Niliwapenda sana hawa vijana (Mwana FA, GK, AY, Stanboy, Buff G, Zongo) na ilisikitisha wengi waliposambaratika. Ni ndoto kwa hili kundi kurejesha makali yake ya mwanzo. Kuna sababu kadhaa.
- Staili yao ya muziki wa majungu wasipoiacha, hawawezi kuinuka. Nyimbo kama 'Ama zangu ama zao", "Itikadi zetu" na nyingine za maudhui hayo ndizo ziliwakimbiza akina AY na FA.
- Ujio wa akinda Diamond, Jux, Baraka da Prince, Darasa, Yamoto, Weusi na makundi mengine yamebadili kabisa mwonekano wa bongo fleva, kiasi kwamba inawabidi wafikiri namna bora ya kuja upya. Platform waliyo enjoy miaka hiyo haipo. Wapo waliojaribu kurudi tena kama vile Wateule, Wagosi wa Kaya, BDP, Wakali Kwanza nk lakini walibanwa mbavu na vijana wapya.
- Baadhi ya wasanii wa ECT wamesikika wakilalamikia ubabe wa GK, ndio sababu akina Stanboy wakatimkia USA.
By the way nawatakia kila lililo jema kwenye ujio mpya