Edo Kumwembe: Simba walikata pumzi 2nd half

Edo Kumwembe: Simba walikata pumzi 2nd half

Labani og

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2020
Posts
19,637
Reaction score
29,473
Amechambua @edokumwembe

Ngoja nilete uchambuzi wangu uchwara kuhusu pambano la Simba na Yanga, hasa mabao yote matano ya Yanga. Mabao yao yote yalitokana na kuwa juu kiutimamu wa kimwili na akili. Mabao yote yamekuja kwa kuwahi mipira ya Simba au iliyo nusu kwa nusu. Watu wameshangilia mabao tu lakini hawakuangalia chanzo. Bao la kwanza...beki wa Simba kaosha mpira wa krosi wa Pacoume, Yao akauwahi Simba wakiwa wamezubaa, akampiga chenga mtu kule pembeni. Bao.

La pili, Chama kajaribu kumpasia mshambuliaji wake pale kati, Bacca kauwahi kausogeza mbele ukaenda kwa Aziz aliyempelekea Maxi. Bao. Bao la tatu, Kanoute kataka kumpasia Tshabalala kushoto, Yao kauwahi kampasia Pacome aliyempasia Mzize aliyempa Aziz. Bao.

Bao la nne, Yao kampress Onana, Pacoume akaupitia akapiga kisigino kwa Yao wakatoka wakampasia Mzize aliyemzidi mbio na nguvu Tshaba. Bao.

La tano Simba wameosha kumpelekea mtu, Lomalisa kautokea mbele ya mchezaji wa Simba kampa Aziz aliyempasia Maxi, akakatwa ngwala. Penalti kisha bao. Licha ya ubora wa Interception na kuwahi mipira lakini Yanga ni wazuri katika transition ya mpira. Wana kasi ya kwenda mbele na akili yao ya kwanza ni kuonana kuliko kufanya ubinafsi. Mbaya zaidi kama nilivyosema,

Simba walikuwa wanaporwa mipira na hivyo walijikuta katika wakati mchache sana wa kujipanga. Bao la pili la Yanga Aziz alikokota hatua nane bila ya kukabwa.

Simba wanahitaji fitness ya hali ya juu kabla ya kwenda makundi achilia mbali mbinu za Robertinho. First half walicope, second half pumzi na stamina vikakata. Rudia kutazama mabao ya Yanga kwa umakini.........
Screenshot_20231106-083944.jpg
 
Back
Top Bottom