Eden Hazard; matumizi mabaya ya rasilimali

Eden Hazard; matumizi mabaya ya rasilimali

mwanakaya

Member
Joined
Mar 17, 2012
Posts
56
Reaction score
183
Tangu asajiliwe kutoka klabu ya Lile ya Nchini ya Ufaransa kujiunga na Chelsea msimu wa 2012/13 Eden Hazard amekuwa mchezaji bora sana. Pamoja na kutoka klabu ya kawaida kwenye ligi ya daraja la chini lakini alionyesha kwamba ana kipaji. Tena kipaji kikubwa.

Nimemuangalia Hazard mwaka huu kwenye kombe la dunia nchini Urusi nikamkumbuka Zinedine Zidane wa mwaka 1998. Sio kwa mfanano wa uchezaji lakini ni namna walivyofanikiwa kuzibeba timu zao za Taifa. Zidane alikuwa kila kitu kwa ufaransa kwenye kombe la dunia '98, Hazard alikuwa kila kitu kwa Ubelgiji mwaka huu pale Urusi. Pamoja na kuwepo kwa mafundi wengi lakini timu ilijengwa kumzunguka Hazard.

Pamoja na kuwepo wazoefu wengi wakiwemo Vicent Kompany, Toby Alderweireld na Jan Vertonghen lakini Martinez aliamua kumpa kitambaa Hazard. Ilishangaza sana. Lakini hakumuangusha.

Eden Hazard ndiye kiungo mshambuliaji aliyekamilika zaidi kwenye dribbling inawezekana kuliko Messi, Ronaldo na Neymar. Ndio, naongelea dribbling. Ni vigumu sana mchezaji wa timu pinzani kuchukua mpira miguuni kwa Hazard bila kumchezea rafu. Vigumu mno.

Lakini pamoja na ubora huu, Hazard amepungukiwa na vitu muhimu. Hafungi magoli mengi na hatoi assist za kutosha. Kwa misimu mitano aliyocheza Chelsea amefunga magoli 70 tu kwenye mechi 212. Ni wastani wa magoli 14 kwa msimu. Hapa ndipo inapokuja tofauti yake na wachezaji bora kama Ronaldo, Messi na Neymar.

Kikubwa kinachomfanya Hazard asifikie kiwango cha kuheshimika ni timu anayochezea. Pamoja na uwekezaji mkubwa uliofanywa na chelsea bado inachukuliwa kuwa ni timu ya daraja la kati. Haiwekwi daraja moja na Real Madrid, Barcelona, Bayern Munich au Manchester United. Naamini angeenda timu kama Madrid ingemchukua muda mfupi kuwekwa kwenye orodha ya wachezaji bora duniani.

Inashangaza kuona kwamba kwa miaka hii yote Neymar amekuwa bora juu yake. Kilichombeba Neymar ni kuchezea Barcelona. Hicho tu. Hazard angeenda Madrid hasa baada ya Ronaldo kuondoka timu nzima ingemzunguka. Angefanywa kuwa mfalme mapema.

Kwa vyovyote vile Hazard ataendelea kuwa nchezaji mzuri wa daraja la kawaida akiendelea kubaki alipo. Ni kama ilivyo kwa Sergio Kun Aguero wa Man City. Au ilivyokuwa kwa Allan Sheerer wa Newcastle. Waliishia kuwa wachezaji bora wenye mafanikio madogo. Ni wakati sasa Hazard aamue kuwa raslimali inayotumika vyema.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Omba radhi kwa kusema Harzard ndie aliekua akiibeba Belgium. Ulitizama vizuri mashindano ? De bryne Ulikua ukimuona?
 
Na hiyo aliekwambia Zidane Aliibeba pekeake France 98 ni nani? Ulikua na umri gani kwani kipindi kile?
 

Nakubaliana na wewe kwamba Hazard ni mchezaji mzuri sana anayechezea timu ya kawaida.

Huyu Hazard angekuwa anaichezea Manchester United, angekuwa anaimbwa yeye kila kona.
 
Back
Top Bottom