Edibily Jonas Lunyamila, miguu ya Dhahabu, kichwa chenye mamlaka ya kusoma alama zote ndani ya Uwanja

Hii picha Katika mchezo wa fainali ya kombe la Hedex, uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Hii ilikuwa ni muda mfupi baada ya Lunyamila kutua nchini toka nchini Ujerumani alikokuwa amekwenda kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa, na siku hii akiwapiga Simba moja kati ya mabao mawili na lingine likifungwa na Bakari Malima kufuatia kona ya Lunyamila. Yanga ilishinda 3-0

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Hii ni hazina, na ni vizuri anapata sifa zake akiwa ni hai bado, badala ya kusubiri atakapokufa ndio sifa zake zienee na michango lukuki kama ilivyo mazoea kwa Tanzania yenye unafiki.

Hongera sana E.J Lunyamila

Yanga imekuwa na hazina kubwa ya wachezaji Wazuri sana.
 
Nakumbuka 1993, kwnye mashindano ya Challage navikiri Yanga ikicheza na AS Villa tulipiga bao 2-1 Lunya akifunga bao la pili, Kule Uganda mpka leo kuna Mabasi yammeandikwa Lunyamila

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Tulisoma nae yeye anaingia F1 mi F4, lakini mechi ya Welcome F1 alitutesa sana.
 
Nahisi huyu Jamaa ndio alisababisha mm kuishabikia yanga,
Maana kipindi hicho anacheza nilikua Mdogo hata shule siajaanza , kuna mzee tulikua tunaishi nae alikua anamsifia Sana Jamaa na alikua ni yanga nikajikuta nafuata tu upepo na kua shabiki Wa yanga
 
Karibu tu jangwani
 
Tupe briefly habari zake mkuu

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
Lunya kama alivyopenda kuitwa ni miongoni mwa vipaji murua katika soka kuwahi kutokea nchini. Aliujua mpira nao ulimtii. Wakati wa paper ya mwisho form 4, alifanya mtihani huku akisubiriwa na gari la Gulamali nje.
Kizuri ninachomsifu Lunya ni utulivu na Nidhamu ya matumizi. Fedha aliyoipata alifanya vitu vonavyombeba Leo. Kosa kubwa katika maisha yake ya soka ni kuwa na mapenzi yaliyopitiliza kwa Yanga kwa kisingizio cha kukumbuka fadhila. Safari ya Ujerumani ilikuwa hatua ya kutokea lakini mapenzi kwa Yanga yakamwangusha.
 
Lunyamila,Kizota, Nteze na Mmachinga vipaji hivi havitatokea hivi karibuni kwenye soka la bongo
Lunyanila na Nteze....ni matunda ya umiseta.....tunapoteza vipaji vingi sana kwa kupuuzia michezo mashuleni.... siku hizi Shuleni michezo haichezwi tena Kama zamani.... serikali kwenye hili imetuangusha sana....shule inafunguliwa na vibali vyote kwenye eneo la nusu eka.....hakuna viwanja vya michezo....wanaocheza mpira siku hizi ni ambao hawajafanikiwa kwenda shule....wengi vipaji hawana wanalazimisha tu.
 
Maajabu! na hao wachezaji kwa nini wabakubali kurubuniwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…