E-Filing System TRA una matatizo

E-Filing System TRA una matatizo

Ngongo

Platinum Member
Joined
Sep 20, 2008
Posts
20,654
Reaction score
35,887
Heshima sana wanajamvi,

Mamlaka ya mapato Tanzania ilibadili mfumo wake wa ku fill kodi mbali mbali kupitia mfumo mpya ambao badala ya kurahisisha kazi umeongeza ugumu wa kazi.

Unaweza kuchukua siku nzima ukihangaika kuufungua tu .Bado utasumbuka masaa mengi kurudia rudia kila mara na usifanikiwe.

Wakati mwingine inakubidi kudamka usiku wa manane kufungua lakini wapi .

Najiuliza TRA wameweka mfumo huu ili kutukomoa wafanyabiashara tushindwe kulipa kodi kwa wakati mtubandike mapenalty kwa kuchelewa kulipa kodi au kuna siri gani.

Haiwezekani dunia ya sasa badala ya kurahisisha mambo yaende haraka mnafanya kinyume chake.

TRA mnasubiri Kinana alalamike ndio mchukue hatua kama Police na suala la Trafic au mnataka nini.Mfumo wenu mbovu si rafiki unatumia muda mrefu sana na wakati mwingine siku mbili hadi nne ku fill kodi aina moja tu.Tunaka kulipa VAT kwa wakati shida,tukitaka kulipa SDL shida,tukitaka kulipa PAYE shida hivi mnataka nini ???.

Ngongo kwasasa nahangaika na eFilling nashindwa kulipa PAYE.
 
Ukienda TRA wanakwambia wanafanyia kazi soon mambo yatakuwa safi,huu ni mwezi wa tano tukipewa kauli za kutufariji.

Kwa ujumla huo mfumo uko hivyo ili kupiga watu penalti, kwani penalti ni sehemu ya mapato ya serikali. Haiwezekani kuna server ziko fast kama za Google, kisha mtu ahost mfumo wa serekali kwenye server zenye uwezo duni.
 
Hili la TRA kwakweli ni jambo la aibu sana kwa taifa na linaendelea kuvumiliwa tu kwa mateso ya walipakodi miezi na miezi.

Kwanini mfumo kama huu wasitoe tenda kwa wenye uwezo kuboresha kuliko kung'ang'ana wenyewe ilihali inaonekana kushindikana mpaka sasa??

Taasisi ya usimamizi wa kodi haipaswi kuwa kikwazo cha ulipaji wa kodi....
 
muhusika awajibikeee, halafu kati ya tar 10 - 20 ya mwezi ndo kabsaa mfumo unasinziaa
 
Nina penalty ya late filling May 2022..sitoilipa hio 450k..si kwa shida nlizopitia...wacha ntersest iaccumulate tu.. mtandao wao uko light..users sio wengi najua hawafiki hata 40m lakini kwanini iwe nzito..
 
Heshima sana wanajamvi,

Mamlaka ya mapato Tanzania ilibadili mfumo wake wa ku fill kodi mbali mbali kupitia mfumo mpya ambao badala ya kurahisisha kazi umeongeza ugumu wa kazi.

Unaweza kuchukua siku nzima ukihangaika kuufungua tu .Bado utasumbuka masaa mengi kurudia rudia kila mara na usifanikiwe.

Wakati mwingine inakubidi kudamka usiku wa manane kufungua lakini wapi .

Najiuliza TRA wameweka mfumo huu ili kutukomoa wafanyabiashara tushindwe kulipa kodi kwa wakati mtubandike mapenalty kwa kuchelewa kulipa kodi au kuna siri gani.

Haiwezekani dunia ya sasa badala ya kurahisisha mambo yaende haraka mnafanya kinyume chake.

TRA mnasubiri Kinana alalamike ndio mchukue hatua kama Police na suala la Trafic au mnataka nini.Mfumo wenu mbovu si rafiki unatumia muda mrefu sana na wakati mwingine siku mbili hadi nne ku fill kodi aina moja tu.Tunaka kulipa VAT kwa wakati shida,tukitaka kulipa SDL shida,tukitaka kulipa PAYE shida hivi mnataka nini ???.

Ngongo kwasasa nahangaika na eFilling nashindwa kulipa PAYE.
Wamejiwekea penalt yao ya kuchelewasha kodi ya 225000.
 
mkuu jitahidi ku-file kodi zako mapema, ukichelewa ukaanza kufile karibu na tarehe 20 mfumo hua unazidiwa kwasababu ya wingi wa watumiaji,

mimi nilikuaga muhanga pia.
 
Shida tunakimbilia teknolojia mpya lakini bado tupo gizani.
 
Shida tunakimbilia teknolojia mpya lakini bado tupo gizani.
Hahahaaaa pole inawezekana hata na wao kuna kitu kimewakwamisha sidhani kama wanafurahia kukosa pesa pesa umate mate wa kodi maana siwatashindwa fikia malengo yao.
 
Inawezekana ingawaje hawasemi, mifumo ya TRA ipo hacked and they are unable to solve the problems with their systems
 
mkuu jitahidi ku-file kodi zako mapema, ukichelewa ukaanza kufile karibu na tarehe 20 mfumo hua unazidiwa kwasababu ya wingi wa watumiaji,

mimi nilikuaga muhanga pia.
Hata siku 10 kabla, haisaidii. MM hadi nimechoka, ststem gani ambayo kila utakachogusa inakutaka ulog in tena na tena na tena yaani urojo mtupu
 
Kamishana. Efilling sio. Mtandao wake ovyo. Una log in unakata
Siku nzima. Unakata. Ndioaana unaongeza siku za efilling. Tatozo ni kiwategemea wataalamu bei rahisi.
Usidhani ujanja wa tancis ndio wa tesws. Noo.
 
Back
Top Bottom