East African Federation (EAF) public Views

Hakuna tofauti ya elimu kokote duniani
tofauti ya elimu ni mwanafunzi husika ,mimi hapa hadi sasa nipo europe
mbona wakenya wote nilionao wapo weupe ,siwezi kusema eti labda wakenya wanaelimu hafifu kwa kuwaona hawa maana swala la elimu ni uwezo wa mtu binafsi na background yake.

Elimu ya bongo iko juu tusidaganyane mimi karibu miaka miwili nilikua napeta kutokana na elimu ya bongo tena ya vidato
katu sikubali eti wakenya na waganda wana elimu bora hilo halipo,ila ninachoweza kubali na watu wanachochangia ni kua uwiano wa wanafunzi waliopita na walio ktk vyuo vikuu kwa nchi hizi, tz iko chini.
hizo zote si hoja kuhusu EAF,hoja hapa hatutaki kupelekwa kikondooo eti fast track kwanza hata hiyo EAF hakuna matatizo yatakayotatuliwa ya nchi hizo tukubali waafrika tuna uchu mno wa madaraka na kujilimbikizia mimali pia umimi u ukarejingi hatimae ukenya
Hatu litaki shirikisho.

"eti tukiungana tukawa wengi ndio tutasolve matatizo yetu" Hivi wewe ukishindwa kuiletea familia yako (yani wewe mtoto na mke ) maendeleo na ukawa katika umasikini wa kutupwa na mifarakano ktk familia yako Je? utaweza kuletea mafanikio wanakijiji na ukaondoa mifarakano baina ya wanakijiji???? kichekesho!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Nani alikuambia ukijenga nyumba msingi unaanzia hewani???
Kila mmoja wetu anatambua Nyumba lazima ianze na msingi thabiti tena uliochimbiwa aridhini na kutiwa zege na nondo
Hawa viongozi wangekua na miono iliyo chanya na lengo makini kwa wananchi.

wangeji wekea mikakati ya kujenga misingi za nyuma zao ndio wakainua boma sasa msingi haupo na hata kama upo ni wa ma boksi na boma wanalotarajia jenga ni la mawe na tofari,sasa lita kapoporomoka litaangamiza hadi wadudu na kusambaratika vibaya.

shirikisho bado na wakilianzia tumeumia hapo hakuna shaka
unajua kila mmoja ataka awe rais na tena bado kila state litataka litoe rais hapo ndio kivumbi tutakiona Waafrika tukubali wakati bado kama bado tuko tayari kuuna kwa sababu ya madaraka
da inauma kweli
 
UJIO WA SHIRIKISHO LA AFRIKA MASHARIKI
Habari mbaya kwa Watanzania
NA AZIZ MONGI

NIMESHAWISHIKA kuandika makala haya baada ya kushuhudia kisa cha kusikitisha, kati ya vijana wawili wa kiume, na mmoja wa kike. Kisa hiki kilitokea baada ya vijana hao wa kiume kumuonea gere – aibu na ajabu! – kijana huyo wa kike, eti, amemleta rafiki yake wa kiume mtaani kwao. Hakukuwa na cha ajabu juu ya rafiki huyo wa kiume wa binti huyo, ila, kwao hao vijana, ulikuwa ‘mwiko’ kwa rafiki huyo kufika mtaani huko (wenyewe wanakuita Uswazi) na motokaa yake. Lakini kabda sijaendelea na kisa hiki murua, naingia moja kwa moja na mada kuu ya makala haya.

Naam! Lile Shirikisho (la kisiasa) la Afrika Mashariki, ambalo limekuwa likizungumziwa katika nyanja mbali mbali, mitaani, kwenye taasisi mbali mbali, na hata Bungeni (hili sina uhakika nalo...), linabisha hodi hapa kwetu. Gazeti moja la kila siku linalochapishwa kwa lugha ya Kiingereza hivi majuzi limechapisha taarifa kuhusu maoni ambayo yamekuwa yakikusanywa na Kamati Maalum ya Kuratibu Maoni ya Watanzania juu ya Shirikisho la Afrika Mashariki. Sikufanikiwa kusoma taarifa hiyo, ila, ninaamini, kwa vyovyote vile, hakuna ‘kizuri’ ambacho kimetolewa na taarifa hiyo, kuhusu ujio juo wa Shirikisho la Afrika Mashariki.

Kwa maoni yangu – narudia, kwa maoni yangu – Shirikisho hilo halina habari njema kwa Watanzania, ila, linakaribisha matatizo kwa Watanzania wengi, kutokana na ukweli kwamba Watanzania ni ‘wagumu’ na ‘wazito’ kubadilika. Kwenye mijadala mbali mbali ambayo inaendeshwa na vijana wa Kitanzania, hususan kwenye mtandao wa Intaneti, kumekuwa na maoni mbali mbali juu ya Shirikisho hilo, lakini cha msingi – ambacho ndicho ninachokiamini mimi – ni kwamba, Watanzania sio tu kwamba ni wavivu, bali pia, ni wazembe na wasiojali kujituma hata kama wanaambiwa baada ya kujituma huko kwao watapata zawadi lukuki.

Tuambizane ukweli. Iko mitaa ambayo siku hizi utawakuta vijana wa kiume wakicheza bao, huku wazee wakikerwa na tabia hiyo mbaya, kiasi cha kuwafukuza mitaani hapo. Wazee hao wamenukuliwa wakisema kwamba hawaoni sababu ya vijana wenye nguvu kushindwa kutwa wakicheza bao, huku wakilia kwamba hawana pesa. Wazee hao wamechukizwa na vitendo hivyo kwa kusema kwamba kuna misitu na mapori ambayo, kama vijana hao wangejituma kuyakata na kujilimia mashamba, wangevuna mazao mengi na kuyauza, hatimaye kupata fedha ambazo wamekuwa wakizililia. Wazee hao wamewapiga marufuku vijana hao kucheza bao, kwani mchezo huo ni kwa wastaafu peke yao, sio vijana wenye nguvu.

Mara nyingi nikiwa ninakatiza mitaa ya kati kati ya Jiji la Dar es Salaam, binafsi, ninalazimika ‘kuomba njia’ kutoka kwa vijana wenzangu, wa kike na wa kiume, ambao ninawakuta wakizubaa mitaani, kupiga gumzo lisilokuwa na tija, hivyo kuziba njia chache ambazo zimebakia kwa waenda miguu kutokana na wingi wa motokaa kwenye Jiji hili. Inanishangaza, kuona vijana wenzangu wakipoteza muda wao mwingi kuongea mambo yasiyokuwa na maana, wakisimama mitaani kupiga gumzo, wengi wakidai wanapanga ‘dili’... wakamtapeli fulani, wakamwibie fulani, wakachomoe kifaa fulani kwenye gari fulani... mambo ambayo, ukiangalia, kwanza ni uhalifu, na pili, ni hasara isiyo kifani ambayo haiwezi kukubalika. Na hawa ni wale vijana ambao, pengine, walisomeshwa kule ‘Mlimani’ kwa gharama kubwa, walizembea masomo, hawakufaulu, sasa wako ‘mishe mishe’ wakingojea ‘ujio wa Nuhu’ kuwashushia neema. ‘Nuhu’ alikwishafanya kazi yake, hatarudi tena.

Shirikisho la Afrika Mashariki litawakuta vijana wengi wa Kitanzania wakiwa wamelala usingizi mzito, tena wa pono, jambo ambalo litawafanya hata wale walio kwenye ajira kupoteza ajira hizo kutokana na sababu zifuatazo.

Mosi: Uvivu na uzembe – ukweli ni kwamba Watanzania wengi ni wavivu na wazembe. Kwenye kampuni nyingi binafsi hapa nchini, waajiri hulalamika kwamba wafanyakazi wao hutumia muda mwingi kuongea, kufanya shughuli binafsi, badala ya kufanya kile ambacho wameajiriwa. Iko mifano mingi, kwa mfano, kazi ambayo ingefanyika kwa muda wa siku moja, inafanyika kwa muda wa siku tatu. Mifano mwingine ni pale ambapo kazi fulani ingetakiwa kufanywa na mtu fulani, mtu huyo anatafuta sababu au anakwepa kutokuifanya kazi hiyo (kwa sababu anazozijua yeye mwenyewe), labda akidai kwamba kazi hiyo haina ‘hadhi’ ya kufanywa na mtu kama yeye. Anamtafuta mwenzake (ambaye pengine hana ujuzi wa kutosha kufanya kazi hiyo) aifanye badala yake, jambo ambalo, hatimaye linasababisha hasara kubwa, kwani, mara nyingi kazi hiyo hufanyika katika kiwango cha ubora wa hali ya chini kabisa, na mara nyingi zaidi, kazi hiyo haifanyiki kabisa, kutokana na aliyepewa kuifanya kutokujua aanzia wapi na amalizie wapi. Ni sawa na kumtafuta mwalimu bingwa wa Hisabati, na kumpa darasa la lugha ya Kifaransa. Ni bingwa wa Hisabati, lakini kwenye Kifaransa anatoka kapa.

Pili: Ukosefu wa uzalendo – jambo hili ambalo ni muhimu mno kwa taifa letu, hivi leo limetufikisha katika hali mbaya, wengi wetu hatujui kwamba tuko kwenye hali mbaya. Wengi wetu tunadhani hali tuliyonayo ‘imetokea tu’, na kwamba ni stahili yetu kuishi katika hali hii mbaya. Ninazungumzia hali halisi inayotukabili mitaani kwetu; uchafu uliokithiri kwenye mazingira yetu, uhalifu uliokubuhu, dhulma, unyanyasaji wa wanawake na watoto, wizi, unyang’anyi, ukahaba, uendeshaji madanguro, uoneshaji wa picha za sinema za ngono (ambapo pia watoto wadogo huruhusiwa kuona picha hizo, jambo ambalo ni uhalifu), na hili ambalo limekuwa sugu zaidi, yaani, fujo zilizokithiri za madereva wa daladala wawapo mitaani.

Ninasema ‘uzalendo’ haupatikani tena hapa nchini, kwani, sio tu kwamba umepotea, ila, Watanzania wanajua wajibu wao, ila hawaoni sababu ya kuwajibika. “Sio kazi yangu,” wanadai. Au “Mimi nahusika vipi hapa?” Kuna majibu mengi zaidi.

Inashangaza kuwaona wakimchapa kwa bakora, kumpiga kwa mateke, mawe, mapanga na nondo, kijana ambaye atakamatwa kwa wizi wa kuku mtaani kwao (huku yule ‘Mzungu wa Unga’ akikodoa macho dirishani kwake...), hatimaye kijana huyo kuishia kupata adhabu isiyostahili kosa alilolifanya... kifo kwa kuunguzwa na moto wa petroli. Kesho yake, magazeti yanachapisha habari juu ya ‘kijana aliyeaminika kuwa mwizi aliuwawa na watu wenye hasira baada ya kuchomwa moto na mwili wake kutupwa barabarani...”, watu wananunua magazeti hayo, wanasoma, kisha wanafungia vitumbua, maandazi na chapati, siku imeisha. Yule ‘Mzungu wa Unga’ anayewaharibu vijana wengi kwa kuwauzia madawa ya kulevya bado yuko pale pale, mtaani pale pale, anajulikana, lakini hakuna anayethubutu kutoa taarifa kwenye vyombo husika, kwa kuwa ‘... sio kazi yake...”, vijana wazidi kuteketea. (Labda kwa kuwa askari polisi wanakula rushwa, na wanawataja watoa taarifa za siri?)

Jambo la ajabu ni kwamba, uhalifu unaofanywa na ‘vibaka’ unaonekana kuwa uhalifu mbaya zaidi kuliko uhalifu unaofanywa na madereva wa daladala. Dereva wa daladala akivunja sheria kwa kupita pembeni, kwenye eneo la wapita miguu, abiria wanafurahi, kwa kuwa ‘wanawahi’. Dereva ‘akitanua’ upande wa kulia wa barabara, abiria wanakenua meno kwa furaha, kwa kuwa ‘wanawahi’. Wanawahi wapi? Kuzimu? Kwa nini uhalifu wa kuvunja sheria za barabara unaofanywa na dereva wa daladala usiwe uhalifu, ila, ule unaofanywa na ‘kibaka sugu’ wa mtaani ndio uonekane uhalifu, tena wa kuishia kuchomwa moto na ‘kibaka’ yule kupoteza maisha yake? Huu ni unafiki unaosababishwa na ukosefu wa uzalendo.

Tatu: Kushindwa kuweka kipaumbele cha maisha. Ni kweli kabisa, Watanzania wengi hawajui waanzie wapi kuweka kipaumbele cha maisha yao. Ukienda vijijini, kunakodaiwa kuwa na ‘maisha magumu’, utaona jinsi watu wanavyoendesha maisha yao kiholela. Wanaishi kwenye nyumba za udongo na miti, wasione kwamba nyumba hizo hazifai kwa maisha ya binadam. Mvua kubwa zilizonyesha hivi karibuni zilizomba nyumba za namna hiyo mkoani Shinyanga na kuwaacha maelfu ya wakazi wa mkoa huo kukosa makazi. Ukirudi mijini, ambako kuna ‘maisha magumu zaidi’, hali ni mbaya zaidi. Watu wako radhi kufakamia bia na ‘ulabu’ badala ya kuwekeza kidogo kidogo, kufyatua matofali mawili au matatu kwa siku, kununua viwanja vya kujenga... ni kweli, mimi binafsi sijajenga, najikosoa pia... tumeshindwa kuweka kipaumbele cha maisha. Ni jambo gani muhimu? Starehe au kuwa na nyumba bora za kisasa? Mbona tuko tayari kuchangishana mamilioni ya fedha kwa ajili ya karamu kubwa ya siku moja – Harusi ama ‘Send off’ – wakati tungechanga fedha hizo kuwasomesha watoto wetu kwenye shule bora zaidi, hata nje ya nchi? Hatukujifunza kwa majirani zetu wa Kenya, ambao mpaka leo wanaendesha ‘Harambee’ ya kuwasomesha watoto wao ughaibuni?

Nne: Kushindwa kujiamini. Hili ni tatizo kubwa sana kwa Watanzania walio wengi. Tatizo hili haliangalii uwezo wa kielimu wa mtu mmoja mmoja, au uwezo wa kiuchumi. Linaangalia ujasiri wao, kama wanaamini kwamba wanaweza kufanya wale ambayo wanakusudia kuyafanya, ama la. Ukweli ni kwamba, wengi wa Watanzania hawajiamini kabisa katika kujaribu mambo mapya. Wako radhi kumsubiri mtu afanye jambo, nao waige. Utakuta, mtaa mmoja dada anafungua ‘salon de coiffeur’ yake, ama chumba cha kurekebishia nywele, basi, akina dada wengine watafungua ‘saluni’ hizo bila kujali kama wateja waliopo watawatosheleza, yaani, kutakuwa na uwiano sahihi kati ya watoa huduma na wateja. Hatimaye, inafikia kugombania wateja wachache waliopo, na wengine hata kufanyiana mambo mabaya yasiyofaa kutajwa hapa. Hawakuangalia nini maana ya kuwa mjasiriamali, kwani, mjasiriamali hufanya utafiti na kubaini ni huduma gani ambayo inakosekana katika sehemu fulani, kisha yeye kuchukua fursa ya kuitoa huduma hiyo ili watu wafaidike nayo. Mambo ya kuiga, kweli yanatokea mitaani, kwa sababu Watanzania wameshindwa kujiamini na kujitosa kikamilifu kwenye biashara. Kushindwa kujiamini huku nako kumefikia hata kwa waidhinishaji mikopo, ambao wanaona kwamba watu wenye ngozi nyeusi – Waafrika – hawana uwezo wa kufanya biashara zinazohitaji mitaji mikubwa, hivyo, wajasiriamali wadogo, mathalan, wachimba madini wadogo, wanapopeleka michanganuo yao kwenye benki mbali mbali, haiyumkini wao kunyimwa, kwa kuwa tu ni Waafrika. Kutokujiamini kunatokea hata kwa waidhinishaji mikopo, ambao hawana imani na wao wenyewe, hivyo, kudhani kwamba hata wachimba madini wadogo watashindwa kuendeleza miradi yao. Lakini akija mzungu? Kwani mzungu peke yake ndiye aliyepangiwa kufanya bishara kubwa kubwa?


Hizi ni sababu tatu kuu ambazo zinatutofautisha sisi Watanzania na majirani zetu wa Kenya na Uganda, ambao wamesonga mbele miaka mingi iliyopita. Hizi ndizo sababu ambazo zitatufanya sisi Watanzania ‘tumezwe’ na wenzetu hawa, kwa kuwa wana mtazamo tofauti wa maisha. Sisi, ambao tuko kwenye ‘Nchi ya Neema’, tumesahau kabisa kwamba tuna utajiri kupita wao, ardhi bora zaidi kupita wao (sehemu kubwa ya Kenya ni jangwa...), na mali asili nyingi zaidi kupita wao (Tanzanite hupatikana Tanzania pekee, lakini Kenya ndio inaongoza kwa mauzo yake duniani...), na kadhalika.

Afrika Mashariki itakapoingia rasmi, tusishangae kujikuta vibarua, tutakaoajiriwa na majirani zetu kutoka Kenya na Uganda. Wao wakiwa mabosi, sisi makuli, mambo yatakuwa mazuri zaidi au mabaya zaidi kwetu?

Nikimalizia, wale vijana niliowaona wakimsarandia yule dada aliyepata ugeni wa ghafla mtaani kwake, kumbe walikuwa wamekunywa pombe kali aina ya ‘gongo’. Hivyo, ilikuwa tafrani kubwa mtaani hapo. Badala ya kukaa na kupanga mipango makini ya nini wafanye, wao wanaishia kutwa kulewa mchana, jioni kupora wapita njia. Hayo ni maisha gani? Kijana, fanya kazi, usimwonee wivu dada anayejituma, anayefanya kazi. We unabakia kalaghabaho? Yakhe! Haifai hiyo, mwanaume kumfuatia mambo yake binti anayejituma sio ‘fresh’. Huo ni sawa na umbea! Mwanaume mwenye tabia ya umbea hafai kwenye jamii ya siku hizi. Angalau, tunaweza kumvumilia mwanamke mwenye tabia hiyo, ingawa hata kwa wanawake pia tabia hiyo sio nzuri. Umbea haufai! Tufanye kazi, Afrika Mashariki hiyo inakuja, tutamezwa tukitazama bila kuwazuia.

Tuamke! Usingizi mtamu, lakini mbaya!
 
MWanahaki
kwa hiyo uzalendo kwa tanzania utaletwa na wakenya/waganda/wanyarwanda
na wachapa kazi wa tz watakua pia wakenya/waganda kwa kuwaletea maendeleo wtz.

kifupi wenda hujafanya analysis nzuri kesho shuka wa uwanja wa ndege wa Nairobi ujionee machokoraa watakavyokufanyia
uzalendo wtz wanao sana ila viongozi wetu wanatukatisha tamaa,Angalia mfano mdogo muuaji anapitishwa ktk mlango wa majaji na tena ndugu wanatoa kipigo kwa waandishi je? hapo nani ataendelea kuwa mzalendo?

wtz wanafanya kazi viongozi wanapora eti rada na richmond sasa nani aendelee kufanya kazi ili kiongozi aingie mkataba na richmond/IPTL
wananchi wanasema hili shirikisho bado wmtu mmoja anasema lazima tuingie je?watu milioni kadhaa na mtu mmoja nani mwenye maamuzi mema???harafu tunaendelea eti tz kuna demokrasia
kifupi tunakatishwa tamaa
 
Mwanahaki: Matatizo uliyoyainisha ndugu yamesambaa kote Afrika; hakuna nchi iliyopona. Yote hii imetokana na viongozi wetu kuhimiza uchuuzi kama njia halali ya maisha badala ya mambo kama kilimo. Uchuuzi tuliokemea sana miaka 70 na 80, lakini leo ndo tumeukuambatia kwelikweli.

Lakini wewe kwa nini unawalaumu watanzania moja kwa moja? Huoni kwamba kuna tatizo la mfumo, sera, n.k.?
 

Lakini bado hujanijibu swali langu la vigezo ulivyotumiwa kufikia hitimisho kuwa elimu ya Nairobi/Kampala ni bora kuliko ya Dar.

Je, hao walioupata u-director ni kwa sababu walisoma nje au kwa sababu walikuwa na sifa?

Je, ni kweli kwamba hakuna ma-directors waliosoma TZ?

Dr Khamis samahani sana, lakini kwa mtu mwenye elimu yako na aliyefundisha hadi Ulaya natarajia uchambuzi mzuri zaidi kuliko hapo juu!
 
Beware EU pressure to open markets —Oxfam


http://www.nationmedia.com/eastafrican/current/Business/biz1203077.htm
 
We tanzanians are not risk takers like kenyans and ugandans, a kenyan can work and live any where in the world because they take risks, agood example, iwas really challenged when i went to australia, i found alot of blacks there with business, when i inquired most of them were kenyans, i went to sudan, the majority of experts are kenyans and shockingly the respected currency apart from euros, dollars, was kenya shillings. Its all because they take risks -i mean positive risks.

Lets enumerate them, lets go out there and be like them, lets welcome them and learn from them, lets not be timid we can make it when we accept challenges and allow patience in our endeavours, we love short cuts alot lets change for positive attributes, lets forget gossips, kenyans take initiatives to the last brims amreally challenged by them, lets welcome the federation to enable them teach us, lets not go south or west, better the devil you know than the angel you have never met,- where are the young executives in tanzania?

Take risks and save the country from the old wazees who are power centred, lets show them that we are leaders, lets go and open crdb in kenya, nmb in kenya mbona tuwachie hawo tu kwani hatuwezi?

Lets be risk takers au sio and let all members have a risky day wont you!!!!!!!
 
Tanzanians have taken a risk and are found in most of European Countries. You can find them in Spain, Italy, France, Germany, Holland, England, Denmark, Sweden and Norway to mention just to mention a few countries.

Last year I was in Canada and USA and I was happy to find out Tanzanians have also been able to secure jobs in that part of the world. I think if you will travel to China, Russia, Ukraine and other eastern countries you will find also well established Tanzanians. I know there are Tanzanians working in India and Pakistan.
 
Nikiwa ni mzaliwa wa Tanga, jambo hili la Mkuu wa Mkoa ni mfano mzuri katika kuboresha elimu ya Watanzania. Itakuwa ni vizuri kwa mikoa mingine kuiga mfano huu.

Shule mkoani Tanga zimeanza kuonyesha jitihada za kukabiliana na ushindani

2007-03-12 15:38:35
Na Radio One Habari
Wadau wa elimu hapa nchini wametakiwa kujifunza mikakati inayotumiwa na walimu kutoka Kenya na Uganda ili kukuza kiwango cha elimu na kuleta ushindani katika nchi za Afrika mashariki.

Changamoto hiyo imetolewa na Mkuu wa mkoa wa Tanga Mhe. Mohamed Abdulaziz wakati wa mahafali ya kidato cha sita katika shule ya sekondari ya wasichana ya Mtakatifu Christina yaliyohuduriwa na wadau wa elimu ngazi ya taifa.

Amesema kwa sababu ushindani wa elimu ni mojawapo ya ajenda muhimu ambazo zinaangaliwa katika jumuiya ya Afrika Mashariki ni vyema wadau wa elimu wakajifunza mikakati inayotumiwa na Kenya na Uganda katika suala la kuimarisha elimu.

Mkuu huyo wa mkoa wa Tanga amesema baadhi ya shule za msingi na sekondari mkoani mwake zimeanza kuonyesha jitihada za kukabiliana na ushindani kwa kutoa ajira kwa walimu kutoka nchi za Kenya na Uganda, hatua ambayo imeanza kuonyesha mafanikio katika mitihani ngazi ya mkoa na taifa.
· SOURCE: RADIO ONE
 
East African Federation Team Broke

 
How can we use more than Sh.2.4b for the East African Federation project that is not our first priority?
Tanzania is a poor country with a lot of problems that require immediate solutions.
 
Asalam aliko wakubwa**
Jamani hawa mafirauni wanaoleta haya malink ya viagra na link nyingine za ngono, kwanini msiwa-block ?, sababu most of them are the virus agents.
 
East Africa Federation is advantageous to east african, we will maximize our human resource utilization and other resources, movement of goods and capital would become easier.EAF will appreaciate economies of scale and improve services.
We tanzanians need to change our negative attitude, that we are not ready! not educated, bla bla...
 
Tanzania can trade with any country in the world or any group of countries without forming a federation with them. We have the present East African Community that facilitates the movements of goods, capital and human resources between Tanzania, Kenya and Uganda.
Let us first build up the East African Community and reach that level of cooperation it had during 1970 1978 or before the war between Tanzania and Uganda.
We would like to see first.
1. The East African Airways (owned by Uganda, Kenya and Tanzania).
2. The East African Railways and Harbours.

By that time you could travel by railway from Tanga-Moshi- via Voi to Nairobi in Kenya and to Kampala in Uganda. Goods to the land locked Uganda were off loaded at Mombasa harbour and Tanga harbour and thus created jobs for Tanzanians in Tanga.
Federation is a political union that will involve many things such as:
a. One currency for all member countries
b. One army for all member countries
c. Probably also one education system
d. One parliament for member countries, like that we have seen in EU.All decisions will be taken place in this parliament.
e. There will be one President for the Federation. That means JK, or Msevenji or Kibaki will be probably only Prime Ministers in their respective countries.
f. The federation can have a President from Rwanda or Burundi.

We would like all governments concerned to present The Constitution of this so-called Federation in their respective parliament. We citizens cant buy something that is hidden in a sack.

If in the future Tanzanians will get out of the Federation will they be allowed? How much in terms of US $ shall Tanzania pay as a member of the Federation?

There are many questions to be answered by our government before we can accept federation in the future!
 
EAC

East Africa: Lawyers Claim EA Unity Being Rushed
http://allafrica.com/stories/200703140399.html
 
We have to take the words of President Karume seriously. That is what Tanzanians have been saying all the time. We have still in our memories the collapse of EAC in 1997 and the war between Tanzania and Uganda.



· SOURCE: GUARDIAN
 


is zanzibar one country? I thought you wanted to joint federation as unguja country, or pemba country, but not zanzibar. Kwa sie tunaoujua ukweli wa kihistoria huwezi kutudanganya hapo. Sema ukweli.
 
Ninyi Wazanzibari mnamatatizo yenu. Ninyi ni ndugu zetu halisi na mmetapakaa katika mwamba wote wa pwani toka Mtwara-Lindi-Mafia-Dar es Salaa-Bagamoyo-Pangani-Bweni-Kigombe-Tongoni-Tanga-Vanga na Kijiru na kadhalika.
Samahani kama tuliwaburuza katika Muungano. Lakini ndugu wakiungana ndio vyema na matatizo ya kindugu hayeshi asilan.Wakati ule wa Muungano waamerika walikuwa wameshavamia hivyo visiwa na Station zao kwa ajili ya kupeleka Satellite zao mwezini. Serikali ya Muungano iliweza kuondoa Station hiyo Zanzibar.
Siku zile hayati J.K.Nyerere na hayat A.A.karume waliona ni kheri ndugu kuungana wakachukuwa jukumu hilo la kuunganisha nchi zetu mbili, Tanganyika na Zanzibar.

Sasa hivi tumepewa fursa ya kueleza kama tunataka Federation ama hatuitaki. Hapa ndio Rais Karume anasema kama mtanzania kwamba viongozi wasituburuze. Hii itawafanya viongozi wenzake watafakari.
Hili jina langu Khamis liliniletea taabu 1977 nilipotua Zanzibar. Immigration walinuuliza wewe ni Mzanzibari nikakataa na wakiniweka saa mbili kiwanjani. Kwa bahati nzuri passport yangu ilitolewa Ubalozini, Den Haag,Netherlands(Diplomat pass) na hawakuweza kunipokonya.Sababu mke wangu alikuwa ni Mzungu ndio maana wakafanya hivi. Kwa bahati nzuri rais wa Zanzibar wakati ule alikuwa ni Balozi wetu Den Haag, Netherlands wakati nilipopowa ile passport. Walipopiga simu huko akawaambia mwacheni huyo na mkewe aingie huyo ni mtu wa nchi zote mbili.

Ndugu hivyo visiwa visikuhadae kwani vimetoka katika mwamba wa Tanganyika wakati kontinti zilipoachiana(million of years ago).
 
Tanzania Defiant On SADC Withdrawal


http://allafrica.com/stories/200703170149.html

Well hao WTO walikuwa wapi wakati tunapigania harakati ya kujikomboa? Mbona hawajaweza kutatua matatizo mengi ya biashara na nchi tajiri? Tishio kubwa ni SADC na sio EAC kama wanavyotaka tuamini kwani tumegawanyika katika malengo na policy.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…