Duu!! Div. Four hawatasoma ualimu.

Duu!! Div. Four hawatasoma ualimu.

Majanga..
Serikali imesema kuanzia mwaka huu wanafunzi wa kidato cha nne wanaopata daraja la nne hawataruhusiwa kusomea ualimu. Watakao ruhusiwa ni wale wa daraja la kwanza hadi la tatu.
Source: ITV.

Mimi kwa upande wangu nlisoma QT, na mtihani wa form four mwaka 2013 nilipata D 2, C 1 na E 4, hiyo ni division four points 40,
Chuo gani naweza kusoma wadau msaada tafadhali.
Uamuzi huu umecheleweshwa sana. Nania anapenda mtoto wake asomeshwe na mwalimu asiye mweledi? Mimi ningeshauriwanachuo wa kufunzwa Ualimu wachaguliwe kutokana na wale waliopasi daraja la kwanza na la pili tu! Kwanza kuna shida ya ajira, wachukuliwe wale wenye uwezo wa kujiendeleza. Wewe msomaji, ungependa mtoto wako asomeshwe na mwalimu asiyekidhi viwango?
Tuache masihara. Ukitaka kupata madaktari wazuri, wahasibu, wahandisi na wengineo makini ni lazima watokane na mafunzo yaliyoendeshwa na walimu wenye akili na ujuzi wa kufundisha. Na WALIPWE VIZURI PIA, wapewe nyenzo na mazingira mazuri ya kufundishia.
Canute Temu, Masaera Kilema, Moshi Kilimanjaro. 0754282101, cwtemu@gmail.com
 
Back
Top Bottom