East African Federation (EAF) public Views

East African Federation (EAF) public Views

JUMUIYA YA AFRIKA MA ARIKI- TUKO TAYARI?

Kuna msemo wa Kiswahili usemao mwenda pole hajikwai……hata akijikwaa haumii..hata akiumia ni kidogo sana..

Msemo huu unaendana sambamba na nia yetu ya kuanza utekelezaji wa kile kinachoitwa jumuiya ya afrika mashariki ,mchakato ambao umeenda sambaba na kuundwa kwa kamisheni kwa ajili ya kukusanya maoni kuhusiana na shirikisho husika….

Leo katika maandiko yangu machache nataka kuzungumzia kitu kinachoitwa EAC- Fast tracking…..Nadhani ndugu zangu mnanipata ninavyosema fast tracking , si mnafahamu hata pale muhimbili kuna hiyo kitu……maana yake fasta fasta..Yaani kama una vijisenti vyako na hutaki kupanga foleni kutibiwa unazitoa na unapata huduma chap chap bila usumbufu wowote.

Tofauti na afya ya mwanadamu ambapo huduma ya haraka haraka inaweza kuwa na matokeo mazuri…..katika masuala yanayohusu maslahi ya nchi, mambo yanavyofanywa haraka haraka yanaweza kuwa na madhara makubwa sana …

Kimsingi sipingi hata kidogo uanzishwaji wa jumuiya husika …Nafahamu fika kwamba kama nchi zote zitakuwa na dhamira ya kweli, jumuiya ya afrika mashariki itakuwa fursa ya kukuza soko la bidhaa na huduma mbali mbali .Jambo la msingi ambalo napenda kujihoji ni kama tumejiandaa vya kutoshwa kuweza kukirejesha kile kilichotushinda mwaka 1977 mpaka kupelekea kuvunjika kwa jumuiya au tumeamua kuingia kichwa kichwa ?

Ukiangalia kwenye utangulizi (Preamble) wa mkataba wa Afrika Mashariki, paragraph ya nne imeeelezea sababu zilizopelekea kuvunjika kwa jumuiya.

Sababu hizo ni :
i)Kutokuwa na dhamira ya dhati ya kisiasa
ii)Kutokuwa na ushiriki mkubwa wa sekta binafsi na mashirika ya kijamii
iii)Mgawanyo usio sawa wa pato la jumuiya kati ya mataifa kutokana na
kuwa na tofauti kubwa ya kiuchumi
iv) Kutokuwa na sera mahsusi za jumuiya

Hivi ni kweli tumeshayajadili haya mapungufu kwa mapana na kuyatafutia tiba?
Hivi ni kweli tuna dhamira ya kisiasa kufanya hivyo? Dhamira hiyo ya kisiasa ni ya nani? Ya viongozi wa ngazi za juu pekee au imetokana na majadiliano ya nguvu na kisha kufikiwa muafaka baina ya viongozi wa nchi husika na makundi mbali mbali ya kijamii yanayojumuisha viongozi wa dini, asasi za kijamii na viongozi wa kisiasa katika ngazi zote mpaka ngazi ya kijiji?.

Hivi ni kwa kiasi gani tatizo la sekta binafsi na mashirika ya kijamii yamehusikwa katika mchakato huu?

Ni kweli kwamba yale yaliyotusambaratisha , hasa hasa linalohusiana na mgawanyo wa mapato baina ya nchi hizi kutokana na kuwa na tofauti kuwa ya kiuchumi tumeyaaddress vya kutosha kuweza kutojirudua tena ikizingatiwa kwamba watanzania tumeachwa mbali sana na wenzetu hasa hasa Kenya, katika nyanja ya uchumi na elimu? Ni hivi majuzi tu nilikuwa napitia gazeti moja la biashara. Moja ya kitu ambacho kilinishtua sana ni pale niliposoma taarifa inayoonyesha kwamba katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita Kenya imefanya biashara ya thamani ya US $ milioni zaidi ya 500 (Bilioni 500) kwa nchi za Tanzania na Uganda wakati Uganda na Tanzania kwa ujumla wake wamefanya biashara na kenya yenye thamani ya US$ milioni 100 (Shilingi bilioni 100..)na ushehe.

Ikumbukwe kwamba haya yote yamefanyika wakati milango ya kibishara bado haijafunguliwa? Tumejiandaa kiasi kwa hili? Tusije tukajikuta tunakuwa walalamikaji tu!

Hivi ni kweli tunazo sera za kutosha?Kama zipo nani anayezifahamu? Na nani anayetakiwa kuzitekeleza? Kwa kautafiti kadogo nilikokafanya wakati nikifuatilia kamati ya kukusanya maoni ilivyokuwa ikipita kukusanya maoni kuanzia kwenye level za viongozi mpaka wananchi wa kawaida….ufahamu wao kuhusu jumuiya husika ni mdogo sana au haupo kabisa… wengi wanaonekana kushangaa………

Taarifa zilizopo zinaeleza kwamba sample ambayo itatumika kwa ajili ya kujua kama fast track ianze ama la ni watanzania 15,000 …Hivi kwa mtu mwenye akili timamu anaweza kuchukua maamuzi ya watu 15,000 kuwa maamuzi ya watu Mil 37? Hali inazidi usikitisha ni pale wengi wa watu wanaohojiwa ni viongozi wa kisiasa yaani madiwani nk. Kutokana na hali hii ku a hatari maamuzi yakafanyika kwa kuangalia unterest za chama zaidi kuliko utaifa..

Katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania……………………..

Ni kweli kwamba hivi vyombo vilivyoundwa kwa ajili ya kufanikisha uwepo wa Jumuiya vina nguvu za kutosha kuweza kuhimili mikikimikiki.

Nilipokuwa darasani nilifundishwa kwamba katika utawala wowote ili mambo yaende kwa ufasawa lazima kuwe na mgawanyo wa madaraka (separation of power) baina ya vyombo vikuu vitatu ( mahakana , bunge na serikali ) ili kila kimoja kiweze kumkemea mwenzake pale anapozidisha /anapovuka mipaka ya kazi yake, wenyewe wanaita checks anda balance.

Naomba kuanza na Mahakama :
Mahakama ni mhimili wa muhimu sana wa utawala wowote ule ulio makuni, kwani ni hapa ambapo mtu yeyote ambaye anaona hakutendewa haki na vyombo vyovyote vya utawala anaweza kwenda kudai haki yake na kuipata -hivi karibuni bunge la jamuhuri ya muungano lilipitisha mabadiliko ya Mkataba wa Afrika mashariki. Ikiwa imeshinikizwa na Rais Kibaki wa Kenya aliyekasirishwa sana na kitendo cha mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kusita kuwaapisha wabunge aliowataka yeye( ambao hawakuwa chaguo la wakenya) ambaye pamoja na mambo mengine alitishia kurudi nyumbani kuwaapisha wabunge wake- kuliko endana sambamba na kufungua kesi mahakama ya Afrika Mashariki kuwataka majudge wakenya ( waliopo kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki ) wasiwepo katika jopo litakalosikiliza kesi ya kupingwa kuapishwa kesi ambayo serikali ya Kenya ilishindwa .
Kufuatia mashinikizo hayo, na hofu ya kuwa na chombo cha mahakama kilicho huru na chenye nguvu viongozi wetu hawa walikuja na kile kitu kinachoitwa mahakama ya rufaa .

Ni muhimu ikaeleweka kwamba hakuna mtu yeyote makini atakayepinga kuanzishwa kwa Mahakama ya Rufaa, tatizo ni ukiukwaji mkubwa wa sheria na taratibu na Mkataba ambao uliofanywa na Marais wetu. Ni jambo la hatari sana unapokuta viongozi wakuu wa nchi wakiuvunja mkataba na kusimama kidete kutetea ukiukwaji huo wa taratibu.

Ibara ya 150 ya Mkataba wa Afrika Mashariki unazungumzia Marekebisho ya Mkataba . Kipengele husika kimeeeleza wazi kabisa namma mabadiliko ya mkataba yanavyopashwa kuwa .
150(3) inazungumzia katibu mkuu wa jumuiya kupokea pendekezo toka kwa nchi mwanachama,ambapo ndani ya siku 30 baada ya kupata pendekezo husika anatakiwa kupeleka kwa nchi wanachama .
150(4) inasema kwamba nchi mwanachama anayetaka kutoa mapendekezo yake kuhusiana na mabadiliko husika anatakiwa kufanya hivyo ndani ya siku tisini toka alipopewa proposal toka kwa katibu mkuu ( Dhana ya kuweka siku tisini ni kuziwezesha nchi wanachama kuwasiliana na wadau kama mkataba unavyotaka- hii ni kwa kufahamu kwamba Jumuiya ya Afrika Mashariki si ya Marais , Mawaziri na wataalam wao bali ni ya watanzania wote).
150(4) inaeleza kwamba siku zilizotajwa hapo juu( yaani siku 90) zitakapokwisha katibu mkuu anatakiwa alipeleke suala husika Summit ( Kikao cha Marais) kupitia baraza la mawaziri ( Council).
Kilichofanywa na Marais wetu, ni wao kukutana , wakiwahusisha wataalam wao i.e Wanasheria wakuu wa kila nchi pamoja na mawaziri na kufanya kile walichokifanya ndani ya siku saba! Kinyume kabisa na mkataba. Kama ilivyo ada na kama ambavyo itakuwa kwenye fast tracking suala likaletwa bungeni, likapita pamoja na mapugufu yake! Inasikitisha zaidi unapokuta wabunge wa chama tawala baada ya kuelemishwa kukubaliana na ukweli kwamba Marais wamevunja mkataba- lakini wanabariki kwa kusema kwamba hatuwezi kumwaibisha Rais kwa kuupinga!


Sasa tuje kwenye maudhui yenyewe ya mkataba.

Mkataba husika umekuja na mabadiliko ambayo yanaonyesha ni kwa jinsi gain jaji wa mahakama anaweza kuondolewa . Katika hali ile ile ya kutaka kuwa na majaji mamluki mkataba husika umeweka wazi kwamba pamoja na mambo mengine jaji anaweza ondolewa kutokana na sababu yoyote ( haijaelezwa sababu yoyote ni kitu gain!)Kipengele hiki cha 26 kinaondoa kabisa dhana ya uhuru wa mahakama kinyume hata na Ibara 110A ya katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ibara 110A ( mabadilko ya 2005-sheria namba 1)majaji wamepewa kinga ya ajira ( security of tenure).Ibara hii inaweka wazi jinsi majugde wanavyoweza kuondolewa i.e pamoja na kwamba Rais ndio anaowateua majudge hana mamlaka yoyote ya kuwaondoa. Na kwamba kama kukiwa na tuhuma zozote zinazomuhusu judge itaundwa tume maalum ambayo nsu ya majaji wake watatoka jumuiya madola na uamuzi wa tume hiyo dhidi ya tuhuma husika ndio utakuwa wa mwisho hata kama Rais atakuwa alipendekeza vinginevyo. Dhumuni kubwa la kuweka kinga kwa majaji ni kuwawezesha kufanya kazi yao ya utoaji haki pasipo kuwa na woga wowote wa kufukuzwa kazi. Cha kushangaza kipengele cha 26 cha Mkataba husika kimeipoka kinga hiyo ya majaji wetu. Mbali na kwamba jaji anaweza ondolewa kwa sababu yoyote , pia kuondolewa kwake kutabarikiwa na adhoc tribunal itakayochaguliwa na summit(Marais )-hakuna wajumbe wengine zaidi ya watu watakaochaguliwa na marais- katika hali kama hii unategemea mahakama ya Jumuiya itakuwa na meno ya kuamua vitu kwa haki huku ikifahamu kwamba wanaweza kupoteza kibarua chao wakti wowote?.........Mpo mandugu? Tutaonana nikiendelea na uchambuzi wa Bunge na Baraza la mawaziri!

SH
 
Ndugu Mwapachu afafanua kuhusu Federation.Ni vizuri watu kuambiwa kinaga naga kwa vile serikali haisemi ukweli.Inaelekea tunacheza mchezo wa mwajificho.
::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::
Fast-tracking federation wrong idea-Mwapachu

2007-05-11 09:50:29
By Judica Tarimo
The EAC Secretary General, Ambassador Juma Mwapachu, has criticized the idea of fast-tracking the East African Federation and timeframe as indicated in the Wako Report.

``It seems that people are completely confused. What we are currently doing is not fast-tracking the East African Federation. We are fast-tracking a process towards the federation,`` said Mwapachu. He was speaking during the 50th European Union Anniversary held in Dar es Salaam yesterday.

The Wako Committee was formed by EAC heads of state to collect public opinion across the region on the integration processes including the federation and make recommendations. The committee was chaired by Kenyan Attorney General Amos Wako.

In their report, the Commission recommended the fast-tracking of East African Federation and put 2013 as timeframe for a full-swing federation.

``I want people to understand these things. We are actually fast-tracking the building of blocs customs union, common market, monetary union towards the federation,`` he added.

He said Wako Commission`s recommendations on fast tracking the East African Federation and the suggested 2013 timeframe were not only wrong, but also went against terms of references given by the heads of states of Kenya, Uganda and Tanzania.

``What the Wako Committee recommended was contrary to the idea of the heads of state. In fact, the committee came up with a different thing out of the terms of reference,`` he said.

``Even the recommended 2013 as timeframe for a full-swing federation was wrong,`` said a vividly upset Mwapachu.
He explained that main idea was to fast-track the building blocs customs union, common market, monetary union, and ultimately, the East African Federation.

``Time for a full-swing federation may take years. That is something that cannot be decided now. The 2013 timetable was not supposed to be there as indicated in the Wako Report,`` said Mwapachu.

The Chairman of the National Committee tasked to collect public views on the proposed fast-tracking of the East African Federation, Prof. Samwel Wangwe, seconded Mwapachu?s argument, saying the report fueled wrong public perceptions about the federation.

``Even the title of the report reads: ?Report on the fast-tracking of the East African Federation.`` The current problems and controversial debates started from the title of this report,`` he said.

``People find it difficult to differentiate between a process towards federation and the East African Federation,`` said Wangwe.

He recommended extensive public education to people of the region on the differences between process and the federation.

IPP Executive Chairman Reginald Mengi appealed to East Africans and actors to look at the on-going integration processes as steps towards federation.

``Planning is important before we move to the federation. However, before we reach that destination, we have to plan,`` he said.
``Deliberate efforts by partner states are needed to know each other.

We have to extensively sensitize and educate our people on integration processes. People are complaining because they have little knowledge on regional integration processes,`` said Mengi.
· SOURCE: GUARDIAN
 
Dr. Khamis,

Ndugu yangu mimi nilimsikia na kumuona balozi Mwapachu anavyoelezea hilo na nikajawa sana na furaha. Tumefumbuliwa macho juu ya ulaghai mkubwa ambao ripoti ya Wako ilitumika kufanikisha malengo ya Kenya. Sasa mambo yameanza kuonekana wazi, watu wanataka haraka haraka tuingie tugombanie kama ilivyokuwa 1977. Hongera Mwapachu kwa kuwa na ujasiri kueleza ukweli halisi ili mambo yasiende kinyemela. Shirikisho lisifikiwe bila upigaji kura kwa wananchi wote ili waamue hatima yao.

Jambo linalonikera kwa sasa ni kwa Watanzania kubandikwa bango la "waoga"! Hivi mtu anayechukua tahadhari kwa jambo nyeti kama hili ni muoga? kama kuna kasoro tutazidi kuonyesha wasiwasi mpaka mambo yawekwe sawa.

Yaani Wako anataka niwe mTAKEU, mKEUTA au mUKETA 2013 bila ridhaa yangu!!! Hapana..uTanganyika uliniponyoka lakini u Tanzania nitaupigania mpaka nipate sababu ya kuubadili.

TzPride..Tzpride........ forever ever.... Amen.
 
Angalau kelele tunazopiga zinaanza kuonyesha matunda. Kuna watu ambao walikuwa wanapotosha ukweli wa mambo. Hata vyombo vya habari baada ya wiki mbili zilizopita walikaripiwa na vibaraka wao wakaanza kupiga madebe bila mpango. Kuna watu waliisha jipanga ati nani awe rais na baada ya hapo nani afuate hii ni hatari kubwa na ni lazima huu mzizi wa fitna umalizwe. Wanakomba pesa za walalahoi bila sababu yeyote. Badala ya kuweka nguvu sehemu nyingine wamezuka watu kutaka kupotosha kule tunakoelekea walidiriki hata kusema the deal is signed and sealed, GIVE ME A BREAK!

Huu ni ujinga na Wabunge lazima waamke zaidi. Hongera kwa Balozi Mwapachu kwa kusema kile ambacho wengi ni waoga. FACTS
 
Nimeiona hiyo kwenye Gazeti la Waafrika litolewalo huko Minnesota na IOWA kwa yeyote anayetaka kuisoma habari hiyo aangalie kwenye website ya Gazeti la Mshale!.Kwa wale waliopo huko ni event nzuri hiyo ili kupata mawazo tofauti kuhusu Federation.

Kenyans, Tanzanians and Ugandans in Minnesota to Share Views on the East Africa Political Federation, May 13 @ 1:00 PM

From Left: Dr. Ahmed Samatar, Dean of International Studies
at Macalester College (Kofi Annan's Alma Mater), Jackie Abebe of Umoja Society, Joash Maangi of Kenya Community in Minnesota and Izooba Mugabi of Ugandan Association in Minnesota


Plans for a political federation comprising the three East African nations of Kenya, Uganda and Tanzania are at an advanced stage. The march towards a federation is on a "Fast Track". In existence already is Customs Union and work is in progress for a single market.

There is also the expected admission of Rwanda and Burundi into the union and according to Beatrice Kiraso of the EAC Secretariat, Rwanda will be officially admitted with full voting rights on June 18. She spoke in Nairobi this week during the East Africa media awards.

The respective associations of Kenya, Uganda and Tanzania in Minnesota is hosting a listening session next Sunday, May 13 to allow their national s here to express their views which will be compiled and forwarded to the heads of state summit in Arusha this summer. Dr. Ahmed Samatar, Dean of International Studies at Macalester College in Saint Paul will be the featured speaker.

Similar listening sessions are taking place around the United States and are being spearheaded by the East African Cooperation Forum in Hudson , New Hampshire and the Atlanta based East Africa America Business Council.
 
Mimi kama Mtanzania ,nina haki ya kikatiba kusema kwamba kwa matatizo tuliyo kua nayo kwa sasa kiuchumi,kisiasa na kijamii hatuko tayari kujiunga na jumiia hiyo.

Mbali na Nini Mwapacha anaweza kuwa amekisema tuna paswa tujue kama wananchi kwanini hatupaswi kufanya makosa yaliyo kwisha fanywa nyuma.

Baadhi tu ya maswali ambayo razima tuji ulize Je, serikali yetu imeweza kutotesheleza na
au kufikia robo tu ya yale amboyo ita tubidi to share na wenzetu wa kenya na Uganda?Je tunayo elimu ya kutosha kushindana na wenzetu kwenye soko hilo linaloitwa la ajira?

Na je, viongozi wetu wako tayari na wataweza kuwakirisha vyema maslai yetu watanzania au watafanya yale wanayo yafanya sasa kuweka maslai binafsi kwanza?

Yapaswa tujue vipi jumui itatuathiri positively na negetively kisha tulinganishe lipi tunataka.
Sio leo kwenye michezo ya kuigiza kwenye TV au baada ya taarifa ya habari wanatuwekea tuchague mwimbo wa Jumuia,Hapana jumia haiundwi kwa nyimbo nzuri au biashara ya vitenge au khanga.

Kutoka jumuia yakwanza kuvunjika mambo mangapi nchi yetu ime achieve kama pekee yake? ni mengi sana na je tutaweza kufikia nusu ya yale yaliyofikiwa kwa miaka mingapi baada ya kujiunga na jumuia?
 
The unlikely supprit from a malicious, irrascible and irrational lonely old fool

We celebrated at EAC collapse, says Njonjo


By Martin Mutua

Former Attorney General, Mr Charles Njonjo has for the first time spoken publicly about the collapse of the East African Community in 1977, saying he had no regrets.

Njonjo, who was then the chief Government legal adviser said he and "other people who were currently in Government" tossed champagne to celebrate the collapse of EAC."I celebrated with quite a number of people whom I don’t want to name and we tossed champagne because we believed the community was not helping our people," he added.

The former A-G criticised the creation of an EAC flag as well as composition of an anthem describing them as presumptuous. He added that Kenyans did not support the federation. Njonjo said if he was the A-G today he would still advise against Kenya getting into the East African political federation, adding that it could take another 50 years before the country was ready for such a move.

Njonjo, however, declined to name the people with whom he tossed the champagne and are currently in Government saying they no longer shared his views. "Those people now do not share my views," added Njonjo but declined to explain. He spoke when he met the National Consultative Committee on Fast-Tracking of the East African Federation at their Cooperative House offices in Nairobi, on Wednesday. Mr Njuguna Ngunjiri chairs the committee.

Njonjo said there was no one in their right senses who would want to enter into a federation that could not help their people, adding that structures were lacking for it. Njonjo said the country was still reeling with myriad problems top of which was tribalism, which the Government needed to sort out before engaging in such a move.

"We must first put our house in order by improving the lives of our people and ensuring they are economically empowered before we think of joining others," he added. He said it was the duty of the Government to ensure that those who are paid peanuts got their wage bill improved before joining them with other people whom they did not yet know.

He further said the country was in dire need of reorganisation in terms of infrastructure, education, health and the need to stem tribalism, which he said is foreign to the younger generation. "I vehemently believe in the sovereignty of a nation and Kenya is a sovereign State, which we fought for and to surrender it to another organisation is something I feel painful about," he added.

Even Britain, Njonjo said, valued its pound and would not let it go after having joined the European Union where the Euro is the currency."I value my shilling just the same way the British value their pound and I would not like to see it go," he added.


http://www.eastandard.net/hm_news/news.php?articleid=1143968698
 
For those in dar, there should be a Pan Africanism & the East African Federation at UDSM. Keep us posted of issues raised.

The title of t panel discussion is Pan Africanism & the East African Federation: Venue: Theatre 2; Time: 4-6pm; Thursday 17th May 2007

Chair is: Dr.Martha Qorro

The panelists are: Prof.Issa G.Shivji
Prof. Mwesiga Baregu
Dr.Adolp
 
Wako wapi waandishi,chukueni issues kama hizi wapelekeeni wasio weza kuziona kwa lugha waliyo zoea ili waache kuburuzwa na utawala.
Wajue kwamba hata wenzetu hawataki.
 
Hey guys. Mnaogopea nini Wakenya? kwani hamuamini elimu yenu. Hamjiamini binafsi? Niambieni uoga wenu? Cha kuogopa hapa sioni. Watanzania mnajifanya kama watoto kwa kupiga kelele kila siku juu ya uundaji ya Afrika mashariki. Hakuna chenye Kenyan inacho ambacho Tanzania haina. Ukabila iko Tanzania na ni vile tu hawaingolei tu kwa sauti sasa mnaishi kwa dhana kwamba nyinyi hamna ukabila. Ujambazi wa Kagera, Arusha na Dar ni mbaya kushinda nairobi. Nairobi vibaka hawatumii msumali kuweka mkononi na kunyonga nao watu. Nimeuona tu tanzania. Watanzania badala ya kupiga kelele naombeni muache uzembe. Kuna uzembe ya kupita kiasi kwa wafanyikazi wengi wa Tanzania. Hivyo ndio unaona kama kuna kila aina cha Kijiwe kwenye sehemu nyingi ya Tanzania. Watu wanakunywa kahawa mchana kutwa.

Jamani mnaishi kwa uoga wa kivuli chenu.
 
Hey guys. Mnaogopea nini Wakenya?


Oh buddie, hakuna anayewaogopa wakenya HATA CHEMBE. Ukihisi mnaogopwa basi elewa si kuwa mnaogopwa bali mnataka mwogopwe! You have nothing special than Tanzania. Labda ukabila na hoja za nguvu. Watanzania si kama wanaogopa bali 'hawapendi' kuwa na umoja nanyi sababu hamweleweki ninyi. Tamaa kubwa sana ya ardhi, usanii mwingi katika elimu (kwa imani kuwa kiingereza ndio usomi - na kama ungekuwa usomi basi watoto wadogo wa UK ni wasomi kuliko wakenya kwakuwa wanaongea kiingereza full na chenye lafudhi nzuri kuliko chenu kilichochanganyika na ki-kikuyu, luo etc).

Mimi nakupenda sana Alai na nazimia kazi zako. Huwa siamini kama wewe R. Alai ni Mkenya; hebu waulize wazee asili yenu haswa... Utagundua wewe ni mtanzania kwa mbali na ndio maana unafanya mambo mengi mazuri SANA! I know you man.

kwani hamuamini elimu yenu. Hamjiamini binafsi? Niambieni uoga wenu? Cha kuogopa hapa sioni. Watanzania mnajifanya kama watoto kwa kupiga kelele kila siku juu ya uundaji ya Afrika mashariki. Hakuna chenye Kenyan inacho ambacho Tanzania haina.


Oh yeah, kama nilivyosema YOU HAVE NOTHING SPECIAL BUDDIE! Here you confirmed. Lakini sisi tuna something special; hapo ndipo tusipotaka kushirikiana na watu wanaodharau utu wetu. Hivi R. umewahi kufuatilia haswa kujua kama watanzania wanawaogopa wakenya au vp? Wa kuogopwa labda ni waganda ambao wanaenda kimyakimya. Uzuri wa wakenya ni kuwa mnajiamini hata kwenye makosa hivyo lazima kuwa na tahadhari na watu wa aina hiyo. Mtu anayejiamini kupitiliza tambua kuharibu ni rahisi sana na hata kujitamba juu ya kitu kisicho chake ni rahisi pia. Hope you got my point mate!

Ukabila iko Tanzania na ni vile tu hawaingolei tu kwa sauti sasa mnaishi kwa dhana kwamba nyinyi hamna ukabila. Ujambazi wa Kagera, Arusha na Dar ni mbaya kushinda nairobi. Nairobi vibaka hawatumii msumali kuweka mkononi na kunyonga nao watu. Nimeuona tu tanzania.


Hebu huko! Hivi una hakika watanzania wakabila kwa namna ulivyosema mzee? Ah, umekosea mzee! Ingekuwa hivyo tusingekuwa tunaoana bila vikwazo kama tufanyavyo. Tunaamini sote ni wamoja na huwa tuko tayari kumsaidia yeyote ambaye ana uhitaji na msaada wetu. Shukrani za watu wachache kama Wakenya (tena wengine waishio Tanzania bila vibali na tunawachunia tu) kuwa mateke hazituchanganyi. Jaribu kufuatilia na utaijua kweli na hiyo kweli itakuweka huru bro!

Watanzania badala ya kupiga kelele naombeni muache uzembe. Kuna uzembe ya kupita kiasi kwa wafanyikazi wengi wa Tanzania. Hivyo ndio unaona kama kuna kila aina cha Kijiwe kwenye sehemu nyingi ya Tanzania. Watu wanakunywa kahawa mchana kutwa.


Alai Alai Alai! Mimi nimeishi hapo Nai muda wa miaka kama 4 hivi. I know Kenyans bwana! Pia niliishi Kisumu, Mombasa nilikuwa naenda kwa muda mchache kibiashara, Naivasha kwa sana tu; na kwingineko. I know Kenyans bwana. Wewe usilichukulie kabila flani Tz kuwa ni wapenda kucheza mchezo wa bao ukadhania ni watanzania wote. Hiyo ni jadi yao na wana vyanzo vyao vya mapato. Uh, bro... Assuredly I tell you, sisi ni wakarimu SANA na tunachapa kazi SANA tu.

Matatizo ya kuwa na serikali ambayo haiwatimizii mahitaji wananchi wake si ya Tanzania pekee. Tatizo la watu kukaa au kuzurura ovyo lipo hapo Nai kwa sana tu.

Not only in Africa; even in US... The problem is there bro. Cha msingi ni kuzishauri serikali zetu ziwawezeshe wananchi wake. Kenya wananchi ni choka mbaya kuliko Tz. Serikali inaweza kuwa na vyanzo vingi vya mapato lakini raia wenu mzee nadhani binafsi unaweza kukiri kuwa NI CHOKA MBAYA SANA.

Jamani mnaishi kwa uoga wa kivuli chenu.


LABDA kama wewe wadhania hivyo; lakini hoja hujibiwa na hoja daima. Ninachotaka ni kukupa reality ya watanzania na mawazo yao. Watanzania nao wameathirika na imani ya kwamba kujua (tena sio kujua bali kuongea) ndio usomi. Hapo ndipo wanapokosea. Kosa hilo pia nililiona nikiwa hapo Nai; wengi wanakazania kuongea kama wamarekani ili waonekane Baab Kuba!

Alai, kwa pamoja tunaweza... Tunaweza kuuelimisha umma wa watu wa Afrika Mashariki kuwa ni yepi matatizo yao; yanaweza kutatuliwaje na kwa kuanza vipi. Imani za ninyi mko bora ama ninyi mmeelimika sana zifuteni vichwani mwenu. Watanzania wanachopinga ni UHARAKISHWAJI wa shirikisho. Hizo haraka ndizo zinawafanya wahisi kuna ka-mchezo kachafu kanaweza kutendeka maana wao huamini kuwa Pole pole ya kobe humfikisha mbali ati; na wengine wanaamini kuwa Haraka haraka haina baraka pia usisahau kwamba Tamaa mbele Mauti nyuma kwakuwa tamaa ya kuweza kuwa na soko la biashara la haraka zinaweza kututumbukia nyonga na tukajikuta tunajiuliza how did we reach there?

Brother; hope umenisoma na kama bado mimi nipo ajili yako tu.
 
Alai, kumbe uligusia UJAMBAZI WA KAGERA? Well well, umetoka kwa wanyarwanda na warundi.

Hatuwachukii warundi na vitendo vya wao kujishirikisha na masuala ya ujambazi. Ni ugumu wa maisha unaozikabili nchi nyingi za Afrika. Na kwakuwa Tanzania kuna neema wanaamua kuja kuiba huku kwa kutumia silaha ambazo kwao zinapatika kirahisi tu.

Fuatilia na utaujua ukweli. Nilitaka kukuelewesha juu ya hilo. Am always onlie and ready for a debate bro
 
Mimi nafikiri hawa jamaa wa Rwanda na Burundi nia yao ya kutaka kujiunga na EAC siyo nzuri. Wanataka kuitumia jumuiya kama ngao ya kukingia matatizo yao ya vita vya ukabila. Hivyo wakati wa mchakato ni vema pia wahusika wakaliona hili na kuangalia nchi hizi hizi COMMITED namna gani kuhakikisha matatizo yao yasije yakawa mzigo kwenye Jumuiya.
 
UN Refugee Agency Begins Assisting Resettlement of Citizens in US

UN News Service (New York)
NEWS
18 May 2007
Posted to the web 18 May 2007

With the assistance of the United Nations refugee agency, the first group of some 8,500 Burundians to be resettled in the United States today left a refugee camp in Tanzania, where they had taken refuge after fleeing mass violence 35 years ago.

The 88 who left today are part of 3,000 so-called '1972 Burundians' - about 35 per cent of the number accepted for resettlement - who are expected to leave over the next 15 weeks for Nairobi and then travel on to various US cities, such as Atlanta and Phoenix, according to Jennifer Pagonis, spokesperson for the UN High Commissioner for Refugees.

"The 1972 Burundians represent one of the world's most protracted refugee situations, and resettlement is the only viable durable solution for most of them," Ms. Pagonis said in Geneva.

Hundreds of thousands of Burundians fled to neighbouring countries that year to escape ethnic violence which killed an estimated 200,000 people, she said, adding that children of refugees born in exile were also considered for resettlement in the US.

"While repatriation of Burundian refugees remains a priority, we believe that successful repatriation and reintegration of this particular group is not possible," she commented. "After nearly 35 years in exile, they would face complex and unresolved land issues. Moreover, some refugees believe they are viewed as outsiders and would never be able to fully integrate in Burundi," she said.

She added that those born in exile identify closely with their host country, Tanzania, but it cannot offer them integration either. The resettlement operation is being organized by the US Government, the International Organization for Migration (IOM) and UNHCR. Before their departure from Nairobi, the refugees will undergo an orientation workshop organized by IOM.

This will help prepare them for a new life in the US and ease their integration, UNHCR said.

Tanzania still hosts some 276,000 refugees, mainly from Burundi and the Democratic Republic of the Congo.

Marekani wafanye hima kuja kuwachukua hawa wote waliobaki ili nasi tuendelee na mikati yetu ya kujikwamua na umasikini.
 
Kwa mimi ambaye nimefanya kazi kwenye makambi ya wakimbizi, naweza kusema kuwa hiki ni kiini macho. Kwa sababu idadi ambayo inatajwa hapo ni sehemu ndigo sana ya idadi ya wakimbizi wote nchini Tanzania. Leo hii Marekani inataka kuchukua wakimbizi 3000 tu, ikiwa kama mpango wa Umoja wa Mataifa wa kusaidia kuwalea hawa jamaa "Burden sharing in refugee protection". Lakini nchi ya Tanzania ikiachilia mbali hiyo idadi ya wakimbizi iliyotajwa hapo ambayo ni wakimbizi wanaishi mkoa wa Kagera (Ngara) na Kigoma (Kibondo, Kasulu na Kigoma vijijini) na wengi wao waliikimbia nchi yao miaka ya 90, pia kuna wakimbizi kutoka Burundi wapatao 150,000 wanaishi makambi ambayo yapo mkoa wa Rukwa (Mpanda), na wengine wapatao 60,000 wanaishi mkoa wa Tabora (Ulyankuru) ambao pia waliikimbia nchi yao miaka ya 70. Pia kuna wakimbizi kutoka Somalia wapatao 3,500 wanaishi mkoa wa Tanga (Handeni) hawa nasikia kwamba wanafanyiwa mpango wa kupewa uraia wa TZ. Sasa hebu chukua hiyo idadi iliyotajwa na UN pia ongoza hii niliyokuandikia ili uweze kuona USA kuchukua idadi hiyo ya wakimbizi kweli tunapata dhana ya "Burden sharing" Hiki ni kiini macho tu hakuna lolote.
 
`EU bloc no model for EAC integration`

2007-05-14 08:55:30
By Judica Tarimo

A top European Union official dismissed perceptions that regional integration in his area could serve as a model for the East African economic and political integration Community.

The head of delegation of the European Commission, Ambassador Frans Baan said last week in Dar es Salaam, that EU project is far from complete and that the implementation of full monetary union and agreement to European constitution continue to be elusive goals.

Ambassador Baan was speaking at a forum co-organised by the Dar es Salaam Institute of Technology and the EU to mark EUs 50th anniversary aimed at exchanging notes between the two blocs, in the wake of myths and perceptions amongst East Africans that EU might serve as a model for progressive and result-oriented EAC

`I am not revealing secrets if I admit that EU achievements made in the first fifty years came with uncertainties and hesitations and occasionally through painful arguments and recriminations` he said. Ambassador Baan said there are many things EU and East Africa Commuity could have done differently and some even better.

`I mention this to illustrate that there is nothing such as a model of good practice in political or economic integration,` he said

He said each EU member has its own ideas on the limits of widening and deepening the union. These ideas, he said, were not always openly stated. Baan quoted a recent statement by Belgium Prime Minister who said: `It is necessary for each EU member to come with their perception of how European integration must move forwardmasks must fall.`

EAC Secretary General, Ambassador Juma Mwapachu, said at the event that EAC served a model for the EU, as the latter learned a lot from the collapsed EAC.

`Unlike EU, we (EAC) have shared values in terms of language (Kiswahili), culture, and lifestyle etc. On top of that, there was effective participation of people in the course of establishing EAC,` said Mwapachu.

`Free movement of people in the EU is still nightmare,` said the secretary general.

The official appealed to East Africans to shun wrong perceptions on the EAC integration process in many contextsincluding enlargement programme, which seeks to embrace Rwanda and Burundi, which have been rocked in civil strives and ethnic-driven clashes.

`If we left out these people (Burundi and Rwanda), we will fuel more conflicts and political instabilities. The best approach is to embrace them to enhance durable peace and political stability,` said Mwapachu.

IPP Executive Chairman, Reginald Mengi, could not agree more with EAC boss when he said sidelining Rwanda and Burundi would not solve security-related problems in the region.

`It is easy to control problematic persons when you are close to them than when they are far. It is risky in terms of regional security to leave out Rwanda and Burundi. We have to accommodate them,` said Mengi.
SOURCE: Guardian
http://www.ippmedia.com/ipp/guardian/2007/05/14/90437.html

Free movement of people in EU is still a nightmare, there were some members who wanted us to believe that they use same passport to travel within EU.
 
Jamani mimi siungi mkono uharakishaji wa muungano wa Afrika Mashariki. Uharakishaji ulianzishwa na Moi, Mkapa na Museveni. Museveni anauendeleza hoja hii. Tena nasema kwamba kila saa watanzania wanaongelea Africa Mashariki, wanasema tu juu ya Wakenya. Uoga huu unatokana na hali ya uchumi ya Kenya ambayo ni bora kuliko nchi zote za africa mashariki. Elimu ya kenya ni bora kuliko nchi hizi zote. Ndio maana unapata kampuni nyingi nzuri kwenye eneo hili zinaendeshwa na wakenya.

Watanzania wangekuwa wazuri na kuendelea kushinda kila nchi kwenye shirikisho lakini viongozi wame tu-let down. Sasa Kikwete anadanganywa na washauri juu ya elimu. Ni nchi gani hapa duniani inategemea kuendelea kwa kupunguza msaada kwa vyuo na wasomi chuo kikuu. Tunapunguza loan kwa wanafunzi wa chuo kikuu wakati tunanunua silahaa za zamani Urusi na China. Tunatunmia hela nyngi kununua silaha na vifaa ambavyo havitatusaidia wakati wanafunzi wetu wanakosa elimu.

Jamani our priorities are wrong. Lets change for the better. Tunadhani shida zetu tutazitatua kwa kuendeleza shtuma dhidi ya Wakenya. Tujue kwamba kwenye shirikisho hili hakuna watu watanzania wanaweza kuishi nao vizuri na wamefanya nao mengi kama sio Wakenya. Wakenya ni kama Wandugu kwa Watanzania. Mpaka sasa hivi kuna Watanzania 5000 waliokimbia machafuko za kisiasa Zanzibar. Au Zanzibar sio Tanzania?

Tupinge hoja ya uharakishaji lakini tusilenge pasipofaa kwa sababu hivyo tunakosa hoja na tunapoteza wakati mwingi tungetumia kwa kuweka mswada mbali za kuboresha Shirikisho. Tutafute njia za kuziba shimo mbali mbali yanayoweza kufanya exploitation na inchi moja au nyingine ifanyike kwenye jumuiya.

Jamani tulenge hoja na tusaidie nchi yetu tunayoipenda.
 
Wanasheria wawashitaki Kikwete, Museveni, Kibaki

2007-05-21 08:39:10
Na Asraji Mvungi, PST Arusha


Chama cha Wanasheria wa Afrika Mashariki, kimefungua kesi katika mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, kikiwatuhumu wakuu wa nchi za Jumuiya hiyo kukiuka mkataba unaounda Jumuiya hiyo.

Wakuu wanaounda Jumuiya hiyo ni Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda, Mwai Kibaki wa Kenya na Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania. Nchi za Rwanda na Burundi zimeshakubaliwa kujiunga na Jumuiya hiyo lakini hazijawa wanachama rasmi.

Kesi hiyo imefunguliwa juzi katika Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na viongozi wa chama hicho.

Akizungumzia uamuzi huo wa kuwaburuza mahakamani viongozi wa nchi za Jumuiya hiyo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa chama hicho, Bw. Donald Deya, alisema uamuzi huo ulifikiwa katika mkutano wa wadau wa chama hicho uliofanyika juzi mjini hapa.

Alisema, baada ya kujadili kwa kina mwenendo mzima wa maamuzi yanayotolewa na viongozi wa Jumuiya hiyo ambayo yanakwenda kinyume na mkataba wa Jumuiya, waliona wafungue kesi hiyo kama hatua ya kuinusuru Jumuiya hiyo.

`Tumeona kuwa tuwahusishe wadau wetu, wakiwemo wasomi na walimu wa sheria, kuhusu suala hili baada ya kubaini kuwa kuna makosa yamefanyika na mkataba umekiukwa,` alisema Bw. Deya.

Aidha, alifafanua kuwa makosa yaliyofanywa na viongozi hao ni pamoja na kuamua kubadilisha baadhi ya vifungu vya sheria inayounda mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki bila kuwahusisha wadau, wakiwemo wananchi.

Walisema, wameona ni vyema kupinga hatua hiyo mapema kabla haijaleta madhara makubwa zaidi, hasa ikizingatiwa kwamba miongoni mwa vitu vilivyochangia kuvunjika kwa Jumuiya hiyo mwaka 1977 ni kukosekana kwa ushirikishwaji wa wadau katika maamuzi mbalimbali yakiwemo yanayowahusu wananchi.

`Tumeona ni vyema tusikae kimya hasa tukizingatia kwamba wananchi wote wa nchi za Jumuya hii wanahitaji msaada wetu wa kisheria na pia tukielewa kwamba kufumbia macho makosa ni kuiua Jumuiya, hivyo tumefungua kesi mahakamani ili kwa nia nzuri tu ya kujaribu kuinusuru Jumuiya hii kwa faida ya wananchi wa nchi hizi,` alisema Bw. Deya.

`Miongoni mwa mambo yaliyotiliwa mkazo katika mkataba na yanayozungumzwa kila siku ni pamoja na kuhakikisha Jumuiya ya Afrika Mashariki iwe ya wananchi wa Afrika Mashariki na wala isiwe ya viongozi na watu wachache wala ya vikundi vya watu na madhara ya kuwa na muundo wa aina hii yako wazi.

Hivyo ni vyema wananchi na wadau mbalimbali wakawa macho kuhakikisha sheria na makubaliano yaliyopo katika mkataba yanaheshimiwa kwa faida ya walio wengi ambao ni wananchi wa Afrika Mashariki,` alisema Bw. Deya.

Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyoundwa mwaka 1967 ilivunjika mwaka 1977 kutokana na sababu mbalimbali ambapo inadaiwa kuwa kilichochangia kwa kiasi kikubwa ni kukosekana kwa ushirikishwaji.

SOURCE: Nipashe

Let us see how the court will decide. It is a good sign
 
jumuiya ya afrika mashariki kwa sasa kwa watu km wabongo haina maana yyt so kwa kweli sisi wananchi hatutaki kabisa hili shirikisho la afrika mashariki kwani ni mizenguo 2
 
Jumuiya ina manufaa mengi kwa Watanzania kushinda chenye Wakenya watapata humu. Bisha nikupe points.
 
Back
Top Bottom