Na Maggid Mjengwa,
MCHEZO wa ngumi una taratibu zake. Yanaweza kutokea madhara makubwa ulingoni kama taratibu hizi hazifuatwi. Hii ni pamoja na mtu kupoteza uhai. Mathalan, inapotokea mabondia wawili kutaka kuwania ubingwa wa uzito wa juu, basi, mabondia hao ni vema wawe na uzito wa juu. Kama sivyo, basi walau uzito wao ukaribiane.
Kama bondia mmoja ana uzito wa kilo mia na mpinzani wake kilo hamsini, basi, meneja makini wa bondia mwenye kilo hamsini hawezi kukubali kumwingiza bondia wake ulingoni. Na hata akithubutu kufanya hivyo, meneja makini wa bondia mwenye kilo mia, anaweza kuingiwa na busara ya kutomwingiza bondia wake ili kuepusha madhara yatakayotokea. Hata hivyo, hilo la mwisho ni nadra sana kutokea. Hii inatokana na hulka ya mwanadamu kupenda kutanguliza maslahi binafsi.
Lakini, meneja wa bondia mwenye kilo hamsini anaweza kuamua kumwingiza bondia wake ulingoni kama atajiridhisha, kuwa bondia wake, pamoja na uzito mdogo, bado ana mbinu na maarifa ya kutosha kuweza kummudu mpinzani wake mwenye kilo mia.
Katika hili la Tanzania kama nchi kujiunga na Shirikisho la Afrika Mashariki, tunahofia, kuwa kunaweza kuwa ni sawa na meneja anayemwingiza ulingoni bondia wake katika mazingira niliyoyaelezea hapo juu. Busara ni kwa meneja huyo kumwandalia bondia wake mazingira ya kumfanya aongeze uzito wake ikiwa ni pamoja na mbinu na maarifa kabla ya kuingia ulingoni.
Unapozungumzia Shirikisho unazungumzia ushindani, hususan wa kiuchumi miongoni mwa watu watakaounda shirikisho. Watu hawa wanshirikishwa kwenye kushindana, iwe kwenye ajira na mengineyo. Tunasema hivi kwa vile hata ndani ya shirikisho, Wajaluo watabaki na ujaluo wao, Wakikuyu na Wabaganda vivyo hivyo.
Mara ya mwisho nilipokuwa nchi jirani ya Kenya nilishtuka sana mara ile dereva wa teksi alipojitambulisha kwangu kwa jina lake na kabila lake. Kwa hapa nyumbani sijapata kukutana na dereva wa teksi aliyejitambulisha kwangu kwa namna alivyofanya Mkenya yule.
Hakika, kitendo kile cha dereva yule wa teksi kilinifanya nichukue muda kutafakari kwa kina. Ni hapo nilizidi kuuona ugumu uliopo katika kufikia azma ya kuwa na shirikisho la nchi za Afrika ya Mashariki ukijuumuisha pia Rwanda na Burundi.
Hakuna haja kwa sasa kukimbilia kwenye shirikisho. Katika mazingira ya sasa, bado tunaweza kushirikiana kama watu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki katika maeneo tutakayokubaliana,iwe kiuchumi au kijamii. Ushirikiano huo tayari upo, lakini si lazima kuunda shirikisho kabla hatujawaandaa watu wetu vya kutosha. Ni nia nzuri ya kuwa na shirikisho, lakini tunadhani muda haujafika kwa hilo.
Na kama ni kupata maoni ya kweli ya Watanzania, basi wasiulizwe kwa kuzungukiwa na kamati ya kukusanya maoni. Badala yake kuwepo na kura ya maoni.. Kura hiyo ya maoni itanguliwe na elimu ya kijamii juu ya shirikisho na yote yenye kuhusika nayo. Mashirika ya hiyari na makundi yenye kupinga shirikisho kwa sasa nayo yapewe nafasi ya kuwaelimisha Watanzania ni kwa nini Shirikisho halifai kwa sasa.
Tunadhani, kukimbilia kwenye shirikisho ni kuwakimbiza Watanzania kwenye zizi ambalo wataishia kuwa ni ngombe wenye kunyanyasika. Watanzania hawako tayari kwa sasa kuwa ngombe wanyanyasika mbele ya jirani zao. Kulazimisha jambo hili ni kujenga chuki isiyo ya lazima miongoni mwa majirani hawa.
Tunadhani, kutokana na mazingira yao, ikiwemo ukosefu wa ardhi ya kutosha, Wakenya wengi wangependa liundwe shirikisho ili nao wapate fursa ya kuja Tanzania. Waje kama nchi ya shirikisaho na kupata fursa sawa kama Watanzania ikiwemo kugombania ajira kwenye soko la ajira la Tanzania, kugombania ardhi pia. Jambo hili laweza kuchochea chuki miongoni mwa Watanzania dhidi ya jirani zao, hii itatokana na Watanzania kujiona wako chini kulinganisha na wenzao wa Kenya.
Ni vema tukatambua, kuwa kuingia kwenye shirikisho kwa sasa ni kuwaingiza watu wetu kwenye ushindani wa kiuchumi bila ya kuwaandaa vya kutosha kuikabili mikiki mikiki hiyo. Uduni wa elimu yetu ukilinganisha na nchi jirani na sisi ni moja ya hatari zilizo mbele yetu, kwamba tutawaingiza Watanzania wengi kwenye shirikisho bila kuwa na misingi mizuri ya elimu.
Tunahitaji kusubiri kwa kujipa muda. Hata majirani zetu nao pia wanahitaji kusubiri. Kabla ya shirikisho, nchi zetu hizi zijikite katika kuendesha michakato ya kujenga mataifa yao kwa kuanzia na kuondoa tofauti za kikabila na kimaeneo. Ni ajabu sana kuzungumzia kuunda shirikisho la Afrika Mashariki litakokuwa na Rais mmoja, bunge na mawaziri wa shirikisho wakati katika nchi kama Uganda wanahitaji kuwa na shirikisho lao la ndani. Uganda leo inahitaji kuwashirikisha Wanyankole, Wabaganda, Wa-Acholi na wengineo wajisikie kama Waganda.
Kenya nao wanahitaji shirikisho la Wajaluo, Wakikuyu na wengine kabla ya kufikiri juu ya shirikisho la Afrika ya Mashariki. Tanzania nasi tunahitaji kutafuta majawabu ya kero zetu za Muungano kabla ya kufikiri kuwaingiza Wapemba na Waunguja kwenye shirikisho
Hakika, kabla ya kuota kuwa na Rais wa shirikisho, serikali za nchi zetu hizi zinapaswa kuiendeleza michakato ya ndani ya kuboresha demokrasia na kujenga misingi ya utawala bora.
Inavyoonekana sasa, mradi huu wa kuundwa kwa shirikisho ni mradi wa viongozi zaidi kuliko wananchi. Viongozi wanatuomba wananchi tutoe maoni yetu juu ya shirikisho wakati wengi wa wananchi hawajui hasa ni kitu gani wanachokitolea maoni.
Kama tutaupuuza uhalisia hu
u, basi, mradi huu wa Shirikisho utabaki kuwa ni Mradi wa Marais wa nchi hizi badala ya kuwa ni mradi wa wananchi. Katika nchi zetu hizi, tunapaswa kwanza kutatua matatizo yetu ya ndani ya kijiografia, kisiasa, kijamii na kiuchumi kabla ya kupanga kuunda shirikisho.
Tunahofia pia, kuwa shirkisho halitajengeka katika misingi ya usawa. Kwani, Tanzania kama nchi, ina hatari ya kuwa ya tatu na pengine ya mwisho kimadaraja. Elimu ni sababu mojawapo itakayopelekea tubaki nyuma.
Naam. Historia ni mwalimu mzuri. Tuziangalie historia zetu kwanza ili tujiweke katika hali nzuri ya uelewa na kutafuta yale ya kimsingi tutakayokubaliana kwa pamoja. Kwa kuingalia historia ya Afrika ya Mashariki, inaonyesha wazi, kuwa Tanzania kama nchi inapaswa kujiadhari na kumezwa na nchi nyingine, kwamba ibaki kama ilivyo hususan kwenye nyanja ya kisiasa.
Itakumbukwa, hata miaka kabla ya uhuru, wazo la kuwepo kwa shirikisho la kisiasa kwa nchi zetu hizi liliwekwa pembeni na watawala. Na katika hili la sasa, yaani shirikisho, tunahofia, kuwa azma kwa wengine yaweza isiwe ni kwa maslahi ya wengi bali ya wachache kwa kutumia udhaifu wa nchi moja au mbili wanachama wa shirikisho.
Hakika, uwepo wa shirikisho unahitaji muda mrefu wa maandalizi. Kwa mtazamo wangu, Watanzania tunahitaji zaidi ya miaka 30 kutoka sasa. Miaka 30 ya kuandaa mazingira ya kuwepo kwa shirikisho litakodumu kwa muda mrefu zaidi. Na pengine kizazi cha Watanzania watakaojitambua kama raia wa Afrika Ya Mashariki bado hakijazaliwa. Lakini, misingi yake tunaweza kuanza kuijenga sasa. Kwa makala zaidi na picha, tembelea; http://mjengwa.blogspot.com