Dybbuk Box; Boksi la maajabu lililoleta mauzauza kwa kila aliyejaribu kulimiliki na kuishia kuliuza

Dybbuk Box; Boksi la maajabu lililoleta mauzauza kwa kila aliyejaribu kulimiliki na kuishia kuliuza

Military Genius

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2019
Posts
761
Reaction score
1,464
IMG_20200407_051728_385.jpg

IMG_20200407_051724_543.jpg

Umaarufu wa box hili ulianzia katika mtandao wa kuuzia na kununua bidha wa eBay ambapo Kelvin Mannis aliliweka kwa ajili ya kuliuza mtandaoni humo September 2001, yeye alilinunua kwa mwanamke mmoja wa miaka 103 aliyefariki huko Poland, hivyo mjukuu wa marehemu akamsihi Kelvin anunue.

Mjukuu huyo alimweleza Kelvin kua bibi yake siku zote hakutaka mtu afungue box hilo, Kelvin akaliweka dukani kwake US akipanga kulisafisha ili amzawadie mama yake katika siku ya kuzaliwa, siku ilifika na akampa, kufika nyumbani mama aliugua kiharusi na hakuwahi pata uwezo wa kuongea tena.

Box akampa dada yake, baada ya wiki akarudisha, akampa rafiki ake, baada ya wiki akarudisha. Baadae wote walianza kuota ndoto mbaya zinazofanana, Kelvin akawa anaona vivuli usiku na mambo mengi ya ajabu, mara box linafuka moshi NK, Kuna siku anasema alishtuka saa kumi usiku baada ya kuhisi mtu anampumulia shingoni.

Baada ya hayo yote ndipo akaamua kuliweka eBay ili aliuze kwa mtu atakaeweza kumsaidia, ndipo mwaka 2003 likanunuliwa na Losif Nietzke aliyekuwa mwanafunzi wa chuo huko Missouri US. Miezi 8 baadae akaliuza baada ya yeye na familia yake kuugua ghafla na kushindwa kulala, aliliuza kwa $ 280.

Mununuzi alikuwa ni Jason Haxon mkurugenzi katika jumba la makumbusho la Osteopathic huko Missouri US. Jason alisema kuwa kuligusa tuu akakohoa damu, akaanza kushuhudia vivuli na moshi ukifuka, licha ya kujitahidi kulitunza lakini baadae akashindwa, akaliuza kwa Zak Bagans wa Las Vegas.

Dibbuk ni jina la kiyahudi linaloelezewa kuwa ni roho mbaya ya mtu aliyekufa, roho yake haikwenda mbinguni, ilibaki kusumbua watu duniani ambapo inakiganda kitu hadi itakapoondoka yenyewe, ikaliganda box hili. Neno Dibbuk linatokana na neno la kiebrania linalomaaanisha 'kung'ang'ania.'

Box hili lipo tangu miaka ya 1800 likitajwa kusumbua kila aliyekuwa akilimiliki hadi sasa likiwa katika jumba moja la makumbusho huko Las Vegas US.

Story ya box Hili ndyo iliyotumika kutengeneza movie ya The Possession ya 2012 na series ya Deadly Possessions ya 2016 yenye stories nyingine ambazo ni Bella Lugosi Mirror na Peggy the Doll

IMG_20200407_051722_697.jpg

IMG_20200407_051726_112.jpg

@military_Genius
 
Dibbuk ni jina la kiyahudi linaloelezewa kuwa ni roho mbaya ya mtu aliyekufa, roho yake haikwenda mbinguni, ilibaki kusumbua watu duniani ambapo inakiganda kitu hadi itakapoondoka yenyewe, ikaliganda box hili. Neno Dibbuk linatokana na neno la kiebrania linalomaaanisha 'kung'ang'ania.'
Nasubiri Michango yenu

Jr[emoji769]
 
Ubarikiwe Kiongozi
 
.kuna kijna anahis hii ni chai

@military_Genius
 
Tunakolona bado unataka uchukue hill lidude utakufa kwa pressure ohoo! Ila likija huku tunachoma moto maana naona wazungu wanalizungusha tu wakati linaleta mushikeli.
.wanambwembwe sana wazungu

@military_Genius
 
Back
Top Bottom