EAC Tanzania kinara kuvutia Wa-USA

Kazi nzuri
 
Mabeberu ni wale waliokuwa wanasaini mamikataba ya kinyonyaji, kiwizi, kifisadi enzi za Jakaya Mrisho Kikwete. Wawekezaji wakija kwenye win win situation tutaheshimiana.
 
Mkuu kuna jambo haliko sawa,Hizo investment nadhani ni mpya mpya.
Kenya ina investments nyingi hasa kutokea Marekani kuliko Tanzania na Uganda kwa kipindi kirefu sana.
Tuseme Kenya its saturated zone with American investment, hivyo wametafuta new territory.
Na hizo American investments katika Tanzania ni zipi?
 
Kenya haina madini kama Tanzania, Wamarekani wanataka madini.Kenya pia haina vivutio vingi vya utalii kama Tanzania.
Hakuna cha ajabu hapo kama ambavyo si ajabu mwenye nywele kichwa kizima kutumia muda mrefu kunyoa kuliko mwenye upara kwenye utosi.
 
Mkuu hii habari yako unaitoa wapi, Let's share
 
Mabeberu ni wale waliokuwa wanasaini mamikataba ya kinyonyaji, kiwizi, kifisadi enzi za Jakaya Mrisho Kikwete. Wawekezaji wakija kwenye win win situation tutaheshimiana.
Unaoushahidi mjomba? Kwanini umrukie JK?
 
... Mkuu AGGGOT TZ, tafadhali rephrase heading ya thread na content ya Kiswahili. At glance it is as if it is a comparison of what the US, Kenya, Uganda, Rwanda, and Burundi have invested in Tanzania in 2019 of which the US leads as the biggest investor!

Kumbe badala yake ni ulinganisho wa ambacho US imewekeza Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, na Burundi of which Tanzania leads as the biggest recipient in the same year! Kwa thread hii sasa napata picha ni kwanini ukitokea mkanganyiko wa kisheria hususan tafasiri, the English version overrides!
 
Imewekeza katika miradi gani?
 
Tukisema Rais Samia anakasi nzuri mjaribu kituelewa tu

Sasa huu ushirikiano ndio fungakazi,

Tuendelee kuiombea nchi yetu
2019 Samia alikua Rais? Watu wa Lumumba mjaribu kupunguza mihemko. Andiko linasema kufikia 2019 uwekezaji wa Marekani ulifikia USD 1.5 Billion. Wewe unakuja na porojo za kasi ya Samia.

Nchi ina watu wa hovyo sana hii!
 
Nimekubali mziki
 

Mkuu AGGGOT TZ , kwanza asante kuleta mada hii, na huu ndio uzuri wa jf, kila mtu yuko free kuleta mawazo yake na yataheshimiwa, hivyo hata mimi hapa naheshimu mawazo yako ila pia nakuelimisha maana kuna vitu inawezekana huvijui kuhusu ubeberu na kudhani ukisaidiwa tuu ndio ukubali kufanyiwa kila kitu.

  1. Beberu ni nani na ubeberu ni nini na kwanini nchi iitwe beberu?. Beberu ni mbuzi dume, huwa anazungukwa na majike wengi, huyo beberu anapotaka, haombi bali anajichukulia tuu kitemi, kibabe. Hivyo ubeberu ni tabia ya nchi moja kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine kibabe, kitemi kwa kuilazimisha hiyo nchi kufanya anachotaka beberu vinginevyo beberu atamfanya kwa nguvu.
  2. Kwa lugha ya Kiingerere ubeberu ni imperialisms na ndio the highest stages of capitalism, mabeberu ni imperial powers na nchi ya Marekani ndio kubwa la mabeberu!. Ubeberu huu uko wa aina tatu, political imperialism, economical imperialism na social imperialism.
  3. Kwa vile ubeberu ni tabia chafu na mbaya, mfano wewe ni masikini wa kutupa unaeishi kwenye lindi la umasikini, akatokea tajiri kukusaidia kukupa chakula masherti ya msaada wake kwako ni pamoja na kukusaidia kum service hadi mkeo, jee utakubali tuu kwasababu ni masikini?.
  4. Au kwa vile una njaa sana, usipopata chakula utakufa njaa, anatokea tajiri anakutupia chakula kama mbwa, anakutupia kitumbua kwenye mchanga wewe unakiokota, unakifuta mchanga na kukila, utamsifia aliyekutupia chakula au utatunza heshima yako na utu wako na ikibidi kulala njaa utalala njaa kuliko kudhalilishwa!. Japo ni masikini lakini unakuwa ni masikini jeuri.
  5. Kubwa la mabeberu aliyataka mafuta ya Iraq, akalobby lobby kwa Saadam akashindwa, akamsingizia Iraq ina WMD, yeye na washarika wake wakamtandika Saadam na sasa mafuta ni kama yao. Je what the Americans did in Iraq, is it right?. Is it justified?. Huu ndio ubeberu!.
  6. Baada ya kumuona Gadafi analiughanisha bara la Africa ndilo Bara linaloongoza kwa rasilimali duniani ila pia ndilo bara linaloongoza kwa umasikini. Akaamua Africa tuungane tuunde Bank of Africa, tuachane na WB. Tuunde Africa Monetary Fund tuachane na IMF.
  7. Mawasiliano yote Africa lazima yapite kwa mabeberu kwanza. Kupiga simu Rwanda, simu hiyo lazima kwanza ipite London, Paris, ndipo ije Kigali. Gadafi hajasema huu ni upuuzi, akapandisha Satellite angani Africa tuachane na ITU. unajua kilichotokea?.
  8. Ni kweli Marekani na mabeberu wengine ni rafiki zetu, ni nchi rafiki, nchi Wafadhili, development partners, na wakitusaidia tunawashukuru sana.
  9. Lakini pia ndio hawa hawa wanaotuingilia mambo yetu ya ndani, kwa kutupa misaada yenye masherti. JPM alikataa Jee anajua kwa hakika what happened to him?.
  10. Naamini nimekuelimisha vya kutosha kuhusu mabeberu na ubeberu na kukuomba sana usiwe kibaraka wa mabeberu, kuwa mzalendo kwa nchi yako. Nakuachia na links ya kukuelimisha zaidi.
Mimi ni Mwalimu Paskali

Rejea





 
Pia hizi ni kampuni za Marekani ziliwekeza:
1) Richmond Development Company LLC of Houston
2) Symbion
3)….

 
Hata richmond waliwekeza 400m USD 🤣 🤣 , Barrick gold waliwekeza 2 billion 🤣 🤣...nafikiri umepata jibu lako
 
America hakuna pesa ya bure au rahisi, walioishi US wanaelewa vizuri, baba mkopo wa 5000$ ukicheza utalipa 100,000$, utapewa student loan, credit card wanamalizia na mortgage ukija kushtuka uko kona mbaya kuliko mtumwa na hakuna pa kutokea tena, acha waitwe mabeberu tuu tulioishi US tunaelewa hii game
 
Umetafsiri vizuri sana neno "Ubeberu "

Unadhani kwa mifumo ya dunia ya sasa neno hili linastahili kupewa wengine?

Huwezi kutukana mamba ukianza kuvuka mto mjomba,
Ndio maana nikasema ujue kuishi nao kwa faida...lakini ukweli waliyotutawala na marekani daima ni mabeberu.
 
Verse versa is True
No free lunch
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…