East African Presidents turning states into Political chaos!

East African Presidents turning states into Political chaos!

Ninahisi hujitendei haki wewe mwenyewe katika nafsi yako, ama kwa sababu huwa huna muda wa kufikiria kwa undani au huna uwezo wa kufanya hivyo, tuanze na hili la kutofuata katiba, kwa kiwango kikubwa sana Magufuli anafuata katiba ya nchi, kama ni marks ningempa 85%, hizi 15% anazikosa kwa sababu ya kubana vyama vya siasa na uhuru wa habari.
Katika maisha yako ushawahi isoma KATIBA, ama unaufahamu wowote wa sheria za KIKATIBA?
Kwa taarifa yako, katika serikali yeyote ile chini ya JUA ama jambo lolote linalo husu maslahi ya UMMA tambua UMMA huo una HAKI YA KUPATA TAARIFA ya JAMBO HUSIKA! Kinyume chake unakuwa umekiuka misingi ya KIKATIBA-Umevunja Katiba, na ukienda kinyume na KATIBA ndio udikteta wenyewe.

Mfano: Ibara ya 4(2) ya Katiba ya JMT inasema Bunge na Baraza la Wawakilishi vitakuwa vyombo ya kutunga sheria. Lakini leo hii tunaona kauli ya Magufuli ya kusema mikutano ya kisiasa isubiri 2020 imekuwa sheria! Huyu mtu kakiuka KATIBA -DIKTETA.

Katiba hii hii inasema wakati Serikali ikitekeleza majukumu yake, lazima ihakikishe UTU NA HAKI NYINGINEZO ZA BINADAMU ZINAHESHIMIWA NA KUTHAMINIWA - Vipi Wananchi wanaobomolewa makazi yao UTU NA HAKI ZAKE KAMA BINADAMU ZIMEZINGATIWA kama Katiba inavyotaka, wakati huo huo usisahau KATIBA hii inasema kazi ya Serikali ni USTAWI WA WANANCHI- huyu mwananchi aliyevunjiwa nyumba na kutopewa chochote na serikali KASTAWISHWA NINI?
Kwanini huyu bwana ako asiitwe DIKTETA?

Katiba inasema Serikali na vyombo vyake VYOTE VYA UMMA vinatoa nafasi zilizo sawa kwa raia wote, wake kwa waume, bila kujali rangi, kabila, dini au hali ya mtu - Rais wako kafukuza watu kwa kughushi vyeti, WaTZ wamedai Makonda achunguzwe kwani naye ni mmoja wa Watz walio ghushi vyeti Rais wako KAKATAA zaidi kamuomba Makonda apige kazi - Huu sio UDKTETA?
Kwahiyo ule USAWA MBELE YA SHERIA ULIO ZUNGUMZWA KWENYE KATIBA Uki kiukwa tunatakiwa kusemaje juu ya anayekiuka MISINGI YA KATIBA?


hii ni sawa na wewe na mimi pamoja na kwamba hatutekelezi yale yote yaliyomo katika dini zetu
Mkuu mimi similiki DINI wala siyo mfuasi wa hizo dini ulizo zitaja hapa.

Tatizo kubwa kwa nini Magufuli anaonekana kuwa dikteta, ni kwasababu amewabana wanasiasa, kwamba katika kipengele cha katiba ambacho yeye amekikeuka kinawagusa moja kwa moja wanasiasa.
Kufukuza watumishi walio ghushi vyeti na kumuacha Makonda kimewagusa wanasiasa tu?

Kutoa pesa ya Umma kufanya manunuzi pasipo kuidhinishwa na BUNGE - BAJETI, kinawagusa wanasiasa tu?

Ili mtu awe dikteta ni lazima awe hafuati katiba ya nchi,
Kwahiyo tunakubaliana kuwa Magufuli ni Dikteta baada ya kukuonyesha namna anavyoisigina KATIBA?
Magufuli anaifuata kwa kiwango kikubwa sana, dikteta anakuwa anahusika kwa mauaji ya kiholela kwa wapinzani na wanaharakati mbali mbali, Magufuli hajafikia huko, japo suala la Lisu na Ben limemtia doa.
Sawa KASUKU

Kuhusu kuwa mwanasiasa au hapana,
Mtu asiye Mwanasiasa ana weza kuwa Mwanachama na Kiongozi wa juu wa CHAMA CHA SIASA? hili linahitaji akili kubwa kidogo kulielewa,
Acha upumbavu ndugu yangu, akili gani kubwa inahitajika katika hili? Magufuli ni mwanasiasa kama wanasiasa wengine ujinga wa kusema Magufuli sio mwanasiasa ni mtendaji endeleeni kuihubiri huko kwenu MPWAPWA
inategemeana na tafsiri yako inatokea upande gani, hivi unaweza kumwita Magufuli ni driver kwa kuwa tu umemkuta siku hiyo anaendesha gari lake?, is he a driver or is driving?, sifa ya kuwa driver ni ipi?
AHSANTE KWA HILI SWALI LAKO, NAOMBA UNIPE SIFA ZA KUWA MWANACHAMA WA CHAMA CHA SIASA, ama naomba uniambie sifa za kuwa mwanachama cha chama ambacho Magufuli ni Mwanachama, pia naomba unisaidie sifa za kuwa Mwenyekiti wa chama ambacho Magufuli ni Mwenyekiti sambamba na hilo niambie sifa za mtu anayefaa kugombea nafasi ya rais wa JMT kwa mujibu wa KATIBA YETU YA 1977, je kila aliyepo nyuma ya usukani wa gari anaendesha ni dereva au kila dereva lazima aendeshe gari?[
Jibu lipo kwenye sentesi hapo juu/QUOTE]
 
Ningeweza kuendeleza huu mjadala kama ningegundua kwamba lengo lako ni majadiliano ili kupata maoni mbalimbali ambayo ni tofauti na yako, lakini inaonekana wewe ni mtu wa hovyo unaweka matusi na kuitana wapumbavu kwa sababu tu mtu ametoa maoni tofauti na wewe, kww hiyo nikujulishe kwamba wewe sio mstarabu, huna akili na ni mpumbavu mkubwa sanaa, wewe uliona wapi duniani watu wote wakawa na mawazo yanayofanana?, kwa hiyo kila mtu mwenye mawazo tofauti na wewe basi ni mpumbavu?, kwani baba yako siku zote anakuwa na mawazo yanayofanana na wewe, je na yeye pia ni mpumbavu?.. Nguruwe wewe kasoro mkia.
 
Ulichosema ni kweli.afrika viongozi wa serikali wanatamaa ya madaraka,nadhani wengi wao wanachangiwa na umasikini wa familia zao,kwahiyo wanataka waendelee kuwepo madarakani ili waendelee kuiba.
 
Back
Top Bottom