISHE (1962), Mwalimu anasema:
[Ukiondoa matatizo wayapatayo binadamu kwa sababu kama mafuriko, nzige, kiangazi, n.k, matatizo yao mengi hutokana na unafsi. Unafsi ni wa aina nyingi. Swali ambalo twalisikia mara kwa mara, Hali yetu ya baadae itakuwaje?, ni swali ambalo sina shaka kuna wanaouliza kwa nia safi kabisa. Lakini mara nyingi linatokana na unafsi. Mtu anayeuliza anafikiri TANU iliundwa kwa faida yake binafsi. Ni kama kwamba TANU ilipoundwa ilimwahidi kwamba ikiwa atakubali kuwa mwanachama, au kiongozi, basi TANU itamfanyia yeye jambo fulani kama tunzo! Anasahau kabisa kuwa TANU inajishughulisha na haja za Jumuiya kwa ujumla. Lakini kwa mtu wa aina hiyo, hata kama TANU inatimiza madhumuni yake kwa jumuiya, ataona kuwa ni umoja ambao hauna maana kwa sababu haumtimizii haja zote za nafsi yake. Huu ni unafsi. Kama wanachama wa TANU, na hasa viongozi, hawatakihukumu chama chetu kwa mahitaji na nafsi zao wenyewe, chana hakitadumu. Wanachama wa aina hiyo ni ugonjwa katika chama.
Dalili nyingine ya unafsi, na ambayo ni ugonjwa mbaya sana ni fitina. Kanuni moja ya TANU inasema hivi: Nitasema Ukweli Daima. Fitina Kwangu ni Mwiko. Lakini bado tunao wanachama ambao ni wafitini wakubwa bila kujitambua. Ni wa aina mbali mbali. Wengine humwona mwenzao anafanya kosa. Badala ya kumwambia pale pale kijamaa kwamba atendalo ni kosa, watanyamaza kimya. Lakini hawanyamazi kabisa. Watakwenda kumteta katika vikundi vya siri. Mateto haya si ya kumsaidia mwenzao, ni ya kumdhuru. Hii ni aina moja ya fitina. Wengine hugawa watu katika mafungu. Fulani japo kafanya kosa kubwa sana hasemwi. Lakini Fulani wa pili akifanya kosa japo dogo, kosa lile hukuzwa likawa kama mlima Kilimanjaro. Hawa hutafuta sababu ya kumtetea Fulani wa kwanza, au za kumaulumu Fulani wa pili, ambazo hazifanani kabisa na ukweli. Kwa watu wa aina hii, ukweli ni jambo ambalo hutegemea mtu, si kitu kinachojitegemea chenyewe bila kujali mtu.Fulani wa kwanza akisema katika majadiliano kuwa mbili na mbili ni tano, wao watakubali. Lakini Fulani wa pili akisema sivyo, mbili na mbili ni nne, watamwona ni mtu mbaya kabisa ambaye hastahili hata kusikilizwa. Hawa hawajali ukweli, hujali nafsi tu. Kwao, ukweli ni maoni yao na matakwa yao. Hatuna budi, hasa katika majadiliano na mazungumzo yanayohusu jumuiya, tujifunze kusikiliza hoja zenyewe zinazotolewa na wenzetu, na kuzijibu zile hoja kwa kuzikubali au kuzikataa, bila kujali kama anaezitoa ni rafiki au si rafiki. Pia wanaopingwa hawana budi wakubali kuwa kinachopingwa ni zile hoja zao, sio wao wenyewe. Bila mazoea haya, mazungumzo hayana maana; yanakuwa ni kupoteza wakati, maana huwa tumekwisha kuzihukumu hoja za mtu hata kabla hajazitamka; kadhalika, hoja zetu zikijibiwa kwa kupingwa halafu tunawakasirikia waliozipinga tunafanya mazungumzo yasiwe na maana, kwa sababu tunapenda hoja zetu zikubaliwe tu hata kama si hoja safi.
Ukweli una tabia moja nzuri sana. Haujali mkubwa wala mdogo; haujali adui wala rafiki. Kwake, watu wote ni sawa. Pia ukweli unayo tabia ya kujilipiza kisasi kama ukipuuzwa. Ukiniona nataka kulipiga teke jiwe kwa kuwa unafikiri kuwa ni dongo au mpira, natumaini utanionya. Lakini nikilipuuza onyo lako kwa sababu eti wewe ni mdogo au kwa sababu sikupendi, nikalipiga teke, basi litanivunja dole japo ningekuwa nani. Ukweli haupendi kupuuzwa.
Wakati mwingine, mtu tunayempinga huwa ana makosa kweli lakini hoja tunazozitoa ni za kinafsi na hazihusiani kabisa na hoja zake. Nikisema mbili na tatu ni sita, nakosa. Lakini ni bora kunionyesha kwamba pengine nafikiri tunazidisha kumbe tunajumlisha. Ni kweli mbili mara tatu ni sita; lakini mbili na tatu ni tano, siyo sit.a Lakini ukijaribu kuwashawishi wenzetu wakatae mawazo yangu na kukubali yako kwa kusema kuwa meno yangu ni machafu, au natoa kamasi daima, utakuwa unatumia hoja ambazo hazina maana. Huu ni mfano wa upuuzi; lakini mara nyingi hoja tunazotumia kuwashawishi watu wakatae mawazo ya wale tusiowapenda, au kukubali mawazo yetu, huwa hazihusiani kabisa na mambo tunayoyajadili.
Makosa yetu mengine hutokana na woga; woga unaotuzuia kumlaumu mkubwa japo tunajua kuwa kakosa, au unaotuzuia kumtetea mdogo anayelaumiwa na wakubwa japo tunajua hana makosa. Na msingi wa woga ni unafsi. Pengine huwa tunaogopa sisi wenyewe kulaumiwa au kupata hasara fulani. Pengine twaweza kuwa hatuna cheo chochote ambacho tunaogopa kupoteza; pengine huwa hatuna tamaa yoyote ya kupata cheo fulani. Lakini woga unaweza kutokana na tamaa ya kila binadamu kupendwa na binadamu wenzake. Sisi sote tunayo tama hii, au sivyo tusingekuwa binadamu. Woga huu huweza kumfanya mtu kuvumilia maovu, hasa kama maovu yale yanatendwa na walio wengi kwa walio wachache, au yanatendwa na wakubwa kwa wadogo. Kwa kuogopa kuwaudhi wengi tunawaacha watende makosa bila kuwasahihisha, wasije wakatuchukia. Huu ni unafsi mbaya sana Ni kweli kwamba demokrasi haiwezi kudumu ikiwa wachache watakubali matakwa ya wengi. Lakini matakwa ya wengi hujulikana katika majadiliano au mazungumzo wa wazi.
Kadhalika, matakwa ya wachache hujulikana katika majadiliano na mazungumzo. Bila wachache kusema wazi wazi matakwa yao, majadiliano hayana maana. Wakati mwingine, hata baada ya majadiliano, wachache japo wamekubali kutii uamuzi wa wengi wanaweza kuendelea kuamini kwamba mawazo yao ni sawa, na ya walio wengi yamepotoka. Demokrasi inawapa haki, na ukweli unawapa wajibu wa kuendeleza mawazo yao mpaka wengi waone kuwa ni ya kweli. Bila hivyo Maendeleo katika mawazo hayawezekani, kwani mara nyingi wazo zuri hutokana na mtu mmoja tu. Mwanzo laweza likapingwa, pengine kwa nguvu kabisa, na walio wengi, lakini hatimaye wengi hulikubali. Huu ndio msingi wa Maendeleo katika mawazo ya binadamu.
Makosa ni makosa na dhuluma ni dhuluma, japo watendao makosa hayo au dhuluma ile ni wakubwa au ni wengi. Chama kinachopenda ukweli na haki hakina budi kiwape wanachama wake uhuru na nafasi ya kusahihisha makosa na kuondoa dhuluma. Wanachama hawana budi waone kuwa ni wajibu wao kuutumia uhuru huo, na nafasi hiyo. Wanachama wasiotumia uhuru huo na nafasi hiyo, kwa sababu ya kuogopa kuchukiwa au kupoteza nafasi zao, wanafanya kosa kubwa la unafsi, ambalo ni adui wa haki na ukweli."]
Wanaotakiwa kujisahihisha ni wale wana CCM wote ambao wanaendeshwa na uwoga na unafsi Katika suala hili la katiba mpya.
Sent from my iPhone using JamiiForums
Last edited by a moderator:
