Easy coach kupoteza kibali kuhudumu mpaka warekebishe walioagizwa na NTSA ni hatua nzuri

waltham

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2014
Posts
2,522
Reaction score
1,045
NTSA SUSPENDS TLB licence of Easy Coach over Sachangwan crash, operator calls off services of its 200 buses to train drivers on road safety.
1223-696x396.jpg

Easy coach kupoteza kibali kuhudumu mpaka warekebisha walioagizwa na NTSA ni hatua nzuri. Ni mojawapo ya kampuni iliyo na nidhamu ya juu sana!!!

Kuna kipindi ajali za gari za abiria zilikua juu sana kenya japo siku hizi sio sana zimepungua pamoja na vifo zake!!!

Hatua inaonekana kuchukuliwa siku hizi. Kwa majirani ajari pia ni kwa kiasi kikubwa japo uganda ni kama hakuna!! Sijui...
 
Hatua endelevu zinafaa kuzingatiwa na kusisitizwa hadi hizi ajali zipungue kwa kiasi kikubwa. Kule Bongo kuna madereva wa wa mabasi ya mikoani hubadilishana barabara wakati wanapishana, yaani kuchezea maisha ya binadamu. Niliona kwenye TV wakieleza vile wao hufanya hicho kitu hadi nikaingiwa na hofu kweli kweli.
 
Sababu zinazosababisha ajali Afrika ni nyingi sana
-Madereva wa magari ya abiria wahuni, walevi na wavuta bangi. Pia, madereva wanapata maslahi kidogo na kufanya kazi katika hali ngumu.

-Serikali zetu kutokudhibiti elimu inayotolewa na vyuo binafsi vya udereva.

-Kuwepo kwa leseni za udereva nyingi bandia ambapo mtu yeyote anaweza kupata bila kupata mafunzo ya kutosha (mambo ya River road).

-Kutokuwa na sheria kali za kudhibiti madereva wazembe.

-Askari wa usalama barabarani kupokea rushwa na kuacha magari mabovu yaendelee na safari.

-Viongozi wetu kupuuzia ajali na kutokufanya juhudi zozote za kumaliza tatizo.

Suluhisho
-
Serikali zetu zidhibiti vyuo binafsi vya udereva na kuhakikisha leseni hazitolewi mitaani kama njugu.

-Serikali zihakikishe kuwa madereva wa mabasi na malori wana mikataba ya kazi na kufanya kazi katika mazingira rafiki.

-Kuweka sheria kali za makosa ya barabarani.

-Dhana potofu kuwa ajali ni mapenzi ya Mungu zikomeshwe.
 
Duh, mkuu ni kampuni gani hiyo?
Halafu ukisafiri bongo usisafiri na kampuni zisizoeleweka, Kuna baadhi zina madereva vichaa sana.,
Kuna kampuni nzuri zinaajiri professional drivers,
 
Umeidadavua vizuri sana, ila hiyo sentensi ya mwisho ndio tatizo kubwa Afrika, kwamba kila ajali au kifo ni mapenzi ya Mungu. Watu tumejiaminisha mambo yasioendana hata na dini zetu, mtu anakua mvivu kwenye kuzingatia usalama barabarani halafu anasema anamtegemea Mungu atamlinda.
 
Unakuta dereva amevuta bangi na viroba amepeleka gari mtoni halafu wanasema eti Mungu alipanga,... Ufala kweli !
 
Hiyo dhana ni potofu, hutumiwa Mara nyingi sehemu tofauti,
Hata kijana kufa katika umri mdogo bado haimake sense,
Mtoto anakufa kwa kukosa Tiba ya Malaria and they say the same thing.
Hizi dini wengi wanasoma na hawazielewi.
 
Duh, mkuu ni kampuni gani hiyo?
Halafu ukisafiri bongo usisafiri na kampuni zisizoeleweka, Kuna baadhi zina madereva vichaa sana.,
Kuna kampuni nzuri zinaajiri professional drivers,

Ni hatari, hebu soma hii hapa madereva wa mabasi hayo walikuwa wakifanya mzaha wakati wa kupishana.

Baada ya ajali mfululizo zilizohusisha mabasi, polisi wamekuja na hii taarifa - millardayo.com
Ni takribani wiki moja yametokea matukio makubwa matatu ya ajali za barabarani mfululizo ambayo yamehusisha mabasi yanayofanya safari zake mikoani, taarifa ya polisi imesema ajali hizo zimesababisha jumla ya vifo vya watu 46 na majeruhi 73.

Matukio hayo yanahusisha ajali iliyotokea June 28 2016 Misungwi Mwanza ambapo basi la kampuni ya Super Samy likitokea Shinyanga kwenda Mwanza lilipata ajali kwa kuacha njia na kupinduka hivyo kusababisha vifo wa watu 5 na majeruhi 13.

Tukio lingine ni mnamo July 01 2016 VETA Dakawa katika barabara ya Morogoro/Dodoma malori mawili yaligongana na kuwaka moto na kusababisha vifo vya watu 5 na na baadae katika eneo hilohilo siku July 02 2016 usiku gari la kampuni ya OTA lilipata ajali kwa kuyagonga mabaki ya malori yaliyopata ajali na kubaki eneo la tukio na kusababisha vifo vya watu 6 na majeruhi 6

Halikadhalika mnamo July 04 2016 maeneo ya Maweni-Kintiku Singida mabasi mawili ya kampuni ya City Boys yaligongana na kusababisha vifo wa 30 na majeruhi 54 ambapo hadi leo wamebaki majeruhi 33 wakiendelea na matibabu. Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa polisi, kikosi cha usalama barabarani, Mohamed Mpinga amesema

>>>’kwa ajali iliyotokea Maweni Singida siyo ajali ya kawaida bali ni tukio la kufanya mauaji bila kukusudia, hivyo polisi imedhamiria kuwafikisha mahakamani madereva waliohusika na ajali hiyo kwa mashtaka ya mauaji bila kukusudia kutokana na taarifa za awali za chanzo cha kutokea kwa ajali hiyo kwamba madereva wa mabasi hayo walikuwa wakifanya mzaha wakati wa kupishana.

>>>Aidha tumewasiliana na wenzetu wa SUMATRA, kampuni ya mabasi ya City Boys na makampuni mengine yaliyohusika katika ajali yafungiwe kutoa huduma za usafirishaji katika njia zote hapa nchini
 
Ni mapenzi ya mungu my foot!!!!!!!.............ndio hizo dini kabsa mie sipo. naamini mungu yupo kwa sababu kabla ya mzungu kuja mababu zangu waliabudu mungu sawa tu!! kwa hivyo mapenzi ya mungu sio ufe kwa sababu ya dereva mlevi!! hizo dini ni tamaduni tu za mzungu na mwarabu!!!
 
Hatua endelevu zinafaa kuzingatiwa na kusisitizwa hadi hizi ajali zipungue kwa kiasi kikubwa. Kule Bongo kuna madereva wa wa mabasi ya mikoani hubadilishana barabara wakati wanapishana, yaani kuchezea maisha ya binadamu. Niliona kwenye TV wakieleza vile wao hufanya hicho kitu hadi nikaingiwa na hofu kweli kweli.

Dah, mkuu na wewe uliisikia hii, haki hii hata mimi iliniogofya haki ya mungu. Duniani kuna mambo
 
tz tumedhibiti ila naona kuna shetani anataka kuzileta tena hiyo night club....night shift hiyo night route.....
 
Kuna dereva flani nilimkemea nikiwa naenda zangu Nanyuki. Matatu za Nanyuki Cabs, afu abiria wenzangu wananikemea, eti wamechelewa. Kilichoniudhi kulikuwa na mwanamke ana mtoto mchanga sana, ameketi ile siti nyuma ya dereva, anateseka akizuia mtoto wake asiumie. Gari linaendeshwa kama safari rally. Tunarushwa huku na kule. Nilitulia tuli nikataimu tulipoingia petrol station, nikawai nje haraka nikamshika dereva mashati, nikashikwa na wazimu nikamzaba kofi kadhaa za kilo, alikuwa amenitusia mamangu bana. Yaani baada ya hapo gari liliendeshwa mos mos, utadhani tunaenda zetu harusini. Afu hamna abiria aliyetaka kunitizama machoni. Hawa madereva wanachojua ni hela tu. Washenzi sana.
 
[emoji2] [emoji2] [emoji2]
 
Heheheh!! Huyo atakua dereva Mtanzania, maana kama ni Mkenya lazima mngezipiga, sitegemei Mkenya azabwe makofi halafu yaishe, inabidi muende chini kwa mieleka, nakumbuka enzi zangu za Konyagi halafu nilikua nacheza tae-kwondo, ugomvi na vita dhidi ya makondakta na madereva, ila kuna siku nilichezea kichapo maana walinizingira.

Anyway pole bana, na hongera sana kwa kuzusha maana huwa nakerwa sana unakuta baada ya ajali jamaa wanahojiwa wakiwa wamelazwa hospitalini huku wakikiri eti dereva alikua anaendesha gari vibaya.
 
Heheheh!! Huyo atakua dereva Mtanzania, maana kama ni Mkenya lazima mngezipiga, sitegemei Mkenya azabwe makofi halafu yaishe, inabidi muende chini kwa mieleka, nakumbuka enzi zangu za Konyagi halafu nilikua nacheza tae-kwondo, ugomvi na vita dhidi ya makondakta na madereva, ila kuna siku nilichezea kichapo maana walinizingira.

Anyway pole bana, na hongera sana kwa kuzusha maana huwa nakerwa sana unakuta baada ya ajali jamaa wanahojiwa wakiwa wamelazwa
Alikuwa mkenya baadaye tulipata kwenye route hiyo maanake nilikuwa nasafiri sana, hadi tukajuana vyema. Nilimchapa suprise alikuwa ananidharau nikiwa nimeketi kwenye gari. Tulipoonana one on one jamaa mwenyewe hata kichwa ningemkaba tu nimsukumie kwapani. Alidhani ntammaliza lakini frastreshen zangu zilikuwa kidogo tu. 😀😀😀
 
Back
Top Bottom