EACOP: Kwanini wasingetanua reli ya kati mpaka Uganda badala ya kuchimba bomba la Mafuta (Hoima - Tanga)??

Mafuta yanaingiza hela kuliko kusafirisha hizo bidhaa mkuu

Hela inayoingia kama ni uongozi mzuri unajenga hiyo reli unayoitaka
Mkuu, kumbuka pia investments zoote atakazofanya Total Energies atakata katika katika mapato ya Mafuta kabla ya Uganda kuanza kuvuna faida, hivyo sio mapema kama ambavyo unaweza kufikiria.
 
Yeah,gravitational force
Sio kweli ndugu nipo kwenye huu mradi kuna pump station 6 uganda 2 bongo 4 pia kuna pressure reduction station 2 ziko Bongo kupunguza pressure mafuta ya kikaribia Tanga terminal.
Kuhusu kuchagua Bomba ni njia ambayo ni nafuu sana halafu kwa nature ya mafuta ya Uganda yameganda lazima yapashwe joto nyuzi joto zaidi ya 55 ili yawe kimiminika yatembee kwa hiyo ni rahisi kuweka cable za upashaji joto along the pipeline kuliko hizo njia nyingine.
Mapipa 216,000 kwa siku kuyasafirisha kwa treni sio mchezo.
Road and railway ndio njia zenye gharama sana kwenye usafirishaki wa mafuta vessel na pipeline ndio njia zenye bei nafuu
 
Okay
 
Ni long term investment; bomba lina gharama nafuu kuliko kusafirisha kwa treni. Ingekuwa nio kwa matumiz ya muda mfupi tu, kama miaka mitano hivi, huenda isingekuwa na faida lakini kwa operation ya miaka 20 na zaidi ni bomba ni nafuu sana kuliko treni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…