JUMUIYA YA AFRIKA MA ARIKI- TUKO TAYARI?
Kuna msemo wa Kiswahili usemao mwenda pole hajikwai hata akijikwaa haumii..hata akiumia ni kidogo sana..
Msemo huu unaendana sambamba na nia yetu ya kuanza utekelezaji wa kile kinachoitwa jumuiya ya afrika mashariki ,mchakato ambao umeenda sambaba na kuundwa kwa kamisheni kwa ajili ya kukusanya maoni kuhusiana na shirikisho husika .
Leo katika maandiko yangu machache nataka kuzungumzia kitu kinachoitwa EAC- Fast tracking ..Nadhani ndugu zangu mnanipata ninavyosema fast tracking , si mnafahamu hata pale muhimbili kuna hiyo kitu maana yake fasta fasta..Yaani kama una vijisenti vyako na hutaki kupanga foleni kutibiwa unazitoa na unapata huduma chap chap bila usumbufu wowote.
Tofauti na afya ya mwanadamu ambapo huduma ya haraka haraka inaweza kuwa na matokeo mazuri ..katika masuala yanayohusu maslahi ya nchi, mambo yanavyofanywa haraka haraka yanaweza kuwa na madhara makubwa sana
Kimsingi sipingi hata kidogo uanzishwaji wa jumuiya husika Nafahamu fika kwamba kama nchi zote zitakuwa na dhamira ya kweli, jumuiya ya afrika mashariki itakuwa fursa ya kukuza soko la bidhaa na huduma mbali mbali .Jambo la msingi ambalo napenda kujihoji ni kama tumejiandaa vya kutoshwa kuweza kukirejesha kile kilichotushinda mwaka 1977 mpaka kupelekea kuvunjika kwa jumuiya au tumeamua kuingia kichwa kichwa ?
Ukiangalia kwenye utangulizi (Preamble) wa mkataba wa Afrika Mashariki, paragraph ya nne imeeelezea sababu zilizopelekea kuvunjika kwa jumuiya.
Sababu hizo ni :
i)Kutokuwa na dhamira ya dhati ya kisiasa
ii)Kutokuwa na ushiriki mkubwa wa sekta binafsi na mashirika ya kijamii
iii)Mgawanyo usio sawa wa pato la jumuiya kati ya mataifa kutokana na
kuwa na tofauti kubwa ya kiuchumi
iv) Kutokuwa na sera mahsusi za jumuiya
Hivi ni kweli tumeshayajadili haya mapungufu kwa mapana na kuyatafutia tiba?
Hivi ni kweli tuna dhamira ya kisiasa kufanya hivyo? Dhamira hiyo ya kisiasa ni ya nani? Ya viongozi wa ngazi za juu pekee au imetokana na majadiliano ya nguvu na kisha kufikiwa muafaka baina ya viongozi wa nchi husika na makundi mbali mbali ya kijamii yanayojumuisha viongozi wa dini, asasi za kijamii na viongozi wa kisiasa katika ngazi zote mpaka ngazi ya kijiji?.
Hivi ni kwa kiasi gani tatizo la sekta binafsi na mashirika ya kijamii yamehusikwa katika mchakato huu?
Ni kweli kwamba yale yaliyotusambaratisha , hasa hasa linalohusiana na mgawanyo wa mapato baina ya nchi hizi kutokana na kuwa na tofauti kuwa ya kiuchumi tumeyaaddress vya kutosha kuweza kutojirudua tena ikizingatiwa kwamba watanzania tumeachwa mbali sana na wenzetu hasa hasa Kenya, katika nyanja ya uchumi na elimu? Ni hivi majuzi tu nilikuwa napitia gazeti moja la biashara. Moja ya kitu ambacho kilinishtua sana ni pale niliposoma taarifa inayoonyesha kwamba katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita Kenya imefanya biashara ya thamani ya US $ milioni zaidi ya 500 (Bilioni 500) kwa nchi za Tanzania na Uganda wakati Uganda na Tanzania kwa ujumla wake wamefanya biashara na kenya yenye thamani ya US$ milioni 100 (Shilingi bilioni 100..)na ushehe.
Ikumbukwe kwamba haya yote yamefanyika wakati milango ya kibishara bado haijafunguliwa? Tumejiandaa kiasi kwa hili? Tusije tukajikuta tunakuwa walalamikaji tu!
Hivi ni kweli tunazo sera za kutosha?Kama zipo nani anayezifahamu? Na nani anayetakiwa kuzitekeleza? Kwa kautafiti kadogo nilikokafanya wakati nikifuatilia kamati ya kukusanya maoni ilivyokuwa ikipita kukusanya maoni kuanzia kwenye level za viongozi mpaka wananchi wa kawaida .ufahamu wao kuhusu jumuiya husika ni mdogo sana au haupo kabisa wengi wanaonekana kushangaa
Taarifa zilizopo zinaeleza kwamba sample ambayo itatumika kwa ajili ya kujua kama fast track ianze ama la ni watanzania 15,000 Hivi kwa mtu mwenye akili timamu anaweza kuchukua maamuzi ya watu 15,000 kuwa maamuzi ya watu Mil 37? Hali inazidi usikitisha ni pale wengi wa watu wanaohojiwa ni viongozi wa kisiasa yaani madiwani nk. Kutokana na hali hii ku a hatari maamuzi yakafanyika kwa kuangalia unterest za chama zaidi kuliko utaifa..
Katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania ..
Ni kweli kwamba hivi vyombo vilivyoundwa kwa ajili ya kufanikisha uwepo wa Jumuiya vina nguvu za kutosha kuweza kuhimili mikikimikiki.
Nilipokuwa darasani nilifundishwa kwamba katika utawala wowote ili mambo yaende kwa ufasawa lazima kuwe na mgawanyo wa madaraka (separation of power) baina ya vyombo vikuu vitatu ( mahakana , bunge na serikali ) ili kila kimoja kiweze kumkemea mwenzake pale anapozidisha /anapovuka mipaka ya kazi yake, wenyewe wanaita checks anda balance.
Naomba kuanza na Mahakama :
Mahakama ni mhimili wa muhimu sana wa utawala wowote ule ulio makuni, kwani ni hapa ambapo mtu yeyote ambaye anaona hakutendewa haki na vyombo vyovyote vya utawala anaweza kwenda kudai haki yake na kuipata -hivi karibuni bunge la jamuhuri ya muungano lilipitisha mabadiliko ya Mkataba wa Afrika mashariki. Ikiwa imeshinikizwa na Rais Kibaki wa Kenya aliyekasirishwa sana na kitendo cha mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kusita kuwaapisha wabunge aliowataka yeye( ambao hawakuwa chaguo la wakenya) ambaye pamoja na mambo mengine alitishia kurudi nyumbani kuwaapisha wabunge wake- kuliko endana sambamba na kufungua kesi mahakama ya Afrika Mashariki kuwataka majudge wakenya ( waliopo kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki ) wasiwepo katika jopo litakalosikiliza kesi ya kupingwa kuapishwa kesi ambayo serikali ya Kenya ilishindwa .
Kufuatia mashinikizo hayo, na hofu ya kuwa na chombo cha mahakama kilicho huru na chenye nguvu viongozi wetu hawa walikuja na kile kitu kinachoitwa mahakama ya rufaa .
Ni muhimu ikaeleweka kwamba hakuna mtu yeyote makini atakayepinga kuanzishwa kwa Mahakama ya Rufaa, tatizo ni ukiukwaji mkubwa wa sheria na taratibu na Mkataba ambao uliofanywa na Marais wetu. Ni jambo la hatari sana unapokuta viongozi wakuu wa nchi wakiuvunja mkataba na kusimama kidete kutetea ukiukwaji huo wa taratibu.
Ibara ya 150 ya Mkataba wa Afrika Mashariki unazungumzia Marekebisho ya Mkataba . Kipengele husika kimeeeleza wazi kabisa namma mabadiliko ya mkataba yanavyopashwa kuwa .
150(3) inazungumzia katibu mkuu wa jumuiya kupokea pendekezo toka kwa nchi mwanachama,ambapo ndani ya siku 30 baada ya kupata pendekezo husika anatakiwa kupeleka kwa nchi wanachama .
150(4) inasema kwamba nchi mwanachama anayetaka kutoa mapendekezo yake kuhusiana na mabadiliko husika anatakiwa kufanya hivyo ndani ya siku tisini toka alipopewa proposal toka kwa katibu mkuu ( Dhana ya kuweka siku tisini ni kuziwezesha nchi wanachama kuwasiliana na wadau kama mkataba unavyotaka- hii ni kwa kufahamu kwamba Jumuiya ya Afrika Mashariki si ya Marais , Mawaziri na wataalam wao bali ni ya watanzania wote).
150(4) inaeleza kwamba siku zilizotajwa hapo juu( yaani siku 90) zitakapokwisha katibu mkuu anatakiwa alipeleke suala husika Summit ( Kikao cha Marais) kupitia baraza la mawaziri ( Council).
Kilichofanywa na Marais wetu, ni wao kukutana , wakiwahusisha wataalam wao i.e Wanasheria wakuu wa kila nchi pamoja na mawaziri na kufanya kile walichokifanya ndani ya siku saba! Kinyume kabisa na mkataba. Kama ilivyo ada na kama ambavyo itakuwa kwenye fast tracking suala likaletwa bungeni, likapita pamoja na mapugufu yake! Inasikitisha zaidi unapokuta wabunge wa chama tawala baada ya kuelemishwa kukubaliana na ukweli kwamba Marais wamevunja mkataba- lakini wanabariki kwa kusema kwamba hatuwezi kumwaibisha Rais kwa kuupinga!
Sasa tuje kwenye maudhui yenyewe ya mkataba.
Mkataba husika umekuja na mabadiliko ambayo yanaonyesha ni kwa jinsi gain jaji wa mahakama anaweza kuondolewa . Katika hali ile ile ya kutaka kuwa na majaji mamluki mkataba husika umeweka wazi kwamba pamoja na mambo mengine jaji anaweza ondolewa kutokana na sababu yoyote ( haijaelezwa sababu yoyote ni kitu gain!)Kipengele hiki cha 26 kinaondoa kabisa dhana ya uhuru wa mahakama kinyume hata na Ibara 110A ya katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ibara 110A ( mabadilko ya 2005-sheria namba 1)majaji wamepewa kinga ya ajira ( security of tenure).Ibara hii inaweka wazi jinsi majugde wanavyoweza kuondolewa i.e pamoja na kwamba Rais ndio anaowateua majudge hana mamlaka yoyote ya kuwaondoa. Na kwamba kama kukiwa na tuhuma zozote zinazomuhusu judge itaundwa tume maalum ambayo nsu ya majaji wake watatoka jumuiya madola na uamuzi wa tume hiyo dhidi ya tuhuma husika ndio utakuwa wa mwisho hata kama Rais atakuwa alipendekeza vinginevyo. Dhumuni kubwa la kuweka kinga kwa majaji ni kuwawezesha kufanya kazi yao ya utoaji haki pasipo kuwa na woga wowote wa kufukuzwa kazi. Cha kushangaza kipengele cha 26 cha Mkataba husika kimeipoka kinga hiyo ya majaji wetu. Mbali na kwamba jaji anaweza ondolewa kwa sababu yoyote , pia kuondolewa kwake kutabarikiwa na adhoc tribunal itakayochaguliwa na summit(Marais )-hakuna wajumbe wengine zaidi ya watu watakaochaguliwa na marais- katika hali kama hii unategemea mahakama ya Jumuiya itakuwa na meno ya kuamua vitu kwa haki huku ikifahamu kwamba wanaweza kupoteza kibarua chao wakti wowote?.........Mpo mandugu? Tutaonana nikiendelea na uchambuzi wa Bunge na Baraza la mawaziri!
SH