Hajakosea mkuu.........
Hammie Rajab amefariki wiki iliyopita tarehe 21/04/2011 katika hospitali ya Amana Ilala ambako alilazwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Malaria.....Mungu ailaze Roho yake mahali pema peponi,Amina
Mkuu hebu cheki tena taarifa zako. Hammie Rajab amefariki lini? Huyu nadhani bado yupo ila siku hizi anashiriki zaidi kwenye utengenezaji wa filamu na sio uandishi wa Vitabu. Kama sikosei.
Yap nami namkumbuka sana huyu mwandishi pamoja na akina Sam Kitogo, S.M.Bawji, faraj Katalambula, Agolo Andulu. kwani na hammie rajab yu wapi?
Baadhi ya vitabu nilivyosoma vya waandishi hawa ni hivi
>Roho mkononi
>Awe hai au amekufa namtaka
>Nimekoma ukuwadi na shogayo hasidi
>Njama, Kikomo, Kikosi cha kisasi & kufa na kupona
>Simu ya Kifo
>Joto la fedha
ha ha ha ilikuwa raha kwakweli wakati ule.
Kuna mtunzi anaitwa anaitwa Hussein Tuwa.........Jamaa ni mzuri sana kwenye utunzi,anatunga Riwaya/Vitabu vitamu sana...
Binafsi nimebahatika kusoma Riwaya zake kama Mdunguaji,Mtuhumiwa,Mkimbizi,Mfadhili, Bondia na Utata wa 9/12.......Jamaa anatisha hasa
Umenikumbusha John Rutayisingwa na Agoro Anduru, kwa nini waandishi wazuri maisha yao ni mafupi. RIP WOTE, AMENHao jamaa walikuwa Magwiji mahiri wa riwaya za kusisimua pia alikuwapo John Rutayisingwa na Agoro Anduru
kwa sasa wanajitahidi kuendeleza fani ni Beka Mfaume na Ndalichako
huyo jamaa mwingine uliyemtaja cjui huwa anaandika nini mpaka page inajaa
Mkuu kweli kwa uandishi huu ulikuwa mwandishi wa vitabu za hadithi?Uandishi haulipi niliwahi kujidanganya after being inspired nikaandika HEKAHEKA ,kashifa .hadithi zikatoka msanii miaka ya tisini malipo yakawa kidogo na sikupata mtu wa kunisponser nikaghairi.baadae nikaona nitest novel.nikaandika HÖTSOUP in the beginning.ni cha kijasusi kinahusu gulfwarone irag .nilikua bush skupata spönser miaka hyo ya tisini na tano.
Mwisho nkaandika HOTSOUP the aftermath hicho miaka 2005 after gulfwar two nikaishia chapter six nikawa nimepata ajira nikabullshit.
Kwa hapa bongo fani hailipi labda upublish na kuuzia majuu
Hili jina lako la Masulupwete kwa mara ya kwanza nililisoma kwenye kitabu kiitwacho Mtu ni Utu. Alikuwa ni mmoja wa wahusika wakuu. Jina la mtunzi wa kitabu ni George A. Mhina.Kuna mwandishi niliwahi soma kitabu chake zamani hizo anaitwa john simbamwene. yupo wapi naye?
vipi nikuwekee chapter moja hapa?Mkuu kweli kwa uandishi huu ulikuwa mwandishi wa vitabu za hadithi?
Weka mkuu. Weka mambo tufanye tathimini.vipi nikuwekee chapter moja hapa?
Unazungumzia Gamba la Nyoka cha Mwanafalsafa mbobezi Euphrase Kezilahabi. Padri Madevu jasusi la CIA na mjane Mama Tinda. Kazi zingine za Kezilahabi ni Kichomi na Karibu Ndani (Mashairi), Nagona na Mzingile (Novela), Rosa Mistika, Gamba la Nyoka, Kichwamaji na vingine viwili vitatu hivi nimevisahau. Kama unaweza kufikiri tafuta vinovela hivyo (Nagona na Mzingile) ujisomee halafu ulete mrejesho hapa.Kuna kitabu kimoja nadhani kiliandikwa na mtunzi wa Rosa mystika kilikuwa kinamhusu padri in the making kinaitwa'PETE' sikumalizia kukisoma and I have often wondered about it...kama hiyo ndio correct title nijuveni
Hivi vitabu viko bookshop gani i.e. Vya Eddie Ganzel, Agoro Anduru nk? (NB: Najua Pundit ha-exist tena ila kama yeyote mwenye jibu tafadhali!Eddie Ganzel nimemsoma vitabu vyake, pamoja na kina Ben Mtobwa, Hammie Rajab na baba lao Eristablus Elvis Musiba.
Sw umebobea huko nafikiri...Unazungumzia Gamba la Nyoka cha Mwanafalsafa mbobezi Euphrase Kezilahabi. Padri Madevu jasusi la CIA na mjane Mama Tinda. Kazi zingine za Kezilahabi ni Kichomi na Karibu Ndani (Mashairi), Nagona na Mzingile (Novela), Rosa Mistika, Gamba la Nyoka, Kichwamaji na vingine viwili vitatu hivi nimevisahau. Kama unaweza kufikiri tafuta vinovela hivyo (Nagona na Mzingile) ujisomee halafu ulete mrejesho hapa.