E fm yazidi kuwafunika Clouds fm

E fm yazidi kuwafunika Clouds fm

Ratiba ya monday to friday hii
Joto la asubuhi saa 12 asubuhi hadi saa 3 asubuhi ( gerad hando, p.j na adeliya)

Sports headquaters saa 3 asubuhi hadi 6 mchana(kitenge, oscar, sudy, maestro, musa, omary, tunu)

Uhondo saa 6 mchana hadi saa tisa mchana( dina, swebe, bi hindu)

Ladha 3600 saa tisa hadi saa 10 jioni (jabir saleh)

Ubaoni saa 10 jioni hadi saa moja ucku (emma, mpoki, bikra wa kisukuma)

E Sports saa moja ucku hadi saa mbili ucku (omary katanga, ibrahimu masoud "maestro", maulid kitenge, tunu hassan, musa n soudy)

Genge saa mbili hadi 5 (kicheko) hapa ndo zinapigwa sana visingeli

Weekend uwa sikilizagi sana radio ila kuna vipindi km old skullz jam, muda wetu, afro bet
E.Sports saa moja ucku hadi saa mbili jumamoc n jumapili ipo pia
Mkuu umewasahau wale jamaa wanaotangaza Raggae wale , wanagonga kijamaika hatari nawapenda sana wale jamaa sijui ndoo hawa walikuwa times fm mwanzo?
 
Mkuu kidogo wewe umechangia bila kuonyesha mihemko yako binafsi...napenda sana jinsi ulivyochambua hivyo vipindi pamoja na wahusika wake,niko mkoani sijawahi kuisikiliza hii radio E-FM ila majina ya vipindi tu jinsi yalivyo umenishawishi namimi niwasikilize nione kama yaliyomo yamo kweli au laah....ebu tusaidie na mida ya vipindi vyao bhasi ili niwasikilize kwenye tunein app
Kama una dish la Azamu jamaa wa E fm wanapatikana vizuri kabisa!!!
 
Nakubaliana na hoja me n msikilizaji wa radio zote e.fm wanafanya vizuri hata ukilinganisha vipindi clouds washapigwa gap
Power breafast vs Joto la asubuhi > p.b cku izi ina imeopooza ngoja j'3 tutaona joto la asubuhi itakuaje

Leo tena vs Uhondo > leo tena ya sasa sio km ya zaman yule da huu, mus na jose mara hamna wanchofanya zaidi ya kuongea umbeya, n uteam uhondo hata mpangilio vitu unavyosiki vimepangiga dina n swebe wanafanya vizuri

Jahazi vs Ubaoni > jahazi kimebaki kipindi cha matangazo na kupeana salama mda mrefu n bora hata usikilize ubaoni utojuta n utafurahi

Sports xtra/roundup vs Sports headquaters hapa clouds ndo wameachwa mbali wakina shafii wamebaki kutoa habari za goal.com kwny uchambuzi yule alex na wakina issa maeda hamna kitu, mbwiga anapiga kelele tu na ukija e.fm unasikiliza michezo n uchambuzi hadi unafurahi uku oscar ocar, ibrahim masoud "maestro", tunu hassan, kitenge maulid, suddy mkumbo, musa mwakisu. Yusuphmkule uwezi kuona gap hata mmoja asipokuwepo

Clouds wamebakiwa n xxl na amplifier tu ndo vipindi wanaweza kujivuniA
Mkuu kula like zangu nyingi.

Yani sport extra sasa hivi imepoteza diraa kabisaa. Wanasubiri mnoo kwa sport headquarter

Nimebaki nasikiliza amplifaya but nayenyewe naona kama imekosa ubunifu mpya.

Huku kwenye jahazi pamoja na gadna kaja but nothing new...

Asubuh kwa kina bonge ,fredwaa sijui na nan yulee naona pia chenga tuuuu
 
xxl yenyewe mbovu siku hizi, utakuta wana interview msanii huku wanajadili vitu vya kijinga wakati huo mda unaenda. Mda umeisha hawajamuoji kitu cha maana, achilia mbali hayo matangazo sasa.
Mkuu unasikilizaga xxl????
Twende E fm
 
Katika hali ya kustaajabisha ni kwamba redio mpya tena ina miaka miwili tu tangu ianzishwe na inakamata mkoa mmoja tu(DSM),inazidi kubamba na kupaa kila kukicha kiasi kwamba imezifunika redio kongwe zote,hadi Clouds fm ambayo ndio redio inayosumbua kwa hapa Tz inafunikwa na redio ndogo tu (E fm),kama unabisha basi wewe una lako ila kwa hapa DSM habari niE fm tu kila kona.na ndio maana clouds wameamua kuibadilisha ile redio yao ya Choice fm(102.5).wameamua kuiharibu hiyo redio na kuifanya iwe kama E fm ila haiwezekani,kwa wanaoijua choice fm ilivokuwa mwanzo na sasa watanielewa ninachomaanisha.soon tutaisikia clouds nao wanaanzisha vipindi vya miziki ya minanda na miduara,tusubiri kuona clouds ikiendelea kuongeza watangazaji kila siku
marekebisho, efm inasikika duniani pote, kupitia on line, unaweza ku download apply ya radio kwenye pray store utaipata, m nko huku mbali naiskia,

zipo radio nyingi sana, isipokuwa rfa, nahisi hawajajipanga bado,
 
Shika Adabu yako! Heshimu Makabila ya Wenzio. Sio kila la Hovyo ni la wanyamwezi.
Mkuu unajua maana ya neno alilotumia? umekurupuka (amesema hyo radio ilikuwa ya kinyamwezi sana) kwa maana nyingine ya kimjini mjini alimaanisha (hiyo choice fm radio ilikuwa ya waskilizaji wa kishua)
 
na hapa hawajaanza kutoka nje ya dar,,wakianza toka nje ya dar clouds bye bye
 
Efm huu mchezo hauitaji hasira... Jamaa wanatisha.

Tatizo clouds matangazo tupu tumeshawachoka. Amekuja Gadna na Kipanya ila hakijabadirika chochote.

Efm ndio habari ya mjin.

Namsikizaga ma nigga kibonge toz kwenye ladha 3000
 
Mkuu kidogo wewe umechangia bila kuonyesha mihemko yako binafsi...napenda sana jinsi ulivyochambua hivyo vipindi pamoja na wahusika wake,niko mkoani sijawahi kuisikiliza hii radio E-FM ila majina ya vipindi tu jinsi yalivyo umenishawishi namimi niwasikilize nione kama yaliyomo yamo kweli au laah....ebu tusaidie na mida ya vipindi vyao bhasi ili niwasikilize kwenye tunein app
Kama una king'amuzi cha Azam unaweza kusikiliza fresh sana....
 
Mkuu umewasahau wale jamaa wanaotangaza Raggae wale , wanagonga kijamaika hatari nawapenda sana wale jamaa sijui ndoo hawa walikuwa times fm mwanzo?
Hahaha hawa jamaa wana swaga hatari nilisikiliza siku moja nilicheka sana wanavutia kuendelea kusikiliza kipindi.
 
Back
Top Bottom