Wameahidi kuchimba visima ishirini katika maeneo kadhaa yanayozunguka Jiji la Dodoma. Tusidanganyane, maeneo yaliyo karibu na Jiji maji yake si salama kwa matumizi ya binadamu. Tunahitaji suluhisho la kudumu la tatizo hili na siyo majibu mepesi mepesi ya kupoteza muda. Hatari inalinyemekea Jiji na DUWASA inaelemewa na mzigo mkubwa iliyobebeshwa. Watatumbua sana watendaji, lakini je, mbona wanaangalia walipoangukia badala ya kutizama kwanza walipojikwaa?