Eddo na wenzie walipokea fedha kututoa kwenye reli?

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Jana tulianzishiwa mada mahususi ambayo ilikuwa ya KIMKAKATI na vijana wakaiparamia kama ilivyo mwisho wa siku lengo likatimia.

Lengo lilikuwa ni kututoa njiani badala ya kujadili mambo ya msingi watu wakaingia kujadili mambo ya nini kijadiliwe na wachambuzi na kipi ni haramu.

Nimejiuliza ilikuwa ni bahati mbaya kwamba siku mkataba wa GSM & YANGA unatangazwa ndio siku hiyo hiyo tunaambiana tujikite kwenye dakika 90 na mengine tuyaache? Jibu baki nalo mwenyewe

Vijana kabla hamjaingia kwenye mada elekezi jaribuni kuona mitego kuizunguka hiyo mada. Ni kama swali unaloliona rahisi kwenye mtihani ukalivamia bila kujua kwamba lina mtego uliojificha, mwishowe unakwama.

Swipe hiyo video uone picha ya Wakurugenzi 2 wa GSM wakibadilishana mikataba kati ya Yanga na GSM.

Mkurugenzi wa Biashara wa GSM ALAN CHONJO na Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM HERSI SAID, wakipozi kwa picha ya mkataba wa GSM na YANGA.

Kwa mtu ambaye anafikiri sawasawa hii inafikirisha sana vinginevyo kuna shida mahala. Najua Hersi ni Rais wa Yanga ndiyo, lakini hili kama wangekua smart enough wangeweza kumuweka Makamu wa Rais na au CEO kuwakilisha klabu.

Rais ndiye Chief Signatory wa klabu, lakini ndiye Mkuu wa kitengo cha uwekezaji wa Kampuni ya kazini kwake. Jamani hata hili nalo ni kwamba tunaichukia klabu? Jibu baki nalo mwenyewe.

Tukubaliane kwamba tunaweza kupishana kwenye kufikiri na wala hakuna chuki ila ni mitazamo tu.

BIN KAZUMARI (Voice Of The Voiceless)

My Take
Ruksa kututukana
 
Ni rasmi klabu kubwa nchini zimeenda mikononi mwa mabwanyenye....mashabiki tukaijaze taifa tuwachangie mabwanyenye utajiri
 
Utawaambia nini manyani wale. Luc Emely alikua sahihi. Na alichokiandika bin kazumari nilikua nakitafakari kila mara why kila yanga wakiweka mikataba yao ya kimagumashi huyo eddo na kina oscar na kitenge wanakujaga na vistory vyao vya kisoro tu. Leo kumwemve anasema yeye hapaswi kuongelea mikataba hivi yule aliyekua abaongelea simba kushindwa kumsajili adebayo na mambo mengine ya mikataba ya wachezaji wa simba kuachwa ni nani..? Akili kichwani bin kazumari ni mwandishi ninaye mkubali aisee
 
Simba alishinda makombe yote 4 years consecutively kipindi ambacho yanga alikua hoi bin tabaan.

Shida za yanga ni furaha kwa simba maana hatokua na ubavu wa kuleta wachezaji wazuri. Ni nani aliwahi kuwaza kama yanga angeweza kumleta aziz ki na simba akashindwa?

Ni kipindi ambacho simba anaishi kwa sonona maana mpinzani wake yuko vizuri. Kwa pesa hamuwezi, kwa vyote vile hamuwezi na hata uwanjani hamuwezi maana anapigwa na kupigika kama ngoma.
 
Napongeza uwekezaji wa GSM.
Hongera Le president Eng.Hersi.
Yanga wakitaka mchezaji anapatikana
Wakiamua kocha abaki anabaki hata Kama waarabu wa kaskazini wanamtaka.
Wakiamua kulitibua Manzoki asije makolo linafanyika.
Wakiamua mchezaji wao aondoki hata Kama matajiri wa bondeni SA wanamtaka hang'oki.
Yanga haazimi kocha
Haiuzi kocha.
Ipo process ya kujiimarisha.
Kama hauamini mikataba Jemedari omba CAG azikague hizi klabu.mtaokoa bilioni 20 zenu au mtarudishiwa hisa49% mlizopolwa
 
Kama ambavyo "Mwamedi" amejimilikisha timu ya makolo, na mpaka leo hawajui bilioni 20 ilienda wapi. Makolo ni mbumbumbu!
Uzuri wa utopolo kila analofanya simba na yeye anaiga tu. Kubadilika kuwa kampuni - utopolo wanaiga (sio mbaya), kupata dili za mikataba mikubwa ikiwemo dili za jezi- utopolo wanaiga (sio mbaya), kuweka malengo makubwa kimataifa kutoka kushindana kijinga hapa ndani - uto wanaiga (sio mbaya), kuuza timu kwa mo kwa bilioni 20 - utopolo wanaiga (hapa ndipo napo washngaa). Yani hawajifunzi kwa simba.

Kama kweli watopolo wangekuwa na akili kama mzee kikwete na babake haji basi wangekuwa makini na sana sana kwenye kuiuzia timu gsm. Yaani hawa jiesim hawako kimpira pale, tofauti na Mo ambaye simba ikifungwa na yeye anaumwa. Ona leo hersi anatoa pesa mfuko huu na kuiweka mfuko wa kushoto matopolo yanashangilia. Kifupi matopolo yanafikiri yanaikomoa simba kwa kudanganywa mikataba hewa.
 
Ni rasmi klabu kubwa nchini zimeenda mikononi mwa mabwanyenye....mashabiki tukaijaze taifa tuwachangie mabwanyenye utajiri
Sasa si na wewe utafute hela kwa bidii ili uwe bwanyenye! Kulalamika na kulialia, itakusaidia nini?
 
Ni rasmi klabu kubwa nchini zimeenda mikononi mwa mabwanyenye....mashabiki tukaijaze taifa tuwachangie mabwanyenye utajiri
Na wewe kuwa bwanyenye kama hujajinyea fala wewe
 
Msitutoe kwenye reli... Wananchi wanataka furaha na makombe tu...
Ikiwezekana ofisi za Yanga S.C zihamishiwe pale Salamander kabisa....
Na huu ni mwanzo tu wa mateso ya muda mrefu mnayoenda kuyapitia nyie mbumbumbu fc kwa maana Yanga iliyo imara kiuchumi itawapa mateso ya muda mrefu sana
 
Hersi alisimama kama nani kwenye huo usainishaji mikataba?
 
Cha muhimu

Timu inakaa kambi sehemu nzuri

Wachezaji wanalipwa posho na mishahara kwa wakati

Timu inasafiri bila kuunga unga

Timu inasajili bila longo longo

Timu inapata ushindi

Haya uloyaleta we kakae na jemedari muyachambue mpaka njaa ziwaume
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…