Jamani,
Huu mjadala wa shirikisho ni mzuri kweli kweli na hasa kwa sisi watanzania.
Kwa hakika wale wote, kwa maana ya watanzania, wanaoshabikia shirikisho la Afrika Mashariki nadhani wana matatizo yao, tena basi makubwa. Kwa maoni yangu shirikisho ni kitu ambacho hakifai, mimi hata kusikia tu neno lenyewe napata kichefuchefu.
Ni lazima tujiulize sana sisi watanzania faida na hasara za kujiunga na shirikisho. Kama ziko faida ni chache kuliko hasara ambazo ni nyingi. Ni wazi kuwa shirikisho linafagiliwa na wakenya ambao ndio walikuwa msitari wa mbele kuvunja jumuiya ya afrika mashariki mwaka 1977. Hasara kubwa itakayotokea kwa shirikisho hilo ni kuingizwa kwa utamaduni mpya wa chuki za kikabila nchini Tanzania zitakazoletwa kutoka Kenya. Wakenya ni wabinafsi na "arrogant". Wao wenyewe hawapendani- mjaluo, mkikuyu, mluhya na kadhalika. wanabaguana kweli kweli. Ubaguzi huo utaletwa tanzania na kuleta machafuko makubwa.
Kenya inataka shirikisho kwa kuwa ina viwanda vingi hivyo wanataka soko pana la bidhaa zao ambapo umoja wa kiuchumi tu hautoshi isipokuwa ni bora kuwa na umoja wa kisiasa(kwa maana ya shirikisho) ili kuwa na uhakika zaidi, kwa mawazo ya wakenya. Wakenya hawan ardhi ya kutosha na siku zote wamekuwa wakitoa mate ya tamaa mithili ya fisi wenye uchu wakitamani ardhi ya tanzania ili waje wafaidi ndani ya shirikisho. Ni kweli tanzania inaweza ikafaidika hapo baadaye katika shirikisho hilo na hasa kwa upande wa mbinu za kibiashara, lakini hii itakuwa ni baada ya muda kupita.
Kimsingi shirikisho ni kitu ambacho kinaweza kikaleta balaa kubwa mno katika eneo hili la Afrika kwa kutokea mapigano ya wenyewe kwa wenyewe. Mapigano ya huko Tarime ni mwanzo tu na yataongezeka zaidi wakija wakenya. huwezi kufanya urafiki na wakenya. Wale waliofanya kazi na wakenya wanafahamu tabia yao ilivyo ya ujeuri, dharau, manayanyaso na hata wizi.
Haya, piganieni hilo shirikisho muone kitachotokea miaka 50 ijayo ambapo vizazi vyetu vitakuja tulaumu sana kwa uijnga tulioufanya mpaka kukubali shirikisho.
tatizo la wanasiasa wetu ni kwamba wakati mwingine huwa hawaoni mbele. wanaangalia manufaa ya leo lakini hawafanyi tathimini ya kina kuhusu kile kinachoweza kutokea baadaye. Shirikisho ni balaa, ni balaa tupu. Wanasiasa wetu wanadanganywa, wanakuwa waoga kusema ukwelim kuhusu ubaya wa shirikisho. Nimewasikia wakisema mazuri ya shirikisho lakini hawasemi mabaya ya shirikisho. Wananchi wa Tanzania ni lazima wafahamishwe mazuri na mabaya ya shirikisho ili tuweze kupima katika mizani. Kinachofanyika sasa ni kuwaburuza wananchi, ili waone shirikisho ni zuri wakati siyo kweli. Hii ni mbaya sana.
mbavile edson