Diamond anachosema ni kweli tena kwa asilimia 70 kwa sasa, hii kauli usiiangalie kama shabiki au hater wake lakini angalia kama msomi anaefanya Trend Analysis.
Hawa watu hawajui kusoma alama za nyakati, angalia MTV ya Marekani siku hizi hawapigi kabisa mziki maana wanajua watu hawa angalii mziki kwenye TV bali wamehamia YouTube na radio zimekuwa replaced na vitu kama Spotify, Apple music na Google play music.
Sasa kwa Tanzania siku baada ya siku hichi kitu kina kuja... Internet penetration inakua na spidi zaanzakuwa za uhakika mfano Halotel kufuga vifaa vijijini pamoja na hawa majamaaa kama kina Samsung na hususani Tecno wakiendelea kusambaza simu kwa bei ya chini consumption ya information ita hama toka kwenye traditional media tu internet.
Na kwa sasa maslahi kwa msanii yapo vizuri zaidi online kuliko huku kwenye TV na radio wanapo piga mziki wako bure. Wakati kwenye Internet ukipromote bidhaa kwenye page yako unapata hela, nyimbo yako ikiwaplayed unapata hela.