EALA wapitisha muswada wa Kamisheni Huduma za Fedha

EALA wapitisha muswada wa Kamisheni Huduma za Fedha

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
BUNGE la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA), limepitisha muswada wa Kamisheni ya Huduma za Fedha ya Afrika Mashariki (EAC).

Muswada huo wa mwaka 2022 unalenga kuanzishwa kwa kamisheni kama taasisi huru yenye majukumu, mamlaka, vyanzo vya fedha na makao yake makuu.

Kupitishwa kwa muswada huo muhimu jana ni kuelekea utekelezaji wa Itifaki ya kuanzishwa kwa Umoja wa Fedha Afrika Mashariki.

Akiwasilisha maoni ya kamati hiyo katika kikao cha nne cha Bunge kinachoendelea jijini Arusha, Mjumbe wa kamati ya Bunge ya Bajeti, Denis Namala, alisema muswada huo umechelewa kwa zaidi ya miaka minne licha ya umuhimu wake tangu kukubaliwa kwa itifaki ya Umoja wa Fedha.
 
Kupitasha ni kitu kimoja na kutekeleza ya lio pitishwa jambo jingine. EAC umejaa na unafiki na kutoaminiana kabisa.
 
Back
Top Bottom