EACSOF yashauri kuwe na hatua za kikanda za kukabiliana na COVID19 ikiwemo kuwa na chanjo itakayotengenezwa chini ya Africa-CDC

EACSOF yashauri kuwe na hatua za kikanda za kukabiliana na COVID19 ikiwemo kuwa na chanjo itakayotengenezwa chini ya Africa-CDC

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
EACSOF ilikaa Februari 26 kujadili muelekeo wa COVID19 na kushauri njia za pamoja za kukabilina na janga hilo

Haya ni Mapendekezo ya EACSOF kwa Marais wa Jumuiya ya Afrika Mashariki siku moja kabla ya Marais hao kukutana

1. Wameshauri kuwa na hatua za kikanda dhidi ya gonjwa hili, hasa kuwa na chanjo iliyotengenezwa na watu wa afrika mashariki kupitia Africa CDC na African Medicine Agency(AMA)

2. Kuhakikisha kuwa kunakuwa na juhudi za pamoja za kuwahamasisha watu juu ya chanjo ili kuondoa utata ambao unaweza kufanya baadhi ya wananchi wa Jumuiya kutopata chanjo

3. Secretariat ya EAC kushirikiana na asasi za kiraia ili kuhuisha mjadala juu ya masuala yanayowaathiri wananchi

4. Kuheshimu uhuru ikiwemo uhuru wa kujieleza na haki ya kupata taarifa

5. Kuwa na uwazi katika fedha zinazopokelewa kama msaada wa kupambana na COVID19

6. Kuwa na sera ya Jinsia ili kuthibiti ukatili wa kijinsia

7. Kukubaliana katika njia za kusambaza chanjo ya COVID19 ili kuzuia kusambaa kwa COVID19 ndani ya nchi za jumuiya. Na kuhakikisha usawa wa upatikanaji wa chanjo kwa watu wa kijijini na mijini

8. Kuyapa kipaumbele magonjwa mengine nkatika kipindi hiki cha COVID19 na kuyatafutia chanjo

9. Nchi zichukue hatua za pamoja kuthibiti madhara ya kiuchumi yaliyoletwa na covid19

1614370096785.png
1614370128497.png
1614370159018.png
 
You can never attain anything on earth except to agree to disagree
 
Back
Top Bottom