EACOP: Kwanini wasingetanua reli ya kati mpaka Uganda badala ya kuchimba bomba la Mafuta (Hoima - Tanga)??

Luis 505

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2025
Posts
676
Reaction score
948
Eti wakuu, kwani si bora wangeirefusha reli ya kati kutoka Kigoma (au pahala pengine pa karibu zaidi) mpaka Uganda kuliko kuchimba bomba la gharama kubwa kiasi kile.

Mafuta yakiisha Uganda hilo bomba litakuwa na kazi gani nyingine?? Mafuta yakiisha reli still inaweza kusafirisha watu na bidhaa mbalimbali kutoka Bandari ya Dar mpaka Uganda.

Ninaomba kuelimishwa wakuu Kichuguu Missile of the Nation
 
NB: Sio mtaalam sana wa Geography ya reli ya kati
 
mafuta yakiisha bomba litasafirisha maji toka ziwa viktoria na tanga kwa mikoa yote watu wafanye kilimo cha umwagiliaji maisha yaendelee
 
Kama gharama ya kusafirisha kwa reli ni kubwa sana kulinganisha na gharama ya kusafirisha kwa bomba, inawezekana gharama ya bomba ikalipiwa vizuri zaidi na mafuta kuliko gharama za reli.
 
Mafuta yanaingiza hela kuliko kusafirisha hizo bidhaa mkuu

Hela inayoingia kama ni uongozi mzuri unajenga hiyo reli unayoitaka
 
Ukiona hivyo ujie hesabu zimeishapigwa, mpaka mafuta yaishe ni leo, huoni waarabu tangu wameanza kuchimba wese ni miaka mingapi??
Vyote vya muhimu tu - bomba lijengwe, reli pia muhimu...
 
Hayo mafuta kusafirisha kwa bomba ni gharama nafuu kuliko kuyabeba na treni.
 

Kwani pesa anatoa nani ndugu yangu? Pesa sio ya Tanzania wanafanya kwa manufaa yao sio Tanzania. bomba la mafuta ni gharama nafuu kwenye uendeshaji kuliko treni
 
Kama gharama ya kusafirisha kwa reli ni kubwa sana kulinganisha na gharama ya kusafirisha kwa bomba, inawezekana gharama ya bomba ikalipiwa vizuri zaidi na mafuta kuliko gharama za reli.
But the world is now shifting to renewables and oil may soon to declared obsolete.
 
Ukiona hivyo ujie hesabu zimeishapigwa, mpaka mafuta yaishe ni leo, huoni waarabu tangu wameanza kuchimba wese ni miaka mingapi??
Vyote vya muhimu tu - bomba lijengwe, reli pia muhimu...
Waarabu walianza kufaidika na Mafuta kabla ya EVs, solar energy and other renewables hazijashika hatamu.

Mafuta soon yatakuwa replaced na renewables.
 
Ukiona hivyo ujie hesabu zimeishapigwa,
Hesabu zimepigwa wapi mkuu?? Afrika?? Dark continent?? Corruption riddled continent?? Hahahaaaa bila shaka unachekesha mkuu
 
But the world is now shifting to renewables and oil may soon to declared obsolete.
Tutatumia fossil fuels for quite some time. The shift to renewables is not that easy and will take some time.

Mfano, magari ya umeme yanasumbukiwa sana na range. Hayana range kubwa. Halafu kutumia umeme kwenye magari makubwa ni changamoto.

Uganda wamepiga hesabu wakaona wapige kuuza nafuta ya mwishomwisho wakichelewa yatawadodea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…