EALS, PALU, SADC-LA, IBAHRI na Lawyers for Lawyers waitaka Serikali kuacha kumkandamiza Rais wa TLS

EALS, PALU, SADC-LA, IBAHRI na Lawyers for Lawyers waitaka Serikali kuacha kumkandamiza Rais wa TLS

Manyanza

Platinum Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
22,269
Reaction score
58,563
Mtandao mzito wa taasisi na vyama vya kitaaluma vya sheria barani Afrika na duniani vikiwemo EALS, PALU, SADC-LA, IBAHRI na Lawyers for Lawyers ,vimeungana kutoa tamko zito la kuitaka Serikali ya Tanzania kuacha kuingilia na kutumia vyombo vya nidhamu kumkandamiza Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Mwabukusi.

Taasisi hizo zimeeleza wasiwasi mkubwa juu ya mwenendo wa kinidhamu unaoendeshwa na Kamati ya Taifa ya Mawakili (NAC) unaolenga kumfuta kabisa Mwabukusi kwenye Orodha ya Mawakili. Shauri hilo (Maombi Na. 04 ya mwaka 2026) linatokana na kauli halali alizozitoa Mwabukusi Mei 2026 kuitaka Serikali imwachie aliyekuwa Rais wa TLS na kiongozi wa CHADEMA, Tundu Lissu, aliyekuwa akikabiliwa na mashtaka ya uhaini.

Katika tamko hilo la pamoja, vyama hivyo vya kimataifa vimebainisha kuwa adhabu inayotafutwa ya kumfuta kabisa uanakijiji huyo wa sheria ni kali kupita kiasi na inalenga kuweka hofu kwa mawakili wote wanaojitokeza kutetea haki za binadamu. Vimeibua pia wasiwasi juu ya ushiriki wa maafisa waandamaizi wa Serikali akiwemo Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na DPP katika kamati hiyo ya nidhamu, hali inayokiuka Kanuni za Msingi za Umoja wa Mataifa kuhusu Wajibu wa Mawakili.

Aidha, Vyama hivyo vimekaribisha uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania wa tarehe 7 Oktoba 2026 uliosimamisha mwenendo huo wa NAC kusubiri Shauri la Kikatiba Namba 25918 la Mwaka 2026 lililofunguliwa na Mwabukusi mjini Dodoma. Vimeitaka NAC kuheshimu amri hiyo ya Mahakama Kuu huku vikizitaka mamlaka kufanya mageuzi ya Sheria ya Mawakili ili kuondoa kabisa udhibiti wa Serikali kwenye vyombo vya nidhamu vya taaluma hiyo.

Zaidi ya hayo, mashirika hayo yametoa wito kwa Mtaalamu Maalumu wa Umoja wa Mataifa (UN) na Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kuchukua hatua za dharura na kutoa mawasiliano rasmi kwa Serikali ya Tanzania kuzuia ukiukwaji wowote wa haki za mawakili.

Yamesisitiza kuwa uhuru wa TLS na viongozi wake ndio msingi wa pekee unaolinda utawala wa sheria na kuzuia matumizi mabaya ya madaraka dhidi ya raia na wanachama wa taaluma hiyo nchini.
 
Back
Top Bottom