FYI the economist ni adui mkubwa wa Magufuli, wao wamejiweka nta (wax) masikioni mwao wasisikie wala wasione kinachoendelea.
Ni hivi, kuna investment kubwa sana kwenye private sectors, kuna wawekezaji wa viwanda wengi kutoka nje wameanzisha viwanda na baadhi Magufuli mwenyewe amevifungua. Utaona hao the economist hawasemi hayo, wao wanaongelewa NGO na upuuzi mwingine wa kipropaganda. Watu tunajenga moja ya Bwawa kubwa kabisa Afrika, reli ndefu na yenye uwezo wa kubeba mzigo mzito kabisa Afrika halafu wanajifanya hawaoni?
Magu mwenyewe amekuja na mpango wa kusikiliza malalamiko ya wafanyabiashara Ikulu na kuwapa namba ya simu maalumu ambayo watampa malalamiko moja kwa moja Ikulu kama wakinyanyaswa au kuombwa rushwa na wafanyakazi wa serikali halafu watu wanasema hajali private sector?