East African middle class

East African middle class

Mimi nadhani kitu kimoja kinacho changia slums kuongezeka Tanzania ni tabia ya kutoza kodi kuanzia miezi mitatu na zaidi. Na ni bora ingelikuwa mitatu, wapangishaji walio wengi wanataka mwaka au miezi sita. Hiyo, mtu anaye anza maisha inabidi aanzie kwenye nyumba za hali ya chini. Mtu anapaswa alipe kuanzia mwezi moja na deposit ya mwezi mmoja. Kuna miji watu wakiambiwa walipe kodi miezi miwili miliwi tu watu wote watarudi mashambani
 
Naipenda Tanzania nchi yangu niliyozaliwa. Lakini siko tayari kujidanganya kwa ujinga mwepesi...

Kwa anayebisha awe anaangalia Citzen TV taarifa za habari saa 3 usiku.. harafu chukua kituo chochote cha luninga hapa bongo kilicho bora/ namba wani ona habari zinazorushwa linganisha....

Kama mnavyoona Uchagani elimu ilivyowakomboa ukilinganisha na sehemu nyingine hapa tanzania ndiyo wakenya walivyokombolewa na elimu toka zamani kwenye miaka ya 6o...

Tukubali changamoto..tuchukue hatua sio kupinga...shule za kiwango cha kata hazitupeleki mbali. Boresha shule za Serikali zipatazo ka 100 kwa kiwango cha St Marian au Francis utapata matokeo katika kipindi cha miaka kumi tu. SULUHISHO NI ELIMU BORA= ANGUKO LA CCM
 
Wakuu mniruhusu niwaelimishe kidogo kuusu uchumi wa Kenya na Tanzania. Ukilinganisha utakuwa unakosea kwa sababu ni vitu viwili tofauti kabisa. Hivi vi economics havi-apply Tanzania na ni muhimu Kampuni zinazo ingia Tanzania zisitumie hivyo vi-economics vya middle class na upper class. Tanzania haina defined class system. Huwezi kusema huyu ni middle au ni low class hata bilionares wengine Tanzania wanavyo ishi utasema ni low class lakini ni very high class. Kenya kuna ubaguzi wa class, Tanzania hamna. Watu wanajinchanganya. Nitoe mifano uchumi ulivyo tofauti. Kenya asilimia kubwa sana ya magari unayo yaona barabarani say 80% of all new registrations ni ya mikopo. Nyumba za kuishi zinazo nunuliwa kenya 80% zina mikopo. Tanzania is the opposite. Asilimia 90% ya new registration vehicles zimenunuliwa cash. Nyumba 99% residential zimejengwa au kununuliwa cash. Hii imetokana na kuwa Benki za Tanzania zimeanza kutoa hii mikopo hivi majuzi, Mtanzania alikuwa hana kitu kinaitwa loan. Masikini ndio walikuwa wanakopa kwenye micro finance institutions, vicoba, saccos nk. Tuingie kwenye baa sasa tukanywe bia. Utapata bar za matajiri na za middle class na za masikini, Kenya. Tanzania utapata groceries na huko wamechanganyika masikini na tajiri, na ukiingia zile zingeitwa high class bars unapata wageni ndio wengi. Kenya kuna mitaa ya matajiri na ya masikini tofauti. Tanzania isipokuwa mitaa miwili au mitatu watu ni mchanganyiko. Tajiri anajenga jumba lake kati ya masikini na vice versa. Unajenga kadri na uwezo wako. Aliye kuwa nacho utampata anaishi next na mwenye Kidogo. Sasa sielewi kwa hali hii nani ndiye middle kuliko mwingine. Unapata huyo middle class wa Kenya ana car loan, house loan, furniture loan na inewezekana emergency loan, kitu ambacho Tanzania hakipo vizuri na buying power lazima itatofautiana sana kwa ajili yule anaye exist on loans anakuwa na uwezo wa kujinunulia luxuries zaidi na kuwa na spending money. Pia utapata Mkenya wa middle class ni wasteful kati ka budget yake ana uwezo wa kununua kitu ambacho hakihitaji. Kwa sababu hii unapata makampuni yakiingia Tanzania na mentality ya Kenyan economy yanayumba sana. Middle class ya Kenya inaangalia kuonekana kuwa na class nanichoyo sana kwenye mahitaji ya extended families ambao utapata cousins, uncles, aunts sio ndugu bali ni relatives.. Ya tanzania ni ndugu na uwezi kumuachia shida to a very big extend. Hii ina affect sana spending power. Mkenya ata target kununua gari, music system nomaaaaaa, led TV ya hatari, makochi ya nguvu alafu ataanza kufikiria kuusu kununua au kujenga nyumba. Mtanzania atafikiria nyumba kabla ya mambo yote hayo kwa hiyo atatafuta kununua ploti na kujenga gheto yake hata kama sio nzuri ndio afikirie kuusu luxuries zingine. Hiyo ina sababishi mitaa kuonekana kama vile haipendezi sana ukulinganisha na kule estate developer atajenga nyumba nzuri uletewe on a plate, upewe mkopo wa kuinunua nk.Maisha yamtanzania ni tofauti na ya Mkenya na hizo tofauti naweza nikaendelea kuzizungumzia hadi kesho asubuhi na conclusion yangu ni kwamba lifestyle ya Tanzania haina defined class system. Nawakilisha
 
safi sana mkuu hapo juu, pia huwa nawadha, hivi kuke mitaa ya singida kule ambapo ndio nimekulia, kule huwa tunahitaji hela ya kwenda kusagia tu debe la ,mahindi au mtama, na mafuta ya taa kwa ajili ya koboroi tena unawasha wakati wa kutandika tu au kama kuna mwanafunzi anapigia book, LOL, maana msosi upo, mboga ipo, maana mifugo kibao maziwa nakadhalika, shopping labda mpka siku ya mnada au gulio, sasa kwa watu wanaojitosheleza hivi, na statistics za spending zao ni vigumu kupata ila hawa watu sio masikini, watu hawa huwa wanakua clasified vipi? maana nimetolea mfano kieneo kimoja , maeneo mengi TZ bado ni vijiji na hizi statistics za spending , CPI, sijui hata wanapimaje,
 
Sipingi kuwa Kenya kuna middle income class kubwa kuliko TZ that's is the fact,Lakini hizo takwimu hapo juu zinafikirisha sana kama mkuu Chash alivyonena hapo juu Lifestyle ya TZ is a bit complicated na kama income & Expenditure pattens pekee ndo kigezo cha kudefine hizo class utamdefine vp mtu ambaye income yake ni kubwa lakini hawezi kuishi maisha kama middle income earner kwasababu ya mzigo mkubwa wa dependents aliokuwa nao? watoto wa Mjomba,wa Shangazi,baba mdogo,ndugu wa Mke,wanao wote hao wanakutegemea wewe utaweza kweli kwenda hata shoprite kufanya shopping? utaweza kuafford kuwa na gari au kuishi kwenye nyumba nzuri?
 
Sipingi kuwa Kenya kuna middle income class kubwa kuliko TZ that's is the fact,Lakini hizo takwimu hapo juu zinafikirisha sana kama mkuu Chash alivyonena hapo juu Lifestyle ya TZ is a bit complicated na kama income & Expenditure pattens pekee ndo kigezo cha kudefine hizo class utamdefine vp mtu ambaye income yake ni kubwa lakini hawezi kuishi maisha kama middle income earner kwasababu ya mzigo mkubwa wa dependents aliokuwa nao? watoto wa Mjomba,wa Shangazi,baba mdogo,ndugu wa Mke,wanao wote hao wanakutegemea wewe utaweza kweli kwenda hata shoprite kufanya shopping? utaweza kuafford kuwa na gari au kuishi kwenye nyumba nzuri?

Kweli Mkuu. Mambo haya ni magumu kuelewesha economists wa nje, kwa hiyo watakaa ku mis -advise investors wanao ingia Tanzania.
 
Takwimu za uongo hizo wamezichukulia wapi? Middle class wanatumia dola ngapi kwa siku? Mkumbuke wazungu siku zote watapalilia Kenya, SA et al kwa sababu wamejaza mirija yao huko. Hiyo ADB yenyewe inafadhiliwa na nani? Mtumikie kafiri upate mradi wako.
 
Back
Top Bottom