DUWASA mamlaka inayoshindwa kuhudumia mji wa Dodoma

DUWASA mamlaka inayoshindwa kuhudumia mji wa Dodoma

MANG'ONYI

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2013
Posts
403
Reaction score
342
Ni wiki ya tatu sasa maji hayapatikani maeneo mengi ya mji wa Dodoma hasa Ilazo, Nzuguni na Kisasa.

Waziri wa maji amemtumbua mkurugenzi wa DUWASA mhandisi Pallangyo mara tu baada ya kuapishwa lakini tatizo inaonekana ni zaidi ya huyo Mkurugenzi kwani shida ya upatikanaji wa maji iko pale pale.

Maji bado ni tatizo sana jijini Dodoma.
 
Wenyewe wanasema kuna tatizo la umeme kule kwenye visima vyao.
 
Hakuna namna , inaabidi tu muanze kutumia maji ya visima ili maisha yaendelee
 
Wameahidi kuchimba visima ishirini katika maeneo kadhaa yanayozunguka Jiji la Dodoma. Tusidanganyane, maeneo yaliyo karibu na Jiji maji yake si salama kwa matumizi ya binadamu. Tunahitaji suluhisho la kudumu la tatizo hili na siyo majibu mepesi mepesi ya kupoteza muda. Hatari inalinyemekea Jiji na DUWASA inaelemewa na mzigo mkubwa iliyobebeshwa. Watatumbua sana watendaji, lakini je, mbona wanaangalia walipoangukia badala ya kutizama kwanza walipojikwaa?
 
Back
Top Bottom