DV-2020/DV-2021 Watanzania waliochaguliwa mfanye subira, njia nyeupe

dalalitz

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2013
Posts
3,476
Reaction score
2,087
Heri ya Mwaka Mpya Jamia.

Nichukue fursa hii kuwatia Nguvu/Mpya wa-Tanzania wenzetu (wenye Bahati zao) ambao walichaguliwa katika Michakato Miwili ya 'Kubahatisha ' yaani DV-2020 na DV-2021. Kupata Mhuri wa na Gamba la Kijani (Diversity Visa/Green Card) ya huko Marekani.

Ikumbukwe mara tu bada ya Washindi wa 2020 kuanza kupata mialiko kwa ajili ya usaili rasmi, wachache tu walifanikiwa kupata nafasi hiyo kisha zoezi likasitishwa kufuatia janga la Corona.

Lakini pia wa-Tanzania tukapata pigo la pili, Pale nchi yetu ilipoorodheshwa na kusimamishwa kushiriki, tamko la Rais anaeondoka madarakani huko Marekani.

Hali hiyo imepelekea hata wale ambao walikwisha kutuma vielelezo vyao KCC. Na wakawa bado hawajapata mialiko ya usaili (Hapa nchini) pamoja na wale ambao walishapata mialiko mkononi na kusubiria tarehe zifike. Wote kubaki katika hali ya sintofahamu hadi kufikia sasa.

Mtihani mkubwa zaidi kwa nchi ni kwa Hawa wa DV-2021, ambao wao hata hatua ya kuanza kuitwa kwa ajili ya usaili bado ingawa kwa mujibu wa taratibu walitakiwa hadi tarehe hizi baadhi yao wawe tayari wanajua. Walitakiwa wawe wanajua Tarehe zao za Usaili.-Hasa kwa wale wenye namba za chini za kuchaguliwa.

Ingawa Rais anayeondoka madarakani kaongeza tena muda wa sitisho la Uingiaji hasa kwa 'Wahamiaji' hadi mwezi March akidai ni kutokana na Ugonjwa, mwenzake anaapishwa Januari 20, naye anaweza kufanya lolote atakalojisikia.

KWANINI NASEMA NJIA NYEUPE?
1. Rais Mteule kaahidi kuwa;
Mojawapo ya mambo atakayoyashuhulikia mwanzoni kabisa akiingia maarakani, ni kero za uhamiaji.

Iwapo atakuwa Mkweli basi, mbivu na mbichi zitajulikana mapema sana bada ya Tarehe 20 Januari.

2. Tukiondoa Habari ya Ugonjwa, hoja ya Tanzania Kusimamishwa haina Mashiko makubwa hivyo Mliochaguliwa muondoe shaka (ni yule Jamaa tu na mambo yake yasiyoeleweka)

3. Kutokana na nchi kadhaa kuondolewa kabisa kwenye Program za DV (Sio kusimamishwa kama Tanzania) idadi ya anaocheza/ Wanaochaguliwa inakuwa ni ndogo.

Ushindani kuwa mdogo na bila shaka itapelekea nafasi ya kufaulu Usaili kuwa kubwa zaidi, ukitilia maanani pia wapo watu wamekata tamaa ama kutoitilia maanani tena hii program hivyo hata kama kachaguliwa mwingine hataifiuatilia zaidi.

Wapo Watu kadhaa nawajua wameshafuata taratibu zote zinazotakiwa na sasa wanasubiria Wito rasmi wa kuitwa kwaajili ya Usaili.
Muwe Wavumilivu Wadau, nyote DV-2020 na DV-2021.

KINGINE: Iwapo ulishiriki kucheza Program yoyote kati ya hizo mbili, usipuuze, rejea katika Wavuti ya Matokeo, angalia matokeo yako tena na tena.

Yupo jamaa namjua hakuitilia maanani baada ya kucheza. Miezi mitatu baada ya matokeo kutoka rasmi ndio anakuja kujua kumbe ameshinda na ndio anaenda mbio sasa.

-Jua mapema uanze mchakato mapema.

Nawasilisha.

WALE WAZEE WA KUBEZA NAKARIBISHA KEJELI ZENU .
 
Unaingiaje kwenye hiyo web site mkuu, ngoja tuende mbele maisha ya msimu tz kama mbwa, au naongea Uongo ndugu zangu.
 
KCC., Na.... Wa-Tanzania, mbio sasa. - Jua, hizi mbili, -Jua
Wewe uliyeandika hii kituko ulisoma shule ya Uyunani? Senteso na vituo haviendani kwani unaanzia herufi kubwa baada ya mkato! Na makosa mengi sana ya uandishi, najua hii ni zao la miaka kibao ya chama mzee yenye sera ya Ualimu Pasipo Elimu (UPE).
 
.....KCC., Na.... Wa-Tanzania, mbio sasa. - Jua, hizi mbili, -Jua
Wewe uliyeandika hii kituko ulisoma shule ya Uyunani? Senteso na vituo haviendani kwani unaanzia herufi kubwa baada ya mkato! Na makosa mengi sana ya uandishi, najua hii ni zao la miaka kibao ya chama mzee yenye sera ya Ualimu Pasipo Elimu (UPE).
Angalia na wewe utopolo ulioandika kweli nyani haoni wowowole
 
Alafu nyie bado mnahangaika tu, si mlishinda amkawaambia wananchi kwamba nchi yenu ya asali na maziwa, ndiyo nyie mnaenda kuharibu nchi za wenzenu kuwafundisha uwizi wa kura huko USA.
 
Wenzako huchutama penye kosa hawasutani, kwani haikusaidii kitu zaidi ya kujitangaza.
Ooh yamekua hayo ukirekebishwa na wewe povu. ungechutama kwanza na wewe, hio ndo inaitwa back to sender. Vodacom kazi ni kwako.
 
KCC., Na.... Wa-Tanzania, mbio sasa. - Jua, hizi mbili, -Jua
Wewe uliyeandika hii kituko ulisoma shule ya Uyunani? Senteso na vituo haviendani kwani unaanzia herufi kubwa baada ya mkato! Na makosa mengi sana ya uandishi, najua hii ni zao la miaka kibao ya chama mzee yenye sera ya Ualimu Pasipo Elimu (UPE).

KCC., Kosa lipo wapi hapa?
Ningeachaje kuweka Kituo ilhali KCC.-ni kifupi?
Nawezaje pia kutoweka Mkato mahala ambapo naorodhesha kitu kingine bada ya hicho Kifupi?

Usitoe watu kwenye Reli.
Hapa tunajadili DV-2020 na DV-2021.

Tafadhali tuache.

USHAURI:
Anzisha Uzi wako rasmi kuonyesha namna ulivyo Mbobezi.
Ila kabla ya kufanya hivyo rejea Utopolo wako kama nilivyokazia.
 
Tatizo sio mtawala wa marekani anayeondoka madarakani sasa, tatizo ni mtawala wa Tanzania aliyopo sasa.

Hivi ujiulizi tu, kwanini Tanzania tuzuiwe wakati nchi kadhaa jirani zetu hazijazuiwa?
Hilo ni Mtambuka😇
 
Sina mpango wa kubeba box aisee, nilikataa tangu nikiwa mtoto. Bora nikalime numbu Iziwa
Kufanya ni kutaka,
Kupanga ni kuchagua.

Sijamfunga Kamba kumburuta 'Ntu' ati.
 
KCC., Kosa lipo wapi hapa?
Ningeachaje kuweka Kituo ilhali KCC.-ni kifupi?
Nawezaje pia kutoweka Mkato mahala ambapo naorodhesha kitu kingine bada ya hicho Kifupi?

Usitoe watu kwenye Reli.
Hapa tunajadili DV-2020 na DV-2021.

Tafadhali tuache.

USHAURI:
Anzisha Uzi wako rasmi kuonyesha namna ulivyo Mbobezi.
Ila kabla ya kufanya hivyo rejea Utopolo wako kama nilivyokazia.
Kama ameshindwa kuona KCC., kosa lake wewe bado sana, angalia tofauti ya KCC., na hizi zangu KCC. na KCC, sina zaidi kwani hauelimiki.
 
Kumbe ulikuwa unanielimisha?

Ungenijibu kwanza juu ya utopolo wako niliokuuliza hapo juu ningekuelewa.

Kumbuka; Huu Uzi ni wangu,
Ukome kuniletea kejeli ndani ya himaya yangu.
Nitakupa maneno hadi utaugua Tumbo la kuhara huko uliko Paka wewe.
 
Heri ya Mwaka Mpya Jamia.

Nichukue fursa hii kuwatia Nguvu/Mpya wa-Tanzania wenzetu (wenye Bahati zao) ambao walichaguliwa katika Michakato Miwili ya 'Kubahatisha ' yaani DV-2020 na DV-2021. Kupata Mhuri wa na Gamba la Kijani (Diversity Visa/Green Card) ya huko Marekani.

Ikumbukwe mara tu bada ya Washindi wa 2020 kuanza kupata mialiko kwa ajili ya usaili rasmi, wachache tu walifanikiwa kupata nafasi hiyo kisha zoezi likasitishwa kufuatia janga la Corona.

Lakini pia wa-Tanzania tukapata pigo la pili, Pale nchi yetu ilipoorodheshwa na kusimamishwa kushiriki, tamko la Rais anaeondoka madarakani huko Marekani.

Hali hiyo imepelekea hata wale ambao walikwisha kutuma vielelezo vyao KCC. Na wakawa bado hawajapata mialiko ya usaili (Hapa nchini) pamoja na wale ambao walishapata mialiko mkononi na kusubiria tarehe zifike. Wote kubaki katika hali ya sintofahamu hadi kufikia sasa.

Mtihani mkubwa zaidi kwa nchi ni kwa Hawa wa DV-2021, ambao wao hata hatua ya kuanza kuitwa kwa ajili ya usaili bado ingawa kwa mujibu wa taratibu walitakiwa hadi tarehe hizi baadhi yao wawe tayari wanajua. Walitakiwa wawe wanajua Tarehe zao za Usaili.-Hasa kwa wale wenye namba za chini za kuchaguliwa.

Ingawa Rais anayeondoka madarakani kaongeza tena muda wa sitisho la Uingiaji hasa kwa 'Wahamiaji' hadi mwezi March akidai ni kutokana na Ugonjwa, mwenzake anaapishwa Januari 20, naye anaweza kufanya lolote atakalojisikia.

KWANINI NASEMA NJIA NYEUPE?
1. Rais Mteule kaahidi kuwa;
Mojawapo ya mambo atakayoyashuhulikia mwanzoni kabisa akiingia maarakani, ni kero za uhamiaji.

Iwapo atakuwa Mkweli basi, mbivu na mbichi zitajulikana mapema sana bada ya Tarehe 20 Januari.

2. Tukiondoa Habari ya Ugonjwa, hoja ya Tanzania Kusimamishwa haina Mashiko makubwa hivyo Mliochaguliwa muondoe shaka (ni yule Jamaa tu na mambo yake yasiyoeleweka)

3. Kutokana na nchi kadhaa kuondolewa kabisa kwenye Program za DV (Sio kusimamishwa kama Tanzania) idadi ya anaocheza/ Wanaochaguliwa inakuwa ni ndogo.

Ushindani kuwa mdogo na bila shaka itapelekea nafasi ya kufaulu Usaili kuwa kubwa zaidi, ukitilia maanani pia wapo watu wamekata tamaa ama kutoitilia maanani tena hii program hivyo hata kama kachaguliwa mwingine hataifiuatilia zaidi.

Wapo Watu kadhaa nawajua wameshafuata taratibu zote zinazotakiwa na sasa wanasubiria Wito rasmi wa kuitwa kwaajili ya Usaili.
Muwe Wavumilivu Wadau, nyote DV-2020 na DV-2021.

KINGINE: Iwapo ulishiriki kucheza Program yoyote kati ya hizo mbili, usipuuze, rejea katika Wavuti ya Matokeo, angalia matokeo yako tena na tena.

Yupo jamaa namjua hakuitilia maanani baada ya kucheza. Miezi mitatu baada ya matokeo kutoka rasmi ndio anakuja kujua kumbe ameshinda na ndio anaenda mbio sasa.

-Jua mapema uanze mchakato mapema.

Nawasilisha.

WALE WAZEE WA KUBEZA NAKARIBISHA KEJELI ZENU .
Kuna waliochaguliwa wakati mwenye nchi kaipiga marufuku Tz?
 
Tusikariri.
Mimi nasema;
Wapo na michakato inaendelea.
Huyo unaedai ana Nchi kwataarifa yako, anaweweseka tu sasahivi.
 
Back
Top Bottom