EATV na EA radio wamjia juu Diamond , kisa kusema hategemei redio na Tv pekee

Sidhani kama mmezingatia matumizi ya 'pekee' hapo
Na katika neno hilo ndio utajua nguvu ya uelewa wa mtu.Sio kubisha tu na kusema maneno ya kuponda tatizo letu wabongo tunasikiliza ili tujibu na sio kuelewa kwanza.
 
Wewe unadhani kwanin katika vituo vyote EATV na Redio ndo wamemaindi hii kauli?
Kwanini vituo vingine hawajamaind?
 
Saijui ila nimezungumza kiujumla.

Kama ingekuwa kweli alichokisema, basi asingepata Fulsa kutambulisha nyimbo TV kuwa.
Yeye kasema hategemei TV na radio pekee , unaelewa maana ya hii kauli? Maana take anatumia pia vyanzo vingine pia
Sijui hapo watu hawajaelewa nini
 
Yeye kasema hategemei TV na radio pekee , unaelewa maana ya hii kauli? Maana take anatumia pia vyanzo vingine pia
Sijui hapo watu hawajaelewa nini
Ndo mabashite hao kitu kinaeleweka kujitoa tu ufahamu tunaita kukurupuka kama kitu hujaelewa uliza afu mbona kujitesa si walete iyo clip ya mondi wanaleta ya vilaza wenzao kina dulla
 
Oyaa, kubali yaishe Diamond hapaswi kutamka hayo maneno kwa biashara anayoifanya.

Unazidiwa upeo wa kufikiri hadi na watu wenye akili fupi ya shule ya msingi tu.
Hajafanya kosa kutamka hayo maneno, huwezi tegemea tv na radio pekee kwa nyakati hizi. Sasa mbona huo ni ukweli unaojulikana na mond anawaamsha wasanii ambao hawatumii social net kuuza kazi zao. Mond anaakili sana
 
Hajafanya kosa kutamka hayo maneno, huwezi tegemea tv na radio pekee kwa nyakati hizi. Sasa mbona huo ni ukweli unaojulikana na mond anawaamsha wasanii ambao hawatumii social net kuuza kazi zao. Mond anaakili sana

jamani ehh, sio sawa kusema eti "kwa sasa sijtegemei radio na tv"

acheni mahaba yaliyopitiliza hadi mnajivua ufahamu.
 
Social media inanguvu tukubali.. watu gani hamtaki mabadiliko?? Media zenyewe zinapiga nyimbo za wasaniii hata haziwalipi.. watia wasanii umaskini tu
 
Social media inanguvu tukubali.. watu gani hamtaki mabadiliko?? Media zenyewe zinapiga nyimbo za wasaniii hata haziwalipi.. watia wasanii umaskini tu

social media zina nguvu ila radio na tv zina umuhimu mkubwa sana.

usiache mbachao kwa msala upitao,

anapaswa kusema kuwa sasa hivi nafanya biashara zangu kupitia radio, tv na social media.
 
Diamond anachosema ni kweli tena kwa asilimia 70 kwa sasa, hii kauli usiiangalie kama shabiki au hater wake lakini angalia kama msomi anaefanya Trend Analysis.

Hawa watu hawajui kusoma alama za nyakati, angalia MTV ya Marekani siku hizi hawapigi kabisa mziki maana wanajua watu hawa angalii mziki kwenye TV bali wamehamia YouTube na radio zimekuwa replaced na vitu kama Spotify, Apple music na Google play music.

Sasa kwa Tanzania siku baada ya siku hichi kitu kina kuja... Internet penetration inakua na Kasi yake inakuwa ya uhakika (hamna tena mambo ya buffering) mfano Halotel kufuga vifaa vijijini pamoja na hawa majamaaa kama kina Samsung na hususani Tecno wakiendelea kusambaza simu kwa bei ya chini consumption ya information ita hama toka kwenye traditional media tu internet.

Na kwa sasa maslahi kwa msanii yapo vizuri zaidi online kuliko huku kwenye TV na radio wanapo piga mziki wako bure. Wakati kwenye Internet ukipromote bidhaa kwenye page yako unapata hela, nyimbo yako ikiwaplayed unapata hela.

Na mwisho tuangalie swala la coverage Eatv na radio zao inaweza fikia watu wachache tena local lakini social media zinaweza kukupa global market kirahisi sana tena bure (bila kuhonga au kumpigia magoti vj au mtangazaji apige nyimbo yako)
 
Ukweli mtupu mkuu mfano hai in HarmoRapa amekuwa maarufu mtandaoni akiwa hana hats nyimbo moja redioni
Hata wakina gigy money
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…