Ebola Ebola Tanzania mipaka yetu tumejipangaje????

Ebola Ebola Tanzania mipaka yetu tumejipangaje????

Big jay

Member
Joined
Mar 14, 2013
Posts
96
Reaction score
33
Wakuu hii habari si mpya hapa jamvini na serikali inatambua kuwapo na ugonjwa huu lakini kinachosikitisha hakuna hatua zozote za kujihami zilizochukuliwa hususani mipakani na viwanja vya ndege,,,,

juzi nimetoka congo kupitia barabara niliookua nagonga passport upande wa Zambia nilishangaa kuona maafisa uhamiaji wamevalia vitambaa maalumu kuziba midomo na mikononi wakiwa wamevalia grooves na kabla haujagonga passport unakaguliwa na daktari ktk chumba maalumu na kupewa yellowcard (ya chanjo)

baada ya kutembea leo hii nimefika border ya Tunduma kwa upande wa zambia ni kama vile kasumbalesa dr na maofisa wote wapo kwa protector Cha kushangaza ni upande wa Tanzania uhamiaji wamejiachia tu bila kinga wala kujali na kuna dada ambae ni dr wa serikali akiwa na jamaa nae ni dr pale costorm ni kama wanapiga story wakisubiria mda uishe wanyanyue kwenda makwao.

ni kwamba serikali haijali kwa kudhania ugonjwa huu hautafika huko waliko ? labda nikuhakikishieni wakuu hapa border Ndipo naishi na nilipozaliwa kwa siku wageni wanaoingia si chini ya watu 3000 na hao hao wengi wanakuja dar na wengine nairobi je Ebola ikipenya kwa hapo je Tutasalimika? naomba serikali iwe makini na swala hili na kwa congo huu ugonjwa umedhitishwa kuingia na waziri wa afya,,,au sie mpaka tufe ndio serikali ijue?
 
Wakati sisi tuko kwenye hofu ya huo ugonjwa kuna watu wanaomba usiku na mchana uingie nchini ili wapige pesa
 
Ngoja uingie mana bado tumelala

Lakini huu ugonjwa labda kama atapona mtu kuna gari zinatoka congo zaidi ya gari kumi na na zinavuka border mpaka dar zinaitwa Taqwa na zingine classic kila leo zinapita zikitoka Congo hii wasicheze siasa ni hatari sana
 
Wakati sisi tuko kwenye hofu ya huo ugonjwa kuna watu wanaomba usiku na mchana uingie nchini ili wapige pesa

Kunakupiga hela huko? nimeacha gunia za mchele na maharagwe kwa kuiogopa Ebola niokoe maisha biashara baadae na sio. mimi tu zaidi ya watanzania ishirini na ushee tumerudi nyumbani
 
Tunalindwa na mungu tu hakuna jitihada zozote zinazochukuliwa watanzania sikuzote ni wazembe kwa kila kitu
 
Kunakupiga hela huko? nimeacha gunia za mchele na maharagwe kwa kuiogopa Ebola niokoe maisha biashara baadae na sio. mimi tu zaidi ya watanzania ishirini na ushee tumerudi nyumbani

Sijamaanisha wewe
 
Sijamaanisha wewe

Nimekupata mkuu hao wanasiasa wakitaka kugeuza huu ugonjwa biashara wamepotea labda wahamie mwezini ila tu nikiupata kama mimi nakimbikia bungeni kwa gharama yoyote ili wakome tufe wote
.
Zambia ni nchi ndogo sana na maskini lakini ipo karibu na mwananchi wake Tanzania kwanini tuishi kama tupo kam
bini hatuna uongozi?
 
Back
Top Bottom