Economic hitmen

Economic hitmen

Mu-sir

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2010
Posts
3,621
Reaction score
1,636
hiki ni kitabu kinachoitwa... CONFESSION OF AN ECONOMIC HITMAN.

Iko hivi:

Kabla nchi zetu maskini kukopeshwa zinafanyiwa study ya nguvu na wataalam wa uchumi kutoka IMF, WORLD BANK and the so wakopeshaji wakubwa. Lengo lao hasa ni kujua unexplored resources zilizopo.

1. Sasa hayo mataifa makubwa yanatoa the so called MIKOPO au MISAADA ya ujenzi ai Ufadhili wa Mradi fulani lakini sharti kubwa ni kuwa main contractor anatoka kwao. Lets say anayoa pesa ni IMF au world bank so most likely contractor atakuwa kampuni ya kimarekani. Anakuja anapiga kazi analipwa huko huko kwao ila nyie mnabeba deni tu. Yaani mnaishia kuona barabara au daraja au umeme au chochote lakini pesa hampewi na deni linakuwa la taifa. (Hapa local contractors hawapati hizi tender kubwa)

2. sasa wakisha wakopesha sana then the next move ni kuomba Access kwenye natural resource mlizonazo kama nchi. Kwa sababu mnadaiwa na hawa jamaa inawawia vigumu kuwanyima fursa hiyo adimu na adhim. (Mfano hai upo hapa kwetu..wakopeshaji wetu wapo kwenye madini na gesi yetu. Hata wachina nao wametumia same technic na wapo)

3. mkiwakatalia Access ya natural resource zenu kisa deni wanalilowakopesha next move ni ku create propaganda. Kumbuka hapa Tanzania ile issue ya mikataba ya madini ya URANI (MKUJU RIVER PROJECT) kupewa kampuni za urusi (NMZ) kulianza kuzuka propaganda eti inatumiwa na Magaidi. Sijui wakubwa wetu walili solve vipi. Niliishia kusikia kampuni husika iliuza hisa zake ulaya.

4.Next move ni kutumia "The Jackals" ku create movement within a country ya kuleta "ukombozi" kwa wananchi...hii hujumuisha kuzuka ghafla kwa kikundi cha waasi wenye silaha kali wanaopigana na serikali ili kuitoa madarakani....hupewa support ya fedha na silaha na hao hao jamaa. Hapa ghafla huzuka vita ya wenyewe kwa wenyewe...Refer Syria, Libya, Congo etc. kwa mifano hai.

5.Hiyo hapo juu ikishindikana ndiyo propaganda inazidishwa na kuonesha nchi fulani inahatarisha "Amani" ya dunia hivyo kuleta ulazima wa kushambuliwa na mataifa makubwa ili kuondoa utawala Hatari kwao. Hapo utaona majeshi yao yakika kupigana na nchi husika kwa kisingizio hicho na Finally wanashinda. LAURENT GBAGBO wa Ivory coast. (Japo alishinda uchaguzi kihalali kwa mujibu wa tume), Saddam n.k

NB:
nimejitahid kueleza kwa kifupi kitabu hicho. Wengine wataongezea.
 
LAURENT GBAGBO - french special forces walkua wanashiriki vita mtaan kabisa na waasi kumuondoa tu kwa vile kibaraka wao ana mke wa kizungu wa kifaransa ndugu idrissa outara!!!
 
Ni kweli na alikataa kabisa kutoka madarakani na aligoma kuwapozea wafaransa kwenye mafuta wakamfuata ikulu kabisa. Propaganda ilienezwa kuwa alishindwa na uchaguzi haukuwa huru na haki. Then eti wanamfungulia mashtaka.
 
Asante kwa kukileta, mimi nilishakisoma ndiyo maana nilikuwa namchukia sana lowasa na kundi lake. Tungepigwa mikataba hewa mpaka tungekoma, hiyo hali wanayo sasa hivi Ghana. Tumombee Dr Magufuli maisha marefu maana yule rais wa Ghana aliyekuwepo kabla ya huyu wa sasa alikuwa kama Dr Magufuli, ila alivyofariki tu yaani kila kitu kikageuka, yaani hao jamaa wa serikali ya sasa ya Ghana wapo kama lowasa, ni wezi balaa.
 
Tatizo hayo mataifa yana nguvu sana..huenda hata huyo Rais wa ghana walimuondoa baada ya kuona hana strong Institutions nyuma yake ili waingie wapigaji.

Hawa Hitmen wana technic nyingi sana and they will stop at nothing to get what they want. Wana money, media, Army n.k.
 
kumbe ndio maana ccm wanaiba kura, wanavuruga haki za binadamu, umaskini na njaa ila tunaambiwa ni utawala bora na demokrasia. maana wachina wapo kwenye gesi, waamerika kwenye dhahabu na almasi duuh kweli ndio maana tanzania upinzani unakandamizwa
 
Tatizo hayo mataifa yana nguvu sana..huenda hata huyo Rais wa ghana walimuondoa baada ya kuona hana strong Institutions nyuma yake ili waingie wapigaji.

Hawa Hitmen wana technic nyingi sana and they will stop at nothing to get what they want. Wana money, media, Army n.k.
Kwa Tanzania ya Dr Magufuli hawawezi kabisa. Kingine umoja wetu ndiyo ushindi. Sema chadema na ukawa ndiyo wanalengo la kutuvuruga ndiyo maana vyombo vya usalam vipo makini sana kwa sasa. Nikuhakikishie tu kuwa Tz tupo imara! Tatizo la hawa jama huingia pale tu panapokuwa hakuna umoja, na serikali iliyojaa wapiga dili. Ndiyo maana ukiangalia JK alipgwa economic hitman chache baadaye akastuka akamfukuza mwizi lowasa, na hiyo mikataba bado tunalipa.
 
Unadai umekisoma hiki kitabu halafu unafanya assessment ya kitoto namna hii. Kwenye kitabu chote huyu EHM (John Perkins) anapata exclusive rights za kudeal na Govts kupitia reputable International orgnizations kama USAID, IMF, WORLD BANK na MNCs. Kwa hapa Tz hizi zote zimeiweka serikali mfukoni. Serikali ikitaka kukopa na kuomba budget support inaenda kupiga magoti kwa hawa. Tumeona kwenye sekta ya nishati kulivyojaa kampuni za kimarekani na ahadi za umeme usiotosheleza kwa zaidi ya miaka 15. Sasa wewe unakuja kulink EHM na periphals wakati tayari miundombinu yao imesimama katikati ya Govts. Either umeamua kupotosha makusudi au unaongozwa na siasa uchwara au una uelewa mdogo.
 
Mkuu Mudawote nilitaka nikujibu lakini Kingmairo ameniwahi. Kwa ufupi hawa sio watu wa mchezo na hakuna serikali inayoweza kusimama wakiamua kufanya yao. Nchi za amerika ya kusini zime suffer sana Equador, Panama etc. Labda hukukielewa hicho kitabu vizuri
 
Last edited by a moderator:

Ni kweli mkuu. Hichi kitabu kipo very current na situation tulionayo hapa nchini hasa hasa kutokana na rasilimali (gesi, madini, potential oil) ambazo tunazo sasa hivi na ambazo ni core focus ya haya Mataifa. Sasa akitokea mtu anapotosha badala ya kusaidia watu wengi ambao hawajapata fursa ya kujua hawa jamaa wanavyooperate inaboa sana.
Ishu yote ya umeme Tanzania kuanzia enzi za IPTL, Aggreko, Songas mpaka sasa Dowans ni replica ya jinsi EHM walivyoiteka Indonesia na kampuni yao ya MAIN.
 
Kabisa hakuna mtu anayeweza kusimana kwenye interest za hawa jamaa hata kama tuna umoja hao watu wana uweza wa ku create chaos (The Jackals) sijui jamaa hakusoma vizuri kitabu au makusudi. Tanzania ni playground yao kwa muda mrefu. Hata local contractors wamewahi kulalamika kunyimwa tender kubwa za serikali ambazo kimsingi ni Misaada na Mikopo. Sababu kubwa ni hiyo. Pia kwenye bandiko langu nimejitahidi kuonesha na mifano. Leo eti Magufuli.! Is he strong both Institutional and Economicaly than the late Gaddafi? Siku hizi vita ni ya kiuchumi sio ya ujinga ujinga.
 
Mie naamini Rais Magufuli he has been in the system for a while, he knows kuhusu uwepo wao in some sectors of interest to them. I am sure he is not going to trouble them. Hata kwenye Campaign zake na speech yake hajayagusa yale maeneo yao with high tempo kiviile I am seeing the Govt is going to cooperate and Tz will be safe.
 
Asante kwa kukileta, mimi nilishakisoma ndiyo maana nilikuwa namchukia sana lowasa na kundi lake. Tungepigwa mikataba hewa mpaka tungekoma, hiyo hali wanayo sasa hivi Ghana. Tumombee Dr Magufuli maisha marefu maana yule rais wa Ghana aliyekuwepo kabla ya huyu wa sasa alikuwa kama Dr Magufuli, ila alivyofariki tu yaani kila kitu kikageuka, yaani hao jamaa wa serikali ya sasa ya Ghana wapo kama lowasa, ni wezi balaa.

We jamaa mbona mikataba feki tayari ipo.Deni kubwa maendeleo hamna madini yanaisha.CCM ni madalali wakubwa wameuza nchi,Magufuli anahangaika tu na Muhimbili huku sehemu nyeti anaogopa kugusa
 
Mkuu Mudawote nilitaka nikujibu lakini Kingmairo ameniwahi. Kwa ufupi hawa sio watu wa mchezo na hakuna serikali inayoweza kusimama wakiamua kufanya yao. Nchi za amerika ya kusini zime suffer sana Equador, Panama etc. Labda hukukielewa hicho kitabu vizuri
Mu-sir ninakielewa vizuri sana. Hizo nchi unazozitaja ni kuwa zinatawaliwa na magenge. Yaani iko kama TZ kama tungempitisha lowasa. Kwa hali ilivyo sisi tupo kama China au Russia kwa sasa. Vyombo vyetu vya ulinzi ni waadilifu na tunatawaliwa na system ambayo imejaa wazalendo, tofauti na nchi kama kenya ambayo huua mtu yeyote akiingilia dili. Tusingekuwa sawa ki usalama leo hii lowasa angekuwa rais na tungeona mtanange wa mikabata hewa na kila kitu angewasukumia wengine. Kingine ni ule umoja wetu kama watanzania, kwa mfano ondoa kipindi hiki ambacho lowasa kavuruga watu (yaani hata wachungaji walikunywa maji yake, wasomi walikunya maji yake, watetezi wa haki za binaadamu walikunywa maji yake) watanzania tumekuwa wamoja ktk kukataa uovu. Kingine lowasa na kundi lake la economi hitman walijaribu sana kutumia media, na kuhadaa wananchi ila walishindwa kwa sababu JK ni mjanja zaidi yao, maana amekuwa huko na anawajua maana walimsumbua kipindi chake sana ndiyo maana jina lowasa halikuvuka kabisa. Kwa ufupi kuna mambo mengi yapo nyuma ya pazia juu ya hawa watu. Ila kwa Dr. Magufuli na vyombo vyetu vya ulinzi nakuhakikishia hawafui dafu. Tuzidi kusherehekea tu na kutafuta fursa za biashara maana TZ inakwenda kuwa nchi ya kipato cha kati soon. Ila akina lowasa they will never rise again, that's their end. Na utaona mpaka 2020 chadema itakuwa imebaki mifupa tu.
 
Last edited by a moderator:
We jamaa mbona mikataba feki tayari ipo.Deni kubwa maendeleo hamna madini yanaisha.CCM ni madalali wakubwa wameuza nchi,Magufuli anahangaika tu na Muhimbili huku sehemu nyeti anaogopa kugusa
Wewe ni shetani, hivi umeliona la Muhimbili tu? Wewe lofa kweli kweli, nachukia sana watu kama wewe. Huko kote tumefikishwa na watu wezi kama lowasa
 
Mie naamini Rais Magufuli he has been in the system for a while, he knows kuhusu uwepo wao in some sectors of interest to them. I am sure he is not going to trouble them. Hata kwenye Campaign zake na speech yake hajayagusa yale maeneo yao with high tempo kiviile I am seeing the Govt is going to cooperate and Tz will be safe.
Not the matter of cooperating, those guys are evil! Look at China, all those who are found cooperating with economic hitman are sentenced to death, and there is no economic hitman in China.
 
Unadai umekisoma hiki kitabu halafu unafanya assessment ya kitoto namna hii. Kwenye kitabu chote huyu EHM (John Perkins) anapata exclusive rights za kudeal na Govts kupitia reputable International orgnizations kama USAID, IMF, WORLD BANK na MNCs. Kwa hapa Tz hizi zote zimeiweka serikali mfukoni. Serikali ikitaka kukopa na kuomba budget support inaenda kupiga magoti kwa hawa. Tumeona kwenye sekta ya nishati kulivyojaa kampuni za kimarekani na ahadi za umeme usiotosheleza kwa zaidi ya miaka 15. Sasa wewe unakuja kulink EHM na periphals wakati tayari miundombinu yao imesimama katikati ya Govts. Either umeamua kupotosha makusudi au unaongozwa na siasa uchwara au una uelewa mdogo.
Don't be so negative. Kumbuka economic hitman siyo mfumo rasimi. Watu wengine kama CIA huweza kutumia ili kupata hela za kujiendesha. Rais akiwa na msimamo hakuna wanaloweza kufanya zaidi ya fair game. Ingekuwa hivyo basi dunia hii US wangekuwa wao na utajili pekee. Chini ya Serikali ya Dr Magufuli hawatafua dafu nakuhakikishia!
 
Mu-sir ninakielewa vizuri sana. Hizo nchi unazozitaja ni kuwa zinatawaliwa na magenge. Yaani iko kama TZ kama tungempitisha lowasa. Kwa hali ilivyo sisi tupo kama China au Russia kwa sasa. Vyombo vyetu vya ulinzi ni waadilifu na tunatawaliwa na system ambayo imejaa wazalendo, tofauti na nchi kama kenya ambayo huua mtu yeyote akiingilia dili. Tusingekuwa sawa ki usalama leo hii lowasa angekuwa rais na tungeona mtanange wa mikabata hewa na kila kitu angewasukumia wengine. Kingine ni ule umoja wetu kama watanzania, kwa mfano ondoa kipindi hiki ambacho lowasa kavuruga watu (yaani hata wachungaji walikunywa maji yake, wasomi walikunya maji yake, watetezi wa haki za binaadamu walikunywa maji yake) watanzania tumekuwa wamoja ktk kukataa uovu. Kingine lowasa na kundi lake la economi hitman walijaribu sana kutumia media, na kuhadaa wananchi ila walishindwa kwa sababu JK ni mjanja zaidi yao, maana amekuwa huko na anawajua maana walimsumbua kipindi chake sana ndiyo maana jina lowasa halikuvuka kabisa. Kwa ufupi kuna mambo mengi yapo nyuma ya pazia juu ya hawa watu. Ila kwa Dr. Magufuli na vyombo vyetu vya ulinzi nakuhakikishia hawafui dafu. Tuzidi kusherehekea tu na kutafuta fursa za biashara maana TZ inakwenda kuwa nchi ya kipato cha kati soon. Ila akina lowasa they will never rise again, that's their end. Na utaona mpaka 2020 chadema itakuwa imebaki mifupa tu.

Nadhani unaandika kwa Hisia mbaya dhidi ya Lowassa and he is not in power nor in the disscusion. Naamini kama wangekuwa wanataka Lowassa awe kwa vyovyote vile angekuwa. Nilitoa mfano wa Gbabo walivyomfuata Ikulu kwa risasi na mabomu japokuwa alishinda uchaguzi. Tatizo umejikita kwa Lowassa wakati mada sio Lowassa. EHMs hawachaguliwi Rais na wananchi hata hiyo system ya Wazalendo unayosema usoshangae ndio wao. Hakuna kiongozi asiye co-operate nao akawa safe.
 
Last edited by a moderator:
Not the matter of cooperating, those guys are evil! Look at China, all those who are found cooperating with economic hitman are sentenced to death, and there is no economic hitman in China.

China is one of the strongest Economies mfano wako ni Invalid. Unataka EHMs waende kui sabotage Marekani?, Ulaya, China, etc wakati wanatoka huko huko???
 
Back
Top Bottom