Eddy kenzo awatolea uvivu MTV Base, adai upigaji kura waseme kama hauna umuhimu

brave one

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
4,879
Reaction score
7,386
Msanii wa Uganda eddy kenzo asema kuna namna inafanyika kuamua washindi wa mtv mama na si upigaji wa kura maana kwenye kipengele change yeye ndo alikuwa na kura nyingi akifuatiwa na mr. Flavour huku alieshinda Casper nyovest alikuwa na 3 kwa wingi wa kura

 
Haya sasa kumekucha msanii kutoka afrika mashariki amefunguka na kudai kuwa amehujumiwa katika tuzo za MTVmama katika kipengele cha Mtumbuizaji bora wa kiume!

Eddy Kenzo amesema alistahili kupata tuzo hiyo maana alipigiwa kura nyingi kuliko msanii yeyote! Amesema kuwa katika kipengele hicho yeye ndo aliongoza kwa kupigiwa kula na Alie chukua tuzo alikuwa nafasi ya nne

Amesema kuwa hata hao MTVbase walipost na kusema ndie msanii anae ongoza kwa kupigiwa kura!

Amesema kuwa kisa yeye ni Ambassador wa Airtel Afrika na Cassper akiwa ambassador wa MTN ambao ndio wadhamini wa MTVMama awards! Amesema amefanya zaidi ya show 35 katika nchi 10 afrika katika viwanja vikubwa

Amelalamika na kusema labda yeye haelewi maana ya kumpigia kura msanii unaempenda ila mashabiki wake walipiga vya kutosha

Picha limeanza
 
Akachukue tuzo AEA hahaha.
 
Nafikiri tuzo huamuliwa kwa kura za mashabiki na maoni ya majaji. Hizi habari za kura peke yake huwa hazitoi mshindi peke yake, mtu mwenye followers wengi atashinda hata kama sio mwanamuziki halisi. MTV naona wameliona hilo ndio maana wakina wizkidayo sasa wanapata wanachostahili.
 
Kupigiwa kura sana siyo ndo uhakika wa msanii kushinda Tuzo ndomana kuna majaji/kamati inayoamua nani ni mshindi,wangekuwa wanaangalia mashabiki kuna watu wangekuwa hawashindi hata siku moja
 
Tuzo za Africa hazieleweki sometime , Naona kila tuzo zinavigezo vyake, afrimma msanii bora West Africa OLAMIDE, Msanii bora wa mwaka MR FLAVOR, ukija AEA msanii bora wa kiume Diamond platnumz, ukija BET black coffee (yaani na kuangalia kwangu kote mtv, trace sijawahi kuiona hata nyimbo yake moja), ukija MTV MAMA best male na artist of the year wizkid, FULL MVURUGANO hata mm mwenyewe nakaa natafakari wanatumia kigezo gani kupata mshindi, mpaka sasa sielewi nasubiria AFRIMA mwezi huu sijui nao watasemaje.
 
Ila kukosa kunauma asikwambie mtu [emoji23][emoji23][emoji23] usipokua mvumilivu lazima utokwe povu kama Eddy Kenzo. Hata Diamond mwenyewe kajikaza tu kulinda heshima yake.

Ila hawa nao MTV wamezidi yaani vipengele vyote muhimu Ukiacha best group tuzo zimeenda SA na Nigeria daah
 
Vile najiuliza hapa.. Hvi Danny Welbeck anaweza kua na follower wengi kuliko Cristiano Ronaldo? Kinacho mnyima Danny hawa follower n nn na kinacho mpa Cristiano hawa follower n nini?

Nachomaanisha n kwamba.. Msanii ili aweze kuteka nyoyo za watu na awe na wafuasi wengi n lazima awe bora, hao follower n kielezo cha ubora wako, kama wasikilizaj au mashabik wa hao wanamzik n hao majaji basi n sahihi kufanya hvyo
 
NAONA LEO UKIMUULIZA WIZKID KUHUSU TUZO ZA AFRICA ATABADILI KAULI,MAANA YEYE NDIO ANAONGOZA KWA KUZIPONDA TUZO ZA AFRICA ILA JANA NI FULL KUZISIFIA.
 
wanampa wanaemtaka nahisi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…