NI ndoto inayotisha. Pambano la Simba dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco ni ndoto inayotisha. Simba wametoka kufungwa jumla ya mabao 6-1 katika mechi mbili walizocheza na Raja, timu nyingine kutoka jiji hilo lenye wakazi milioni tatu na zaidi nchini Morocco.
Lakini kuna ndoto nyingine inayosikitisha. Pambano la Yanga dhidi ya Rivers United ya Nigeria. Kwanini Yanga walikuwa wanashangilia baada ya kupangwa na Rivers? Bado sijaelewa vizuri. Kwamba ni timu rahisi? Kwamba labda Rivers wana nafuu tofauti kama wangepangwa na wakubwa wengine wa kundi kama Pyramids?
Tuanze na mechi ya Simba. Sioni nafuu. Ni ndoto inayotisha. Ninachoamini ni kwamba ikitokea Simba wakaitoa Wydad basi wataenda kuchukua taji lenyewe. Ni ngumu Simba kuwatoa Wydad kwa sababu tatu kuu.
Inawezekana pia ni ngumu Simba kuitoa timu nyingine yoyote ambayo wangepangwa nayo kando ya Wydad.
Labda tujikite kwa Wydad pekee ambao tayari wamewekwa katika mikono ya Simba. Simba watahitaji maajabu. Ukitazama namna ambavyo walitawaliwa na Raja katika mechi zote mbili kisha ukaenda kutazama msimamo wa Ligi Kuu ya Morocco utajua mazingira ya hatari ambayo Simba wapo.
Katika uhalisia wa kawaida Wydad ni timu kali kuliko Raja. Na katika uhalisia wa nje tu Wydad imeizidi Raja pointi 12 katika Ligi yao. Raja inashika nafasi ya tano wakati Wydad inashika nafasi ya pili. Inakuonyesha tu kwamba hata katika Ligi yao ya Morocco kwa sasa Wydad ni wakali kuliko Raja achilia mbali kwamba wao ni mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Lakini kuna ukweli kwamba Wydad wanacheza na Simba hii ambayo imeendelea kujitafuta. Simba ambayo haijafikia bado makali ya ile ya kina Louis Miquissone, Clatous Chama, Hassan Dilunga, Rally Bwalya. Simba hii ambayo viwango vya kina Josh Onyango vimeanza kuwatia shaka mashabiki. Wataiweza kasi ya Wydad kama walishindwa kuendana na kasi ya Raja?
Lakini sababu ya tatu ni ukweli kwamba mechi ya kwanza itachezwa kwenye Uwanja wa Mkapa pale Temeke. Simba sio tu watahitaji kushinda, lakini watahitaji kushinda mabao mengi. Hili la kushinda mabao mengi dhidi ya Wydad ni jambo ambalo litawastaajabisha watu wengi. Kuifunga Wydad ni jambo moja, kuifunga mabao mengi ni jambo jingine ambalo litastaajabisha. Simba wataweza kweli?
Ni wazi kwamba kule Casablanca Simba wanaweza kupewa ubatizo wa moto. Kama wanatamani kujaribu kupita basi kila kitu kimalizike Casablanca. Kinachoweza kuwapitisha ni kufungwa idadi ndogo ya mabao kuliko ambayo wao watakuwa wamefunga Dar es Salaam. Hili litawezekana? Naona ni jambo gumu.
Casablanca Simba watakutana na mashabiki wenye mzuka wa Wydad. Katika mechi ya mwisho waliyokwenda Casablanca walikutana na jukwaa moja la mashabiki wa Raja ambao bado waliwapa shida. Mashabiki wengi hawakwenda uwanjani kwa sababu Raja alishapita na tayari alishapata uongozi wa kundi.
Mechi hii ya robo, bila ya kujali ambacho kitatokea Dar es Salaam pale Temeke, Wydad watataka kuziyumbisha akili za wachezaji wa Simba. Wale mashabiki wao vichaa wataingia uwanjani kama sherehe ya kuipeleka timu yao nusu fainali kwa mara nyingine tena huku wakiamini kwamba wanakwenda kutetea ubingwa wao kwa mara nyingine tena.
Vyovyote ilivyo, Simba wanahitaji kupambana. Kucheza kiume hasa kwa ajili ya kulinda heshima ya nchi. Watahitaji kupambana nyumbani na ugenini kwa ajili ya kulinda heshima ya nchi. Kutolewa ni jambo moja, kutolewa kifedheha ni jambo jingine.
Ninachofahamu ni kwamba Simba ikicheza mechi kama hizi huwa inabadilika zaidi. Watahitaji kubadilika zaidi.
Vipi rafiki zao Yanga? Nilishangaa kuona wanashangilia baada ya kupangwa na Rivers. Akili yangu inanituma kwamba kama Yanga hii ingecheza na Rivers ile ya miezi 24 nyuma huenda Yanga hii ingepita.
Walitolewa kwa kufungwa kwa matokeo ya aina moja ya 1-0 nyumbani na ugenini. Fiston Mayele na Khalid Aucho hawakucheza baada ya leseni zao kuchelewa.
Pia Yanga hawakuwa katika ubora kama ambao leo wanao. Hata hivyo, hii ni hadithi ya upande mmoja. Vipi kuhusu Rivers? Yanga wanajua kwamba Rivers wamekwenda juu maili ngapi baada ya kucheza nao pambano la mwisho pale Port Harcourt? Nadhani Yanga walifurahia kupangwa na Rivers kwa sababu wamewakwepa Pyramids na USM Alger.
Lakini walishangilia kwa sababu ya kuona walikuwa wamepangwa na Rivers ambayo bado ipo katika vichwa vyao. Ile Rivers ya kawaida ambayo walicheza nayo mechi mbili na kisha wakatolewa. Katika vichwa vyao wangefanya uchunguzi kwanza kujua kama watacheza na Rivers ile ile au nyingine ambayo inalisaka taji la Shirikisho.
Vile vile naamini kwamba wameshangilia kwa sababu wanajua kwamba safari hii wataanzia pambano lao ugenini kisha kumalizia nyumbani. Kwamba watafanya kila wanachoweza kupambana ugenini na kupata ushindi au sare halafu wamalize kazi nyumbani. Siamini sana katika jambo hili kwa sababu majuzi tu Waganda wametukumbusha kitu.
Taifa Stars walikwenda Ismailia wakapata ushindi dhidi ya The Cranes. Waliporudi Uwanja wa Taifa wakachapwa kwa kipigo kile kile ambacho walikitoa Misri. Ni hadithi kama ile ya Simba mwaka 1993 walipoingia fainali za CAF. Walikwenda Abidjan kucheza dhidi ya Stella wakatoka suluhu. Waliporudi nyumbani wakalala 2-0.Yanga wasishangailie sana kupangwa na Rivers.
Kikawaida tu katika heshima ya mchezo huu haupaswi kushangilia kupangwa na timu yoyote ile. Unahitaji kuonyesha heshima. Kama hauonyeshi heshima unaweza kujikuta katika ndoto inayosikitisha mbele ya safari.
MWANASPOTI