Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
MREJESHO KWA WADAU: DUWASA YATATUA KERO YA MAJITAKA
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) inapenda kutoa mrejesho kwa wadau na wateja wake kuwa changamoto ya iliyokuwepo ya kusambaa kwa majitaka kulikosababishwa na chemba kuziba imetatuliwa mapema mara baada ya kupokea taarifa ya kuwepo kwa changamoto hiyo kutoka kwa mdau wa Jamii Forum Septemba 30, 2024.
Tayari DUWASA imefanyia kazi kero hiyo kwa kufanya Usafi wa Mazingira na kuweka dawa ya kuua vimelea katika chemba iliyopo mbele ya Ofisi za TAKUKURU na CWT Jijini Dodoma zoezi ambalo limekamilika Jana usiku Septemba 30, 2024.
Zoezi la uzibuaji wa chemba iliyopo karibu na eneo la Soko la Machinga Complex Jijini Dodoma linaendelea Leo Oktoba Mosi kwa siku ya pili baada ya siku ya Jana kutokamilika kutokana na ukubwa wa kazi.
DUWASA tunawashukuru wadau na wateja wetu kwa utayari wao wa kutoa taarifa kwa wakati pale wanapoona kuna kero, changamoto ama uharibifu unaohusu huduma ya majisafi na usafi wa mazingira.
Kadhalika, DUWASA tunaendelea kuwakumbusha wananchi wote kuzingatia matumizi sahihi ya miundombinu ya majitaka kwa kuacha kutupa taka ngumu kwenye mifumo ya majitaka kunakosababisha kuziba kwa chemba.
Taarifa hii imetolewa na Mhandisi Bernard Rugayi, Mkurugenzi wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira -DUWASA
#Usafi wa Mazingira ni Utu