E.P.L inazidi kuabika

el nino

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2013
Posts
4,712
Reaction score
5,058
Nadhani sote ni mashahidi wa kelele zilizopigwa humu baada ya England kuingiza timu zake 5 kwenye hatua ya mtoano.

kelele mzilipigwa kwelikweli, kuwa England imerudi tena, mara spain hamna kitu, sisi tunaojua ligi bora na ligi ya matangazo tukakaa kimya kusubiri kisu kiwakate England, mara paaap timu 3 zimefyekwa wamebakiza timu 2, tena kati ya hizo 2 yenye kuleta matumaini ni 1 tuu na yenyewe sio nyingine bali ni Man city inayonolewa na mtaalam aliyesukwa na kupikika kutoka spain.

Sijaona wa kuizuia Barcelona au madrid, labda tuu wakikutana wenyewe huko watoane, ila kwa hali ya kawaida hawazuiliki labda kidogo upinzani unaweza kutolewa na bayern munich ama sivyo la liga watachukua uefa kwa mara ya 5 mfululizo na kuwaacha E.P.L na kina Lukaku wao wakiendelea kuota mafanikio haya maana hata kipindi E.P.L ilipokuwa ikitamba haikuwahi kubadilishana UEFA hata mara moja(yaani kwa miaka miwili au zaidi uefa iende England mfululizo)

nawaaga kwa picha ya msiyempenda

 
Madrid alipigwa vizuri tu na spurs..ubora cjui ulienda wapi!
 
Ligi kuu ya Uingereza ni ligi ngumu kabisa duniani chakushangaza haina ubora. Hakuna ligi ngumu duniani kama ya Uingereza ikifuatiwa na vpl.

Ugumu wake umeifanya vyombo vya habari vimeipaisha ndio maana kila mpenda soka anaifahamu lakini hakuna cha maana pale. Waingereza bhana we acha tu wanapenda vya kwao balaa.
 
Tena hizo 3 zimetoka kwenye hatua ya mtoano, na zimetolewa kupitia timu za nje ya EPL.
 
yaan timu za EPL wa zile za laliga ni km uji kwa mgonjwa.....ule msako waliofnyiwa united na sevilla kule spain ulikua balaa kuja nyumban wakashndwa kuvumilia.....hawa waliokuwa wanajinadi kutofungwa na messi duh jana ni matobwa tu,
 
Kwa hatua inayofuata Barcelona na Real Madrid wanaweza kuondolewa kwenye mashindano Aidha Bayern au Juventus kwa kipindi cha takribani misimu miwili waliondoshwa na hizo timu kama Juventus ilishawaondoa wote hao wawili Real Madrid msimu wa 2015/16 na Barcelona 2016/17
 
Umetumia kigezo gani kusema man city ndio yenye matumaini?,maana kwenye takwimu Liverpool uefa ndio bora kuliko man city .halafu swala la kuingiza timu timu nyingi hatua hiyo si hoja,subiri timu za spain wachukue kombe ndio upige kelele,nimekuzarau na nimekuona ujui mpira eti labda upinzani kidogo unaweza kutoka kwa bayen,umesahau huyo coacher wa bayen ndio ndio aliwafunga barcelona jumla ya goli 7-1 home/away Baada ya hapo alienda kuchukua kombe la uefa,Baada ya hapo tena akaachakufundisha soka 2013//2014,sasa katikati ya msimu huu bayen wamemuomba aruditena kuifundisha timu kwa muda mpaka pale watakapo pata kocha ,baada ya kuchukua timu huyo kocha hivyo vipigo alivyovitoa ni vya ujazo.
 
Mkuu, misimu inabadilika. Juve huyo huyo si kapigwa 3 na Barca Camp Nou msimu huu?
 
we unayeujua mpira tuambie tokea 2015 UEFA huwa inachukuliwa na timu gani?

tokea 2015 Ueropa imechukuliwa na la liga mara ngapi?

ukishapata jibu utaniambia hizo bayern munich na timu za England huwa zinakuwa wapi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…