East Africa redio mrudisheni shule huyu mtangazaji February Omary maana huu ni upuuzi

East Africa redio mrudisheni shule huyu mtangazaji February Omary maana huu ni upuuzi

secretarybird

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2024
Posts
2,998
Reaction score
4,948
Niko hapa nasikiliza Planet bongo ya East Africa radio ambayo inaruka kutoka Tumaini university.

Huyu mtangazaji aitwaye February amefanya kitu cha ovyo kabisa leo, wakati anamhoji amemuuliza dogo mmoja jina dogo akamwambia mimi ni mhadzabe February akasena "wale wanaokula vitu vichafu vichafu...".

Nimemshangaa Sana huyu binti mpaka macho yamenitoka kama mjusi aliyanwa na mlango.

realMamy toa neno lako.
 
Khaaaa watangazaji wetu ni balaaa sanaaaa....hawajui wanachofanyaa
 
Hiyo ya dogo kuambiwa kuhusu kabila lake kula vitu vichafu vichafu ndiyo imepelekea wewe kulia sana au kuna kitu kingine zaidi ya hicho?
Labda yeye ndo mtangazi aliyefanya huo utumbo.
 
Uchafu ni nini ? Kwa muktadha wa muuliza swali huenda kwake ni vichafu ila kwa wale wanaovila sio vichafu...

Sababu nina uhakika kwa utamaduni wa sasa na hao kama walikuwa shule wanafundishwa hata kula kitu bila kuosha au kunawa ni uchafu..., hivyo kwa mtu wa leo akiangalia ancestors wake (duniani pote) ambao walikuwa hunters and gatherers, ataona kwamba walikuwa wanakula vitu vichafu, ingawa na wale wanaweza kuona huyu wa leo immunity yake ni ndogo sana wala hawezi survive nature kutokana na kwamba yupo so protected...

Moral of Story, usijali fulani anakuonaje wewe ishi unavyoishi yeye akikuona mchafu wewe mshangae mtu anahangaika siku nzima apate pesa ili tu afunike mguu wake (eti kavaa kiatu) wakati ungebaki wazi ungepumua vizuri zaidi...

To each their own...; I might disagree with what she / he said but I will defend her/his right to Say it...
 
Back
Top Bottom